Kanisa lafunzwa juu ya katiba

Kanisa la Tanzania kwa mara nyingine limetakiwa limetakiwa kutumia fursa mbalimbli zinazopatikana kwa kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwa lengo la kuleta ukombozi na kulinusuru taifa na changamoto ambazo kwa upande mwingine zimekuwa zikihatarisha amani iliyopo, huku likitambua kuwa ndilo mhimili wa nchi,Elimu hiyo ya katiba inazidi kutolewa makanisani kuhakikisha waksristo wanaelewa elimu hiyo.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Wakili Magdalena Rwebangira wakati akitoa semina juu ya kanisa na Katiba, iliyofanyika katika kanisa la City Harvesty lililopo Garage, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumuwezesha mkristo kutambua umuhimu wa katiba na jinsi ya kusimama kudai haki yake.
Wakiri huyo alisema kuwa kanisa lazima liitumie katiba katika kudai haki na sii kukaa kimya huku wakristo wakibaki kulalamika pindi linapotokea tatizo lolote, linalohusu masuala ya kanisa na kusema kuwa huko ni kushindwa kutafuta haki yao ya msingi kwa masilahi ya kanisa na taifa kwa ujumla.


Wakili Magdalena Rwebangira
Kadhalika Bi.Rwebangira alilikumbusha kanisa kutambua kuwa nchi hivi sasa iko katika mchakato wa kuandaa katiba mpya, hivyo kuwataka kutumia nafasi hiyo katika kutoa maoni yao juu ya kile wanachokihitaji huku akiongeza kuwa ni sehemu ya pekee ya kanisa kuhusika zaidi na si kurudi nyuma katika mambo ya kiserikali kama hayo.
Aliongeza kuwa lazima maoni ya uhuru wa kuabudu katika katiba ijayo uzingatiwe, kutoingiliwa kwa namna yoyote katika ibada zinazo fanyika, kutoangalia masuala ya kidini ikiwa ni pamoja na kanisa kupewa nafasi ya kutosha katika kumhubiri Kristo wa kweli, huku akisema kuwa nchi iko mikononi mwa kanisa.


Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kutoa elimu juu ya mambo ya Katiba Dk.Paul Shemsanga, ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Victory Gospel Assembly Tanzania aliyepata nafasi ya kutoa elimu siku hiyo alisema kuwa ni wakati wa kanisa kutambua nafasi yake na kuitumia ipasavyo na wala si kubaki likilalamika.


 Mchungaji Kiongozi wa kanisa la City HarvestYared Dondo
Aliongeza kuwa mambo magumu ambayo kwa namna moja ama nyingine kanisa limesahau wajibu wake, hivyo nchi kuzidi kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoleta mfarakano na amani tuliyojaliwa na Mungu kuzidi kutoweka siku hadi siku.
Askofu huyo alisema kuwa umefika wakati kanisa kutokaa kimya, na badala yake kusimama kidete katika maeneo yote, kwa lengo la kuleta ukombozi ndani ya taifa la Tanzania na kukomesha migogoro inayojitokeza. 
“Lazima katika Katiba, kanisa lishiriki sana, lazima tuzungumzie uchumi, umiliki wa ardhi, kutokubali ushawishi kutoka nchi za nje ikiwa ni pamoja na masuala ya kuabudu kutoingiliwa” alisema Askofu huyo. 


Aidha akikazia zaidi Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo la City Harvest, Architecture Yared Dondo, ambao kuanzia siku chache zilizopita wameanza kufanya ibada zao katika kanisa lao jipya lililopo Garage jijini hapa, alisema kuwa ni lazima kanisa kuwa makini na suala la Katiba ili mambo yanapoharibika badaye kanisa lisiweze kulalamika.


“Lazima Kanisa kuwa makini na kutopuuza suala hili la Katiba ni muhimu sana, ili badaye tusije tukawa watu wa kulaumu, kama hatutasimama kama wakristo, ambao tuna dhamana kubwa juu ya nchi hii,” alisema Mchungaji huyo.  

Askofu Paschal Kikoti afariki dunia



Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, limepata pigo la kumpoteza askofu wake wa kwanza, Paschal William Kikoti (55), aliyefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Taarifa za kifo kicho zilitolewa kwa waumini juzi usiku katika Kanisa Kuu la kiaskofu na Makamu Askofu wa jimbo hilo, Padre Patrick Kasomo.

Alisema kuwa Askofu Kikoti alipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu Jumapili iliyopita, majira ya saa moja asubuhi wakati akioga bafuni, na ndipo alipoanguka ghafla kisha kupoteza fahamu.

Padre Kasomo alifafanua kuwa, Askofu Kikoti aligunguliwa baadaye na mapadri na masista walipokuwa wametoka kwenye ibada ya misa ya kwanza saa 2:30 asubuhi huku akiwa ajitambui.

“Baraza la Maaskofu lilitafuta usafiri wa ndege siku hiyo, ambayo ilimsafirisha hadi mkoani Mwanza na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu hadi hapo juzi saa 2:30 jioni alipofariki dunia,” alisema.

Taarifa hiyo ya Padre Kasomo, iliwashtua waumini wengi ambapo baadhi yao walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio na wengine kuzirai.

Askofu Kikoti alizaliwa mkoani Iringa katika Parokia ya Nyabula mwaka 1957 na kupewa daraja la upadre Juni 29, 1988 humo humo mkoani Iringa.

Mnamo Januari 14, 2001 Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, aliliunda jimbo jipya la Mpanda na kumteua Kikoti kuwa askofu wa kwanza kuliongoza.

Kuhusu mazishi, Padre Kasomo alisema kuwa mwili wa marehemu Askofu Kikoti utawasili jimboni humo kwa ndege leo ukitokea Mwanza na unatarajiwa kuzikwa rasmi Jumamosi katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Mpanda.

Mauaji ya Mhubiri wa kiisilamu nchini Kenya yasababisha ghasia na uvunjifu wa Amani.

Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa kiisilamu ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa pwani mwa Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa.


Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.


Aboud Rogo 


Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.


Wapiganaji wa al Shabaab

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi.

bbcswahili

Kasoro zashamiri Sensa ya Watu na Makazi

Sensa ya Watu na Makazi jana iliingia siku yake ya tatu, huku kasoro kadhaa ikiwamo ukosefu wa vifaa, upungufu wa makarani na watu kugoma kuhesabiwa vikiripotiwa.Katika baadhi ya maeneo hadi jana, wananchi walikuwa hawajaanza kuhesabiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na ukosefu wa vifaa na makarani.

Ofisa Uhamasishaji wa Sensa Taifa, Said Ameir alikiri kupata taarifa za kasoro hizo lakini akaeleza kushangazwa na chanzo chake, akisema: “Vifaa tulivigawa maeneo mbalimbali nchini kulingana na mahitaji. Tunashangazwa na taarifa hizo kwamba hata wengine wamekosa reflector (makoti ya kuakisi mwanga) na vitambulisho.”

“Tunachofanya sasa ni kuchunguza tatizo hilo limeanzia wapi na limesababishwa na nini. Vilevile tunajitahidi kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapelekwa sehemu hizo ili kazi hiyo iendelee kama kawaida.”
Alisema pamoja na kasoro hizo, kazi hiyo inaendelea vizuri na itakamilika ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.

Kasoro
Baadhi ya makarani wa Kata ya Ubungo wamesema baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi wamekataa kushirikiana nao.
Mratibu Msaidizi wa Sensa kata hiyo, Pertronia Lyamuya alisema tatizo jingine ni baadhi ya waumini wa Kiislamu kugoma kuhesabiwa kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wakazi wa Kinondoni Shamba, Dar es Salaam.
Katika baadhi ya maeneo, makarani, walilazimika kutumia polisi kutekeleza majukumu yao. Baadhi ya mitaa ambayo polisi walitumika ni Juhudi, Kingugi na Kiburugwa iliyoko Temeke. Mitaa hiyo ilikuwa imebandikwa matangazo ya kuwahamasisha watu wasishiriki Sensa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Engerasia Lyimo alisema kazi ya kuhesabu watu ilisimama kwa muda kusubiri polisi wa kuwasindikiza makarani hao kwenye nyumba hizo ili kulinda usalama wao.
Lyimo alisema katika Mtaa wa Kingugi, alijitokeza mjumbe wa shina wa CCM (jina tunalo),ambaye aliwahamasisha wakazi wa eneo lake wasijitokeze kuhesabiwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Basihaya, Kinondoni, Daniel Aron alisema kaya nane zilikataa kuhesabiwa kwa maelezo kwamba hazioni umuhimu wake. Alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa Ofisi ya Kata ya Boko.
Alisema kimsingi, changamoto kubwa katika eneo lake ni uchache wa vifaa kiasi cha makarani kushindwa kuanza kazi hiyo.
Msimamizi wa Kata ya Buguruni, Wilaya ya Ilala, Stella Mshana amesema kuwa baadhi ya watu wamekataa kuhesabiwa, wengine kutokana na imani za kidini na wengine kwa kutoelewa umuhimu wake.
“Maeneo ya Mnyamani tumekutana na vikwazo lakini kusema ukweli idadi yao ni ndogo kuliko wanaotupa ushirikiano. Unaweza ukakuta labda katika watu sabini, mmoja ndiye anakataa,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amesema Serikali itaendelea kupambana na kundi la watu wanaojihusisha na kusambaza ujumbe wa kupinga kushiriki Sensa.

Alisema jana kwamba hadi sasa Polisi inawashikilia watu wanne kutoka Wilaya za Temeke na Kinondoni.... “Kijana mmoja alijulikana kwa jina la Yusuph Ernest alikamatwa akisambaza ujumbe huo maeneo ya Magomeni Kagera.”

Arusha, Watu wasiojulikana, juzi walibandika mabango yanayowazuia makarani wa Sensa kutekeleza wajibu wao katika Kata za Ngarenaro na Unga Ltd. Mabango hayo yalibandikwa katika eneo la Daraja la Ngarenaro.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo pamoja na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Arusha, Magreth Martin walisema hadi jana hakukuwa na tukio la kukwamisha Sensa licha ya kuwapo kwa tukio hilo.

“Nawashukuru sana wananchi wa Arusha kwa kushiriki vyema Sensa katika siku hizi mbili za mwanzo baada ya kuelimishwa na kuelezwa umuhimu wake kwa mipango ya Serikali na maendeleo ya taifa licha kuwapo baadhi ya watu waliojaribu kuwashawishi kususia.”

Tanga,Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ibrahim Matovu wamewaagiza makarani wa Sensa kwenda kuwahesabu wanawake ambao waume zao wanadaiwa kukimbilia kusikojulikana kukwepa kuhesabiwa.Walitoa amri hiyo baada ya kuripotiwa kuwa baadhi ya Waislamu wa Kijiji cha Kigombe, Muheza, wamekimbilia porini kukwepa kuhesabiwa.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wanaume waliondoka na kutoa amri kwa wake zao kutohesabiwa vinginevyo wangepewa talaka.
Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Kigombe, Mashauri Kanyama alisema tatizo hilo limesababisha baadhi ya makarani kushindwa kutekeleza kazi zao kikamilifu.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigombe, Mohamedi Hatibu alisema baadhi ya wakuu wa kaya wametishia pia kuwapa talaka wake zao iwapo watahesabiwa.
 

Kilimanjaro
Baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro wamesema Sensa ya Watu na Makazi imekwenda vizuri.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walilalamika kwamba makarani walikuwa wakisuasua kufanya kazi hiyo.
Walisema makarani wamekuwa wakitumia muda mwingi na kwamba waliotegemea kuhesabiwa Jumapili, hawakuwaona makarani.

“Tulitegemea tutahesabiwa Jumapili na wengi hatukutoka nyumbani tukiwasubiri hasa ikizingatiwa ilikuwa siku ya mapumziko,” alisema Eben Ndosi, Mkazi wa Njiapanda Himo, Wilaya ya Moshi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mto Mabungo, Wilaya ya Moshi, Estarick Mbuya alisema kazi hiyo ni ngumu lakini itafanikiwa.

Wananchi wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro wamehimizwa kujitokeza kuhesabiwa katika Sensa bila kujali wito wa kutojiandikisha.Msimamizi wa Kata ya Masama Mashariki, katika Kitongoji cha Modio, Mwalimu Bernedicta Kilasara alisema katika taarifa yake kuwa mpaka kufika jana jioni, kaya 320 zilikuwa zimeshahesabiwa nyingi zikiwa za waumini wa Kiislamu.Kilasara alisema Waislamu wa Kitongoji cha Modio walikuwa wakihimizana kujiandikisha.

Igunga walipwa
Wenyeviti  wa vitongoji wilayani Igunga, Tabora wameanza kulipwa posho zao za Sensa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga, Protace Mgayane alisema wenyeviti hao kutolipwa fedha hizo ilikuwa ni moja ya sababu za kutofanikisha kwa kiasi kikubwa kazi hiyo kwani viongozi hao ndiyo wanaofahamu maeneo yao pamoja na jamii ya eneo husika.

Wilaya ya Igunga ina wenyeviti wa vitongoji 632 na kila mmoja atalipwa Sh10,000.
Alisema fedha hizo ni kutoka katika bajeti ya Sensa ambayo imetokana na marekebisho yaliyofanywa katika baadhi ya matumizi ili kuwalipa viongozi hao muhimu wa vitongoji.
 

Ngorongoro,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutowaficha na kuwaandikisha watu kutoka Kenya, katika Sensa ya Watu na Makazi inayoendelea nchi nzima.

Lali alisema wananchi kutoka nchi hiyo jirani wamekuwa na uhusiano na mwingiliano wa kikoo na wakazi wa Ngorongoro hasa wa jamii ya Kimasai na kwamba hawatakiwi kuandikishwa kama Watanzania.
“Naomba kutoa wito kuwa wanaopaswa kuandikishwa ni Watanzania na kama kuna hao wageni kuna taratibu zake na wasiandikishwe kama ni Watanzania,” alisema Lali.

Ngorongoro ni moja ya wilaya za mpakani ambazo watu wake wana uhusiano mkubwa ukiwamo wa kikoo na moja ya koo hizo ni ya Loita ambayo ni ya Wamasai waliopo Kenya na Tanzania.

Watimuliwa Morogoro
Baadhi ya makarani wa Sensa katika Tarafa ya Turiani, Morogoro wamedai kufukuzwa kwenye baadhi ya kaya kwa kutuhumiwa kuwa matapeli kutokana na kukosa fulana na kofia kama Serikali ilivyotangaza kwenye vyombo vya habari.
Tukio hilo lilitokea juzi ambako karibu makarani wote wa Sensa kwenye tarafa hiyo hawakupata sare licha ya kuwa na vitambulisho jambo ambalo baadhi ya wenye kaya walikataa kuwakubali.

Serikali kupitia vyombo vya habari, ilishatangaza kwamba makarani wa Sensa watafika kwenye nyumba wakiwa wamevalia fulana na kofia zilizoandikwa Sensa, mifuko myeusi, lakini makarani wa Turiani hawakutekelezewa hayo.
“Nilifanya kazi ya ziada kumwomba mwenyekiti wa kitongoji ili anisaidie kuwaelimisha kwani walikuwa wanakataa,” alisema karani mmoja wa Kitongoji cha Kigugu.

Alisema changamoto nyingine ni kuchelewa kwa baadhi ya vifaa vya Sensa pamoja na kutumia ramani ya mwaka 2004 ambayo imepitwa na wakati kwani baadhi ya watu waliotajwa kuwamo walishafariki au walishahama.

Habari hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Pamela Chilongola, Aisha Ngoma, Kelvin Matandiko, Zaina Malongo, Zacharia Osanga, Aziza Masoud, Geofrey Nyang’oro, Dar; Josephine Sanga - Moshi, Mustapha Kapalata - Igunga, Hussein Nyari - Hai, Mussa Juma - Arusha, Mustapha Kapalata - Igunga, Peter Saramba, Arusha, Lauden Mwambona, Turiani. 

source: mwananchi

Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani,"Viongozi wa Dini chanzo cha migogoro"


Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuacha kuwa chanzo cha migogoro makanisani na badala yake kurudi zaidi kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza kusudi walilopewa katika utumishi wao.
Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa miaka hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) zilizofanyika katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya Muhimbili wakati alipohudhulia kama mgeni rasmi wa tukio hilo.
Alisema tatizo kubwa lilipo makanisani kwa hivi sasa linasababishwa na viongozi wenyewe ambao badala ya kumtumikia Mungu wamegeuka na kuangalia vyeo hivyo basi ni vyema kurudi kwa Bwana ili waweze kumtumikia.
“Migogoro mingi iliyopo makanisani hivi sasa matatizo makubwa yako kwenye uongozi wala sio wanaoongozwa cha muhimu tu ni kwamba viongozi warudi zaidi kwa Bwana wanayemtumikia” alisema Jaji Augustino Ramadhani.
 Sherehe hizo zilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Jaji Angera Kileo, Askofu Philemon Tibanenason, Mweka Hazina wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Donata Mugassa pamoja na viongozi wa shirika hilo, Mwenyekiti Dk. Edda Mwandi aliyekuwa mwenyeji wa sherehe hizo pamoja na Katibu Rev. Emaus Bandikile.

Scripture union kuzindua Jubilee ya miaka 50 kwa kishindo

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Scripture Union Tanzania, Bw.Chuwa (Katikati) akiwa  pamoja na baadhi ya watendakazi wa wakati huo

Jaji wa Mahakama ya Rufaa Engera Kileo akiongoza maombi ya shukurani kwa ajili ya uzinduzi wa kutimiza miaka 50 ya Scripture Union Tanzania

Jaji Mkuu Agustino Ramadhani ambaye alitoa Neno la shukurani kwa kuwa hata yeye ni mmoja wa washiriki wa umoja wa kujisomea Biblia,  (kulia) ni Askofu Philemon Tibanenason ambaye ndiye aliyehubiri kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Scripture Union Dk. Edda Wandwi (kushoto), Jaji Mkuu Agustino Ramadhani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Askofu Philemon Tibanenason pamoja na Katibu Emaus Bndikile wa Scripture Union.


Uzinduzi huo ulikuwa wa tofauti sana kutokana na watu mashuhuli na wenye majina makubwa Tanzania kuhudhulia miaka 50 ya Umoja wa kujisomea Biblia (UKB)

Studio ya Kisasa ya NIKO AMBAYE NIKO yazinduliwa Dar.

Studio ya Kisasa ya NIKO AMBAYE NIKO yazinduliwa Dar,tukio hilo ni la Kihostoria maana halijawahi kutokea kuwepo na studio kubwa kiasi hicho katika kuzalisha mziki wa Injili kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki pia kazi za hapo ni nzuri zenye uwezo na  viwango vya juu zaidi,shughuli hiyo aliudhuliwa na Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini Dk. Lawrance Kametta akiwa pamoja na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake,Rogathe Swai pia walipata mda kujaribu vifaa vya Studio Niko Ambaye Niko,ambapo Mkurugenzi ni Steve Wambura.Ambapo waliiweka wakfu studio  huyo tayari kwa kazi,pia kumwombea Steve Wambura kwa kumbandika Mikono kwa kazi hiyo.
 
Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini Dk. Lawrance Kametta akiwa pamoja na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake, Rogathe Swai wakijaribu vifaa vya Studio Niko Ambaye Niko jana

Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiwa pamoja na Mgeni rasmi Dk. Lawrance Kameta na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake, Rogathe Swai wakati wa uzinduzi wa studio hiyo.

 t
Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiweka wakfu studio hiyo

Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiombewa na Watumishi wa Mungu, (kushoto), Mchungaji Timbothy Wambura

Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akitoa maelekezo kwa watumishi wa Mungu.

Pallangyo Brothers wampa shetani kipigo Uyole Kati

Waimbaji watatu kutoka Arusha, wanaounda kundi la Pallangyo Brothers, wenye kimo kifupi (Kibirikizi) kwa kushirikiana na Kanisa la flani Uyole Kati mjini Mbeya, wameleta mamia msalabani katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku sita.

Mkutano huo uliokuwa ukiendeshwa katika viwanja vya Kanisa hilo, huku Mhubiri akiwa Askofu Steven Mulenga toka Mombo mkoani Tanga, uliokusanya mamia ya wakazi wa mji huo, waliokuwa wakisumbuliwa na mapepo, huku wengine wakibubujikwa na machozi baada ya kutua mizigo yao msalabani.

Akihubiri katika mkutano huo, Askofu Mulenga, huku akisindikizwa na ujumbe uliokuwa na kichwa kisemacho; FILIPO ALIVYOMDHIBITI  SIMONI MCHAWI KWA JINA LA YESU, alisema, Yesu alidhihirishwa ili kuzivunja kazi zote za shetani.

Alibainisha kwamba, mwanadamu yoyote akimwamini Mungu ni wazi kuwa hakuna jambo lolote linaloweza kushindikana, huku akielezea kwamba, dhambi ndiyo inayomtenganisha mwanadamu na Muumba wake.

Mtumishi huyo aliweka wazi juu ya hilo alisema: “Hata leo Yesu yu hai na anaweza kumpa mtu mahitaji yake wakati wowote anapoitwa.”

Askofu Malenga, huku akiwa sambamba na Mchungaji mwenyeji wa Uyole Kati, Immanuel Mwalyenga alitanabaisha kwamba, hata yale ambayo watu wameyakatia tamaa, Bwana anaweza kuleta ukombozi na kumuaibisha shetani.
Katika mkutano huo, Pallangyo Brothers walikuwa na mguso wa pekee kwa jamii, huku watu wakijiuliza namna maumbo yao yalivyo, lakini wanaweza kumnyang’anya shetani mateka.
Huduma ya uimbaji katika mkutano huo, mbali na kuwepo kwa Pallangyo Brothers pia walikuwepo wengine kama akina Amani Mwasote, Kwaya kutoka makanisa mbalimbali na kwaya wenyeji Usiogope na Kedroni.
Ingawa mkutano huo ulifanyika wakati wa kipindi cha maonesho ya Kikanda ya Nanenane ambayo pia huvuta watu wengi, lakini Mungu hakuweza kuruhusu shetani afanye uharibifu kwa kuwakalia watu wa Mungu na hivyo kwa uwingi wao walikusanyika kwenye mkutano huo mkubwa.
 Katika mkutano huo watu zaidi ya 60 waliokolewa, wengine walifunguliwa katika vifungo vya magonjwa na maonezi ya pepo wabaya, huku wengine wakileta vitu vyao ambavyo walitumia kwa uganga vichomwe moto.
Moja ya vitu vilivyomuacha shetani taabani ni la mama mmoja kutoka kijiji cha Isyonje wilayani Rungwe ambaye baada ya kusikia tangazo la mkutano kupitia Redio Ushindi, alisafiri hadi Uyole kusikia Bwana anasema nini juu ya maisha yake na katika siku ya pili ya mkutano alifunguliwa kutokana na mapepo ambayo yalikuwa yamemtesa kwa muda mrefu.
Kama hilo halitoshi, mwisho wa mkutano Askofu Mulenga wakishirikiana na Mchungaji Kiongozi wa Uyole Kati Immanuel Lyego Mwalyenga, pamoja na jopo la wachungaji waliohudhuria mkutano huo, walifanya maombi ya kuliombea Taifa kwa kushika bendera ya Tanzania.
Waamini hao wapya, waliompokea Bwana Yesu katika mkutano huo; wanaendelea na mafundisho ya msingi yanayoongozwa na Mchungaji Bahati Mwandemba katika kuhakikisha wanaendelea katika imani na kufanyika baraka kwa Kanisa, Taifa na jamii kwa ujumla

RC, Paroko kutokomeza mauaji kanda ya ziwa

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo kwa kushirikiana na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Nansio, Padri Charles Masaga wameahidi kutokomeza mauaji ya kishirikina yanayofanywa na kikundi cha Makilikili na kusababisha hofu kwa wakazi wa Ukerewe.

Rai hiyo ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa  wa Mwanza  kuelezwa kwa nyakati tofauti na wakazi,  wilayani humo kuwa kundi hilo linajihusisha na mauaji ya watu na kisha kunyofoa viungo vya mwili hasa sehemu za siri.

Akiwa katika kijiji cha Bugorola Ndikilo alielezwa kuwa, hivi sasa wakazi wa Wilaya hiyo wanashindwa kutimiza majukumu yao vyema wakihofia kuuawa na kundi ambalo hata hivyo wahusika wake hawajulikani.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili wilayani Ukerewe kuhamasisha  sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agositi 26, 2012 aliahidi kuwa serikali ikitumia vyombo vyake vya dola itafanya kila linalowezekana kuhakikisha  vitendo hivyo vinakomeshwa.

Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikilalamikiwa na watu wengi na kwamba wanajipanga kuhakikisha wanalimaliza kabisa kwa sababu liko chini ya uwezo wao.

Naye Paroko wa Parokia ya Nansio, Padri Masaga akiongelea jambo hilo, huku akiahidi kuwa bega kwa bega na kamanda huyo; aliitaka serikali kutokaa kimya badala yake ikemee maovu hayo, ikiwa ni pamoja na vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini.

Mtumishi huyo wa Kanisa Katoliki ambaye aliendelea kubainisha kwamba anasikitishwa na tabia ya serikali kubaki  kimya bila kutoa tamko na hata kukemea mambo kama haya ya mauaji ya watu na kisha kunyofolewa viungo sehemu za siri na  kikundi cha Makilikili.

Hata  hivyo uchunguzi wa Polisi unaonyesha kuwa  hofu hiyo imesababishwa na uvumi ulioenea  takribani miezi miwili iliyopita, baada ya kuwepo vifo vya watu watatu ambao kati yao wanaume wawili wamepigwa hadi kufa kwa tuhuma za wizi; huku mwanamke mmoja akipoteza maisha katika harakati za kutoa mimba.

Wakati huo huo; watu watatu wamekufa maji wilayani Ukerewe, Mwanza baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba na kuzama katika ziwa Victoria.

Habari zilizopatikana  toka kisiwa kidogo cha Kweru na kuthibitishwa na Polisi zinasema kuwa katika mtumbwi huo wa kasia walikuwemo watu 15  na kati yao watatu walikufa  maji huku wengine 12 wakiokolewa na wavuvi waliokuwa karibu na eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mery Tesha alisema watu hao walikumbwa na mkasa huo wiki iliyopita majira ya saa 10.00 jioni, wakati wakitokea kijijini kwao Buzegwe kwenda kisiwani Kweru kuhani msiba wa ndugu yao.

Habari zaidi zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Leberatus  Barlow zimewataja waliokufa kuwa ni  Mgalla Yustinian (55), Pascazia Lyaganga (55) wakazi wa kijiji cha Buzegwe na Nyanjala Dotha (45) ambaye ni mkazi wa  kijiji cha Bukongo.

Diwani wa kata ya Kagunguri, Misana Ghatawa, akiongelea tukio hilo, alisema watu hao walipata mkasa huo muda mfupi baada ya kuondoka katika mwaloni wa Ilondo, miili yao tayari imepatikana na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

Baadhi ya wavuvi walioshuhudia tukio hilo walisema, mtumbwi huo ambao ulionekana kulemewa na mzigo, ulizama baada ya kupigwa na mawimbi makubwa ya ziwa Victoria na kuongeza kuwa, kama wangekuwa na vifaa vya uokozi pengine wote wasingepoteza maisha.

Jaji atoa hukumu mtoto abatizwe.


Jaji wa nchini Uingereza, John Platt ametoa hukumu ya mtoto wa miaka 10 abaki kuwa mkristo na ikiwezekana abatizwe kabisa, baada ya kuwepo kwa msuguano baina ya wazazi wake ambao mmoja alitaka awe mkristo.

Hukumu hiyo ilitolewa wiki iliyopita katika Mahakama ya Romford, baada ya wazazi wa mtoto huyo kusuguana tangu Novemba 2011 huku mama akipinga mtoto wake wa miaka 10 kubatizwa kwa maelezo ya kigezo cha umri huku akitaka tendo hilo lifanyike akiwa na umri wa mika 16.

Baada ya kutoelewana, mama ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alifungua kesi mahakamani ili iweze kuruhusu mwanaye kutobatizwa kwa kigezo cha kutojua baya na zuri, huku baba naye akidai ni muda muafaka na hakuna ulazima wowote wa kusubiri miaka 16.

Malalamiko mengine aliyokuwa akidai mama huyo ni umri wa mwanaye huyo kuwa ni mdogo kiasi cha kubadilisha imani. Jambo lililopokelewa na baba kwamba anaweza kueleza kulingana na sheria za Mungu na kwamba hata nyakati za Biblia Mungu aliweza kumtumia Daudi aliyekuwa mdogo.

Hata hivyo mwisho wa siku mahakama hiyo haikukubaliana na mama huyo na kumuamuru kuwaachia watoto wawe wakristo na wabatizwe na kwa sasa wanapewa mafundisho yanayoelezea nini maana ya kubatizwa na watakapomaliza watakuwa huru kubatizwa.

Wazazi hao walifikia mafarakano hayo baada ya kugombana na hivyo kuamua kutengana na hapo baba aliamua kubadili dini na kuwa mkristo.

Happybirthday Joyce Chalse,Mtangazaji wa Praise Power Radio asherekea siku ya kuzaliwa.

Mtangazaji wa Praise Power Radio afanya sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa namna ya pekee,sherehe hiyo ilikuwa na kusifu na kuabudu tofauti na nyingine zinavyokuwa.
Mtangazaji huyo ambaye ni Joyce Chalse aliyejumuika na ndugu wa karibu,marafiki na wazazi katika kufanikisha siku hiyo,watangazaji mbalimbali wa Redio na Bloggers mbalimbali walikuwepo kumpa kampani Mtangazaji huyo na kufanikisha shughuli nzima!



Joyce Chalse akitoa Neno la Shukrani kwa wegeni waliofika.
Joyce Chalse akiwa na mumewe


Joyce Chalse akiwa na mume wake na mtoto wake wa kwanza kati ya wawili

President Chavalla katikati Mc Pilipili kwa pembeni mtangazaji wa Praise Power wakifungua
Shampaign

Vijana wa Apostle Ndegi baada ya kupiga kazi Living Waters ndio waliongoza sifa siku hiyo.

Mc Pilipili akiwa kazini kama kawaida yake

The Blogger Uncle Jimmy-unclejimmytemu.blogspot.com
The Blogger  Papa Sam Sasali bila kukosa -samsasali.blogspot.com

Living Waters wakiwa kwa stage wakifanya mambo yao.


Lisa na mwenzie  wakiwakilisha Praise Power Radio



Living Waters kutoka Makuti Kawe wakihudumu siku hiyo.