Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani awa mchungaji Anglikana.



Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani
 Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati  Mzee Abeid Amani Karume.

“Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi,” alisema.

Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.

Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo. 

Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.

Source:Mwanachi

Masanja,Bukuku,Mbasha Kutinga Tamasha la Kufunga Mwaka EAGT City Centre


Mwaka 2013 untaraajia kuupisha kiti mwaka mpya wa 2014 kwa kishindo cha tamasha maalumu lilpewa jina la anza mwaka na Bwana, litakalopambwa na waimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini.

Kwa mujibu wa mchungaji Floriani Kantuzi wa kanisa la Evangestic Assembleis of God (EAGT – CITY) waimbaji watakaopamba tamashahilo ni pamoja na Emanueli Mgaya (a.k.a Masanja mkandamizaji), Bahati bukuku Florah Mbasha, Bon Mwaitege, Christian Matai, Neema Mwaipopo na jane Misso wengine ni Jenifer Mgendi, Kabula George, Martha Mwaipaja na Neema Gaspar na wengineo. Kwaya zinazotajwa kushiriki ni pamoja na Chang’ombe, Bethel na Majestic.

Mchungaji Floriani Kantuzi wa Kanisa la Evangestic Assembleis of God(EAGTCITY CENTRE)

Mchungaji Katunzi aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kwamba tamasha hilo limekusudiwa kuwapa watu fursa ya kumshuru mungu kwa ulinzi wa mwaka unaomalizika na kuwapa kibali cha kuuona mwaka mpya.

Kwa mujibu wa Mchumgaji Kantunzi kiingilio katika tamasha hilo pia kitahesabiwa kuwa mchango maalumu wa ujenzi wa jingo la kuabudia kwa ajili ya kanisa la EAGT- CITY CENTRE, Hivyo watakuwa wamepiga ndege  wawili kwa jiwe moja, ibada ya shukrani ya utoaji.

Viingilo katika tamasha hilo vinaanzia  na kiwango cha shilingi 5,000/= kwa watoto na wakubwa shilingi 10,000/=, viti maalumu shilingi 20,000/= na VIP 50,000/=. Kanisa la

EAGT- CITY CENTRE, lilianzishwa mwaka 2007 katika jiji la Dar es salaam, na tangu wakati huo limekuwa likisali katika kumbi mbalimbali ikiwemo viwanja vya Nyerere  (SABASABA) vilivyoko katika barabara ya kilwa ambako kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Mchungaji Katunzi alisema tayari kanisa lake limefanikiwa kupata uwanja wenye ukubwa wa eka saba na nusu kwa ajili ya ujenzi wa jingo la kuabudia na kwamba malipo yote pamoja na maandalizi mbali mbali vimegharimu karibu shilingi milioni thelathini.

 Watakao viingilio na kuhudhuria tamasha hilo la kufunga mwaka watakuwa wameanzisha safari ya ujenzi wa jingo lilokusudiwa kuingia watu wapatao 20,000/=.

Bahati Bukuku

Emanueli Mgaya (a.k.a Masanja mkandamizaji)



Pray for Darlene Zschech

Please join the world to pray for Darlene Zschech as we are standing and believing for complete healing. She recently discovered that she has / had breast cancer. For updates you can visit her blog site and www.darlenezschech.com/blog/


Hey lovely people,

I am overwhelmed today by your love and phone calls, gifts and especially your prayers. From the bottom of my heart I Thank You. I am resting in God’s love for me and the finished work of the cross.

One of the great worship leaders of Hope UC, Amanda Batterham, sent me a song she has written as a gift to my soul today. I laid on my bed, worshiped, wept, and felt to share this (with her permission) with any of you going through a tough time.

Click on the link to listen ….  Amanda Batterham – Saviour Of The World
God is with us. The great Emmanuel.. Xx take heart.
Love you,
Darls


New Year Overnight Event at Dar es salaam Pentecostal Church



NEW YEAR OVERNIGHT at DAR ES SALAAM PENTECOSTAL CHURCH

Waziri Mkuu Mh. Pinda ahudhulia Jubilee ya Kanisa la Katoliki Jijini Arusha

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki baada ya Ibada ya Jubilei ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha  iliyofanyika mjini Arusha jana Desemba 30,2013.
 (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

                    Katika Jubilei hiyo ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha viongozi mbalimbali walikuwepo kuhudhilia akiwemo Waziri Mkuu Msaafu Edward Lowasa

Padri atahadharisha ndoa za jinsia moja, uzazi wa mpango

Imeelezwa kuwa kuna hatari ya familia kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kufikia ukomo wa ustawi na furaha na pamoja na kujenga taifa lisilo na uhai wa nguvu kazi na lenye maadili kutokana na ndoa za jinsia moja zinazoshika kasi katika mataifa ya Ulaya na Amerika.
 
Padri wa Kanisa Katoliki nchini amesema kuwapo kwa mazingira hayo matokeo yake ni watu kukoma kuzaa watoto na kukosa familia.
 
Padri Angelus Shikombe alisema hayo wakati wa ibada maalumu ya siku ya Sherehe ya Familia iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Bikira Maria la mjini Geita.
 
“Hali hiyo ikichangiwa na kivuli cha utandawazi, ndoa moja ni suala ambalo hatukubaliani nalo..kwani linachimbia kaburi ustawi wa familia siku zijazo nchi itakosa vijana',” alidai Padri Shikombe.
 
Padri Shikombe ambaye pia ni Katibu wa Askofu wa Jimbo la Geita mahubiri yake ambayo yalionekana kuwagusa mamia ya waumini, yalisababisha vicheko na wengine kuguna.
 
Alisema maadili ya Kanisa ni kwamba hakuna ukomo wa kuzaa, ingawa mataifa makubwa yamebuni mpango wa uzazi wa kisasa ambao unaweka ukomo ambao hata hivyo, alisema utasababisha athari kwa mataifa yamayoendelea.
 
“Ndugu zangu, mataifa makubwa sasa yanatushinikiza kuwepo na ndoa ya jinsia moja na ukomo wa kuzaa mtoto mmoja ni mbinu ya kutuangamiza baada ya mataifa hayo kujikuta hayana vijana wala nguvu kazi ya vijana, yamebakiwa na wazee na sasa yanataka nasi tuwe hivyo,” 'alisema Shikombe.

CHANZO: NIPASHE

KKKT yazindua mtambo kuzalisha nishati mbadala

Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), limeanza kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuzindua mtambo wa kuzalisha nishati mbadala ya kinyesi cha wanyama wilayani Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza baada ya kuzindua mtambo huo, Askofu wa dayosisi ya Mara, Maiko Adam, alisema mtambo huo, utawasaidia wananchi kuyatunza mazingira kwaajili ya kuepuka uharibifu unaoendelea katika sehemu nyingi hususani katika hifadhi ya wanyama pori nchini.

Askofu Adam alisema Serengeti imepewa kipaumbele kwaajili ya kutunza hifadhi ya wanyama na mazingira ili kuleta ustawi wa vivutio vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo.

Alisema kufanya hivyo ni moja ya kuzuia uharibifu wa mazingira unaoendelea katika sehemu mbalimbali  nchini, ambao unaweza kuleta athari kubwa ya kutokea kwa ukame na kupoteza rasilimali zilizopo kama wanyama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Serengeti, Guddy Pamba, alisema kuzinduliwa kwa mradi huo kutasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanaleta uharibifu wa mazingira na kusababisha ukame.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kutunza mradi huo ili kuhifadhi mazingira.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Kanisa lililopigwa bomu Arusha lazinduliwa chini ya ulinzi mkali

Balozi wa Papa, Askofu  Padilla, akikata utepe wa kuzindua Kanisa la Mtakatifu Joseph Arusha jana.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Hatimaye  Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti, jijini Arusha, lililopigwa bomu Mei 5, mwaka huu na kuahirishwa uzinduzi wake, limezinduliwa jana na Balozi wa Papa na Mwakilishi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Fransisco Padilla.

Kabla ya uzinduzi huo, ibada hiyo ilianza kwa kubariki makaburi matatu ya Regina Laizer (50), James Kessy (16) na Patricia Assey (10), ambao wote waliuawa katika tukio hilo.

Uzinduzi huo ulikuwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi waliokuwa wametanda kuzunguka kanisa na wengine wakiwa juu ya paa.

Akizungumza wakati wa mahubiri Askofu Padilla alisema mara baada ya tukio hilo alikwenda kwa Papa, ambaye alimwamuru arudi Tanzania kuwapa pole waumini wote waliofikwa na tukio hilo.

“Sasa nawapa pole sana na amenituma nije kupatakasa mahali hapa, pawe patakatifu kwa ajili ya utoaji wa huduma za kimungu,” alisema.

Aliwaasa waumini kuwa na umoja na mshikamano katika kujenga kanisa, ili kuwe na matunda mazuri kwa kanisa.

“Nasema hivi sababu nitafurahi kuja kuona watoto wenu wametoka hapa kuwa watawa, masisita na mapadre,  wa kiongoza ibada hapa, nitafurahi sana,” alisema.

Alisema kuwa kanisa hilo baada ya kuzinduliwa litumike kuwa msingi wa kusaidia wasio na uwezo na siyo kulitumia jengo hilo kwa njia isiyofaa wala kuleta matunda kwa kanisa.

Alisema wanapopata majaribu ya shetani, wasikate tamaa, kwani hawana budi kuimarisha imani zao, kwa kuwa shetani hana mamlaka ya kuangusha nguvu za Mungu.

Alitaka kanisa hilo litumike katika kuibua vipaji vya miito na kuwahubiria wengine juu ya wokovu ili nao waokoke.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, aliyekuwa mwenyeji wa Balozi huyo, alisema kuwa ni vema waumini wakajua kuwa mipango ya Mungu, haiwezi kuangamizwa na shetani, hivyo walishindwa kuzindua kwa wakati ule uliopangwa kwa sababu ya vikwazo vya shetani na sasa wamemshinda shetani na wamezindua kanisa hilo.

“Mjuwe wazi mpango wa Mungu hauwezi kuangamizwa na mtu yeyote na ndio sababu leo tupo hapa tukiweka wakfu katika kanisa letu na kubariki makaburi ya waumini wetu waliofia imani yao ya katoliki,” alisema.

Alisema hata katika Biblia inasema wakati ule Mfalme Herode alipanga angamiza watoto wote wa kiume ili amwangamize Yesu, lakini alishindwa na ndivyo hata leo shetani atajiinua na atashindwa.

Askodu Lebulu alisema waliofariki kwa kupigwa na bomu kanisani hapo, walifariki, lakini waliobaki wamepata uponyaji na nguvu ya maombi zaidi ya hapo mwanzo kabla ya tukio hilo.

Askofu Lebulu aliongozana na Askofu wa Jimbo la Mahenge, Agapite Ndorobo na Askofu Padilla, kwenda kwenye makaburi yaliopo mbele ya kanisa hilo na kuyanyunyuzia maji kama njia ya kuyabariki.

Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Jubilei ya Jimbo la Arusha, ambayo kilele chake, kinatarajia kufanyika leo katika kanisa la mtakatifu  Theresia wa Mtoto Yesu na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, pamoja na Maaskofu na Mapadre mbalimbali toka ndani na nje nchi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Viongozi wa serikali waombewa msamaha kwa Mungu

Waumini wa huduma ya Mtakatifu Prince Mission yenye Makao Makuu yake Sinza jijini Dar es Salaam, wameomba msamaha kwa Mungu kwa baadhi ya viongozi  wa umma kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuusaliti umma wanaoungoza.
 
Hatua hiyo inatokana na matumizi ya misahafu wanapokula viapo vya kuutumikia umma, kisha kutotimiza azma hiyo badala yake kujinufaisha binafsi na ‘kuwaangamiza’ raia wanaowachagua.
Kiongozi huyo wa kiroho, Nabii Cres1, aliwaambia waumini hao  wanaojulikana  kwa jina  la Wateule katika  ibada iliyofanyika mapema wiki jana kuwa, watu wengi  wamekuwa wakiapa bila  kujua  madhara yanatokana  na viapo hivyo.
 
“ Viapo vingine vinasababisha  mahangaiko  makubwa, na hii inatokana kukosa uaminifu binafsi, wapo wanaohangaika  kwa ajili ya hilo, tumuombe Mungu atuondolee adhabu hiyo,” alisema akiwalenga viongozi hao.
 
Kiongozi wa kiroho, Nabii Cres1
Alisema, baadhi  ya  viongozi  wa serikali duniani, wanaapa katika  maeneo mbalimbali kwa  kutumia vitabu vitakatifu ambavyo ni neno la Mungu, kuwa watenda kwa mujibu wa haki sawa na maslahi kwa watu wote, lakini wanapomaliza inakuwa kinyume chake.
 
“Baadhi yao  wanaapa  kuwa watalinda  mali za wananchi, watatenda haki, lakini badala  yake wanatenda tofauti na wengine wakijitajirisha wao na familia zao, jambo ambalo ni dhambi mbele za Mungu,”alisema.
 
Nabii Cres1, alisema miongoni mwa matendo yaliyo kinyume na viapo hivyo, ni kwa baadhi ya viongozi kuishi maisha ya kuhangaika moyoni na kukosa amani, kuondokewa na mvuto wa kupendwa na wananchi,  pamoja  na kuwa ana mali nyingi.
 
“Wengi unakuta wanaapa huku wakijua hawataweza kutenda kama  walivyoaapa. Inatakiwa kuwaombea msamaha kwa Mungu kwani viapo  visivyo vya dhati huleta madhara kwa jamii mzima,” alisema.
 
Aliongeza, “inakuwa laana kwa taifa, kama  tunapenda dunia ipone, lazima tuombee viongozi wote walioko madarakani, kuanzia ngazi ya juu hadi familia ili Mungu awawezeshe watende mema na kuzingatia viapo vyao kwa ustawi  wa taifa letu na jamii kwa ujumla.”

CHANZO: NIPASHE

Usiku wa Crowning 2013 ndani ya Word Alive Center,Matukio katika Picha.



Watumishi wa Mungu mbalimbali walikuwepo akiwemo Pastor Carlos  Kirimba


           Watumishi wa Mungu mbalimbali walikuwepo akiwemo Pastor Carlos  Kirimbai na wengine


                                                           Angel Bernad akiwa na Doxas


                                     Doxas  Praise and Worship Team ya Word Alive Centre




                                              Doxas Praise and Worship Team ya Word Alive Centre

 
                                         Pastor Deo Lubala Mchungaji Kiongozi Word Alive Centre





                                                        Jesica wa Magupa akiwa na Doxas

                                      Pastor Carlos  Kirimbai akiombea wenye mahitaji usiku huo

                                                Rivers of Life na Pastor Safari kutoka DPC



Ephraem Kahuluda 'la Masias'

                                         Gospel comedian MC Pilipili akifanya vitu vyake.

                          Living Waters kutoka kawe walikuwepo kuhudumu katika usiku huo.

                                                   Henry akiwa na Living Waters



Picha gospelkitaa.co.tz

Maaskofu watema moto Katiba, Tokomeza ujangili

Siku ya Juzi Wakristo nchini waliungana na wenzao duniani kuadhimisha sikuu ya Krismasi kama kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo takribani miaka 2,000 iliyopita huku maaskofu wakitoa maubiri mbalimbali ukiwamo mchakato wa Katiba Mpya.

Katika mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki  Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, aliwataka Watanzania kuiombea rasimu ya pili ya Katiba Mpya ili  ipatikane katiba  inayokidhi mahitaji ya watanzania kwa maslahi ya nchi na ustawi wa jamii.

Aidha, alisema viongozi wanapopewa madaraka wametakiwa kuacha kujineemesha na kujilimbikizia mali na kushindwa kuwasaidia wale ambao wanatakiwa kuwahudumia na kuwaacha katika hali duni.

Alisema kipindi hiki cha maandalizi ya kupata katiba mpya wananchi wanapaswa kuiombea nchi ibaki katika umoja, mshikamano na amani kwa kuwa mwaka 2013 amani ya nchi ilitikisika katika mambo mbalimbali.

Askofu Nzigilwa alisema ikipatikana katiba inayokidhi mahitaji ya watanzania italeta ustawi wa nchi na jamii kwa ujumla na nchi itabakia kuwa amani na utulivu.

Kuhusiana na viongozi wanapopata madaraka, alisema utakuta mtu akiwa duni kabisa, lakini anapopewa nafasi anajineemesha kwa kununua magari, kujenga majumba bila kuwasaidia watu wanaowatumikia.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikan la Mtakatifu Alban, jijini Dar es Salaam, Aidano Mbulinyingi, aliwataka Watanzania kuondoa woga juu ya mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya, ambayo alisema imebeba mawazo mbalimbali,yakiwamo potofu.

Mchakato huo wa katiba utafanikiwa kwa kuwa Kristo aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita aliwaasa Wakiristo kuwa wasiogope kwa jambo lolote litakalotokea mbele ya jamii.

Alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa na woga kuhusu mchakato wa katiba huku wengine wakitafuta mbinu mbalimbali ili zoezi hilo la kuandika katiba lishindikane.

“Tusiwe waoga kiasi hicho, bali tumtegemee Mungu na neno, usiogope katika Biblia limeandikwa mara 360, hii nikionyesha yote yaliyopo sasa tayari Mungu anayajua na kutuasa,” alisema.

Mchungaji Mbulinyingi alisema ni ajabu kuona wengine wakihofia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuanza kujitangaza kwa wananchi, na kusema kuwa hali  hiyo inapaswa kuombewa ili iwatoke  wenye roho hizo na kuwa raia wema.

MAPIGANO YA ARDHI
Selyvester Thadey wa kanisa la International Evangilism Sinai Ipagala mkoani Dodoma, alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa kusikia vurugu za mapigano zinazotokea za wakulima na wafugaji, hivyo kuwataka viongozi wa serikali waliokabidhiwa dhamana ya kiutendaji wanakomesha hali hiyo.

“Sisi kama kanisa tuna mashaka miongoni mwa viongozi wa serikali wananufaa pindi inapotokea vurugu kati ya wakulima na wafungaji kuwa, wanapata maslahi kwa ajili yao binafsi,” alisema.


ASKOFU PHAM APONGEZA MAWAZIRI KUJIUZULU
Askofu wa Kanisa la PHAM Kanda ya Kati Dodoma Julius Bundala, aliwapongeza mawaziri ambao wizara zao zimeshutumiwa kuhusika katika unyanyasaji wakati wa Operesheni ya Tokomeza Ujangili kwa kukubali kuachia madaraka yao.

Bundala akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika ya Krismas Kanisa la Makole mjini Dodoma.

Alisema hatua walizochukua mawaziri hao kujiuzulu ni ukomavu.
Hata hivyo, alisema watendaji wengine wanapaswa kufahamu kuwa hakuna kificho kutokana na mawaziri hao kuwekwa wazi na Kamati ya Ardhi, Maliasili, Ardhi na Mazingira kwenye kikao kilichomalizika hivi karibuni mjini Dodoma.

Hata hivyo Askofu huyo amemtaka Rais Kikwete kutoishia kwa Mawaziri hao bali anatakiwa kuchunguza baraza lake hilo ili kuwabaini ambao wanaotumia madaraka yao kinyume na sheria na utaratibu zilizopo ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

TAG yalaani TOKOMEZA UJANGILI
Mchungaji wa Kanisa la TAG Mlima wa Moto lililopo soko la Sabasaba mjini Dodoma, Silivanus Komba, alisema njia iliyowezesha kuweka wazi unyama waliofanyiwa wananchi na mawaziri ambao walioondolewa kwenye nyadhifa zao ni  baada ya kufanyika  kwa mahojiano mbalimbali na kamati.

Alisema hali hiyo inatokana na vilio vingi vya wananchi ambao walionyanyaswa wasiokuwa na hatia na kunyanganywa na mali na fedha zao kwa watendaji wasiokuwa na huruma.

Hata hivyo, alisema kuwa ni matumaini yake na kanisa kuwa serikali pia inasafisha safu yake kwa wale ambao bado wanaonyoshewa vidole kutokana na utendaji wao mbovu.

ASKOFU MKUDE APINGA UMEME KUPANDA
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphory Mkude, alieleza kushangazwa na serikali kwa kuruhusu bei ya umeme kupanda kwa asilimia 50 na kueleza kuwa hali hiyo itazidi kuongezea mwananchi mzigo na kuendelea na hali ya umasikini kwa kuwa watashindwa kumudu gharama hizo.

Badala yake Askofu Mkude alitaka serikali kutoruhusu kupanda kwa bei ya umeme kwani wananchi watashindwa kutumia huduma hiyo na kubaki kwa watu wachache ambao watakuwa na uwezo.

Katika mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Patrice, alisema inasikitisha kuona bei ya umeme inapandishwa kwa kiwango kikubwa na kuendelea kumuumiza mwananchi wa nchini ambaye kipato chake ni duni na kueleza hali hiyo itasababisha watanzania waendelee kudidimia na hali ya umaskini.

Alisema cha kusikitisha ni kwamba Tanzania ndiyo nchi inayotoza gharama kubwa za umeme ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.

“Watanzania wanakipato duni sana, leo hii wanapandishiwa bei ya umeme, mimi nadhani sasa watashindwa kuitumia huduma hiyo na kurudi katika matumizi ya vibatari ,” alisema na kuongeza:

“Katika hili serikali inapaswa kulitafakari kwa kina suala hili la kupandisha bei ya umeme.”

Alisema anadhani kwa nchi kama ya Tanzania ambayo inanza kupiga hatua ya kutafuta maendeleo kwa kasi, huduma hiyo ilipaswa kutolewa kwa gharama nafuu ili kila mtu amudu, lakini hali imekuwa tofauti kutokana na kupandishwa mara kwa mara huku umeme ukiendelea kuwa tatizo.

ASKOFU MALASUSA
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, amesema viongozi na wanasiasa waliopo madarakari kwa njia zisizo za halali wamekuwa wakihangaika kufanya jambo lolote liwezekanalo ili kuzilinda  nafasi zao, pindi unapotokea mtetereko katika nafasi walizopo jambo alilosema linasababisha uvunjifu wa amani.

 Aidha aliwafananisha viongozi hao na Mfalme Herode ambaye alikuwa mfalme wa Wayahudi na baada ya kusikia kuwa Yesu Kristo amezaliwa ambaye atakuwa mfalme wao, alitetereka na kuanza kutafuta mbinu za kumuangamiza.

 Akihubiri katika Kanisa hilo Kuu la Azania Front, jijini Dar es Salaam, Dk. Malasusa, alisema ni vema jamii ikasherehekea Krismasi kwa kuyafanya yale mema ambayoYesu aliyatenda ili kudumisha amani na ushirikiano duniani kote.

Aliwataka watanzania na dunia nzima kusherehekea sikukuu hiyo kwa kuishi maisha ya amani ambayo yataendelea kutuunganisha dunia nzima ili kuepukana na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyotokea duniani.

“Rasilimali nyingi duniani  hutumika kutengeneza na kutafuta amani kwa mambo ambayo hayampendezi Mungu badala ya kuelimisha watu ili  kuzilinda imani zao, mfano mzuri ni kwa watu ambao wamekuwa wakirekebisha maovu ya watu au viongozi, huonekana hawafai kwa kupigwa vita badala ya kuungwa mkono,” alisema Dk. Malasusa.

ASKOFU AICT: VIONGOZI NI WABINAFSI
Askofu wa Africa Inland Church (AICT)  Jimbo la Geita, Mussa Magwesela, alisema amani barani Afrika haitapatikana iwapo viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza wananchi hawataacha ubinafsi wa kung’ang’ania madaraka, kujilimbikizia mali, rushwa na matumizi mabaya ya raslimali za umma vinavyosababisha mataifa mengi duniani kumwaga damu.

Akizungumza katika Ibada ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika kitaifa katika kanisa hilo Kalangalala mjini Geita, alisema hali hiyo inatokana na viongozi kukosa hofu ya Mungu na kutaka kujinufaisha kwa maslahi binafsi.

Askofu Mwagwesa, alisema viongozi hao wameshindwa kufuata misingi iliyoachwa na watangulizi wao (waasisi wa mataifa hayo) Kwame Nkuruma, Mwalimu Julius Nyerere, Jomo Kenyatta na Nelson Mandela ambao walikuwa wanyenyekevu mfano wa Yesu Kristo alipojitoa na kukubali kufa msalabani ili kuwakomboa watu na dhambi za ulimwengu.

“Viongozi hawa waliimarisha misingi ya Utawala bora, lakini suala la uongozi katika Taifa letu na bara la Afrika kwa miaka 50 hadi 60 iliyopita tumejionea matukio mengi ya umwagaji wa damu kwa sababu ya baadhi yao kung’ang’ania madaraka,” alisema Askofu Magwesela.

Kadhalika, alisema sekta ya ardhi imekuwa kinara wa  rushwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha uvunjwaji wa sheria na hatimaye mauaji baada ya viongozi hao kutumia madaraka yao vibaya kama ilivyojitokeza kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina.

Alisema kugoma kwa madakatari na walimu nchini  kwa kisingizio cha ukosefu wa vitendea kazi sehemu za kazi na mishahara  midogo inatokana na kukosa wito wa kazi zao licha ya kuwa elimu hiyo wameipata kutokana na kodi za wananchi.

“Serikali iboreshe miundombinu ya maji,barabara na hospitali badala ya kuendelea kuwahadaa wananchi.

ASKOFU DALLU: RASILIMALI ZISITUGOMBANISHE
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Damian Dallu, aliwataka Watanzania kuepuka mafarakano na uvunjifu wa amani  kunakosababishwa na rasilimimali za nchi.

Aidha, aliwata kushirikiana katika kuondokana na mambo yanoyoleta uadui kati ya wenye madaraka, vyeo na waliyonacho na wasiyo chacho  kwani vinaweza kuligawa taifa katika matabaka.

Rai hiyo aliitoa jana mjini Geita katika ibada ya Krismasi iliyoadhimishwa kitaifa katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani mkoani Geita.

Alisema ni vyema Watanzania kusherehekea Krisimas kwa amani na upendo wa kweli kwa kusaidiana bila kujali tofauti zetu  katika njia halali ya kujikomboa  na umasikini na kujenga mshikamano.

“Ni vema mambo yanayoonekana kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani vikaepukwa mapema kwa kushirikiana kwamba aliye nacho aumie kwa ajili ya yule asiye nacho ili kuishi kwa amani na furaha, kiongozi bora ni yule anayeumia kwa ajili ya watu wake na huo ndiyo upendo unaoleta amani,” alisema Askofu Dallu.

Alisema, ni vema Watanzania wakatafuta amani na furaha ya kweli kwa kuomba, kusameheana yale yote yaliyopita pamoja na kushiriki sala, kuinua elimu na kufanya kazi kwa bidii.

Pia aliwataka wakazi wa mkoa mpya wa Geita kuhakikisha wanauendeleza mkoa huo kwa kusoma na kufanya kazi kwa bidii ili kujiinua kiuchumi hasa katika sekta ya elimu na afya ambazo bado ziko chini.

ASKOKU MKUU ANGLIKANA
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya, ameitaka serikali kuwa na mipango madhubuti ya kuwahudumia watu badala ya kupata dhiki katika nchi yao yenye utajiri mwingi.

Akitoa salamu zake za Krismasi katika Kanisa la Dayosisi ya Mpwapwa mkoani Dodoma, alisema ni lazima Watanzania wote wapate elimu.

”Kwa mfano ukizungumzia habari ya elimu mtanzania anahitaji kupata elimu ambayo itakuwa mkombozi katika maisha yake na serikali iwe na kipaumbele chetu kwa mfano kwenye elimu ya msingi na sekondari kuliko kwenye elimu ya chekechea,” alisema Askofu Chimeledya.

Alibainisha kuwa Watanzania wanahitaji kupata elimu ambayo itakuwa mkombozi katika maisha yao na kusema kuwa matarajio yake ni mtoto aingie elimu ya msingi anajua kusoma na kuandika hivyo aandaliwe chekechea akiwa na miaka mitatu hadi mitano.

“Pia Watanzania watapata matumaini kama serikali itashuka chini na kwenda kushughulikia watendaji mmoja mmoja na waziri anawajibika kama mimi ninavyowajibika kwa kanisa langu au dayosisi yangu kama kweli chini kuna watu wanafanya vibaya kwa hiyo kuwajibika kwangu hakutaleta faraja kama bado watendaji hao wapo,” alieleza.

Alisema kuwa inatia moyo mawaziri wanne wamewajibika kwa kujiuzulu na anawapongeza sana, lakini serikali irudi kufuatilia watendaji wote katika ngazi mbalimbali kamwe kuna mtu hataweza kutowatendea haki wananchi.

Askofu Shao: Tuwaombee Sudan Kusini
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Dk. Martin Shao, amesema ingawa Tanzania inatajwa kukomaa kisiasa katika ukanda wa Afrika, lakini iko haja kama taifa kuandaa funga maalumu kwa ajili ya kumwomba mwenyenzi Mungu aingilie kati na kukomesha mapigano yanayoendelea Sudan ya Kusini kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanaomuunga mkono hasimu wake, Riek Machar.

 Alisema machafuko ya kisiasa yanayoendelea kuangamiza wanadamu katika mataifa yenye utajiri mkubwa wa mafuta ikiwemo Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Misri ni mwangwi ambao Tanzania haipaswi kukaa kimya kama kinara wa ukombozi katika nchi za Afrika.

Dk. Shao alikuwa akihubiri katika ibada iliyofanyika katika Usharika wa Moshi mjini.

 “Asilimia 73 ya Wakristo duniani kote leo jana) wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo, lakini wakati tunashangilia na kufurahi kwa kula na kunywa, kila kona ya nchi,wenzetu wanaendelea kufa huko Sudan ya Kusini,Kongo na Misri kutokana na machafuko ya kisiasa na ulafi wa madaraka ambao tuna kila sababu ya kuomba yasiendelee kuua maelfu ya wanadamu wenzetu,” alisema Dk. Shao.

Kuhusu hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na mataifa kwa ajili ya kuepusha dhahama hiyo, askofu huyo alisema bila ya kujali ni dhehebu gani mtu anakoabudu, watanzania kwa ujumla wake wanapaswa kuweka pembeni itikadi zao na kuomba waafrika wenzetu waondoke katika mahangaiko na mateso yanayotokana na siasa hasi za kung’ang’ania madaraka.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Katoliki Sombetini, jijini Arusha, Padre Peter Shibale, alisema kuwa inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wa  Kikiristo wanaacha kufuata nyayo za Kristo na wanaanza kurubuniwa na baadhi ya wahubiri wanaotoa mahubiri yanayokwenda kinyume na ya Yesu Kristo.

Akihubiri kwenye Kigango cha Utatu Mtakatifu Kwamurombo, alisema wahubiri wanaopotosha wanadai wanatoa wokovu.

“Wokovu mwenye kuutoa ni bwana Yesu Kristo pekee na siyo mwingine, hivyo tusiyumbe na tusimame imara katika makanisa yetu,” alisema Padre Shibale.

Padri Leonard Mariva wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Consolata Parokia ya Mshindo mjini Iringa, aliwataka waumini kuendelea kuiombea dunia ili yasitokee  machafuko ya vita, matetemeko,utoaji wa mimba ovyo na mauji ya kupigania mali.

Alisema siku hizi machafuko kama hayo yametokea na watu wengi kupoteza maisha yao, hivyo tuna kila sababu za kumuomba machafuko kama haya yasitokee tena.

Imeandikwa na Jimmy Mfuru, Leonce Zimbandu, Mary Geofrey, Dar; Augusta Njoji na Peter Mkwavila, Dodoma; Ashton Balaigwa, Morogoro; Godgrey Mushi, Moshi; Cynthia Mwilolezi, Arusha;  George Tarimo Iringa na Daniel Limbe, Geita.

CHANZO: NIPASHE

Solly Mallangu Katika Tamasha la Krismasi 2013 Nchini Tanzania

2BMwimbaji wa muziki wa injili Solomon Mahlangu kutoka nchini Afrka Kusini akiimba jukwaani kwenye uwanja wa Taifa katika tamasha kubwa la Krismas lililofanyika jijini Dar es salaam likishirikisha waimbaji wengi kutoka nchi mbalimbali za afrika wakiwemo waimbaji wa Tanzania.3BWaimbaji wa mwimbaji Solly Mahlangu wakiimba jukwaani 4BMashabiki wakicheza staili ya saluti na mwimbaji Solly Mahlangu5BHakuna aliyekuwa amekalia kiti chake wakati mwimbaji huyo akiwa jukwaani akifanya vitu vyake.6BHapa ilikuwa kila mmoja akinyanyua kitambaa chake juujuu ili mradi burudani tu.7B16Mgeni rasmi Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu Uratibu wa Sera na Bunge Mh. William Lukuvi akizungumza katika tamasha hilo na kuwashukuru waimbaji wa muziki wa injili kwa kuendelea kuhubiri amani nchini lakini pia akawahakikishia kwamba serikali kitahakikisha amani iliyopo inadumu, kulia ni mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na katikati ni Ezekiel Maige Mbunge wa jimbo la Msalala jijini Dar es salaam.14Mwimbaji Ephraim Sekereti akiwa na Living Waters akitumbuiza kwenye  uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la Krismas linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam 159Mwimbaji Rose Muhando akiimba na kucheza kwa hisia  mbele ya mashabiki wake1011Grolius Worship Team wakiimba jukwaani.12Mwimbaji Upendo Kirahiro1aaMwimbaji wa muziki wa injili Boni Mwaiteje 2aBoni Mwaiteje akionyesha uwezo wa kucheza na masteji shoo wake

Living Waters Kutoka makuti Kawe wakiwakilisha