Mkesha wa Kusifu na Kuabudu pia Maombi katika Chuo Cha Mzumbe Morogoro.

Katika kuelekea kumaliza muhula katika Chuo cha Mzumbe Morogoro huwa wanaandaa usiku wa Kumsifu na Kumtukuza na Mungu pia kupata nafasi ya kujifunza Neno la Mungu na Maombi kutoka kwa mtumishi anayealikuwa katika usiku huo.

Mkesha huo wa Kusifu na Kuabudu ,Chuoni Mzumbe Morogoro.Ulindaliwa na Umoja wana CASFETA chuoni hapo,Wanachuo walipata kuombewa na vijana wengi walipata kuokoka na kumpa Bwana Yesu Maisha yao.

Apostle Ndegi kutoka huduma ya Living Water Centre Ministry ndiye alihudumu katika upande wa Neno katika Usiku huo,Pia kwa Upande wa Waimbaji walikuwepo Upendo Nkone,Filipo Rupia na
CASFETA Mass Choir

Apostle Ndegi kutoka huduma ya Living Water Centre Ministry


Apostle Ndegi akiwaogoza sala ya toba baadhi ya wanafunzi waliosikia Neno la Mungu katika Usiku huo na kuamua Kuokoka na kumpa Bwana Yesu Maisha yao pia walipata kuombewa
Mwenyekiti CASFETA Chuo cha Morogoro akizungumza katika usiku huo

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mzumbe akizumgumza kuwa stage hiyo hiyo siku si nyingi aliitumia katika kuomba kula ila usiku huo ilikuwa ikitumika katika Kumtukuza Mungu.
Mwimbaji Philip Rupia akiwa na backup ya CASFETA Mass Choir kwa stage
Upendo Nkone

Mwingira ashauri wagombea wapimwe akili

Kiongozi  wa Kanisa la Efatha nchini, Mtume Josephat Mwingira ametaka kila anayegombea uongozi wa umma sharti apimwe akili.

Hayo aliyaeleza jana asubuhi wakati akihubiri katika ibada ya kwanza kwenye makao makuu ya Kanisa hilo, jijini Dar es Salaam.

”Hali ni mbaya, malalamiko ya wananchi dhidi ya wizi wa rasilimali za Taifa kwenda nje yamekuwa mengi,’’ alisema.
Alisema tabia ya mfumo wa uchumi nchini ya kuthamini wawekezaji kutoka nje ya nchi kuliko wa ndani  siyo nzuri na kwamba ni moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi wa taifa.


“Mimi nimewahi kuchimba madini ya Tanzanite, ikanipa kipato kizuri tu lakini nilinyang’anywa wakapewa wawekezaji wakubwa, siasa zisizoona tatizo hata kudhulumu wananchi wake ni siasa chafu,” alieleza Mtume na Nabii Mwingira.

Akifafanua juu ya hali ilivyo nchini, alitoa mfano wa familia yenye kumiliki ardhi kubwa lakini isiyoendelezwa akisema, “wanakuja watu kutoka nje kuomba wapatiwe ardhi hiyo ili waiendeleze kwa kilimo na ufugaji na baba wa familia husika ambaye anawaruhusu kwa kusema, ‘tumieni tu hamna taabu’.

Kiongozi huyo mwanzilishi wa Kanisa la Efatha alieleza kuwa wageni hao wanapohoji kuhusu malipo, wanaelezwa na baba wa familia husika kuwa hakuna tatizo waendelee na shughuli zao kwanza, baada ya miaka mitano ndipo wataamua walipe kitu gani.

Alisema wakati wakulima hao wakivuna mazao na kuuza na mengine kuhamishia kwenye nchi zao, wanafamilia inayomiliki mashamba hayo wanakabiliwa na uhaba wa chakula kiasi cha wengine kufa kwa kukosa chakula, hali inayosababisha baba wa familia husika kuchota fedha za familia, kwenda kwenye nchi za wale wanaolima mashamba yake kuomba misaada.

“Hii si sawa, kuna umuhimu kila mtu atakayetaka kuongoza umma wa Watanzania hata kama ni ngazi ya mbunge, akapimwe akili yake kwanza ili kujiridhisha na uwezo wao wa utendaji kiakili,” alieleza Mwingira.

Mwanamuziki wa Injili wa Tanzania anayeishi Nchini Sweden Rachel Sharp azindua Album yake ya kwanza siku ya jana.

Siku ya jana Mwanamuzi Injili wa Tanzania anayeishi Nchini Sweden, Rachel Sharp ameitambulisha albam yake mbele ya Wanahabari wa Kikristo. Utambulisho huo wa Albam umefanyika Nyumbani Kwake Tegeta nje kidogo ya jiji la Dar-es-Salaam.

Mwanamuziki huyo alisema albam hiyo yenye jina la "Ni Mungu Wa Ajabu" ina jumla ya nyimbo kumi zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.

Rachel anayeishi Malmo Sweden amewataka Wanamuziki Wa Tanzania Kutukuza asili yao na kuacha kuiga tamaduni za South Africa na Africa Magharibi na hata barani Ulaya. Akiongea na Waandishi Wa Habari siku ya leo Rachel alisema " Ipo haya ya watanzania Kuimba nyimbo zenye mahadhi ya Mdumange na Mdundiko ili kulinda radha halisi ya Kitanzania na Kuutangaza Muziki Wa Asili ya Kitanzania nje ya Mipaka Ya Tanzania".

Rachel Sharp kwa stage na dancers wake

Master Prophet C.J. Machibya akiiyombea kazi ya dvd na Audio
Rachel akiwatambulisha Baba mzazi na Mama mzazi

Upendo Kilahiro,Chavala,Uncle Jimmy na Rachel wakifanya performance siku ya jana.
Rache Sharp akisoma Press Release
Wakinadada wadau wa Muziki wa Injili na media wakiwa kazini kuhakikisha mambo event  hiyo inakwenda sawa

Wadau wa media wakiwa kazini kuhakikisha mambo yanekwenda sawa.

source:samsasali.blogspot.com

Achive Your Dreams


Moravian Kusini watoa tamko zito juu ya Mchungaji Fumbo

Halmashauri Kuu ya Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini na bodi ya wadhamini wa mali za kanisa hilo, wametoa tamko zito la kumtaka Mwenyekiti wa Jimbo la Misheni Mashariki aliyesimamishwa, Mchungaji  Clement Fumbo kurudisha mali za kanisa na kuacha kujihusisha na shughuli za kanisa hilo.

Tamko hilo limekuja kufuatia Mchungaji Fumbo kujihalalisha siku za hivi karibuni kwamba yeye ni Mwenyekiti halali wa Jimbo la Misheni, ikiwa ni pamoja na kutangaza viongozi wapya wa halmashauri kuu jambo lililolenga kuwagawa waumini ndani ya kanisa hilo.

Nembo ya kanisa la Moravian

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jimbo la Kusini, Clement Mwaitebele alisema alichokifanya Mchungaji  Fumbo ni ubatili mkubwa na kwamba ni kitendo kinachohatarisha amani ya Watanzania, hivyo kama viongozi wakuu wa kanisa wameamua kuingilia kati.

Alisema barua za kumtaka afanye hivyo tayari zimeshaandaliwa na kwamba akikaidi kurudisha ofisi, kuondoka katika Jengo la Usharika wa Tabata na kurudisha mali nyingine za kanisa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia kesi mahakamani.

Sambamba na hilo, alisema wanatarajia kuwa na kikao leo na wachungaji wote wa eneo la Misheni, lengo likiwa ni kukubaliana nao jinsi ya kufanya kazi, atakayekiuka misingi iliyowekwa atatakiwa kuondoka  katika majengo ya kanisa na kurudisha fedha alizosomeshewa na kanisa na akikaidi atawajibishwa kisheria.
Alisema awali mkutano mkuu wa kanisa Jimbo la Misheni ulioketi  Oktoba 5-6 mwaka jana, ulitoa uamuzi wa kuondolewa madaraka kwa Mchungaji Fumbo na kuachishwa uchungaji, ambapo Oktoba 10 mwaka jana aliandikiwa barua ya kumtaarifu maazimio hayo.
Alisema kufuatia mkanganyiko huo, Umoja wa Kanisa Duniani (Unity Board), walitembelea Jimbo la Misheni lengo likiwa kujionea kama wapo tayari kupewa cheti cha kuwa jimbo kamili, lakini walikuta malumbano na kushauri kupatikana kwa suluhu kwa lengo la kuimarisha umoja katika kanisa .
Alisema jimbo la Kusini ni jimbo linaloongoza maeneo ya Tukuyu, Kyela, Ileje, Zanzibar, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi, hivyo  wameamua kuingilia kati suala hilo kwani kwa sasa linaelekea kuvuruga amani.
Alisema katika kujitanua zaidi na kuwa karibu na Wakristo, waliazimia kulitenga eneo la Mashariki yaani Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Zanzibar na Morogoro ili lianze kutafuta uhalali wa kuwa jimbo kamili, kwani kwa sasa bado halina cheti cha utambulisho wa kuwa jimbo kamili na ndiyo maana linaitwa Jimbo la Misheni Mashariki.

Alisema kanuni na katiba ya kanisa hilo kifungu cha 2 kinaeleza wazi kuwa jimbo la Misheni litachagua halmashauri kuu ya kuliongoza, lakini litawajibika kwa jimbo mama ambalo ndilo jimbo la Kusini hadi litakapokuwa jimbo kamili.

Mchungaji Mwaitebele alisema vurugu za uongozi na madaraka zilipoanza kutikisa, waliamua kuingilia kati kama wasimamizi halali wa eneo hili la Misheni,ambapo waliweza kukaa vikao vingi bila kupata suluhu kwani mara nyingi Mchungaji Fumbo alipoitwa alikaidi.

Alisema kwa kuzingatia katiba ya kanisa kifungu namba 11 kipengele cha C kinachoeleza wazi kuwa mkutano mkuu wa kanisa (Sinodi), waweza kuitishwa wakati wowote na halmshauri kuu ya jimbo kujadili jambo la dharura, lakini itatoa taarifa kwa wajumbe wake kwa muda wa miezi miwili.

Alisema Sinodi imepewa mamlaka kikatiba kifungu cha 10 kipengele cha M na N kutoa maamuzi ye mwisho ya kila Mkristo au kila chombo chochote kilicho chini yake, hivyo alisema mambo yote yaliyokuwa yakitekelezwa na viongozi yalikuwa sahihi kikatiba.

Aliongeza kuwa kifungu cha katiba namba 99 kipengele cha  A - B kinafafanua kuwa makamu mwenyekiti atasimamia shughuli zote za kanisa atakazopangiwa na mwenyekiti, pia atafanya shughuli za mwenyekiti kama akiwa amesafiri ndani ama nje ya nchi.

Hivyo alisema maamuzi yote ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa sinodi ya dharura hayapo nje ya katiba kama inavyopotoshwa na baadhi watu.

Ametoa wito kwa waumini wa kanisa kuwa watulivu kipindi hiki, huku wakimuomba Mungu anayeweza kutuliza dhoruba aweze kusimamia suluhu ndani ya kanisa hilo.

Mchungaji KKKT atoa ushahidi vurugu za Mbagala

Mchungaji Frank Kimambo (32) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Mbagala Zakhem, juzi ameiambia Mahakama ya Kisutu kuwa yeye hausiki na masuala ya kudai mali zilizoharibiwa labda aulizwe mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Dayosisi.

Mchungaji Kimambo alisema hayo jana alipokuwa akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Walialuwande Lema akiwa shahidi wa pili baada ya mlinzi wa kanisa hilo hilo kutoka kampuni ya Pray and Vicent,  Michael Woga (30), kutoa ushahidi wake.

Kimambo alisema yeye ni msimamizi wa kanisa la KKKT Mbagala akiwa anamwakilisha Askofu hivyo jambo la kulipwa mali halimhusu yeye na alieleza hilo baada ya Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka kumuuliza je, watadai malipo ya hasara zilizotokana na uharibifu wa kanisa?

Aliendelea kujibu swali la Kweka kuwa yeye anahusika katika tathmini iliyotolewa ya uharibifu, ambayo alisema pamoja na uongozi wa kanisa hilo walitoa tathmini ya vitu vilivyoharibiwa pia zipo picha za ushahidi.

Alisema hajawahi kusema uharibifu huo ulisababishwa na Waislamu au Wakristo bali anajua uharibifu ulifanywa na kikundi cha watu na kwamba mengine labda yalisemwa na waandishi wa habari.

Aidha aliiambia Mahakama kabla ya uharibifu wa mali hizo yeye alikuwa ofisini kwake akapigiwa simu na muumini wake kwamba kuna watu wanaofanya uhalifu na huenda wakaelekea hapo kanisani ndipo alipofunga mlango wa ofisi ili kwenda kutoa taarifa ila kabla hajafika watu walishafika na kuanza kurusha mawe.

Alisema baada ya kuona polisi wameelekea kanisani aliwafuata nyuma na alivyofika akawekwa chini ya ulinzi hadi alivyotoa kitambulisho ndipo aliposimama  na kuruhusiwa kuangalia kanisa ambalo lilikuwa kwenye hali mbaya.

Wakili Kweka alimuuliza shahidi kama anajua mlalamikaji ni nani katika kesi hiyo na alikiri kuwa hajui ila polisi ndiyo waliyokuja kuchukua maelezo na yeye ametoa ushahidi wa yale aliyoyaona.

Naye Shahidi wa pili Mlinzi Woga aliiambia Mahakama kuwa baada ya kushindwa kupiga risasi alikimbia kwani kulikuwa na watu wengi waliokuwa na mawe ila alirudi baada ya polisi kuja akakuta hali ni mbaya huku ukuta ukiwa umevunjwa.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 2, mwaka huu itakapoendelea na ushahidi.
Katika kesi hiyo, washtakiwa 10 wanakabiliwa na mashtaka matano, kula njama kwa  nia ya kutenda kosa kuvunja jengo na ukuta, kuharibu mali kwa makusudi zenye thamani ya Sh. milioni tano, unyang'anyi kwa kutumia silaha mali za Sh. milioni 20 pia kuchoma mali kwa makusudi na walitenda  makosa hayo Oktoba 10 hadi 12.

Maimamu Mtwara waungana kupinga gesi isitoke

Maelfu ya shura ya maimamu yameunga na wananchi wa mikoa ya Kusini, kuitaka Serikali isitishe mpango wa kusafirisha gesi asilia kwenda Dar es Salaam.

Aidha, wametaka uwekwe mtambo wa kufua umeme uliokusudiwa hapo awali mkoani hapo.

Akisoma tamko kwenye hadhara ya waumini wa Kiislam mjini hapa, Ustadhi Mohamed Salim, alisema kwa kuwa wanaamini serikali yao ni sikivu  basi isitishe zoezi zima la ujenzi wa bomba mpaka pale suluhisho la tatizo hilo litakapopatikana baina ya wananchi na viongozi.

Tamko hilo lilotolewa lilitolewa jana na Shura ya Maimam katika kongamano la dini ya waumi wa Kiislamu lililofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini hapa.

Waumini wa dini ya Kiislam wa manispaa ya Mtwara, wakikusanyika katika viwanja vya Mashujaa jana kwa ajili ya kufanya dua ya kuombea gesi isisafirishwe kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam. Waumini hao
Aidha Ustadhi Salim amesema kuwa kumekuwepo na majibu  ya kutoridhisha na ya kuwakashifu wananchi wa Mtwara kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Madini na Rais mwenyewe, ambayo yanajaribu kueleza vitu vingine na si hoja yenyewe ya wananchi wa Mtwara.

“Majibu yanayotolewa na viongozi hao yanaonyesha na yanajikita katika kuelekea upingaji wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar lakini sababu ya kukataa gesi isitoke si hivyo…,” alisema.

Alisema serikali haina budi kubadilika kimawazo na kuona kuwa mikoa ya kusini ina haki ya kuendelezwa kiuchumi na kuachana na kasumba ya kila kitu kupelekwa Dar es Salaam.

“Ifike wakati sasa wa kuendeleza mikoani … mikoa mingine ili mrundikano wa watu uliopo Dar upungue…na usawa wa maendeleo kati ya mikoa mbalimbali iliyopo hapa Tanzania.

Alisema katika historia mkoa wa Mtwara umetengwa kwa muda mrefu tangu enzi ukoloni.

Akitoa mfano Imamu huyo alisema Mtwara ilikuwa na  reli ikaondolewa, bandari kwa sasa haitumiki, taa kubwa za uwanja wa ndege  zilizoondolewa na kupelekwa Arusha.

Alisema leo gesi imegundulika wanataka kuiondoa na kuifanya Mtwara ibaki kuwa maskini.
Katika tamko lao hilo walisema wamechoshwa na hali hiyo na wako tayari kufa kwa ajili ya gesi.

Nabii ataka Maaskofu Matajili wachunguzwe

Askofu na Nabii Nicolaus Suguye (pichani) wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM), Matembele ya Pili- Kivule, Dar ameitaka serikali kuchunguza uhalali wa mali za watumishi wa Mungu hasa wale wenye utajiri wa kutisha.

Nabii Suguye alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihubiri kwenye huduma hiyo na kusema anasikitika kuona baadhi ya watumishi wa Mungu wanamiliki utajiri mkubwa kama nyumba, magari na mali nyingine lakini hawasemi fedha walizitoa wapi.

“Naiomba serikali ichunguze mali za watumishi wa Mungu kwani wanazipata kwa njia isiyo sahihi. Wengi wamekuwa wakiagiza vitu kutoka nje ya nchi kwa mgongo wa kanisa na vikifika nchini vinakuwa mali zao,”…

Nabii Suguye alisema watumishi wa Mungu watakaobainika kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wafutiwe usajili wa huduma zao ili kuwa fundisho kwa wengine wenye lengo la kutaka kufanya hivyo.
“Katika kazi ya Mungu hakuna biashara, watumishi hao wenye utajiri wa kutisha wanaupata wapi? Mbaya zaidi fedha wanazopata wanashindwa kuwasaidia yatima na wajane badala yake wanazitumia kwenye mambo ya anasa kama kununulia magari ya kifahari,” alisema Suguye.

Askofu na Nabii Nicolaus Suguye wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM)



Mauaji Marekani ni matokeo ya maadili mabovu si silaha walizonazo

Mauaji ya raia wasio na hatia ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana wadogo wa kimarekani kwa kutumia silaha za moto, yanaakisi ukengeufu wa kimaadili na si dhana ya mapenzi yao juu ya silaha wanazomiliki kama wengi wanavyodhani.

Mchungaji Will Marotti, wa Kanisa la New Life lililopo maeneo ya Connecticut, akiongea na OneNews kuhusiana na sakata la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa wanafunzi na mkuu wao na kijana mmoja kabla naye kutimiza azma yake ya kujiua alisema ni ukengeufu wa maadili.

Alisema katika jamii inayothamini maisha ya binadamu, umiliki wa bunduki si tatizo kubwa. Watu huishi maisha bora yenye kuthamini na kuamini juu ya uadilifu; hawahitaji kuchunga maisha yao kwa bunduki, au njia yoyote isipokuwa inapolazimu kujihami.  

“Hivyo sivyo katika muonekano halisi wa maisha yalivyo leo katika hali hii ya mabadiliko makubwa duniani. Katika jamii hiyo ambayo imeruhusu utoaji wa mimba, na kunyonga bila maumivu, maisha kwao imekuwa kitu rahisi,” alisema na kuongeza:

“Mwanamke anaporuhusiwa kuua mtoto asiyemtaka akiwa tumboni mwake, hiyo ni kuhujumu maisha kwa kutoyathamini. Kama hilo halitoshi anaporuhusiwa kubadili mtoto anayekua tumboni mwake, kutoka kitu kisichohalisi hali hufanya maisha yaonekane kuwa kitu kinachoweza kuchezewa.”

Mbali na hilo alibainisha kwamba haya ni maisha wanayoyataka ya kudhani kuwa mwanadamu anaweza kucheza na nguvu za Mungu kwa kucheza na maisha.

Kadhalika aliweka wazi kuwa, kama  mwanamume anahaki ya kumhudumia mkewe anapokuwa akisota katika matibabu na wakati akiwa mahututi katika hospitali ya Terry Schiavo, ujumbe huo uko wazi na unaeleweka; kwa maana huwezi kutenganisha utashi na ukiri kwa jumla.

Kwa namna nyingine alieleza kuwa, siku hizi utakuta watoto wakifurahia kuangalia picha za mapigano na michezo yenye kuburudisha katika luninga, vitu vinavyohamasisha machafuko. Watoto wa kimarekani na wazazi wao wamejifunza michezo inayoondoa maisha.

“Watu wasioamini kuwa maisha ni sadaka inayoweza kuondolewa kwa mihemuko kwa kusababisha kifo, hata pale ambapo kifo kingeepukika. Hivyo, hutokea ulinzi wa kuepusha machafuko ya halaiki, jibu ni kwamba kuheshimu maisha na kujilinda binafsi siyo kumiliki bunduki,” alisema na kuongeza:

"lazima tufahamu kuwa tuko kwenye mapambano si suala la kuamini kuwa Mungu yupo shetani kadhalika, si wakati wa kusema Mbingu ipo na jehenamu, nchi yetu iko kwenye mapigano sasa, najua wakristo mnajua kuwa wajibu wenu ni nini.”

Watumishi wengi kipindi hiki alieleza kuwa, wanakuwa na safari nyingi kutoka sehemu moja hadi nyingine, mimi nawatia moyo kwamba wanatakiwa kutulia makanisani na kuzidi kumtafuta Bwana hata katika kipindi cha Krismas.”
 Aliendelea kueleza kwamba ulinzi uko kwa Bwana na kwenye silaha ambazo watu wamekuwa wakiona kama ni mungu wao na hilo ndio maana limekuwa likileta maafa makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia.

 “Kwa namna moja ama nyingine ninaweza kusema kwamba watu wamemsahau Mungu wa Kweli, tumesahau kukaa mikononi mwake; kingine ni kutubu kabisa kwa uovu mwingi ambao tumekuwa tukiufanya, tumwombe Mungu alinde shule zetu na watoto, kinyume kabisa dhidi ya shetani,” alisema. 

Usiku wa Tafes Mkoa wa Dar es salam ndani ya AIC Magomeni.

Ulikuwa ni usiku wa aina yake ulioohusisha wanafunzi wa waliokoka wa ngazi ya vyuo vikuu wa Jijini Dar es salaam, unaofanyika kila mwaka baada ya uongozi mpya kuingia madarakani ,Mkesha huo ulifanyika katika Kanisa la AIC Magomeni usiku wa Ijumaa.

Usiku huo ulipambwa na TAFES Praise Team,Winners Chapel Worship Team na Living Waters kutoka Living Water Centre Kawe,madhumuni ni kukesha katika kumsifu na kumwabudu Mungu pia kupata muda wa  kusikiliza Neno kutoka kwa mtumishi anayealikwa usiku huo.

Mtumishi aliyehudumu katika Upande wa Neno alikuwa ni Apostle Samuel Sasali na mkesha huo kuhudhuliwa na wanafunzi wanachama wa Tafes Dar es salaam kutoka UDSM,IFM,KIU,CHUO KIKUU ARIDHI,KAHIRUKI,MUHIMBILI,DIT,ST.JOSEPH,IMTU.

TAFES Praise Team
Ilikuwa Fullshangwe
Living Waters Worship Team vijana wa Apostle Ndegi walikuwepo kuhudumu
Winners Chapel Worship Team

Katikati ni Peter Anase alikuwepo pia kama mjumbe msaafu wa Tafes
Papaa The Blogger alikuwepo kama mjumbe msaafu wa Tafes pembeni yake ni Mwenyekiti wa TAFES Taifa na Mkoa Lukas Godfrey


Kitu cha sebene kwenda mbele
Mwenyekiti wa TAFES Taifa na Mkoa pia Lukas Godfrey kutoka cha DIT
Viongozi wa TAFES Mkoa kutoka vyuo mbalimbali wakijitambulisha
Apostle Samuel Sasali  alihudumu pande wa Neno

Wanamuziki wa Injili wa Kimataifa Mbashaz watua London, Uingereza na kutembelea Ofisi za Ubalozi

Mheshimiwa Balozi, Peter Kallaghe, akipokea zawadi ya CD na DVD kutoka kwa Waimbaji wa mziki wa injili Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha. wakiwa nchini Uingereza, walitembelea Miji ya Glasgow, Chemsford na Reading.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamuziki wa nyimbo za Injili Flora Mbasha na Mumewe Bwana E. Mbasha (Kulia), Askofu Ernest Irungu, ambaye ni Kiongozi wa nyimbo za Injili na ni Mkuu wa Chuo cha Vision College of Theology kilichopo London, Uingereza, mama Zest Irungu (mke wa Bishop Irungu) na Bibi. Mwambola, walipotembelea Ofisi za Ubalozi. Bwana na Bibi Mbasha wapo nchini Uingereza, wakitokea Amerika kujitangaza na kutangaza Injili.

 source:fullshangweblog.com

Aliyegoma kupachikwa No. 666 akimbilia kortini


Mwanafunzi wa masomo ya Sayansi, Andrea Hernandez, (15) amezua kizaa zaa katika shule ya  John Jay High School, baada ya kugoma kupachikwa chip maalumu ya utambuzi, inayowawezesha walimu na viongozi wa shule kumuona na kumfuatilia kwa kila kitu anachofanya, akidai kuwa kifaa hicho ni alama ya mnyama au nambari ya Mpinga Kristo iliyotajwa katika Biblia kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura ya 13.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, uongozi wa wilaya ilipo shule hiyo, huko Texas nchini Marekani, umepitisha sheria ya wanafunzi wote kupachikwa chip hizo ili kukabiliana na tatizo la utoro madarasani, lakini kijana huyo akiungwa mkono na wazazi wake walikataa kukubaliana na sheria hiyo kwa madai kuwa kifaa hicho kinachorusha mawimbi ya sauti (RFID) kinaumiza hisia za imani yake ya dini.

Wote Andrea na baba yake, Bw. Steven Hernandez, waliueleza uongozi wa shule kuwa hawana shaka hata kidogo kuwa kifaa hicho ni cha Mpinga Kristo na kwa kuwa kina maelezo ya utendaji ule ule wa Mpinga Kristo, kama ilivyoelezwa katika Ufunuo wa Yohana.

Msichana huyo na  mzazi wake walipokataliwa na uongozi wa shule na ule wa wilaya waliamua kwenda Mahakama ya Mwanzo kufungua shauri  na kesi ikaendeshwa haraka haraka, lakini wakashindwa.

Hata hivyo hawakukata tamaa waliamua kukata rufaa katika mahakama ya juu na uamuzi ulitarajiwa kutolewa wiki chache zilizopita, ingawa warufani waliahidi kuendelea mbele ikiwa Jaji asingetoa hukumu upande wao.

Mradi wa kuwapachika chip wanafunzi wote unajulikana kama  “Student Locator Project,”  unalenga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaotulia shuleni na vyuoni badala ya kuzurura mitaani.
Mradi huo unalenga kuhudumia wanafunzi  4,200  katika shule za John Jay High School na Jones Middle School, ambao wanapaswa kuvaa  “SmartID” ambayo imepachikwa kadi ya mawimbi ya  RFID.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la  San Antonio Express, mzazi wa binti huyo,  Bw. Hernandez alipoulizwa na waandishi wa habari mpinga Kristo ni nani alijibu: “Katika shauri hili wasimamizi wa wilaya hii ndio wamegeuka mpinga Kristo.

Katika mahojiano mengine na shirika la  NPR, Bw. Steven Hernandez alisema kuwa binti yake alikwishasema kuwa kamwe hawezi kuvaa kifaa hicho kwa kuwa kina athiri imani yake ya dini.
Mbele ya waandishi wa habari binti huyo alikaririwa akimweleza baba yake: “ ‘Daddy, I’m not going to do this.’ (baba sitafanya hivyo) aliendelea kudai kuwa kilichopo kwenye kifaa hicho ni kile kilichoonywa kwenye Biblia kuhusu Ujio wa mpinga Kristo na yeye hawezi kuwa sehemu ya ushetani huo.

“Nasema kweli niliyoipata katika Biblia, Ufunuo wa Yohana 13:17  unaeleza wazi kuwa wakati unakuja ambao hakutakuwa na uhuru wa kuuza wala kununu isipokuwa uwe umepachikwa alama ya mnyama ambaye jina lake ni namba.”

Mwanasheria anaye mtetea binti huyo alidai kuwa uongozi wa shule umeamua kumuadhibu  Andrea , kinyume na sheria ya jimbo la  Texas’  inayohusu uhuru wa dini, na hata katiba ya Marekani.

 “Wakati tunapohangaika kuhakikisha shule zetu zinakuwa salama, hasa katika wakati huu ambao tumekumbwa na majanga makubwa ya ufyatuaji wa risasi na mauaji; hatuamini kuwa utumiaji wa vifaa hivi utakuwa msaada, nadhani wauaji wanaweza kufanya vibaya zaidi kama watatumia vifaa hivi kuulia,” alisema  John W. Whitehead, rais wa taasisi ya  Rutherford.

Uongozi wa shule unadai kuwa kufungwa kwa vifaa hivyo kutapunguza idadi ya wanafunzi watoro na kuongeza makusanyo ya ziada kiasi cha Dola za marekani Milioni 1.7, kutoka kwa uongozi wa jimbo wakati wa ufungaji wa vifaa hivyo  katika wilaya nzima yenye shule  112 .

Kibarua chaota nyasi kwa kuombea mteja

Mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Bi. Anhue Doan (59) amejifukuzisha kazi baada ya kumuonea huruma mteja kisha akamuombea kabla ya kumhudumia.

Mkasa huo wa aina yake ulitokea katika duka moja la dawa la Walmart, huko Calfonia  nchini Marekani,  na tukio hilo likanaswa na kamera za usalama.


Viongozi wa duka hilo kubwa la dawa walibaini tukio hilo baada ya kuangalia  picha zilizopigwa za kamera ya CCTV  zilizofungwa ndani ya duka hilo, ambazo zilimuonesha  mhusika  akimshika shika mkono mteja aliyefika kununua dawa kwenye duka hilo, huku akilia.

Tukio hilo lilitafsiriwa kuwa alikuwa akimwombea, jambo ambalo ni marufuku kufanyika katika mazingira ya kazi, japo yeye kama mkristo ilikuwa wajibu na wito wake.
Hata hivyo mwanamama huyo ameamua kulipeleka shauri hilo katika Mahakama ya shirikisho iliyopo California kwa kubaguliwa na kutengwa katika misingi ya dini.

Wakili wa mama huyo, Bi. Darren Harris, kutoka Gould & Bowers LLP, akiongea na ABC News alisema, mteja wake hakuwa akimuombea mteja aliyekuja kuhitaji huduma kama ilivyoelezwa, badala yake alikuwa akiongea naye akiwa amemshika mkono.

Alisema kabla ya kufukuzwa kazi alipewa barua ya onyo ambayo hata hivyo haikuonyesha madai ya kuombea mtu, isipokuwa kwa fikra potofu mtu anaweza kuonekana kama yuko kwenye maombi na kwamba si ruhusa kwa mtu kama yeye ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya kuchanganya mambo ya imani yake na taaluma.

Hata hivyo msemaji wa Walmart, alisema kampuni yao ina sera  zinazoheshimu uhuru wa kuabudu  na kwamba haiwanyanyasi  wala kuwatenga watu kwa misingi  ya dini.

"Tunatoa uhuru wa kuabudu wa kutosha, hata hivyo tutaendelea na uchunguzi,"

Walmart, ina maduka  makubwa ya madawa na imeajiri zaidi ya  watu 1.4 million nchini Marekani pekee.

Inaeleza kwamba June 2011, Bi. Doan, aliandika barua kwa mwajiri wake ili awe na kibali cha kuwaombea wateja na ili waweze kupokea uponyaji kwa nguvu za Mungu, lakini hakukubaliwa,  huku akipewa onyo kwamba ikiwa atabainika amefanya tendo hilo atafukuzwa kazi.

Wakili wa Bi. Doan anaamini anabainisha kuwa, anachojua mteja wake ni msumbufu hasa pale alipomtumia ujumbe wa barua pepe meneja wake dhidi ya wenzake ambao walikuwa wakija na vinywaji kwenye pharmacy, kupiga na kupigiwa simu na wengi hawafuati maadili ya eneo la kazi.

Doan alisema majukumu yake amepewa mtu mwingine ambaye si muumini wa dini ya kikristo, kitu ambacho alisema ni unyanyasaji wa  kiimani.

Alieleza kuwa meneja wake alikwenda ofisini kwake na kumuonyesha tape ikionyesha tendo alilokuwa akilifanya la kumshika mkono mteja lakini haikuwa na sauti.

Hata hivyo wakili wa mwanamama huyo alisema kuwa, mteja wake anatakiwa afanye kazi kwenye nafasi aliyonayo hadi hapo atakapostaafu.

Ephraim Sekeleti ndani Living Water Centre Kawe

Ephraim Sekeleti Mutalange ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia na Afrika nzima kwa ujumla,alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia.

Siku ya jana alikuwa katika Kanisa Living WaterCentre Makuti Kawe Dar es salaam chini ya Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi,Ilikuwa ibada ya baraka sana kwa watu walioudhulia katika Ibada hiyo.


Ephraim Sekereti jioni ya leo atakuwa akihudumu katika Ibada ya madhabahu ya Living Water Centre Kawe na pia Living Waters wenyeji watakuwepo kuhudumu.
Ephraim Sekeleti siku ya jana katika madhabahu ya Living Water Centre
Apostle Ndegi,Ephrahim Sekereti na George Mpella
Apostle Ndegi akitamka Neno na mbaraka kwa Ephrahim Sekereti siku ya jana baada ya Kumaliza kuhudumu katika Ibada Living Water Centre.
Ephrahim Sekereti kutoka Zambia siku ya Jana alihudumu katika Ibada Living Water Centre alipata akifanya Korabo na Living Waters.

Viongozi wa Dini wateta na JK kuhusu kulegalega kwa amani nchini.

Rais Jakaya Kikwete, ameelezea kuogopeshwa na kulegalega kwa amani, utulivu na usalama wa nchi hasa katika kipindi cha mwaka jana.

“Nimeogopeshwa sana na hali ya kulegalega kwa hali ya amani, utulivu na usalama wa nchi yetu, hususani kipindi cha mwaka jana na naomba hali hiyo isitokee tena mwaka huu wa 2013,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

"Maana hata nilipolazimika kutumia vyombo vya dola vyenye dhamana ya kutuliza ghasia, bado hali ilikuwa ngumu…lakini naamini kupitia misikiti na makanisa mkiendelea kuwahubiria waumini wenu, hali itakuwa shwari,” alisema wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)- Dayosisi Kati-Singida, Mchungaji Dk. Alex Mkumbo, iliyofanyika makao makuu ya kanisa hilo, Usharika wa Imanuel, mjini hapa jana.
Rais Jakaya Kikwete
Kwa msingi huo, Rais Kikwete, ameyataka madhehebu ya dini kurejesha utaratibu wa zamani wa kukutana pamoja mara kwa mara kujadili mahusiano baina yao ili kuepukana na uhasama wa kidini unaoweza kusababisha machafuko makubwa nchini.

Alisema masuala ya udini siku za nyuma hayakuwapo hapa nchini kutokana na viongozi wa madhehebu ya dini kukutana na kumaliza tofauti zao mapema.

Hata hivyo, alisema hivi sasa utamaduni huo umetoweka hali inayoweza kuchangia kutokea kwa machafuko ya udini nchini.

Aidha, Rais Kikwete aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwahubiria waumini wao kujiepusha na vurugu za udini, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, uvivu, biashara ya ukahaba na kupiga vita vitendo vya kuomba na kupokea rushwa ili washiriki vema kujiletea maendeleo yao.

“Dini na serikali wote tunafanya kazi ile ile ya maendeleo na wananchi wanahimizwa kujiletea maendeleo na dini pia inahimiza waumini wake kupata maendeleo. Kwa hiyo nawaomba tuendelee kushirikiana pamoja, serikali yangu inaahidi kushirikiana na madhehebu ya dini,” alisema.

Alisema utaratibu wa zamani wa viongozi wa dini waliokuwa wanautumia kukaa na kujadili masuala mbalimbali, ulisaidia kutuliza ghadhabu, kuonya na kufundisha, hali aliyotaka ufufuliwe na kuhuishwa upya ili kuimarisha amani na utulivu nchini.

Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)- Dayosisi Kati-Singida, Mchungaji Dk. Alex Mkumbo mbele, na kwanyuma ni yake ni Askofu Mkuu wa KKKT, Alex Malasusa 

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa KKKT, Alex Malasusa, alimshukuru Rais Kikwete, kwa kutoa kauli hiyo inayowahakikishia waumini wa madhehebu yote uhuru wa kuabudu kila mtu na dini yake pasipo kuingiliwa.

Dk. Malasusa alimweleza Rais Kikwete kuwa Kanisa litakuwa bega kwa bega na serikali kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumu nchini, licha ya wachache kutaka kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.

Mapema baada ya kuwekwa wakfu, katika risala yake, Dk. Alex Mkumbo, alimwomba Rais kurejesha Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruruma iliyopo wilaya Iramba, kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha madhehebu ya Lutherani, kwenye dayosisi hiyo.

Dk. Mkumbo alimweleza Rais Kikwete kuwa shule hiyo ilichukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na yeye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Kanisa linaiomba shule hiyo ili kuweka mambo mengi muhimu ya ukumbusho wa KKKT Dayosisi ya Kati.

Hata hivyo, katika majibu yake, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa kanisa hilo kukutana na wenzao viongozi wa ngazi ya mkoa wa Singida ili kumaliza kabisa tatizo hilo.

Katika sherehe hizo, wageni mbalimbali walihudhuria wakiwamo Maaskofu wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya nchi kama Norway, Ujerumani, Afrika Kusini na Marekani.

Source:Nipashe

Wana bunduki na majeshi, lakini mimi nina Jina la Yesu!

Hatimaye mjane wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa kituo cha Luninga cha Channel TEN, aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa Polisi katika mazingira ya kutatanisha, Bi. Itika Mwangosi, ametoa ya uvunguni mwa moyo wake akisema; amechoka kuhangaishwa sasa anamwachia Bwana Yesu Kristo ampiganie.

Katika mahojiano maalumu na chanzo kimoja cha habari nyumbani kwake, Iringa Bi.Itika alisema: “Nimechoka kuhangaishwa, najua kuwa serikali ina majeshi na silaha kali kama zile walizotumia kumuua mume wangu, lakini mimi nina Jina la Yesu na majeshi ya mbinguni, lazima haki itapatikana siku moja.”

Akionekana kutoamini mchakato wa kiuchunguzi unaoendelea, mama huyo ambaye bado amefunga kitambaa cheusi kichwani kama ishara ya maombolezo alisema: “Uchunguzi gani unaoendelea muda wote huo, jambo hili lilitendeka hadharani kila mtu aliona; kuna haja gani ya uchunguzi wa muda mrefu kiasi hicho kweli? acha tumtwishe Bwana Yesu fadhaa zetu.”

Chanzo hicho kilipotembelea nyumbani kwake Jumanne iliyopita, na kumkuta shambani akipanda mahindi, alisema kifo cha mumewe kimemsababishia mateso mengi kwani mwanaye amemaliza kidato cha Nne lakini hana tumaini la kufanya vyema katika mtihani wake kwa kuwa aliumia sana, tena wakati wa maandalizi ya mitihani.

Alipoulizwa iwapo amekwishafungua kesi mahakamani kudai haki ya mumewe alisema: “Kwenda Kortini…labda niambiwe mwisho wa kesi mume wangu atafufuka, vinginevyo sitaenda kortini. Sihangaiki nimechoka acha tu nimuachie Yesu, yeye ana majeshi mengi ya mbinguni na anaweza kupambana na majeshi ya hawa watu…..”

Aliendelea: “Mimi tegemeo langu ni Kristo kwa sasa bado sijaanza kujishughulisha na kitu zaidi ya hichi kilimo, nasubiri Mungu anataniambia nifanye nini, ila kwa kweli nimeumia sana.”
Mwandishi huyo chipukizi aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa mikononi mwa Polisi, Septemba mbili mwaka huu na askari mmoja aliyedaiwa kuhusika na tukio hilo amefikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za mauaji.

Hata hivyo, bado taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, kuchunguza mkasa huo haijatoa majibu yoyote na taarifa ya awali ilipingwa na wadau; kwa kile kilichoelezwa kuwa ilificha mambo mengi.

Baadhi ya asasi za kijamii, kikiwepo kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini, viliahidi kulipeleka suala la kuuawa kwa mwandishi huyo mbele ya Mahakama ya Jinai ya kimataifa huko The Hague Uholanzi ili haki itendeke.
Baadhi ya wadai na wakereketwa wa haki za binadamu wamehoji ukimya wa suala hilo, na Jibu la Maisha likiwa nyumbani kwa marehemu pamoja na mambo mengine kujionea maisha ya mjane huyo na watoto wake na jinsi ambavyo wale waliotoa ahadi ya kusaidia familia hiyo wanavyotekeleza ahadi zao.

Ingawa mke wa Mwangosi alionekana kukata tamaa au kutokuwa uhakika wa kupata haki ya mumewe, lakini anaonekana mwenye kumtumaini Bwana Yesu zaidi kwani kila baada ya maneno machache alilitaja jina la Yesu kama mfariji wake.

Pia anaonekana kuwa karibu na ndugu wa marehemu wa mumewe kwani, kila anapoulizwa swali anajibu na kisha kuomba shemeji yake naye aulizwe kwa kuwa ana ufafanuzi zaidi.

Baadhi ya wakazi wa Iringa waliohojiwa na Jibu la Maisha, kuhusu suala la Mwangosi linavyoshughulikiwa walieleza wasi wasi wao kutokana na ukmya mwingi wa serikali wakati suala lenyewe lilitokea hadharani na wauaji wanaonekana tu.

“Kwa kweli kama Mungu anaingilia kati watu wanaotendwa uovu basi ataingilia hili. Yeye ni mume wa wajane atapigana upande wa mjane huyu kwa kuwa anakandamizwa kwa makusudi,” alisema mmoja wa majirani wa marehemu Mwangosi ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Mmoja wa wanasheria mashuhuri nchini, Dk. Daniel Mjema, aliliambia Jibu la Maisha kuwa, yeye na baadhi ya wanasheria wenzake wako tayari kusaidia mjane huyo kufungua mashtaka ya madai mahakamani ili kudai fidia ya kifo cha mumewe kwa kuwa hiyo ndiyo njia itakayosaidia kupatikana kwa haki ili familia iliyoachwa ipate kusoma na kuendeleza maisha.

“Fikiria Mwangosi ameuawa lakini familia yake ipo pale inatakiwa iendelee kuishi, itaishije kama hawakupata fidia? kama angekuwa amekufa katika mazingira ya kawaida kusinginekuwa na neno, lakini kwa kuwa kifo chake kimetokana na watu; na watu hao wanamilikiwa na mamlaka fulani, basi mamlaka hiyo inapaswa kuagizwa kulipa fidia stahiki,” alisema Dk. Mjema.

Viongozi wa dini wapinga Serikali kusafirisha gesi

Mgogoro wa gesi umeingia sura mpya, baada ya viongozi wa dini mkoani Mtwara kuungana na wananchi kupinga usafirishwaji wake kwenda Dar es Salaam, huku Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akitoa ufafanuzi wa faida za mradi huo kwa taifa.

Mbali na ufafanuzi huo, Waziri Muhongo amemlipua Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji kwa msimamo wake wa kuungana na wananchi hao, akieleza kuwa hamwelewi kwa kuwa wabunge akiwamo yeye, walishirikishwa vilivyo kwenye mradi huo na kulipwa posho lukuki.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
Viongozi wa dini waliojitosa kwenye mgogoro huo ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a na Askofu Mteule wa Kanisa la KKKT, Dayosisi Mpya ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbedule.

Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamepinga mradi wa kusafirisha nishati hiyo kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa hawaoni ni namna gani utawanufaisha wakazi wa Mtwara.

Askofu Mnung’a alisema anapingana na uamuzi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na badala yake kuishauri Serikali ijenge mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara.

“Lazima wananchi wa Mtwara waamke, tumejifunza kule Songosongo, gesi imekwenda Dar es Salaam, si Kilwa wala Lindi iliyofaidika na gesi ile gesi ibaki Mtwara, mikoa ya kusini iimarishwe,” alisema Askofu Mnung’a na kuongeza:

“Hii yote ni Tanzania, hakuna ubaya wowote ile mitambo ya kufua umeme ikawekwa Mtwara wafikirie leo hatuombei ila watu wakilipua Kidatu (Morogoro), nchi itakuwa gizani, lazima tutawanye rasilimali zetu siyo kila kitu Dar es Salaam.”

Askofu huyo alimpongeza Murji kwa kuweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo na kumshangaa Mbunge wa Masasi Mariam Kasembe anayeunga mkono akisema, mbunge huyo hawakilishi maoni ya wananchi.

“Nimewaambia waumini wangu kuwa tuwe tayari kutetea rasilimali yetu…. nampongeza Murji kwa kutetea masilahi ya wananchi,” alisema Askofu Mnung’a.

Askofu Mbedule alisema hapingi gesi kwenda Dar es Salaam ila hadi pale ahadi za Serikali zitakapotimizwa kwa wananchi wa Mtwara.

“Kwenye salamu zangu za Krismasi niliwaambia waumini kuwa ni wakati wa kuidai Serikali kutimiza ahadi zake kwa wananchi… wananchi wa Mtwara waliahidiwa viwanda, hakuna kiwanda hata kimoja, gesi inaondoka... hapana sikubaliani nalo,” alisema Mchungaji Mbedule na kuongeza:

“Serikali itueleze bomba la gesi kwenda Dar es Salaam litatoa ajira ngapi kwa wananchi wa Mtwara? Hilo moja, pili bomba hilo litachochea vipi uwekezaji kwa mikoa ya kusini… kama hakuna majibu ya hayo basi mimi nazuia gesi isiende Dar es Salaam.”

Alisema Rais Jakaya Kikwete aliwaahidi neema wananchi wa Mtwara kutokana na uchimbaji wa gesi na kwamba kabla ya kufikiria kuisafirisha kwenda Dar es Salaam ni muhimu ahadi hiyo ikatekelezwa.
“Zaidi ya miaka 21, Barabara ya Mtwara - Dar es Salaam haijaisha, mikoa mingine zinajengwa barabara zenye kilomita nyingi na zinakamilika na kuiacha hii ya kusini… hata juzi nimepita hapo bado barabara ni ya vumbi,” alisema.

Source: Nipashe

Sarah Shilla-Natamani


Abdulrahman Kinana ataka amani idumishwe.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema amekerwa na chokochoko za kidini zilizoanza kujipenyeza  na kuomba madhehebu ya dini na taasisi zake nchini,kuendelea kuhubiri amani na  kuliombea taifa, ili wananchi waendelee kujivunia amani.

Kinana alitoka kauli hiyo jijini Arusha katika sherehe za Hussein Day, ambazo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mtume wa dini ya kiislamu, Muhammad inayoandaliwa na tasisi ya kidini ya Khoja Shia.


Kinana alisema upo umuhimu kwa viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na kuonya kuwa serikali haitasita kuchukua hatua za haraka dhidi ya mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjifu wa amani.

Alisema pamoja na changamoto zinazojitokeza hivi sasa kwa baadhi ya dini kukashifu dini zingine, serikali iko macho kuhakikisha inadhibiti hali yoyote ya ukiukwaji wa maadili ya kidini na kusisitiza kwamba dini zote nchini ziendeshe shughuli zake kwa kuheshimiana.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Khoja Shia, Gulam Hussen, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuendelea kukumbuka mazuri yote aliyokuwa akiyafanya mtume  Mohamad,  kwa lengo la kukumbushana na kuyaenzi.