Rais wa Malawi ,Joyce
Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za
jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka
1994.
Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani
mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada kwa nchi za kiafrika ambazo hazitatambua haki za mashoga.
Rais Banda alichukua hatamu za uongozi mwezi jana kutoka kwa mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliyeaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.
Hadi sasa rais huyo amegeuza baadhi ya sera zake ikiwemo kushusha thamani ya sarafau ya nchi kwa lengo la kuanza kupata msaada .
Wafadhili wengi walisitisha msaada chini ya utawala wa Mutharika, wakimtuhumu kwa uongozi duni pamoja na ukandamizaji.
Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani mjini
source :.bbc.swahili
No comments:
Post a Comment