RebeccaMalope
akijulikana kama Malkia wa muziki wa injili Africa amezaliwa 1968
katika kijiji cha Lekazi karibu na mji wa Nelsprut, Mpumalanga. Malope
hakuendelea sana katika elimu na ni mambo machache sana yanafahamika
kuhusiana na enzi za utoto wako. Akiwa katika umri mdogo Malope alipata
ugonjwa uliopelekea kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza
kutembea tena katika maisha yake.
Familia
yake ilikuwa masikini sana na ndipo yeye na dada yake(Cynthia) waliamua
kumbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton kwa ajili ya
kutafuta kazi kujikimu na maisha.
Mwaka
1986,Malope alishirika kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uimbaji
“Shell Road to Fame,(Music talent search) lakini hakufanikiwa kufika
mbali. Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena na
kuibuka mshindi(Best Vocalist) na wimbo Shine on. Ushindi huu
ulimsogeza mbali sana kimuziki na ndipo alipokutanishwa na
muandaaji(producer) mashuhuri Sizwe Zako na akapata meneja wake wa
kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi.
Dr. Rebecca Malope |
Album
yake ya kwanza ilikuwa na nyimbo za kawaida za kijamii,album
haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa moja
kwenye muziki wa injili. Alipata sapoti kubwa sana kutoka katika radio
mbalimbali kwa nyimbo zake za gospel kitu ambacho hakikuwa kawaida sana
Africa Kusini.
Mwaka
1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike wa Afrika
Kusini,na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja walimpigia
kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music
Award Music Show, na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo,
Album zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu(gold).
Katika kipindi hiki kopi zaidi ya milioni 2 zilikuwa zimeshauzwa sokoni.
Mwaka 1995 kwenye CD yake ya Shwele Baba, kopi zadi ya milioni
moja zilikuwa zimeshauzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake,na hii
iliweka rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Africa
kusini.
Dr. Rebecca Malope |
Mwaka
1996 haukuwa mwaka mzuri sana kwa Rebecca,alipoteza baba yake mzazi,
kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya kutatanisha
wakifuatana. Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha
huduma bali alisonga mbele na kazi hii ambayo yeye anaamini ni kutoka
kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia. Kati ya mwaka 1995 na 2004
Rebecca amezunguka ulimwenguni akiwa na band ya Pure Magic akimtukuza
Mungu kwa njia ya uimbaji.
Mwaka
2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Natal
kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Africa kusini. Na
Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora(Kora music award)
mwanamuziki bora wa Injili.
Katika
wanamuziki ambao alishirikiana nao kwa karibu sana na wamekuwa na
mchango mkubwa kwake ni pamoja na marehemu Vuyo Mokoena.
Mwaka 2004 Malope alianza TV show yake “Gospel
time” ambayo inafanya vizuri sana.
Mwaka huu wa
2012 tarehe 25,February ,Malope amefanya Live recording katika jiji la
Pretoria, na hii ni album ya 31.
Msama
Promotions
waandaaji wa matamasha ya makubwa ya injili Tanzania,Katika Tamasha la
Pasaka la mwaka huu wanamleta Malkia wa muziki wa injili Africa,
Dr.Rebecca Malope katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe
08/04/2012.siku ya pasaka.
Rebecca Malope ataongozana na band yake
ya wanamuziki 13. Ameahidi kufanya makubwa siku hiyo katika uwanja wa
Taifa.
Baadhi ya Tuzo ambazo
Dr. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa.
Music awards
1994 – Best Gospel
Singer
1997 – Best Selling
Album for Uzube Nam’
1998 - Best African Gospel Artist & Best Selling Album
for Angingedwa
1999 – Best Female Artist and Best African Gospel
for Somlandela
2002 – Best Gospel Artist for Sabel Uyabizwa
2003 – Best African
Gospel Artist for Iyahamba Lenqola
2004 – Best African
Gospel Artist for Hlala Nami
No comments:
Post a Comment