Christina Shusho Kupepelusha bendera ya TanzaniaAfrica Gospel Music Awards



Kama ambavyo inafahamika, na Kama Ulikuwa Hufahamu basi Wacha Tukujuze kwa sasa, Mwanamuziki Bora Wa Kike Tanzania katika Anga za Kimataifa Christina Shusho ameingia Katika Mchakato wa Kushindania Tuzo Mbili mwaka huu 2012. Tuzo Ya Kwanza ni Mwanamuziki Bora Wa Kike Afrika na Tuzo Ya Pili ni Mwanamuziki Bora Kutoka Africa Mashariki.

Mashindano Hayo yanayoandaliwa kwa jina la Africa Gospel Music Awards Hufanyika kila Mwaka Mara moja katika Nchi ya Uingereza, Mwaka huu Mashindano hayo yatafanyika tarehe 7 Mwezi wa 7.
                        Christina Shusho akizungumza na Bloggers na Watumishi wa Mungu kuhusiana na tukio lililo mbele yake

Christina Shusho ni Mwanamuziki Pekee Wa Tanzania aliyeingia katika Tuzo hizo mwaka Jana na Mwaka huu. Timu Rasmi ya Kuhakikisha Christina Shusho anatwaa Taji Zote Mwaka huu inategemea kuzindua Kapeni Hiyo rasmi katika Viwanja Vya Dar Live Siku Ya Jumapili kuanzia saa 9 Alasili.

Ingawa Kura zimeanza kupigwa tangu tarehe 1 June, 2012 lakini Kampeni hizi Zinazinduliwa ili kutoa hamasa Kwa Watanzania ndani na Nje ya nchi kuweza Kushiriki Kumpigia Kura Mwanamuziki Huyu Wa Injili.
Papaa akimwambia jambo Christina Shusho kwa msisitizo



 Hata wewe Msomani Wangu Unaweza Kushiriki Kumpigia Kura Christina Shusho Mwaka huu Akatwa Tuzo hizi zitakazo Uweka Muziki Wa Injili Tanzania Katika Anga za Kimataifa.

Namna ya Kupiga Kura, Click Hapa.......http://africagospelawards.com/, then Uta click Nominees and Voting....http://africagospelawards.com/nominate.html

Chagua Jina Kutoka Category hii


ARTIST OF THE YEAR- EAST AFRICA
  1. Eko Dydda- Kenya
  2. Emmy Kosgei - Kenya
  3. Exodus- Uganda
  4. Christina Shusho- Tanzania
  5. Lam Lungwar- South Sudan
  6.  Sarah K-  Kenya
  7. Dawit Getachew-Ethiopia
  8. Kambua-Kenya
  9. Willie  Paul- Kenya
  10. Ann Marie Mutesi - Burundi

 FEMALE ARTIST OF THE YEAR
  1. Emmy Kosgei-Kenya
  2. Dena Mwana – Congo
  3. Ntokozo Mbambo- South Africa
  4. Rebecca- UK
  5. Gifty Osei- Ghana
  6. Kefee -Nigeria
  7. Onos Ariyo- Nigeria
  8. Diana Hamilton-UK
  9. Christina Shusho -Tanzania
  10. Lara George- Nigeria








No comments:

Post a Comment