Taasisi isiyo ya kiserikali, inayojihusisha na utafutaji na ukusanyaji wa taarifa na shuhuda, ijulikanayo kama; Moses Kulola Faundation, imeanza kuandaa historia ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk. Moses kulola.
Histolia ya Askofu Kulola kwa ufupi, alizaliwa mwezi Juni 1928 katika familia ya watoto kumi.
Alisomea shule ya msingi ya Ligsha Sukuma, halafu taasisi ya usanifu.
Alibatizwa kikristo mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro. Alimwoa
Elizabeth wakawa na watoto kumi.
Alifanya kazi ya uchungaji wa kanisa la AIC miaka ya 1961-1962
akaendelea na masomo ya kitheolojia. Baada ya kujiunga na dhehebu la
kipentekoste alifanya kazi ya uchungaji ndani ya kanisa la TAG miaka ya
1966-1991. Akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya mwaka wa
1991, kanisa la EAGT (kwa Kiingereza Evangelistic Assemblies of God) akawa askofu wao wa kwanza tangu mwaka uleule.
(Chanzo wikipedia)
Msemaji wa Shirika hilo Mwinjilisti Willy Kulola aliliambia gazeti la Kikristo la Jibu la Maisha siku chache zimepita kuwa lengo la kuandaa historia hiyo ni kutaka kuonyesha kazi kubwa ya Mungu aliyoifanya Askofu Kulola ya kuwaleta watu kwa Yesu.
Aliongeza kuwa mpakwa mafuta huyo wa Mungu ametimiza miaka 67 sasa tangu aanze huduma ya kumtumikia Mungu, huku akibainisha kuwa kuna mafanikio makubwa yamepatikana ya kuvunja ngome za ibilisi katika maeneo mbalimbali ya taifa ya Tanzania hata nchi za nje
“Katika hatua nyingine, ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania walio wengi nchini na nje ya nchi ni kuwepo kwa maandishi ya kueleza huduma ya kiroho ya Mtumishi wa Mungu Dk. Moses Kulola,” alisema Mwinjilisti huyo na kuongeza.
Hivi sasa mpakwa mafuta huyo wa Mungu metimiza miaka 67 tangu alipoitwa kumtumikia Bwana Yesu, kwa hiyo mchakato wa kuandaa historia ya baba yetu Dk. Kulola umeanza na utakamilika hivi karibuni.
Alisema lengo ni kumtukuza Mungu kwa matendo makuu anayoyafanya kwa watu wake na kuangusha ngome za mwovu ibilisi, sambamba na kujipanga imara katika kuifanya kazi ya Bwana, ikiwa ni pamoja na kupata mbinu mpya za kumkabiri shetani.
Askofu Dr Moses Kulo akiwa na kundi la wakristo wa Tanzania walipokuwa Israel |
No comments:
Post a Comment