Wakati wengine wakiendelea kubishania uhalali wa ibada za mafuta na
vitambaa, hatua kubwa ya kufikia umoja wa kidini yaani United Religious,
utakaokuwa na nguvu kuzidi Umoja wa Mataifa (UN) imefikiwa hivi karibu, baada
ya dini zaidi 50 kuandaa ibada siku ya Jumapili na kutumia Bibilia na Qura’n.
Taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la New York Times, ilisema: “Mihimili mikuu
mitatu kuelekea mfumo mpya wa dunia ambayo ni Umoja wa kiuchumi duniani, Serikali
moja na Dini moja. Masikio ya wengi yameelemea kwenye mihimili miwili zaidi
kuliko ule wa tatu ambao wameupuuzia. Lakini huu wa tatu ambao ni dini ya
pamoja (kwa maana ya imani moja) ndio usukani na sasa unakaribia kufikiwa. Huu
ndio unaojulikana kama ‘Interfaith.’
Papa Benedict XVI |
Makongamano na mikutano inaendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku
duniani, huku viongozi wakuu akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja.
Imani ya kuwa na dini moja "Interfaith" imekuwa
ikisisitizwa kote duniani na viongozi wa dini mbalimbali wakitumia mashirika
(NGOs), mashirika ya misaada, na taasisi mbalimbali, wanasisasa wakubwa
wametumiwa kuipa msukumo kwa fedha nyingi katika sayari hii.”
Kisha taarifa hiyo iliongeza: “Hivi karibuni baadhi ya makanisa katika
Amerika yamekwenda mbali zaidi katika suala hilo. Juni 26, mwaka huu, Kathedral
ya Kitaifa (National Cathedral) katika Jiji la Washington D.C. iliandaa ibada
ya pamoja na zaidi ya makanisa 50
yalishiriki kusoma Quran wakati wa Ibada ya Jumapili.”
Wachambuzi wa siasa dini wanaeleza kuwa hiyo ni hatua katika mkakati mkubwa
wa kuundwa kwa shirikisho kubwa la kidini katika kipindi cha mpito kuelekea
kuzaliwa rasmi kwa umoja wa kidini ulimwenguni, ukishinikizwa kwa kipengele cha haki
za Binadamu.
Somo kuu katika Jumapili hiyo lilikuwa “Kushirikishana imani, Kushirikiana
maombi na kuelewana.” Lengo likielezwa kuwa ni kuonesha upendo wa Wakristo kwa
Waislamu waishio Amerika.
Miongoni mwa makanisa yaliyoshiriki ni: Christ Church lililopo jijini New
York City,
All Saints Church lililopo Pasadena California, Park Hill Congregational
huko Denver,
Hillview United Methodist lililopo Boise, Idaho First United Lutheran,
katika mji wa San Francisco, St. Elizabeth's Episcopal Church, huko Honolulu, Makanisa
makubwa (dini mbalimbali) yapatayo 26 katika Amerika yamehusika na mpango huo.
Interfaith logo |
Imeelezwa kuwa usomaji huo wa Quran ni mpango maalumu wa kulainisha dini
zenye misimamo mikali ili kuonesha kuwa upo uwezekano wa kufanya ibada pamoja
na kumaliza tofauti zilizowatenga zamani.
Mpango huo mkubwa unatarajiwa kua endelevu ukijumuisha Wakristo, Wayahudi
na Waislamu kwa njia ya kusikia na kusoma aya kadhaa, za Qur'an mara kwa mara
ili watu wazoee kuwa pamoja na mwisho waunganishe mioyo yao pamoja na kuabbudu
pamoja.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, Interfaith, Waamerika wana uhuru wa
kusoma Quran popote wanapotaka. Lakini kwa Wakristo hawana nafasi ya kusoma na
kujifunza kitabu hicho, hivyo kuwepo kwa utaratibu wa kuisoma kila Jumapili
wanapokutana kanisani kwenye Ibada na kutawafanya waielewe na kuwa na ‘umoja’
na Waislamu na kuonyesha kutowabagua; jambo ambalo linaonesha dalili ya
kuzaliwa kwa kitu kipya duniani.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Kikristo duniani hawako radhi na
muendelezo huo. Brannon Howse, mmoja wa viongozi mashuhuri alisema: “Watu hao
wamekana uungu wa Yesu Kristo; wamekana ukweli wa maandiko matakatifu; wamekana
uvuvio wa Biblia, ni vipi tushirikiane nao na kusoma kitabu chao kwenye ibada
zetu?”
Qur'an |
Kisha aliendelea: “Inasikitisha, hii siyo mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba
umoja huo umepata nguvu miongo kadhaa na baadhi ya wakuu wa dini ulimwenguni
wamehusika.
Kwa mfano; habari zilizopatikana kupitia CNS zinaeleza kuhusu muungano
mkubwa ‘interfaith’ wakati Papa alipotembelea jiji la Washington 2008.”
Alisema kuwa wakati Papa Benedict XVI alipofika kituo cha, Pope John Paul II Cultural Center kilichopo
Washington kwa mkutano wa jioni wa dini zote ‘interfaith’ zilikuwepo dini
mbalimbali ambazo hapo awali isingekuwa rahisi kukutana na kuabudu pamoja.
Waislamu, Wahindu, Wayahudi na dini nyingine zilipata nafasi zilishiriki;
isipokuwa Assemblies of God,hii haikuthubutu hata kusogelea.
Viongozi wa Dini kubwa katika Amerika wanahusika sana na umoja huo "Interfaith
movement," kwa mfano; Brian McLaren, mmoja wa viongozi wa juu wanaoendesha
umoja huo, inasemekana kuwa mwaka 2009 alisherehekea Ramadhan na hata kuvaa
mavazi yanayovaliwa na wahusika.
Katika sherehe hiyo; Rick Warren, mshirika
wa Baraza la Uhusiano wa Nje, alikuwa Mgeni rasmi na mnenaji kwenye Kongamano
la kitaifa la Waislamu huko Amerika ya Kaskazini, (Islamic Society of North
America).
Baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo
Rick Warren, Robert Schuller, Brian McLaren, Richard Cizik na Bill Hybels
walitia sahihi barua kwa Jumuiya ya Kiislamu iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kumpenda Mungu na jirani yako’
Barua hiyo iliweka bayana kuwa viongozi wa
Kikristo wanamtambua Allah kuwa sawa na Mungu wa Wakristo.
Barua hiyo ilisema:“Kabla hatujashikana mikono; katika kukubaliana na barua yetu, tuwatake
radhi kwa kuomba msamaha kwa Muumba wa wote. Kwa Waislamu muumbaji ni Allah.
Kwa barua hii, baadhi ya viongozi wa Kikristo wanamuomba na wanatubu kwa
jina la Allah, na wanamtambua kuwa ndiye Mungu.”
Kama tulishindwa kurejesha amani na kuwa pamoja, sasa tumesahihisha mawazo
yetu na kwamba tunaweza sasa kutakasa nafsi zetu.”
Barua hiyo ndiyo iliyozua hofu duniani
kuwa huenda wakati sasa umewadia wa
baadhi ya viongozi kudhihirisha hali ya vuguvugu na kukosa msimamo wa kiimani.
“Kwa kweli
huu ni usaliti wa hali ya juu, kuandika barua na kueleza kuwa Allah
ndiyo Mungu anayeabudiwa na Wakristo ni
mwanzo wa kuelekea katika dini moja na
utawala wa Mpinga Kristo,” alisema Mchungaji Jonathan Emmanuel, wa Nigeria.
Alisema kuwa anautazama mwelekeo huo kama
jambo la hatari kwa kuwa Biblia katika kitabu cha
Yohana 14:6 , Yesu anasema: “...Mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa baba
ila kwa njia ya mimi.”
Kiongozi huyo alisema kuwa ukweli wa
ki-Biblia uko wazi na wala hauna kificho kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kufika
mbinguni. Ikiwa unaamini hivyo ni vipi
uandike tena barua ya hatari kama hii ya
kumhusisha Allah na ufalme wa Mungu?
Kisha aliongeza: “Katika amri kumi; awali
kabisa tunakutana na maandiko yasemayo; “Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usifanya sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni ,
wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie
wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;
nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha
wanichukizao, nami nawarehemu maelfu
wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
(Kutoka
20:3-6)
Source Jibu La Maisha
Source Jibu La Maisha
No comments:
Post a Comment