WATU wawili wa jinsia moja (mashoga), walioonyesha azma yao ya kutaka kuishi pamoja kama mume na mke, wiki iliyopita walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa kununua nyumba huku mmiliki wa Bakery akigoma kuwauzia keki ya harusi yao na wengine kupigwa mawe hadi kufa nchini Kenya.
Hayo yalitokea wiki iliyopita nchini Marekani, baada ya watu hao, waliokuwa kwenye uhusiano wa siri kwa miaka miwili kuamua kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao ni mume na mke, kinyume na mpango halisi wa Mungu ambao ni ndoa ya muke na mume.
Sakata lenyewe lilikuwa hivi; Kanisa moja lilikuwa likiuza nyumba yake (mansion), tangazo likachapishwa kwenye mitandao na watu wakajitokeza kutoa ofa, lakini miongoni mwao walikuwemo mashoga wawili.
Katika kuchekecha nani wa kununua nyumba hiyo, kanisa likafikia muafaka kwa mashoga hao ambapo awali hawakuwatambua kama ni mume na mke, wenye mahusiano haramu.
Baada ya kubaini uchafu huo, huku watu hao wakiwa na pesa kamili, ghafla waliambiwa na wauzaji ambao ni kanisa kwamba, wanasikitika hawatoweza kuuza jumba hilo kwa watu ambao ni mashoga, kwa kuwa matumizi yake yataendana na wahusika.
Mashoga hao ambao ni; Bw. Alain Beret na mkewe Bw. Jim Fairbanks, baada ya kuambiwa habari hizo, huku wakijiandaa kufanya sherehe ya kukata na shoka, mara waingiapo ndani ya Mansion hilo, walinga’aka.
“Huku ni kunyanyapaliana, jambo kama hili kufanyika katika uso wa dunia mapema kiasi hiki ni mbaya, ni lazima likomeshwe,” alisema huyo anayeitwa mume (Beret) na kuongeza:
“Kwa kweli siamini hiki ninachokiona, tuko katika karne hii ya 21, lakini bado tuna kitu cha ubaguzi.”
Hata hivyo msemaji mmoja wa kanisa hilo akiongea na mashoga hao aliwaambia: “Nimeongea na Askofu juu ya nia yenu ya kununua jumba hili, nilimueleza nyie ni watu wa namna gani, kwa msingi huo tunasikitika kutoendelea mbele kuhusiana na jambo hili, hofu yetu ni kuhusiana na matumizi yake.”
Jumba hilo la kifahari lilijengwa mwaka 1890 ambalo pia ni la kihistoria.
Sambamba na hilo, mmiliki wa duka moja maarufu kwa kuandaa keki za sherehe nchini humo mjini Colorado, Bw. Jack Phillips amekataa kuwauzia keki mashoga wawili waliotaka kufunga ndoa wiki iliyopita.
Duka hilo lilijulikana kwa jina la Masterpiece Cake Shop, imeelezwa kwamba lilipokea oda ya kutengeneza keki, lakini lilipobaini kuwa mashoga ndio walikuwa katika shamra shamra za kufunga ndoa wakagoma kuikamilisha.
Katika mkasa huo, Bw. Dave Mullin na Bw. Charlie Craig,waliambiwa na mmiliki wa duka hilo kuwa asingeweza kuuza bidhaa zake kwa watu wanaotaka kufanya mambo kinyume na mpango wa Mungu, lakini watu hao walidhani alikuwa akiwatania, ndipo siku ya harusi ilipowadia na kwenda kuchukua keki wakakutana na ujumbe ule ule.
Baada ya jambo hilo, ambalo waliliona ni udhalilishaji; waliingia kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yao yaliyosomeka namna hii: “Tumekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, tukaamua sasa kuwa kitu kimoja kwa kufunga ndoa, lakini cha ajabu tulipoenda kwa muuzaji maarufu wa keki mambo yakawa mamabaya.”
Kisha aliendelea: “Tulitarajia kuchukua muda mwingi kuelezea namna tunavyotaka keki yetu iwe, lakini haikuwa hivyo, neno langu la kwanza lilikuwa, tunataka kuoana na akatukatiza hapo hapo, tulishangaa.”
Hata hivyo baada ya maoni ya Dave Mullin na Charlie Craig kutundikwa katika mitandao hiyo ya kijamii, (Facebook) watu zaidi ya 1000 walikasirishwa na kitendo hicho, huku wengine wakiamua kwenda moja kwa moja hadi kwa mmiliki kupinga alichokifanya muuza keki huyo.
Miongoni mwa waandamanaji waliokwenda moja kwa moja hadi Masterpiece Cake Shop, ni Bw. Cate Owen aliyeeleza kwa uchungu kuwa, wamekuwa wakisapoti biashara za wazawa, lakini ikiwa naye anatoa huduma kwa ubaguzi basi na wao hawatakuwa radhi kumuunga mkono.
Wakati hilo likifanyika huko Marekani, nchini Kenya nako mashoga wawili walijikuta mikononi mwa kundi kubwa la watu wenye hasira kali baada ya kubambwa kona wakivunja amri za Mungu katika maeneo ya Kayole, ambapo walipigwa mawe na mmoja kufa papo hapo, mwingine akifanikiwa kukimbia, lakini mwisho wa siku mwili uliacha roho kama mwenzake.
Mashoga hao ambao walikuwa ni baba lishe (food venders), inadaiwa kwamba walikuwa wakifanya mchezo huo mchafu kwa miezi kadhaa.
Inaeleza kuwa siku ya tukio walikubaliana kukutana karibu na majengo ya Kanisa Katoliki, eneo linalobainishwa kwamba lina msitu kiasi fulani, wakiwa hapo huku giza likinyemelea walianza kazi iliyowapeleka na ndipo mtu mmoja alipowaona na kuita watu na zoezi zima likachukua nafasi yake.
Wakati zoezi hilo likiendelea mmoja aliweza kukimbia, huku akimuacha mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Kamau akishambuliwa vikali.
Baada ya mauaji ya Kamau, kundi hilo lilimtupa kwenye dampo ambalo lilikuwa karibu na walipokuwa wakifanya ushenzi huo.
Hivi karibuni Rais wa Marekani, Barrack Obama alitamka hadharani kutambua ndoa za jinsia moja, jambo lilipokelewa kwa vifijo na wachache na wengi hasa watumishi wa Mungu kupinga vikali, huku wachambuzi wa masuala ya siasa wakichanganua kuwa hilo limekuja ili kumng’arisha katika medali za siasa, hasa ikizingatiwa wanatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu wa urais mwezi Novemba 2012.
No comments:
Post a Comment