Elimu hiyo ilitolewa na wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kwa muda wa siku mbili kanisani hapo, ambapo walibainisha kuwa, wakristo wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kutoa maoni na wakaweza kupata kile wanachokitaka pasipo kuvunja sheria.
Logo ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu |
Anna
Henga, mmoja wa wanasheria wa Kituo hicho cha Sheria na Haki za Binadamu chenye
makao makuu yake Kijitonyana jijini Dar es Salaam,
alisema Ibara ya 19 inayozungumzia uhuru wa kuabudu, alieleza kwamba wakristo
wanapaswa kutoa maoni yao
ili kuondoa dukuduku na ukiritimba unaohusu vibali vya kuhubiri Injili, ambavyo
vimekuwa vikilalamikiwa na wachungaji kwamba vinawanyima uhuru.
Akitilia
msisitizo juu ya hilo alichanganua kwamba, Katiba iliyopo ambayo ni ya tano ina
viraka vingi ambavyo kwa sasa vina mapungufu yanayohitaji maoni ya watu wa
Mungu ili kuandikwa katiba mpya; alivitaja vichache, kwamba ni pamoja na masuala
ya dini kutoingiliwa na serikali kabisa kwa kuwa uhuru wa kuabudu unapaswa
kuwekwa katika haki za binadamu; ukiheshimiwa na usiotakiwa kuguswa .
Mbali
na hilo alieleza kwamba, wakristo wengi wanafikiri kuomba tu na kukaa kimya
ndiyo jibu la matatizo yao, huku akibainisha kwamba hata mtume Paulo
alipopelekwa kwa Pilato ingawa aliomba lakini ilipofika wakati wa kujitetea
alisema na yeye ni Mrumi wa kuzaliwa na hilo lilimfanya kuachiwa huru.
Kama
hilo halitoshi alibainisha kwamba, wakristo
wengi wamekuwa na kigugumizi juu ya kuwepo kwa mahakama ya Kadhi nchini, ambapo
alieleza kwamba kwa maoni yao
kunaweza kuleta mahakama moja kwa watu wote, kwa haki zote hupatikana
mahakamani na katiba ndiyo sheria mama.
“Ikiwa
mtanyamaza basi mtaiona ikianza kufanya kazi,’ alisema Bi. Anna.
Kuhusu
mfumo wa Serikali; alieleza kwamba, yapo mambo ambayo yanalalamikiwa mara kwa
mara na wananchi ambayo ni kuhusu Tume ya uchaguzi, ambapo alisema inabidi
kuwepo kwa tume huru; isiyoundwa na chama kimoja wakati huu wa vyama vingi.
Mwonekano wa Katiba ya Tanzania kwa juu. |
Akitaja
baadhi ya udhaifu uliopo ndani ya katiba iliyopo alisema kuwa ni; madaraka
makubwa aliyo nayo rais, haki za binadamu kuwekwa wazi kuhusu Afya, elimu na
walemavu, Jaji Mkuu asiwe wa chama kimoja, hukumu ya kifo iliyopo si haki
kuondoa uhai wa mwingine, vyombo nyeti kama Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
na Spika wa bunge asitoke katika chama fulani.
Aliendelea
kueleza kwamba udhaifu mwingine ni; Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa,
tume ya maadili ya viongozi, pia mihimili mikuu mitatu: Mahakama, Bunge na serikali iwe huru, isiingiliwe au
kupata shinikizo kutoka upande wowote.
Pia
aliongeza kwa kushauri kuwa ni vyema Muungano wa Tanzania
na Zanzibar
uangaliwe upya, pia Tume ya Uchaguzi kuwa huru.
“Tanzania ni nchi isiyoongozwa na dini inayofuata mfumo wa kisekula, haifungamani na dini yoyote jambo ambalo limeifanya nchi kuwa shwari bila kuwa na vita vya kiudini; hivyo katiba isiingize masuala ya imani ya mtu au watu,” alisema.
Akiwashukuru
waalimu hao; Mchungaji Paulo Mulokozi wa TAG Ubungo Christian Centre (UCC)
alihimiza Wakristo kushiriki kutoa maoni yao
katika mchakato wa kupata katiba mpya ya taifa na pia kushiriki vyema katika
sensa inayotarajiwa.
“Tumekuwa
tukiliombea taifa letu kila mara, lakini hiyo haitoshi lazima tushiriki
kikamilifu kutoa maoni yetu katika mchakato wa kuunda Katiba mpya, kushiriki
sensa na kuchukua fomu za uongozi inapobidi,” alisema Mchungaji Mulokozi, na
kuongeza: “Tutakuwa hatutendi vyema kama watu wa Mungu tusiposhiriki kikamilifu
kama watanzania.”
Mchungaji
aliwapongeza na kuwashukuru wawezeshaji hao kutoka Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu; Bi. Flaviana Charles na Anna Henga, na kusisitiza Wakristo wengi
kujitokeza ipasavyo katika kutoa maoni, na hata katika kupiga kura; pia
kushiriki kwenye kura na sensa.
No comments:
Post a Comment