Waimbaji watatu kutoka
Arusha, wanaounda kundi la Pallangyo Brothers, wenye kimo kifupi (Kibirikizi)
kwa kushirikiana na Kanisa la flani Uyole Kati
mjini Mbeya, wameleta mamia msalabani katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku
sita.
Mkutano
huo uliokuwa ukiendeshwa katika viwanja vya Kanisa hilo, huku Mhubiri akiwa
Askofu Steven Mulenga toka Mombo mkoani Tanga, uliokusanya mamia ya wakazi wa
mji huo, waliokuwa wakisumbuliwa na mapepo, huku wengine wakibubujikwa na
machozi baada ya kutua mizigo yao msalabani.
Akihubiri
katika mkutano huo, Askofu Mulenga, huku akisindikizwa na ujumbe uliokuwa na
kichwa kisemacho; FILIPO
ALIVYOMDHIBITI SIMONI MCHAWI KWA JINA LA
YESU, alisema,
Yesu alidhihirishwa ili kuzivunja kazi zote za shetani.
Alibainisha
kwamba, mwanadamu yoyote akimwamini Mungu ni wazi kuwa hakuna jambo lolote
linaloweza kushindikana, huku akielezea kwamba, dhambi ndiyo inayomtenganisha
mwanadamu na Muumba wake.
Mtumishi
huyo aliweka wazi juu ya hilo alisema: “Hata leo Yesu yu hai na anaweza kumpa
mtu mahitaji yake wakati wowote anapoitwa.”
Askofu
Malenga, huku akiwa sambamba na Mchungaji mwenyeji wa Uyole Kati, Immanuel
Mwalyenga alitanabaisha kwamba, hata yale ambayo watu wameyakatia tamaa, Bwana
anaweza kuleta ukombozi na kumuaibisha shetani.
Katika mkutano huo, Pallangyo
Brothers walikuwa na mguso wa pekee kwa jamii, huku watu wakijiuliza namna
maumbo yao yalivyo, lakini wanaweza kumnyang’anya shetani mateka.
Huduma ya uimbaji katika mkutano
huo, mbali na kuwepo kwa Pallangyo Brothers pia walikuwepo wengine kama akina Amani
Mwasote, Kwaya kutoka makanisa mbalimbali na kwaya wenyeji Usiogope na Kedroni.
Ingawa mkutano huo ulifanyika
wakati wa kipindi cha maonesho ya Kikanda ya Nanenane ambayo pia huvuta watu
wengi, lakini Mungu hakuweza kuruhusu shetani afanye uharibifu kwa kuwakalia
watu wa Mungu na hivyo kwa uwingi wao walikusanyika kwenye mkutano huo mkubwa.
Katika mkutano huo watu zaidi ya 60
waliokolewa, wengine walifunguliwa katika vifungo vya magonjwa na maonezi ya
pepo wabaya, huku wengine wakileta vitu vyao ambavyo walitumia kwa uganga vichomwe
moto.
Moja ya vitu vilivyomuacha shetani
taabani ni la mama mmoja kutoka kijiji cha Isyonje wilayani Rungwe ambaye baada
ya kusikia tangazo la mkutano kupitia Redio Ushindi, alisafiri hadi Uyole kusikia
Bwana anasema nini juu ya maisha yake na katika siku ya pili ya mkutano
alifunguliwa kutokana na mapepo ambayo yalikuwa yamemtesa kwa muda mrefu.
Kama hilo halitoshi, mwisho wa
mkutano Askofu Mulenga wakishirikiana na Mchungaji Kiongozi wa Uyole Kati
Immanuel Lyego Mwalyenga, pamoja na jopo la wachungaji waliohudhuria mkutano
huo, walifanya maombi ya kuliombea Taifa kwa kushika bendera ya Tanzania.
Waamini
hao wapya, waliompokea Bwana Yesu katika mkutano huo; wanaendelea na mafundisho
ya msingi yanayoongozwa na Mchungaji Bahati Mwandemba katika kuhakikisha
wanaendelea katika imani na kufanyika baraka kwa Kanisa, Taifa na jamii kwa
ujumla
No comments:
Post a Comment