Jaji wa nchini Uingereza, John Platt ametoa hukumu ya mtoto wa miaka 10 abaki kuwa mkristo
na ikiwezekana abatizwe kabisa, baada ya kuwepo kwa msuguano baina ya wazazi wake
ambao mmoja alitaka awe mkristo.
Hukumu
hiyo ilitolewa wiki iliyopita katika Mahakama ya Romford, baada ya wazazi wa
mtoto huyo kusuguana tangu Novemba 2011 huku mama akipinga mtoto wake wa miaka
10 kubatizwa kwa maelezo ya kigezo cha umri huku akitaka tendo hilo lifanyike
akiwa na umri wa mika 16.
Baada
ya kutoelewana, mama ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara
moja alifungua kesi mahakamani ili iweze kuruhusu mwanaye kutobatizwa kwa
kigezo cha kutojua baya na zuri, huku baba naye akidai ni muda muafaka na
hakuna ulazima wowote wa kusubiri miaka 16.
Malalamiko
mengine aliyokuwa akidai mama huyo ni umri wa mwanaye huyo kuwa ni mdogo kiasi
cha kubadilisha imani. Jambo lililopokelewa na baba kwamba anaweza kueleza
kulingana na sheria za Mungu na kwamba hata nyakati za Biblia Mungu aliweza
kumtumia Daudi aliyekuwa mdogo.
Hata
hivyo mwisho wa siku mahakama hiyo haikukubaliana na mama huyo na kumuamuru
kuwaachia watoto wawe wakristo na wabatizwe na kwa sasa wanapewa mafundisho
yanayoelezea nini maana ya kubatizwa na watakapomaliza watakuwa huru kubatizwa.
Wazazi
hao walifikia mafarakano hayo baada ya kugombana na hivyo kuamua kutengana na
hapo baba aliamua kubadili dini na kuwa mkristo.
No comments:
Post a Comment