“If God doesn’t punish
America, He’ll have to apologize to Sodom and Gomorrah.”
Mwinjilisti wa kimataifa, Billy
Graham (95), amesema ikiwa Mungu hatashuka kuihukumu Marekani kutokana na
kufanya uasi wa kila namna bila ya kuwa na hofu, basi itampasa aiombe radhi Sodoma
na Gomora miji ambayo aliangamizwa kwa moto.
Rai hiyo aliitoa wiki chache zilizopita katika sherehe ya kuzaliwa,
kwake ‘birthday’ iliyofanyika wiki iliyopita na kushuhudiwa na maelfu ya watu
ambapo alisema kuwa wamarekani wamekuwa wakifanya dhambi kwa namna ya kutisha
na sasa imefikia hatua mbaya, hawana tena hofu ya Mungu.
Billy Graham Mwinjilisti wa Kimataifa |
Alibainisha kwamba Mungu ni mwingi wa rehema, na kuwa
ikiwa watamaanisha kutubu na kuziacha
dhambi zao ni dhahiri kwamba atawasamehe na kuwarehemu, lakini wakishupaza
shingo wataangamia kabisa.
Mwinjilisti huyo alisema ili kuikimbia ghadhabu ya
Mungu, Wakristo wote nchini humo na mataifa jirani kama Kanada,wanapaswa
kukusanyika kwenye majumba yao na marafiki, majirani na ndugu zao ili kushiriki ibada kwa pamoja
kupitia Luninga zao aliyoiita “Living Room Crusade” kwa
muda wa siku 40 kuanzia September 28 hadi November 6 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa
nchi hiyo.
Mwinjilisti huyo wa kimataifa ambaye amekuwa
akimtumikia Mungu kwa miongo kadhaa sasa, alibainisha kuwa, katika kukusanyika
pamoja kwenye majumba ya Wakristo, kila mmoja atapata wasaa wa kueleza uovu
wake mbele za Mungu, huku akichanganua kuwa suala la utoaji wa mimba limekuwa
kubwa.
Mbali na hilo, mtumishi huyo ambaye amekuwa akiwapa
ushauri wa kiroho marais mbalimbali waliowahi kuitawala Marekani, akisisitiza
juu ya hilo; alitolea mfano wa mji wa Ninawi
ambao ulikithiri kwa dhambi, lakini Yona alipoingia na kuwaambia kutangaza
kuwa utaangamia baada ya siku 40 walisikia na kutubu.
“Ninaamini msamaha walioupata wana wa Ninawi, unaweza
kutokea na kwetu, Yona alipopita na kutangaza, waliitana na kutubu,” alisema
Mwinjilisti Graham.
Miongoni mwa watumishi nchini humo waliounga mkono
kauli hiyo ya Graham, ni pamoja na Mwenyekiti wa ‘American for Jesus’ Anne Gimenez ambaye siku
hiyo ya kutubu atakusanya watu zaidi ya laki moja huko Philadelphia, alieleza
kwamba, jambo kama hilo liliwahi kutokea kipindi cha nyuma Marekani na mataifa
ya Ulaya baada ya kuibuka kwa mmomonyoko wa maadili na mambo ya kiroho.
“Nadhani
wazo la Billy Graham ni sahihi, taifa hili linakuwa na watu wengi wasioamini,
na jambo hilo linavyokuwa kwa kiasi hichi giza huingia, lakini kama tukiomba,
basi nuru itaingia,” alisema.
Mwingine
ni Mwandishi wa vitabu nchini humo, Rabbi Jonathan Cahn, kwa upande wake
alieleza kwamba Mwinjilisti huyo wa kimataifa amekuwa Mchungaji kwa marais na
watu maarufu kwa miaka mingi, na hilo analolisema sasa ni onyo linalopaswa
kuangaliwa na kutendewa kazi.
“Haijalishi
ni giza la namna gani lililopo, bado lipo tumaini na wokovu pia, lakini ni pale
tutakapotubu na maombi ya watu wa Mungu, unajua akisema Marekani ina shida
tunatakiwa kutubu,” alisema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Awakening America Alliance, Billy Wilson, alisema kwa upande wake
atakusanya makanisa ya kipendekoste na Charismatic zaidi ya 300 na kwamba
wamefurahia jambo hilo lililoletwa na Billy Graham.
Tangu
mwaka 2002 mtoto wa Billy Graham, na mjukuu wake Will Graham, wamekuwa
wakifanya uinjilisti katika mataifa kama 50 ya Ulaya, Afrika, Asia, Latini na
Mashariki ya Kati na miongoni mwa makanisa yanayoshiriki ni zaidi ya 305,000 na
kwa msingi huo watu wapatao milioni 10 wameweza kumgeukia Kristo.
Imeelezwa
kwamba makusanyiko ya kusikiliza ujumbe wa Graham, yatayofanyika maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye majumba ya kupata kahawa, na maduka
yanafananishwa na mtoza ushuri nyakati za Biblia, kuwa baada ya kutubu dhambi
aliamua kuita watu na kuwarudishia kile alichokuwa akitwaa kinyume na taratibu.
Wakati
huo huo Askofu E. W. Jackson, mtaalamu wa mambo ya Maji
na sheria kutoka chuo cha Harvard, nchini Marekani, amewataka Wakristo nchini
humo, kutokichagua chama cha Democratic, katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
November, 2012 kwa kuwa kina imani potofu.
Mwandishi
Paul Stanley, wa gazeti la Kikristo nchini humo anaripoti kuwa, hivi karibuni
Askofu huyo alieleza kwamba chama cha Demokratic kinawaingiza utumwani baadhi
ya waamerika.
“Waachieni
watu wa Mungu waende,” alisema Jackson akiwaambia Wakristo kupitia mawasiliano
ya simu ni wazi kuwa Democratic ni chama cha Mpinga Kristo katika nchi hii.
Wameikataa Biblia na kile Wakristo wanachokiamini, na kuhamasisha kile
watakacho wao kinyume na maadili ya familia. Hii ni mbaya kwakuwa wanalimomonyoa
taifa na Mungu wetu,” alisema.
Askofu Jackson
alinyooshea kidole habari za hivi karibuni kutoka kwa Waliberali waliomshambulia
kwa maneno mwanamichezo wa Olympic, Gabrielle Douglas, mwenye umri wa miaka 16,
aliyeshinda medali ya dhahabu huko London 2012 na kusoma Biblia, lakini wapenzi
wa chama hicho wakamjia juu ya kuwa haikuwa sahihi.
Baada ya
ushindi wa mwanariadha huyo alisoma maandiko kwenye Warumi 12:19, yasemayo:
“Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa
kisasi ni juu yangu mimi, mimi nitalipa, anena Bwana.” Mwanadada huyo mahiri
aliazimia kumpa Mungu utukufu kwa ushindi wake,” alisema katika taarifa yake ya
kimaandishi.
No comments:
Post a Comment