Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa
kiisilamu ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo
la Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa risasi
mjini Mombasa pwani mwa Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine
kujeruhiwa katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na
mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo
ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa.
Hali
ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu
kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya
mjini Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya
leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika
mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia
maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali
kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na
polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.
Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari
lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa
za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya
umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya
kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya
Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati
za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo
alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa
anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini
Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa
risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya
Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa kujihihusisha
vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea
vikwazo vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema
kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa
vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu
la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth
Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu
na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo
alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali
hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya
kigaidi.
bbcswahili
No comments:
Post a Comment