Maeneo yaliyoonekana kuwa kivutio na kufanya watu kupiga picha katika maeneo hayo
Askofu Mkuu wa Huduma ya Kimataifa ya BCIC, Sylvester Gamanywa aliongoza kundi la Wakristo wa Tanzania kwenda nchini Israeli pamoja na mambo mengine kuiombea nchi.Akielezea safari hii Mkurugenzi Mtendaji wa Gombo, Bw. Willy Kulola alisema: “Safari yetu ya kinabii ilianzia Misri, tulifika salama na Mungu alikuwa pamoja nasi.Tukatembelea kila eneo kama lililopangwa, isipokuwa Gosheni kutokanana mabadiliko ya ratiba za ndege. Tulivuka bahari ya Shamu eneo walilovuka wana wa Israel wakiongozwa na Musa pakiwa pakavu! Maeneo yote ya Jangwa la Sinai walimoishi wana wa Israel miaka 40 wakirejea nyumbani, tulilala St. Catherine jirani kabisa na Mlima Sinai, ambapo siku iliyofuata tulifika katika kichaka cha Musa ambacho kiliwaka moto, bila kuteketea! Kipo mpaka leo na kinatoa majani ya kijani kibichi hadi sasa! Tulifika eneo la Haruni mahala ambapo wana wa Israel walitengeneza ndama na kumwabudu.
Baadhi ya team ya watu waliokwenda katika picha mmoja wao akiwa na Askofu Gammanywa |
Safari yetu ilianzia katika maeneo ya Tarbenacle, lililopo eneo la kumbukumbu ya mfano wa hema ya kukutania, hakika kila mmoja alishangazwa, na hata Askofu Mkuu Gamanywa alisikika akisema:“Nimepata picha mpya isiyoweza futika katika ufahamu wangu wa utumishi.”
Tulipita Masada, dead Sea na tukaenda Jericho, jirani kabisa na mlima wa majaribu ambao Yesu alikaa huko akiomba na kufunga kwa siku 40, na hata shetani kumjaribu. Tulilala Jerusalemu katika Hoteli nzuri,tulipata chakula kizuri sana, vyumba vizuri kiwango cha juu sana kila mmoja alikiri HAKIKA HII NI NCHI YA ASALI NA MAZIWA.
Askofu Gamanywa na Mtume Nyaga walipokuwa Israel |
Mtendaji wa Gombo Tours, Bw. Willy Kulola aliyekuwa mratibu wa safari nzima,akiwa katika kibao kinachaoonesha njia inayokwenda katika mlima ambao Yesu alijaribiwa na shetani. |
Maombi mengine ya kushtua ambayo mpaka viongozi wa Dini ya Kiyahudi naaskari wa ulinzi na Wayahudi walistaajabu ni katika ukuta wa maombi na maombolezo! (Wailing wall) Apostle Nyaga na Mchungaji Amasi walinena kwa lugha za mbinguni, kwa utukufu mkubwa sana, nguvu ya maombi na kunena iliwashukia kiasi Wayahudi walikuwa wanashangaa na kujikusanya wakiwazunguka kushangaa ni kitu gani, maana kwa kipindi kirefu haijatokea.Ilikuwa safari ya kipekee.
Baadhi ya watu aliokwenda wakiwa kwenye maombi. |
Gombo Tours – Experience The wonder of God!
gombotours@hotmail.com
SIMU: 0713 -304984; 0767 - 304984; 0717 – 798991; 0754 – 333125.
TUPO KARIAKOO ROUND A BOUT jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment