Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani |
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuacha kuwa chanzo cha migogoro
makanisani na badala yake kurudi zaidi kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza
kusudi walilopewa katika utumishi wao.
Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa miaka
hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) zilizofanyika katika
ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya Muhimbili wakati alipohudhulia kama
mgeni rasmi wa tukio hilo.
Alisema tatizo kubwa lilipo makanisani kwa hivi sasa
linasababishwa na viongozi wenyewe ambao badala ya kumtumikia Mungu wamegeuka
na kuangalia vyeo hivyo basi ni vyema kurudi kwa Bwana ili waweze kumtumikia.
“Migogoro mingi iliyopo makanisani hivi sasa matatizo
makubwa yako kwenye uongozi wala sio wanaoongozwa cha muhimu tu ni kwamba
viongozi warudi zaidi kwa Bwana wanayemtumikia” alisema Jaji Augustino
Ramadhani.
Sherehe hizo
zilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Jaji Angera Kileo, Askofu Philemon Tibanenason,
Mweka Hazina wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Donata Mugassa pamoja na viongozi wa
shirika hilo, Mwenyekiti Dk. Edda Mwandi aliyekuwa mwenyeji wa sherehe hizo
pamoja na Katibu Rev. Emaus Bandikile.
No comments:
Post a Comment