Kwa mwimbaji yeyote wa nyimbo za Injili anayehusika...
PRESS RELEASE:
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii
toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na
Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu
za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya
simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati
yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama
wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya
simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya sisi Wasanii
kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza
maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za
mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa
katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya
simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya
mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya
tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote
zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao
husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku
saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo
yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio ,
blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo
tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa
ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha
uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.
No comments:
Post a Comment