Hayo yalisemwa hivi karibuni na Wakili Magdalena Rwebangira wakati akitoa semina juu ya kanisa na Katiba, iliyofanyika katika kanisa la City Harvesty lililopo Garage, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumuwezesha mkristo kutambua umuhimu wa katiba na jinsi ya kusimama kudai haki yake.
Wakiri huyo alisema kuwa kanisa lazima liitumie katiba katika kudai haki na sii kukaa kimya huku wakristo wakibaki kulalamika pindi linapotokea tatizo lolote, linalohusu masuala ya kanisa na kusema kuwa huko ni kushindwa kutafuta haki yao ya msingi kwa masilahi ya kanisa na taifa kwa ujumla.
Wakili Magdalena Rwebangira |
Aliongeza kuwa lazima maoni ya uhuru wa kuabudu katika katiba ijayo uzingatiwe, kutoingiliwa kwa namna yoyote katika ibada zinazo fanyika, kutoangalia masuala ya kidini ikiwa ni pamoja na kanisa kupewa nafasi ya kutosha katika kumhubiri Kristo wa kweli, huku akisema kuwa nchi iko mikononi mwa kanisa.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kutoa elimu juu ya mambo ya Katiba Dk.Paul Shemsanga, ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Victory Gospel Assembly Tanzania aliyepata nafasi ya kutoa elimu siku hiyo alisema kuwa ni wakati wa kanisa kutambua nafasi yake na kuitumia ipasavyo na wala si kubaki likilalamika.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la City HarvestYared Dondo |
Askofu huyo alisema kuwa umefika wakati kanisa kutokaa kimya, na badala yake kusimama kidete katika maeneo yote, kwa lengo la kuleta ukombozi ndani ya taifa la Tanzania na kukomesha migogoro inayojitokeza.
“Lazima katika Katiba, kanisa lishiriki sana, lazima tuzungumzie uchumi, umiliki wa ardhi, kutokubali ushawishi kutoka nchi za nje ikiwa ni pamoja na masuala ya kuabudu kutoingiliwa” alisema Askofu huyo.
Aidha akikazia zaidi Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo la City Harvest, Architecture Yared Dondo, ambao kuanzia siku chache zilizopita wameanza kufanya ibada zao katika kanisa lao jipya lililopo Garage jijini hapa, alisema kuwa ni lazima kanisa kuwa makini na suala la Katiba ili mambo yanapoharibika badaye kanisa lisiweze kulalamika.
“Lazima Kanisa kuwa makini na kutopuuza suala hili la Katiba ni muhimu sana, ili badaye tusije tukawa watu wa kulaumu, kama hatutasimama kama wakristo, ambao tuna dhamana kubwa juu ya nchi hii,” alisema Mchungaji huyo.
No comments:
Post a Comment