Tunampa Mungu utukufu wote kwa Ushuhuda wa uponyaji wa UKIMWI jinsi
alivyodhihirisha nguvu za uponyaji wake, pia kutuwezesha kushuhudia zaidi ya
watu 50 wakiponywa UKIMWI katika huduma yetu. Nina imani kwamba shuhuda hizi
zitaweza kusaidia kuinua imani, ya wale wanaomwamini Mungu kwa ajili ya
uponyaji wa magonjwa yasiyo na tiba kama
UKIMWI na kutoa changamoto kwa watumishi wa Mungu kuwasaidia wagonjwa kupokea
uponyaji wao kwa kuhubiri Neno la imani na uponyaji.
Neema
aliponywa na ugonjwa ambao kwa madaktari hauna dawa wala tiba yaani UKIMWI
Agosti 2012 kwa msaada wa mafundisho ya uponyaji aliyoyapata kwa Mchungaji
Prosper Ntepa mwaka 2006 hadi 2008 baada ya kuishi na virusi vya UKIMWI kwa
takribani miaka sita. Wakati watu wengi wamekata tamaa kwa sababu ya taarifa ya
madaktari inayosema UKIMWI hauna dawa wala tiba kuna dawa imegunduliwa katika
maabara za kiroho na kitabu kinachoitwa Biblia ambayo inaanza kumponya mgonjwa
kuanzia katika mizizi ya roho yake na kufisha vidudu vya UKIMWI. Mafundisho ya
ugunduzi wa dawa hii kiboko yameonekana kuleta matokeo katika huduma ya
mchungaji Prosper Ntepa, ambapo kuna taarifa zinazosema watu zaidi 50 wameponywa
UKIMWI kwa uthibitisho wa madaktari. Dada Neema ni mojawapo wa watu waliopata
neema ya kuponywa kwa njia ya imani katika dawa ya Neno la Mungu ambayo
imethibitika kuleta matokeo ya ajabu kwa wale wanaoiamini na kuimeza kwa
umakini na kufuata masharti yake.
Mchungaji Prosper Ntepa wa The Oasis of Healing Ministries |
Sauti
ya mawazo ya kutokuamini inaanza kumpa taarifa mtu kwamba hana haja ya
kumwamini Mungu kwa ajili ya uponyaji au muujiza wake. Hatimaye anatawaliwa na
mawazo ya kufa zaidi kuliko kupona na kuishi.
Dada
Neema alizaliwa Itigi akiwa mtoto wa pili katika familia ya watoto wawili. Baba
na mama ni Waislamu. Alioana na mume wake wa sasa Novemba 2003. Wamejaliwa
kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Abighail katika ndoa yao ambaye alizaliwa tarehe 27 Mei 2009. Abighail alizaliwa wakati mama yake akiwa
ameathirika na UKIMWI. Wakati wanaoana hawakupima afya kwa habari ya UKIMWI.
Je, uliambukizwaje virusi vya UKIMWI?
Ninashindwa kuelewa jinsi nilivyopata
maambukizo ya UKIMWI. Niliwahi kuolewa na kuachika kabla ya kukutana na mume
wangu wa sasa. Mume wangu wa sasa alifiwa na mke wake kwanza. Tumeshindwa kujua
kwamba tatizo la maambukizo lilitoka kwangu au kwa mume wangu. Taarifa
nilizozipata ni kwamba mke wa kwanza wa mume wangu alifariki Machi 2003 kwa
ugonjwa wa maralia na kuchanganyikiwa. Tatizo ni kwamba hatukupima afya zetu
wakati tunaingia katika ndoa.
Je
ulijuaje kama umeathirika na virusi vya
UKIMWI?
Mwishoni mwa 2006 nilipima katika hospitali ya
Amana na kukutwa na virusi vya UKIMWI. Baadaye nikapima tena sehemu nyingine
mbili ambako walithibitisha pia kwamba nimeathirika na UKIMWI. Vile vile mume
wangu alipimwa na kukutwa kwamba alikuwa naye ana virusi vya UKIMWI.
Je,
ulikuwa na dalili gani za magonjwa nyemelezi?
Nilikuwa na dalili nyingi za magonjwa
nyemelezi ya UKIMWI. Dalili hizi ni pamoja na homa za mara kwa mara, malaria,
kuwashwa sehemu za siri na kuvimba mwili. Pamoja na mwili wangu kubadilika
rangi ya weupe na kuwa mweusi kama mkaa
nikajikuta nikawa na vidonda mdomoni kiasi cha kuanza kutoa harufu. Kuna wakati
ambao niliumwa sana
na kusababisha kupungukiwa na damu kiasi cha kufikia tatu nukta nne. Pia
nikapata mkanda wa jeshi kwa muda wa miezi mitatu ambao ulinitesa sana.
Uliokoka
lini?
Nilikuwa
mwislamu kwa sababu baba na mama ni
waislamu. Nilikuwa nina tabia ya kupenda kusikiliza kanda za nyimbo za
Kikristo. Niliokoka Julai 2003 kupitia vipindi vya Neno la Mungu kupitia redio
za Kikristo za hapa Dar es Salaam.
Baada ya kuokoka nilisali makanisa mbalimbali ya Kipentekoste. Kuna wakati
nilianza kusali katika kanisa la Full Gospel Bible Fellowship la Mwenge, ambako
sikukaa zaidi ya mwezi mmoja. Baada ya kuokoka nilibatizwa kwa maji mengi
katika kanisa la Askofu Sylvester Gamanywa. Mume wangu aliponywa ugonjwa sugu
wa fangasi iliyomsumbua kwa miaka takribani miaka kumi na nne. Baadaye mimi na
mume wangu tulihamia katika kanisa la The Oasis of Healing Ministries, baada ya
kusikia mafundisho kupitia Praise Power Radio. Tulijiunga na huduma hii kuanzia
mwishoni mwa 2006. Tulipokuja katika ukumbi wa Mhasibu house tulisikia ushuhuda
wa dada Hellen ambaye aliponywa UKIMWI katika wiki ya kwanza aliyokuja katika
maombezi wakati ni mjamzito kabla ya kuolewa. Tulisikia shuhuda za watu wengine
ambao pia walikuwa wameponywa UKIMWI katika huduma ya mchungaji Prosper Ntepa.
Matokeo yake tulitiwa moyo sana.
Je,
ulipima mara ngapi kuthibitisha kwamba una virusi vya UKIMWI?
Nilipima
mara tatu kuthibitisha kwamba nina maambukizo ya UKIMWI. Mara ya tatu nilipima
katika kituo katika afya kilichoko Mbagala.
Je,
uliponywaje ugonjwa wa UKIMWI? Ni vitu gani vilikusaidia kupokea uponyaji wa
UKIMWI?
Nilikuwa mshirika katika kanisa The Oasis of
Healing Ministries kuanzia mwishoni mwaka 2006 mpaka mwishoni mwa 2008. Baada
ya hapo tukawa tumehamia Sanya Juu, Kilimanjaro. Kuna mchungaji mmoja ambaye
alikuja kufungua kanisa Sanya Juu tukaongozwa kushirikiana naye katika kazi ya
Mungu. Kama shukrani kwa Mungu kwa yale ambayo
Mungu alitufanyia mume wangu aliamua kutoa sehemu ya kiwanja chake cha urithi
kwa ajili ya kujenga kanisa pale Sanya Juu. Nilipata uja uzito mwishoni 2008.
Tulipata mtoto wa kike ambaye tulimpa jina la Abighail ambaye alizaliwa kabla
ya muda wake tarehe 27 Mei 2009 akiwa na miezi saba. Mwaka 2008 nikiwa na mimba
nilipimwa damu na kugundulika kuwa bado nilikuwa ninaishi na virusi vya UKIMWI.
Lakini bado sikukata tamaa katika imani. Niliendelea kumwamini Mungu na Neno lake bila
kutetereka. Hatimaye uponyaji wangu ulikuja kuthibitika Agosti 2012 baada ya
kuvumilia na kusimama katika Neno la Mungu kwa takribani miaka mitano na nusu.
Uponyaji wangu ulikuja kugundulika wakati nilipoumwa sana malaria nikalazimika kulazwa katika
hospitali ya Kibongoto. Madaktari wakanishauri nilipokuwa ninatibiwa malaria
nipime pia damu kuangalia kama bado nina
UKIMWI. Baada ya madaktari kunipima damu wakashangaa kugundua kuwa nilikuwa
sina maambikizo ya UKIMWI. Jambo hili liliwapa mshangao mkubwa kwa sababu
walikuwa wamewahi kunipima na kunikuta na maambukizo ya UKIMWI. Huko nyuma
wakati nilipokuwa na dalili nyemelezi za UKIMWI madaktari walikuwa wamenipima
mara kadha na kunikuta nina virusi vya UKIMWI. Kwa maneno mengine, baadhi ya
madaktari walikuwa wanajua kwamba nilikuwa nimeathirika na virusi vya UKIMWI. Madaktari
hao walishangaa sana kunikuta nikiwa na majibu
tofauti na matarajio yao
ya awali. Wakaanza kunihoji maswali kwamba imekuwaje hali yangu imebadilika
ghafla hivi na kutokuwa na virusi vya UKIMWI. Nikawajibu kwamba Bwana Yesu
ameniponya na UKIMWI. Nikawapa ushuhuda jinsi nilivyoishi katika imani ya
kulitegemea Neno la Mungu. Nikawasimulia jinsi nilivyokuwa ninakiri au
kutamka mistari ya uponyaji mara kwa
mara. Nikawashauri kwamba kama wana mashaka na
jambo hili basi wawasiliane na Mchungaji Prosper Ntepa kanisa la The Oasis of
Healing Ministries, Ubungo ili wapate ushahidi zaidi wa uponyaji wa UKIMWI.
Matokeo
yake madaktari wale wakarudi tena kunipima kipimo cha CD4 yaani
kiwango cha kinga yangu. Baada ya kunipima walishtuka kugundua kuwa CD4 au
kiwango cha kinga za mwili wangu zikiwa zimeongezeka sana yaani kiwango cha mtu ambaye hana virusi
vya UKIMWI. Kiwango cha kinga zangu zilipanda sana tofauti na kiwango cha awali wakati
nikiwa ninaishi na virusi vya UKIMWI. Pia waliporudia kunipima kipimo cha
kubainisha kama nimeathirika na UKIMWI au sina
maambukizo ya UKIMWI. Wakapima tena damu na kukuta sina maambukizo ya UKIMWI
yaani HIV negative. Kwa hiyo madaktari walinipima mara tatu yaani vipimo viwili
vilivyoonyesha sina UKIMWI au HIV Negative na kipimo kingine cha kupima CD4.
Magonjwa nyemelezi
yalipungua baada ya kujifungua mtoto wangu Abighail kuanzia 2009. Niliacha
kutumia dawa za kurefusha maisha kuanzia Juni 2009. Badala yake nilikuwa
ninatumia dawa ya Neno la Mungu yaani kuzitamka ahadi na kweli za uponyaji.
Nilisimama katika ahadi na kweli za uponyaji mbalimbali ambazo zilinisaidia
kuniimarisha kiimani. Baadhi ya mistari niliyokuwa ninaisimamia kwa njia ya
kuikiri na kuitamka ni hii ifuatayo: Niliamini kwamba Mungu analitumia Neno kama dawa ya kuniponya mimi. Zaburi 107:20, “Hulituma
neno lake, huwaponya, huwatoa katika maangamizo yao.” 1 Petro 2:24, “Yeye
mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa
mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.”
Nilikuwa nanakiri kwamba kwa kupigwa Yesu nimepona na niko huru na UKIMWI.
Mathayo 8:17, “Ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya,
akisema, mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa yetu.”
Katika Mathayo 8:17 nilikuwa ninakiri kwamba Yesu alitwaa udhaifu wangu na
kuyachukua magonjwa yangu. Kutoka 15:26, “Akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii
sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega
masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako
maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.”
Yohana 10:10, “Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.” Nilimtambua Ibilisi kama mwizi wa afya yangu lakini
Yesu alikuja ili niwe na uzima na niwe nao tele. Nilianza kuamini katika hali
ya kutokufa kabla ya wakati wangu. Ayubu 5:26 ilinitia moyo, “Utafika
kaburini mwenye umri mtimilifu, kama mganda wa
ngano ulivyo wakati wake.”
Katika mchakato huu wa kulipanda Neno la Mungu
kama dawa kwa ajili ya uponyaji nilifikia
hatua ya kukariri mistari mingi. Mimi na mume wangu tuligundua kwamba Neno
likiwa katika Biblia ni Andiko lakini linapokuwa ndani ya roho yako linakuwa
Neno lililo hai. Biblia inasema katika 2 Wakorintho 3:6, “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa
wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua,
bali roho huhuisha.” (Kwa maneno mengine, walitofautisha logos yaani
Neno la Mungu la jumla lisemwalo na rhema yaani Neno la Mungu maalum au la
ufunuo linasema kitu sasa. Watu wengine wanashindwa kujenga imani ya uponyaji
pamoja na ukweli kwamba wanalijua Neno kwa akili zao lakini hajafikia hatua ya
kuwa na Neno lililofunuliwa katika roho zao)
Unamshauri
nini mtu anayemwamini Mungu kwa ajili ya uponyaji wa UKIMWI na unaonekana
kuchelewa?
Ningependa
kushauri mambo matatu yafuatayo. Kwanza,
ninashauri wazingatie kumkubali na kumwishia Mungu. Pili, ninawashauri
walikubali na kulitafuta Neno kwa bidii. Tatu, ninashauri wasikate tamaa katika
kumwamini Mungu. Waendelee kukiri mistari ya uponyaji hadi uponyaji wao
utakapodhihirika. Nina imani wataweza kupona kama
mimi nilivyopona.
Je, ulikutana na hali zozote za kukatisha tamaa?
Ni
kweli nilikutana na hali za kukatisha tamaa katika mchakato wa kufikia kupokea
uponyaji wangu. Halikuwa jambo rahisi kuendelea kumwamini Mungu. Sikuwa na roho
ya kuogopa kufa. Nilikuwa ninasikia sauti ndani yangu inayosema, “Unasimama
katika Neno la Mungu lakini hakuna mabadiliko yoyote katika mwili wako. Unaomba
kila siku hupati uponyaji wako. Wewe utaishia kufa tu. Huwezi kupona UKIMWI.”
Nikawa ninakataa kukubaliana na maneno haya kutoka kwa adui shetani. Nilikuwa
ninaipinga sauti hiyo kwa jina la Yesu.
Kwa
upande mwingine nilikuwa ninasikia sauti inayosema “Umekwisha kupona UKIMWI. Wewe ni
mzima.” Sauti ya adui ilikuwa inanihubiri kwamba nitakufa wakati sauti
ya Mungu ilikuwa inanithibitishia kuhusu kupona. Nikaamua kuifuata sauti chanya
iliyosema kwamba nimepona. Mwishowe nikaanza kujiona na kukubaliana juu ya
uponyaji wangu. Nikaanza kumshukuru Mungu kwa ajili ya uponyaji wangu. Nikawa
ninasema, “Asante
Yesu Kristo kwa kuniponya UKIMWI. Asante Yesu Kristo kwa sababu wewe
ni mponyaji wangu.” Kwa maneno mengine niliacha kukazana kuomba dua za
Mungu kuniponya UKIMWI na kuanza kumshukuru Mungu kwa ajili ya uponyaji wangu
kana kwamba tayari ulikuwa umefanyika halisi.
Je,
kuna mtu yeyote aliyeponywa UKIMWI ambaye alikutia moyo katika kumwamini Mungu?
Michael
aliyeponywa na UKIMWI 2006 baada ya kuishi na UKIMWI kwa miaka mitano alitutia sana moyo mimi na mume
wangu. Niliposikia ushuhuda wa kuponywa kwake virusi vya UKIMWI nilifarijika sana kwamba kwa Mungu
hakuna ugonjwa usioweza kutibika. Kuna wakati Michael alikuja nyumbani kumwona
mume wangu wakati anaumwa.
Una washauri nini watu wanaotaka kupokea
uponyaji wa UKIMWI?
Ninataka kushauri mambo manne yafuatayo: Kwanza, ninawashauri wanaotaka kupokea uponyaji wa UKIMWI
waishi maisha matakatifu. Kuishi katika dhambi kama
za uzinzi kunaweza kumzuia mtu kupokea uponyaji wake. Pili, usiwe na shauku
kwamba ukipona ugonjwa wa UKIMWI utajitoa kufanya maovu. Ninashauri mtu
atengeneze shauku ya kumtumikia na kumwishia Mungu. Tatu, ninashauri mtu
anayetaka kuponywa UKIMWI akatae kuathirika kwa ufahamu au mawazo yake. Unaweza
kuathirika na UKIMWI lakini ukakataa kuathirika kimawazo kwa njia ya kuwa
mtazamo chanya. Mungu anaweza kufanya njia pasipo na njia. Asikubali sauti ya
milango mitano ya maarifa inayotumia kuona, kusikia, kuonja, kugusa na kushika.
Ni jambo la muhimu kuipinga sauti ya shetani inayowasiliana katika mawazo yako.
Nne, ni muhimu kujifunza kunukuu na kukiri Neno linavyosema katika hali ya
ugonjwa wako kwa kulitamka. Nina ushahidi wa Neno la Mungu linavyosema. Yeremia
33:6, “Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami
nitawafunulia wingi wa amani na kweli.”
Je,
kuna mtu yeyote ambaye ameponywa UKIMWI kwa msaada wako?
Tulipokuwa
Sanya Juu, Kilimanjaro mume wangu alianza kufundisha Neno la Mungu katika
kanisa moja na kufanya huduma ya kuombea wagonjwa. Watu walianza kuja kuombewa
magonjwa mbalimbali na wakawa wanapona. Mimi na mume wangu tulimsaidia mama
mmoja ambaye yeye na mume wake walikuwa wameathirika na UKIMWI. Huyu mama
alianza kusikiliza mafundisho ya Neno la Mungu, ambayo mume wangu alikuwa
anafundisha. Ilikuwa ni Oktoba 2012. Tulimfundisha kukiri mistari ya uponyaji
ambayo tulijifunza kwa Mchungaji Prosper Ntepa. Huyu mama alikuwa amepima mara
nne kwamba ana virusi vya UKIMWI. Wakampima na kukuta hana virusi vya UKIMWI.
Mama huyu aliambiwa arudi tena Januari 2013 baada ya miezi mitatu.
Mungu ni muweza ya yote
ReplyDeleteMungu hashindwi na jambo, ushuhuda huu unanipa nguvu ya kwenda mbele za Mungu kudai uponyaji wangu pia
ReplyDelete