Katika kile kilichokuwa kinasubiliwa kwa muda sasa
kimeeleweka,ni Kardinali Jorge Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuongoza
Kanisa Katoliki Duniani, akiwa ni wa kwanza kutoka barani Amerika na wa kwanza
kutoka nje ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,000.
Baada ya kuchaguliwa na makardinali wenzake 115, Kardinali
Jorge Bergoglio (76) alichagua kufahamika kwa jina la Francis I.
Maelfu ya mahujaji, watalii na waumini wa Kanisa Katoliki
waliokuwa wamejazana katika Viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican
kushuhudia moshi mweupe uliofuka saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
kuashiria kuchaguliwa kwake, waliripuka kwa shangwe, nderemo na vifijo.
Papa Francis I kiongozi mpya wa Kanisa la Romani Duniani |
Papa Francis I alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanawania
nafasi hiyo na papa anayeondoka, Benedict XVI mwaka 2005, ambapo aliripotiwa
kuibuka wa pili.
Kabla ya kuchaguliwa kwake, Papa Francis I ambaye kwa
wadhifa wake pia anakwenda kuwa Askofu wa Roma, alikuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la
Buenos Aires,
Argentine na kwa muda wote wa utumishi wa utumishi alikuwa huko huko nyumbani.
Anakuwa Papa wa 266 kuwahi kuongoza kanisa hilo lenye waumini zaidi ya bilioni 1.2
duniani.
Baada ya kutangazwa kwake, Papa Francis I alijitokeza kuzungumza kwa mara ya kwanza kama
Askofu wa Roma.
Akiwa amechaguliwa katika awamu ya tano ya upigaji kura,
inaelezwa kuwa alikuwa miongoni mwa mapapa waliochaguliwa kwa haraka baada ya
muda mrefu, akiwa sawa na Benedict XVI (2005) na Pius XII aliyechaguliwa mwaka
1939.
Mshindi alitakiwa kupata kuta 77 au robo tatu ya makardinali
115 walioshiriki uchaguzi huo.
Papa Francis I anachukua nafasi iliyoachwa na Papa Benedict
XVI aliyejiuzulu Februari 28, mwaka huu, ikiwa
ni miaka 600 tangu Papa wa mwisho kujiuzulu.
Papa Francis I, ni Papa wa kwanza kutoka Shirika la Jesuit
ambaye ametumia muda wake mwingi wa utumishi nyumbani Argentina.
Anafahamika kwa utumishi uliotukuka kwa uangalizi wa kanisa
na mapadri, mambo ambayo yanatajwa kuwa sifa kubwa ya kuchaguliwa kuwa Papa.
Papa huyo amedumu katika maisha ya kufundisha na kuongoza
mapadri. Amefanya kazi Amerika ya Kusini ambako kuna Wakatoliki wengi.
Kardinali Bergoglio anatambulika kwa kutamadunisha Kanisa la Argentina,
lililokuwa miongoni mwa makanisa ya kihafidhina huko Amerika Kusini.
Amechagua jina la Papa Francis I, chini ya uangalizi wa
Mtakatifu Francis wa Assisi.
Alizaliwa Buenos Aires katika familia ya mfanyakazi wa reli.
Alipata upadrisho mwaka 1969.
Aprili 15, 2005, mwanasheria wa haki za binadamu
alimfungulia mashtaka ya jinai kwa
kushirikiana na maofisa wa jeshi kuwateka mapadri wawili wa Jesuit mwaka 1976,
akiwa kiongozi wao aliwafukuza katika utumishi kutokana na migogoro katika
jumuiya hiyo.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment