Katika Kuelekea Event ya Aflewo
Tanzania 2013,Siku ya jana ilikuwa Bishops Breakfast Forum katika Hotel ya
Regency Park Mikocheni,ikiwa ni katika kuwashirikisha Maaskofu na Mtume wa
huduma mbalimbali maono na maana ya kuwepo kwa Aflewo Tanzania mwaka
2013.
Mnamo terehe 5-5-2013 BCIC Mbezi
Beach itakuwa ni usiku wa
aina yake katika Kumsifu na Kumwabudu Mungu ambapo Aflewo Mass Choir yenye
waimbaji zaidi ya 90 watapaza sauti zao wakiimba sifa kwa Mungu.
Katika Bishops Breakfast hiyo iliyoudhuliwa
na baadhi ya Maaskofu kama Apostle Ntepa,Bishop Fredie
Kyara, Bishop Elly Mwende,Bishop Simtovu,Bishop Mwasota, Bishop Shegga, Pastor
Fredie (UpperRoom Minisry )Bishop Gamanywa alitoa hudhuru kwa Kuwalilishwa na
Pastor Amoni Kalahilo na wengine wengi na kusifu Aflewo kuweza kuwa kutanisha
na wao kama Maaskofu katika Jiji la Dar es salaam kuwashirikisha Maono ya
Aflweo Tanzania na kusifu juhudi zinafanywa maana ni katika Kuujenga mwili wa
Kristo na kulileta pamoja Kanisa la Tanzania na Afrika Kwa Ujumla.
Pastor Paul Safari na Abel Orgenes
Kama walezi wa huduma ya Aflewo Tanzania,wakieleza umuhimu wa huduma hiyo kwa
waimbaji ni pamoja na kukua kwa maisha ya kiroho kati ya waimbaji na Mungu
maana tofauti na uimbaji pia kuna mafundisho kuhusu Maisha ya wokovu na Maana
ya Kufisu na Kuabudu kwa ujumla
Pastor Fredie Kyara aliweza kutoa
ushuhuda wa jinsi Mkesha huo ulivyo wa baraka sana kwa kusema jinsi ilivyoweza
kukutana na uwepo wa Mungu kwa Mkesha uliopita mwaka 2012,na kusihi Maaskofu
wengine kukubali na kuunga mkono huduma hii ya Aflewo kwa kuwa ruhusu waumini
wao makanisani kuhusika kikamilifu.
Kwa kumalizia Maaskofu hao walipata
nafasi ya kuchangia na kusema kuwa wanakubaliana kwa nia moja na kusema wako
tayari kushiriki kwa namna moja au nyingine kuhakikisha mkesha wa Aflewo
Tanzania 2013 unafanikiwa.
Pastor Pastor Paul Safari mmoja wa mlezi wa huduma ya Aflewo akizunghumza mbele ya akizungumza na Maaskofu. |
Mlezi wa huduma ya Aflewo Pastor Abel Orgenes |
Bishop Elly Mwende kutoka makanisa ya PAG Dar es salam akitoa mchango wake katika Breakfast |
wakwanza kulia ni Aflewo Music Director Samweli Mwangati,akifuatiwa na Bishop Mwasota,Aflewo Event Manager Mc Antony Luvanda na Mwenyekeiti wa Aflewo Tanzania Geofrey Obiro akizungumza na Maaskofu. |
Ndani ya ukumbi kama unavyoonekana Mwenyekeiti wa Aflewo Tanzania kwa mbali Geofrey Obiro akizungumza na Maaskofu. |
Maaskofu wakijadiliana mara baada ya kumalizika wa Breakfast kwa mbali Bishop Shegga akizungumza na Maaskofu wenzake kwa kubadilishana mawazo. |
No comments:
Post a Comment