Nabii Malisa akimuhoji Mwanamama aliyekuwa amekuja na Mgongo Ya Kutembelea katika Semina Hiyo.
Gazeti la Nyakati pekee ndilo lililokuwa limetoa tangazo kwa ajili ya
kuwaalika Watu katika Mkutano Huo Mkubwa iliofanyika katika Ukumbi wa
PTA.
Nabii Malisa ambaye hana tawi lolote katika Jiji la Dar-es-Salaam lakini aliweza wakusanya Watu kuhudhuria katika Mkutano huo.
Kati ya Mambo yaliyoleta Utata katika Mkutano wa Nabii Malisa ni kitendo
cha kualika watu ambao kwenda Kusafisha nyota zao zilizofifia. Blog
ilimuuliza Mmoja wa viongozi wa kanisa moja kwanini hawakumpa
ushirikiano Nabii Malisa alisema "Kwa watumishi wa Dar-es-Salaam
tunafahamiana, huyu kijana Mwanza kwenyewe bado kuna utata wa huduma
yake, kuingia kichwa kichwa kushirikiana nae pasipo kujua foundation
teachings zake unaweza kuta unapoteza watu bure"
Umati Wa Watu Waliohudhuria Semina Ya Nabii Malisa Katika Ukumbi wa PTA
Katika Siku 3 hizo wagonjwa kutoka hospitali mbalimbali katika Jiji la
Dar-es-Salaama walipelekwa katika Ukumbi huo na kufunguliwa kwa uweza wa
Nguvu za Mungu.
Akifundisha kuhusu nidhamu ya Pesa, Nabii Malisa alisema Watu wengi
wamekuwa na nidhamu ya Pesa wakiwa hawana Pesa ama Zinapokuwa
zimepungua, aliuliza watu waliohudhuria ni nani aliyewahi kuwa na
nidhamu ya Pesa alipokuwa kwenye Neema, na watu walishindwa kutoa
majibu. Nabii Malisa amemaliza Siku 3 za Kinabii siku ya tarehe 6 May,
2012 Katika Jiji la Dar-es-Salaam.
No comments:
Post a Comment