Wabunge 400 wapiga kura kumkataa Mungu..!

Majira ya saa moja jioni, Januari 5, mwaka  huu, jumla ya wabunge 575, walipiga kura kuamua kumpendeza Mungu au shetani,  400 miongoni mwao wakamchagua shetani na 175 tu waliosalia wakamng’ang’ania Mungu na maadili yake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Life Sitenews.com wale waliosalia na msimamo wa kupiga kura kuharibiwa kwa maadili ya mwanadamu na sheria za Mungu, wameapa kutokaa chini, watapambana hadi mwisho ufike.

Mbunge wa eneo la Tory, Roger Gale, aliwashutumu wale wanaounga mkono hoja hiyo akisisitiza kuwa hawana msingi wa hoja yao badala ya kushikilia dai la usawa.

“Ni vigumu sana kutafsiri dhana ya ndoa, huu ni Muungano wa mwanamume na mwanamke wenye historia ndefu sana, na kamwe serikali haiwezi kutafsiri na kuirekebisha ili kukidhi matakwa yao na tama zao,” alisema Gale.

Lakini wakati hayo yakiendelea, mbunge mwingine aliliambia  Gazeti la The Sun kuwa Waziri Comeron anashutumiwa tu kwa kutoa mdomoni mwake tamko ambalo ni mpango wa Jumuiya ya Ulaya.

“Nawaambia ukweli kuwa ifikapo katikati ya mwaka huu sheria ya kuunga mkono ndoa za mashoga itatolewa na kuwa amri kwa wanachama wote na baadaye kuenea katika ulimwengu wote,” alisema na kuongeza:

“Utaratibu wa siri uliofanywa na kamati maalumu ya Jumuiya ya Ulaya utalazimisha mataifa yote duniani kubadili sheria zao za ndoa ili ziendane na sheria ya haki za kiutu zinazokubaliana na haki za usawa kibinadamu. Kura ya kupitisha azimio hilo itapigwa Novemba mwaka huu katika Bunge la Ulaya.”

Askofu wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika aikosoa tume iliyotangazwa na Waziri Mkuu

Askofu wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha wanafunzi wa kidato cha nne kushindwa kufaulu mitihani si dawa ya kutatua tatizo la elimu nchini.

Akizungumza na chanzo kimoja cha habari ofisini kwake juzi, aliongeza kuwa kitendo cha wanafunzi kufeli ni hatua mbaya zaidi kwa serikali na kutengeneza taifa la watu ambao hawajui la kufanya hapo baadaye.

Alisema makosa hayo si ya waalimu bali ni ya serikali, kwani imekuwa ikipuuzia maoni ya wadau wa elimu na waalimu ambao huishauri serikali kwa nia njema ya maendeleo.

Alisema tume zinazoundwa na serikali mara nyingi hazina majibu ya kuridhisha na badala yake hutumia fedha nyingi za walipa kodi bila kupatiwa faida wala majibu ya kina.

Askofu Kanyika alisema kuundwa kwa tume kulikotangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hakuwezi kutoa majibu sahihi ya tatizo lililopo.

Akizungumzia masuala ya udini ambao unaonekana kushamili kwa kasi, Askofu Kanyika alisema vuguvugu hizo ni mbegu ya serikali kwani mara kwa mara walikuwa wakieneza chachu ya udini kama sehemu ya propaganda za kisiasa.

Source  http://www.freemedia.co.tz

Rev.Edward Amri asherehekea miaka 25 ya ndoa yake.

Siku kadhaa zimepita Rev. Edward Amri aliandaa  Jubilei ya miaka 25, ya ndoa yake na tukio hilo lilikuwa kielelezo cha jinsi wanandoa wanavyopaswa kuishi. Kwa maneno na matendo. Mbele ya hadhila, kiongozi huyo alikuwa kielelezo cha upendo wa Agape unaofaa kuigwa na wale waliompokea Yesu Kristo kuwa BWANA  na mwokozi wa maisha yao.

Umati mkubwa uliohudhuria Jubilei hiyo, iliyofanyika katika kanisa la AKUZAMU lililopo katika Jengo la IPS Gorofa ya pili, ambapo alipata wasaa wa kutamka Neno la Upendo na baadaye hafla fupi iliyofanyika Hoteli ya Serena iliyopo katikati ya jiji la Dar es salaam.
Rev. Rev.Edward Amri na Mke wake Mama Mchungaji Mary Amri waki furahi kwa kuitazama pete ya ndoa.
Akijawa na furaha  kiongozi huyo alisema: “Nimeamua kuonyesha kwa vitendo mbele ya Mungu na uma wa watu pale nilipotoa upya tamko langu la upendo kwa mke wangu, mpenzi  Mary Amri kuwa ‘NAKUPENDA MKE WANGU KAMA KRISTO ANAVYOLIPENDA KANISA LAKE.’
Pendo la kweli lililotoka ndani kabisa ya moyo wangu!

Itakumbukwa  kuwa somo la upendo wa Mungu ndio msingi halisi wa maono ya huduma yetu ya AKUZAMU nasi tukiwa tunalifundisha, tunahubiri na kutenda upendo wa Mungu, hii ni fursa ya pekee kwangu kudhihirisha upendo nyumbani kwangu kwanza, kama Neno la Bwana linavyosema:
“Kila mume anapaswa kumpenda mke wake kama Kristo anavyolipenda kanisa lake,” ( Waef 5:23).
 Rev. Rev.Edward Amri na Mke wake Mama Mchungaji Mary Amri katika pozi















Karibu  AKUZAMU tushirikiane Neno na Tendo kwa upendo wa BWANA wetu Yesu Kristo.
  



















Kwa maombezi piga: 0753-377776, 0782-377776, 0659-377776
Barua Pepe: info@akuzamu.org
Rev.Amri@facebook/twitter.com
Tovuti: www.akuzamu.org

Semina ya Neno la Mungu na Mwl.Christopher Mwakasege.


Mh.Dr Harisoni Mwakyembe amelitaka Kanisa kuhubiri Amani Nchini, ndani ya Living Water Center Ministy


Mh.Dr Harisoni Mwakyembe asema Amani izidi kuhubiriwa makanisani na kudumishwa Nchini,Maana inaisaidia Serikali katika kuhamasisha Amani na Upendo,nakuongeza kuwa Serikali inatambua na kuheshimu mchango wa Kanisa katika kutetea Amani na Upendo Nchi.

Hayo yamesemwa katika Kanisa la Living Water Center Ministry Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi lililopo Kawe siku ya jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kanisani hapo katika Ibada ya asubuhi ambapo alikuwa amearikwa kama mgeni rasmi katika shughuli ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo la Living Water Center ambapo hakuja peke yake aliweza kuambatana na mke wake pia na Mbunge mwenzake Mh.Victor Mwamalaswa katika harambee hiyo.

Apostle Onesmo Ndegi ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo,akisisitiza suala la Amani na Upendo na kuitaka Serikali kutambua mchango wa Kanisa katika Suala zima la Amani na Upendo Nchini.
Pia aliongeza kwa kusema Watanzania sote ni wamoja tunapaswa kuachana na itikadi za Udini,Ukabira na Uchama baadala yake Kuangalia suala la Amani na Upendo kutufanya kuwa kitu kimoja.

Akaulizwa na waandishi wa habari anazungumziaje suala la vurugu za Zanzibar akasema anaitaka Serikali kuwa makini katika ufuatiliaji wa jambo hilo na wahusika wote watiwe chini ya vyombo vya sheria,hata kama inasemekana kuwa ni wahuni wanaofanya hiyo kama inavyodaiwa basi wakamatwe na kufikishwa mahakamani, akamalizia kwa kusema yote yanayo fanyika kisasi ni juu ya Bwana.

Akamalizia kwa kusema katika Serikali kuna ulegevu katika usimamiaji wa kanuni na sheria za Nchi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,hivyo ameitaka Serikali kuwa makini katika hilo.


Mh.Dr Harisoni Mwakyembe amelitaka Kanisa kuhubiri Amani Nchini, ndani ya Living Water Center Ministy
Mh.Dr Harisoni Mwakyembe asema Amani izidi kuhubiriwa makanisani na kudumishwa Nchini,Maana inaisaidia Serikali katika kuhamasisha Amani na Upendo,nakuongeza kuwa Serikali inatambua na kuheshimu mchango wa Kanisa katika kutetea Amani na Upendo Nchi.

Hayo yamesemwa katika Kanisa la Living Water Center Ministry Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi lililopo Kawe siku ya jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kanisani hapo katika Ibada ya asubuhi ambapo alikuwa amearikwa kama mgeni rasmi katika shughuli ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo la Living Water Center ambapo hakuja peke yake aliweza kuambatana na mke wake pia na Mbunge mwenzake Mh.Mbunge Victor Mwamalaswa katika harambee hiyo.

Apostle Onesmo Ndegi ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo,akisisitiza suala la Amani na Upendo na kuitaka Serikali kutambua mchango wa Kanisa katika Suala zima la Amani na Upendo Nchini.Pia aliongeza kwa kusema Watanzania sote ni wamoja tunapaswa kuachana na itikadi za Udini,Ukabira na Uchama baadala yake Kuangalia suala la Amani na Upendo kutufanya kuwa kitu kimoja.

Akaulizwa na waandishi wa habari anazungumziaje suala la vurugu za Zanzibar akasema anaitaka Serikali kuwa makini katika ufuatiliaji wa jambo hilo na wahusika wote watiwe chini ya vyombo vya sheria,hata kama inasemekana kuwa ni wahuni wanaofanya hiyo kama inavyodaiwa basi wakamatwe na kufikishwa mahakamani, akamalizia kwa kusema yote yanayo fanyika kisasi ni juu ya Bwana.Akamalizia kwa kusema katika Serikali kuna ulegevu katika usimamiaji wa kanuni na sheria za Nchi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,hivyo ameitaka Serikali kuwa makini katika hilo.

Mwisho kabisha wa Ibada yalifanyika maombi yakiongozwa na Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi kwa ndugu hao Mh.Dr.Harison Mwakyembe,Mke wake na Mh.Mbunge Victor Mwambalaswa ili Mungu aambatane nao katika kazi zao,kufanya kwa ujasili pia kuwa na hofu ya Mungu katika kutumika Serikalini.

Waziri wa Uchukuzi Mh.Dr Harisoni Mwakyembe  akizungumza katika Ibada kanisani hapo.
Apostle Onesmo Ndegi ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo akihubiri katika Ibada.

Mh.Dr.Harison Mwakyembe na Mh.Mbunge Victor Mwambalaswa
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi kanisani hapo Mzee Tarimo,Mh.Dr.Harison Mwakyembe,Mke wake,Mh.Mbunge Victor Mwambalaswa na
Apostle Onesmo Ndegi ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo katika Ibada.
Baadhi ya watu kama Alex Msama,Mh.Diwani Janeth na wengine walihudhulia katika ibada hiyo na kutoa mchango wao katika ujenzi wa Kanisa
Mh.Dr Harisoni Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari waliofika  Kanisani hapo.




Apostle Onesmo Ndegi ambaye ndiye kiongozi wa Kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari waliofika  Kanisani hapo

Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi na akiwaongoza wachungaji wengine kufanya maombi kwa  Mh.Dr.Harison Mwakyembe,Mke wake na Mh.Mbunge Victor Mwambalaswa ili Mungu aambatane nao katika kazi zao,kufanya kwa ujasili pia kuwa na hofu ya Mungu katika kutumika Serikalini.

Maznat Bridal anakuleta 10th Anniversary

Maaznat ni mdau wa blog hii ambaye kazi yake ni kupamba maharusi na saluni aliyebobea katika kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu hivyo ameandaa event katika kutimiza miaka 10 ya kazi hiyo anayotegemea kuifanya siku za baadae ikiwa ni namna ya kumshukuru Mungu kwa hatua  aliyomtoa na kumfikisha hatua aliyofikia mpaka sasa.


Katika kusherekea event hiyo ya 10th Anniversary itakayofanyika 5-5-2013 Diamond Jubilee mahususi kwa wale waliowahi kuwa wateja wake au kuhudumiwa naye,wanaotegemea kuwa wateja wake wapya na pia wajasiliamali wa aina zote kuanzia watu wa mapambo,urembo,washehereshaji katika Events na harusi mbalimbali wanakaribishwa.

Katika kuhudhulia event hiyo unatakiwa kuchangia Elfu 50,katika gharama hiyo utapata kitenge ambacho kitakuwa sare ya kuvaa siku hiyo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Chakula,Vinywaji,Zawadi na burudani mbalimbali zitakuwepo siku hiyo kama Bahati Bukuku,The Voice na wengine wengi

Maaznat akizungumzia mafanikio yake mpaka sasa katika kazi yake hiyo amesema mafanikio ni makubwa mpaka sasa tofauti na alikotoka na Kusema Mungu amekuwa mwaminifu na Kumpigania siku hadi siku,akiongeza kuwa ameweza kudumu na kuhimili mikikimiki katika kazi yake akizunguza na kusema alianzia kazi zake kufanyia nyumbani mpaka leo ameweza kumiliki eneo kubwa ambalo amefungua bihashara mbalimbali kama kuuza vifaa vya urembo,nguo za maharusi,vifaa vya urembo na saluni ya kike kubwa yenye kuhudumia maharusi wengi kwa wakati mmoja.

Maaznat tofauti na kazi ya kupamba maharusi na saluni kwa taaluma ni mwanasheria ngazi ya uzamili ila ametokea kubobea katika kazi yake hiyo ya Urembo na Upambaji wa maharusi na saloon zaidi tofauti na tahaluma yake.
Shughuli zake na ofisi ilipo anafanyia Mikocheni jirani na njia ya kwenda Mikocheni B kwa Mama Rwakatare

                 Maaznat  

wadau wa media walioudhulia mkutano huo ofisini kwake maeneo ya Mikocheni 
Kitenge kinachotegewa kuvaliwa siku ya Event hiyo hapo siku za baadae 
Sehemu ya mwonekano wa ndani ya ofisi ya mdau Maaznat maeneo ya Mikocheni 

wadau wa habari wakiwa kazini kumsikiliza Maaznat kuelezea kahusu Event hiyo 
Baadhi ya wafanyakazi saluni kwake


Kwa mawasiliano zaidi kuhusu Event hiyo.
0752444470
0783444470
0718818999


Mokiwa abwagwa Uaskofu Mkuu wa Anglikana

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosia la ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa ameshindwa kutetea nafasi yake ya uskofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania baada ya kushindwa na Dk Jacobo Chimeledya (56) wa Jimbo la Mpwapwa.

Askofu Chimeledya ambaye anakuwa kiongozi wa sita kushika wadhifa huo nchini, aliibuka mshindi baada ya jina lake kupenya katika hatua tatu za kura.

Akitangaza matokeo hayo juzi jioni, Katibu Mkuu wa Anglikana, Dk Dickson Chilongani alisema kanisa hilo halina utaratibu wa kutangaza kura zilizopigwa lakini akathibitisha kuwa Askofu Chimeledya ndiye mshindi.

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,Dk Valentino Mokiwa.
Dk Chilongani alisema kuchaguliwa kwa Askofu Chimeledya ni utaratibu wa kanisa hilo ambalo hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.

Uchaguzi huo ulianza kwa ibada iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, Godfrey Mhogolo na baada ya hapo, Msajili wa kanisa hilo, Profesa Palamagamba Kabudi alitangaza utaratibu wa uchaguzi.

Chilongani alisema wajumbe 129 walihudhuria mkutano huo kati ya wajumbe 140 waliotarajiwa.

“Kwa kawaida katika uchaguzi, askofu yeyote mwenye umri chini ya miaka 60 huwa anaweza kuwa mgombea na katika uchaguzi huo, maaskofu 21 walikuwa na sifa za kugombea,” alisema.
.
Source:Mwananchi

Mauaji ya Padri Zanzibar, JK ataka uchunguzi ufanyike

Pigo jingine kwa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili lililoko Mji Mkongwe Zanzibar, ni Baada ya Padri Evaristus Mushi kuuwaawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana asubuhi wakati akielekea kanisani kuendesha ibada.

Tukio hilo limetokea majira ya saa moja asubuhi wakati padri huyo akijitayarisha kwenda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtoni nje kidogo na Mji wa Zanzibar.

Hilo ni tukio la pili kutokea kwa padri kupigwa risasi Zanzibar baada ya Desemba 26, mwaka jana Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki, Mjini Zanzibar kupigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake wakati akitokea kanisani.
Marehemu Padri Evaristus Mushi enzi za uhai wake
Akizungumzia tukio la jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema pamoja na kuthibitisha, alisema ametuma timu ya wapelelezi kwenda Zanzibar kuchunguza kwa undani kuhusu tukio hilo.

“Watu wasiojulikana wamempiga risasi Padri Mushi, na baada ya tukio alipelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kufariki dunia. Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,” alisema IGP Mwema.

Alisema hadi sasa watu watatu wameshakamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea na kuchunguza tukio zima.

IGP Mwema alisema ametuma timu Zanzibar itakayoongozwa na Manaibu Kamishna wa Polisi wawili ambao ni Samson Kasalla na Peter Kivuyo wakiwa pamoja na Kamanda wa Operesheni wa jeshi hilo, Simon Sirro.

“Tumekuwa tukifuatilia nyendo hizi na hivi sasa tutapambana na wahalifu ipasavyo, vurugu zozote zile lazima tupambane nazo ipasavyo,” alisema Mwema na kuongeza: “Kama kwenye tukio hili kutakuwa na masuala ya kigaidi nayo tutachunguza.”


Mwili wa padri huyo sasa umehifadhiwa katika mochwari ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Katika Kanisa la Minara Miwili, Mji Mkongwe waumini walikusanyika wakionyesha hali ya kuchanganyikiwa baada ya kupata taarifa za kifo hicho cha ghafla.
Ndani ya gari la Marehemu Padri Evaristus Mushi likiwa na damu baada ya kupigwa risasi
“Baada ya kufika karibu na kanisa alipigwa risasi na gari kupoteza mwelekeo kisha kwenda kuonga nyumba,”alisema na kuongeza: “Uchunguzi wa hospitali umegundua alipigwa risasi tatu mbili zimetolewa kichwani na nyingine haijulikani iliko.”

Matukio kama hayo ya kihalifu yamekuwa yakitokea mara kwa mara Zanzibar ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja watu watatu walipigwa risasi maeneo ya Bububu na Mbweni, lakini hii ni mara ya pili kwa padri kupigwa risasi katika historia ya Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),Severin Niwemugizi alisema tukio hilo linatia mashaka kwa kuwa mauaji hayo yanaonyesha kuwa ni ya kupanga.

“Nimepata taarifa kwamba kuna mwenzetu ameuawa huko, lakini inaonekana ni mauaji ya kupangwa kwa kadiri ya hamasa ambazo zinatolewa na dini fulani, kwani waliwahi kusema hatutaifurahia Pasaka, nadhani ndiyo wanatekeleza hilo,” alisema Niwemugizi.

Alisema tukio hilo ni la kuogopesha na linaonyesha nchi inakoelekea si kuzuri kwa kuwa kikundi fulani kimeachiwa na kinafanya mauaji na kuwatendea maovu wengine lakini viongozi wamekaa kimya.

“Hii ni ishara mbaya kwani Serikali ipo hivyo tunahitaji kauli yao kuhusu haya mambo, kwa kweli nina mashaka na yanayotokea ili yasije yakatufikisha kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda,”alisema Niwemugizi.

Rais Jakaya Kikwete alisema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Mushi.

“Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

Soure:Mwananchi

Ugeni wa Papa wa Othodox Afrika kukutana na JK


Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II anatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete.

Kiongozi huyo aliyewasili nchini siku chache zimepita, alisema anatarajia kuwa na mazungumzo na Rais Kikwete na miongoni mwa mazungumzo yao ni jinsi ya kanisa hilo litawaletea maendeleo Watanzania.

“Nitazungumza naye juu ya mipango niliyonayo ya maendeleo Tanzania na kuomba ushirikiano zaidi,” alisema Papa Theodoros II.
Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II
Alisema Kanisa la Othodox limekuwa likiendesha miradi mbalimbali kusaidia Watanzania ikiwapo hospitali itakayogharimu Sh17 bilioni, inayojengwa Nyegenzi, mkoani Mwanza.

Miradi mingine ambayo kanisa hilo linatarajia kuanzisha nchini  ni kujenga vituo vya watoto yatima, vituo vya ushauri na kutoa matibabu kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi (VVU) na ujenzi wa shule.

“Nina mpango wa kukutana pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ili kuweka mikakakti jinsi ya kuendeleza elimu nchini,” alisema Papa Theodoros II.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Othodox, Jimbo Kuu la Mwanza, Jeronmos Muzeyi alisema ujio wa Papa Theodoros II nchini ni kuandika historia ya pekee kwa sababu ni mara ya kwanza.

Alisema Papa huyo amefurahia mazingira na ukarimu wa Watanzania na kwamba, atakuwa akifanya ziara za mara kwa mara  ikiwa ni sehemu ya kuzidi kujenga uhusiano.

Alisema lengo kuu la kanisa hilo ni kuendeleza amani, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote na kuhakikisha wanapiga hatua zaidi za maendeleo.

Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Askofu Laizer Arusha


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer  wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati,Arussha Juzi.

Mchungaji auawa kwenye vurugu Geita

Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania (PAGT) Buseresere, Wilaya ya Chato, Mathayo Kachila (45) amefariki dunia huku watu wengine 15 wakijeruhiwa kwa mapanga kufuatia vurugu kutokana na mgogoro wa bucha.

Tukio hilo lilitokea jana saa 2:27 asubuhi kwenye Soko la Buseresere baada ya kundi la wananchi kuvamia bucha iliyokuwa na maandishi ya ‘Bwana Yesu Asifiwe, Yesu ni Bwana’, kuwataka waliokuwa wakiuza kuifunga hali iliyozusha vurugu.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wananchi hao wanaodaiwa kuwa waumini wa Kiislamu walikuwa wamechukizwa na kufunguliwa kwa bucha hiyo, ndiyo wakachukua uamuzi wa kwenda kuamuru ifungwe.

Inadaiwa kabla ya kufunguliwa kwa bucha hiyo, Wakristo walifanya mkutano wa Injili Uwanja wa CCM Katoro na kutangaza kuwa, watachinja nyama yao na kuiuza kwenye bucha maalumu.

“Tulipata taarifa za kufunguliwa kwa bucha hii na tulipofika kuwaomba waache kuuza nyama yao, waligoma na kuendelea kuuza, baada ya kuona hilo wafuasi wa Dini ya Kiislamu walikimbilia msikitini na kuunda kikosi cha kupambana nao,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Chato, Yusuf Idd.


Alisema licha ya kuwasihi hawakumsikiliza, waliamua kwenda kupambana.Katika vurugu hizo, duka la Idd lilivunjwa na kuporwa simu na fedha, huku pikipiki mbili ambazo hazijafahamika wamiliki zilichomwa moto.

Katika vurugu hizo nyama ndani ya bucha hiyo ilimwagiwa maji, ikiwamo kuharibiwa kwa madirisha na milango yake.

Licha ya majeruhi kutajwa kuwa 15, waliotibiwa Kituo cha Afya Buseresere na kuruhusiwa ni Abdallah Shaaban (25), Abubakar Shaaban (27), Faruk Shaaban (14), Kassim Almasi (23), Yusuf Shaaban (18), Bilal Hassan na Abdallah Ibrahim.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk John Lumona alisema majeruhi wengine waliofikishwa ni Yasin Rajabu (56), Said Taompangaze (47), Masoud Idd (21), Ramadhan Pastory (36), Haruna Rashid (61) na Sadiq Yahya (40), ambaye hali yake ameieleza kuwa mbaya na alipelekwa Hospitali ya Rufani Bugando. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geira, Paul Katabago alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo aliwataka wananchi kutulia kwa vile suala hilo linashughulikiwa na serikali na litapatiwa ufumbuzi.


source:.mwananchi.co.tz

Papa Benedict XVI ajiuzulu

Papa Benedict wa 16 ameshangaza dunia Jumatatu alipotangaza anajiuzulu ifikapo februari 28, na hivyo kuwa Papa wa kwanza kujiuzulu kwa takribani miaka 600 iliyopita.

Papa aliwashangaza viongozi wa juu wa kanisa alipokutana nao huko Vatican alikotangaza uwamuzi wake. Katika taarifa yake amesema “nilitafakari kwa kina juu ya uamuzi huo.”

Benedict alisema anajiuzulu kwa sababu nguvu zake zimepunguwa sana katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita “kufikia kiwango ambacho ilibidi nitambue uwezo wangu wa kutumikia kikamilifu wadhifa wa kidini niliyokabidhiwa.”

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya Vatican na Uingereza.

Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.

Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.

Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.

Papa Benedict XVI
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.

Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, na sherehe za Pasaka.

Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.

Mwandishi wa BBC mjini Roma Alan Johnston anasema habari hizi zimetokea kama radi, na kwamba hakukua natetesi yoyote juu ya uwezekano kama huu.

Msemaji wa Vatikani Father Federico Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu juu ya tukio hili.

Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.

Akizungumza kutoka nyumbani kwake huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya kimaumbile.

Wakati wa kutawazwa kama Papa, Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa mwenye umri mkubwa wa miaka 78.

Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.

Uongozi wake ulitokea wakati wa wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.

Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.

Source:bbc.co.uk/swahili

Tamasha la Pasaka kuhamasisha Amani na Upendo

Waandaaji wa Tamasha la Pasaka mwaka 2013 wameibuka na kauli mbiu inayohamasisha amani na upendo kwa jamii.Akizungumza na chanzo kimoja cha habari,Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama alisema wanashukuru kwamba sasa wamepata kibali cha kufanya tamasha hilo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama

Alisema tamasha la mwaka huu litakuwa zaidi katika kuhubiri amani kwa jamii na kusisitiza kuwa dhamira yao ni kuhakikisha Watanzania wanazidisha upendo na mshikamano uliokuwepo.
Alisema tamasha hilo litafanyika Machi 31 katika ukumbi ambao utatangazwa hivi karibuni na kuwa wana matumaini mambo yatakuwa mazuri kuliko tamasha la mwaka jana lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


 “Hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee na mambo mengine ya maandalizi, nasi tunasema mambo mwaka huu yatakuwa mazuri zaidi,” alisema Msama.
Alisema wamepanga siku yenyewe ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava,na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Askofu Thomas Laizer wa KKKT Arusha afariki Dunia.

Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini.Askofu Thomas  Laizer amefariki duniaalasiri ya jana katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea  na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.Pinda alikwenda hospitalini hapo saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye mpaka pale mauti yalipo mfika.


Askofu Thomas Laizer wa KKKT Arusha enzi za uhai wake

Raisi Kikwete azindua utoaji wa Vitambulisho vya Taifa


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Askofu Malasusa wa KKKT kitambulisho cha taifa.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete siku ya jana azindua rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam jana

Uzinduzi huo ulioudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Dini mbalimbali kama Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, s wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Askofu Malasusa wa KKKT,Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi,Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.Mkurugenzi Mkuu wa PPF,Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na wengine wengi viongozi wote hao walipata vitambulisho vyao hapo hapo katika uzinduzi  huo
  
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi kwa wa watu na utoaji vitambulisho vya taifa, Rais Kikwete alionya juu ya utoaji vitambulisho kwa watu wasiostahili na kusema kwamba Serikali yake haitavumilia kuona hali hiyo ikitendeka.
Alisema suala la vitambulisho vya taifa ni nyeti na linapaswa kuendeshwa kwa kufuata miiko na sheria za nchi, hasa kwa kuzingatia kuwa vitambulisho hivyo vitatumika wakati wa uchaguizi mkuu ujao.

Kama sehemu ya kuimarisha utendaji kazi, mamlaka hiyo ya vitambulisho vya taifa imeanzisha ushirikiano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),ambayo inakusudia kuvitumia vitambulisho hivyo katika uchaguzi mkuu ujao. Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu alisema ushirikiano huo itasaidia kuboresha kazi za utoaji vitambulisho na kwamba utakamilika kwa wakati. Hata hivyo alisema bado ofisi yake inakabiliwa na tatizo la vitendea kazi na kuiomba serikali kuongeza bajeti. 

Vitambulisho hivyo vitaanza hivi karibuni kutolewa kwa watumishi wa umma, kwani taarifa zao pamoja na alama nyingine zilikwisha chukuliwa. Hatua hiyo inakuja katika wakati ambapo taifa liko kwenye mchakato wa uandikwaji wa katiba mpya, ambayo nayo pia imepangwa kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kuhusu Zanzibar ambayo inatumia vitambulisho vya mkazi vilivyoanza kutumika tangu mwaka 2006, kumeelezwa kuwa, wananchi wa eneo hilo nao watajumuishwa kwenye zoezi hilo.


John Lisu azindua Album "Uko Hapa"



John Lisu
















Wachungaji 14 waondolewa Moravian

Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini, limetangaza kuwafukuza kazi wachungaji wake 14 na makatibu wanne wa idara mbalimbali kwa kosa la kuchochea vurugu ndani ya kanisa hilo.

Uamuzi huo ulifikiwa jana na Halmashauri Kuu ya Jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar baada ya wachungaji hao kujitangazia halmashauri yao mpya, wakijitenga na uongozi ndani ya kanisa.

Pamoja na kuwaondoa wachungaji hao, uongozi huo wa jimbo, umefanya mabadiliko ya uongozi katika Wilaya ya Morogoro na kuwateua wachungaji wengine kadhaa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachungaji waliofukuzwa.

Uamuzi huo umekuja wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jimbo la Mashariki na Pwani ya Kanisa la Moravian Tanzania, Clement Fumbo na wenzake saba wakiwa wamefungua kesi namba 222 Mahakama Kuu ya Tanzania, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Moravian Jimbo la Rungwe kupinga kuvuliwa madaraka na kusimamishwa kazi.

Katika kesi hiyo iliyopangwa kuendelea kusikilizwa Februari 6, mwaka huu mbele ya Jaji Augustini Mwarija, Fumbo na wenzake saba wanapinga kuondolewa madarakani na kusimamishwa kazi na wanaiomba mahakama iamuru walipwe Sh500 milioni kama fidia na gharama ya kesi.

Kadhalika uamuzi wa kufukuzwa kwa wachungaji hao umefanywa wakati Mchungaji Fumbo akidai kwamba yeye bado ni mwenyekiti halali na kutangaza halmashauri yake mpya, jambo ambalo uongozi wa Kanisa la Moravian unasema ni kinyume cha katiba wa kanisa hilo.

Akitoa taarifa ya hatua hiyo mbele ya waumini wa kanisa hilo lililoko Ushirika wa Mabibo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar, Adolf Mwakanyamale, aliwataja wachungaji waliofukuzwa kuwa ni pamoja na mwenyekiti wa Wilaya ya Kaskazini, Alinanuswe Mwakilema.

Wengine na nyadhifa zao kwenye mabano ni Noel Mwakalinga,(Mjumbe wa Halmshauri Kuu), Fanny Ndemange (Katibu wa Idara ya Kina Mama), Angelina Mwamakula (Mchungaji Msaidizi Ushirika wa Kimara) na Mariamu Kasendeka wa Ushirika wa Pugu Kajiungeni.

Wachungaji wengine na sharika zao kwenye mabano ni Tumaini Mwakijale (Tanita) Mosted Kibona (Kitunda), Eliza Kipesile (Kawe), Lugano Anganisye (Mwenge), Baraka Mwakijale (Mlandizi), Azaria Lwaga (Segerea) na Fredy Mwakyusa wa Usharika wa Kiwalani.

Katibu huyo aliwataja wakuu wa idara wanne waliofukuzwa kuwa ni Mchungaji Anyasime Kasebele (Uwakili), Emmanuel Mwaijande (Kwaya), Hezron Mwangaja (Uinjilisti) na Silas Mwakibinga (Miradi na Maendeleo).

“Tumeamua kuwaita pia wachungaji wetu wastaafu, lengo likiwa ni kuziba mapengo yote yaliyotokana na ndugu zetu ambao wameamua kuasi na kujitangazia kanisa lao,” alisema Mchungaji Mwakanyamale.

Source: Mwananchi

Uko Hapa uzindizi wa Album

Masaa 24 yamebakia kuanza kwa tamasha la uzinduzi wa Album ya pili ya mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili John Lisu maandalizi yamekamilika kwa 90% akizungumza mwenye Lisu anasema maandalizi mpaka sasa ni mazuri kuanzia upande wa mazoezi na mambo mengine kilichobaki ni tukio lenyewe kuanza.

Katika uzinduzi huo utakaofanyika katika kanisa la CCC Upanga jirani na Chuo cha Mzumbe,kuanzia saa 8 mchana kwa kiingilio cha Tsh.5000 tu.

Akizungumzi tofauti kati ya album ya YEHOVA YU HAI na mpya inayozinduliwa kesho UKO HAPA amesema toauti ya upigaji vyombo umebadilika,ladha ya muziki wenye pia na ujumbe ulio katika nyimbo zenyewe,Maana biblia inasema Utukufu Hadi Utukufu kutoka album ya iliyopita hadi hii ya sasa UKO HAPA. 









Nelly Kaisi-Lisu mke wa John Lisu alikuwepo kufanikisha mazoezi hayo katika upigaji wa bass guitar







nm,,