Askofu wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika aikosoa tume iliyotangazwa na Waziri Mkuu

Askofu wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha wanafunzi wa kidato cha nne kushindwa kufaulu mitihani si dawa ya kutatua tatizo la elimu nchini.

Akizungumza na chanzo kimoja cha habari ofisini kwake juzi, aliongeza kuwa kitendo cha wanafunzi kufeli ni hatua mbaya zaidi kwa serikali na kutengeneza taifa la watu ambao hawajui la kufanya hapo baadaye.

Alisema makosa hayo si ya waalimu bali ni ya serikali, kwani imekuwa ikipuuzia maoni ya wadau wa elimu na waalimu ambao huishauri serikali kwa nia njema ya maendeleo.

Alisema tume zinazoundwa na serikali mara nyingi hazina majibu ya kuridhisha na badala yake hutumia fedha nyingi za walipa kodi bila kupatiwa faida wala majibu ya kina.

Askofu Kanyika alisema kuundwa kwa tume kulikotangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hakuwezi kutoa majibu sahihi ya tatizo lililopo.

Akizungumzia masuala ya udini ambao unaonekana kushamili kwa kasi, Askofu Kanyika alisema vuguvugu hizo ni mbegu ya serikali kwani mara kwa mara walikuwa wakieneza chachu ya udini kama sehemu ya propaganda za kisiasa.

Source  http://www.freemedia.co.tz

No comments:

Post a Comment