Viongozi wa dini wamesifu rasimu ya katiba mpya.

 Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini, alisema kupunguzwa kwa ukubwa wa baraza la mawaziri ni muhimu na kilio cha muda mrefu cha watu wengi na kuwa siyo Tanzania tu hata Kenya wamepunguza ukubwa wa baraza lao.

Kuhusu mgombea binafsi, alisema linafaa maana litawezesha vyama kuleta wagombea makini zaidi  na kuondoa tatizo la kuleta wagombea mashemeji au wajomba ambao wanakwamisha maendeleo ya nchi.

Alisema suala la rais atakayechaguliwa kulalamikiwa mahakamani ni muhimu, lakini hilo litapoteza umuhimu wake endapo kesi itakayopelekwa mahakamani itacheleweshwa.

Kuhusu suala la serikali tatu alisema binafsi angependelea serikali moja tu ila anajua ni vigumu sana kuwepo, lakini akasema kama siyo hivyo, muundo wa serikali tatu ni muhimu maana utawezesha Tanzania Bara kuzungumza masuala yao na Zanzibar pia, huku ya Muungano yakiachwa kuzungumziwa na serikali ya shirikisho.
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Mch. David Mwasota

Kuhusu Spika wa bunge na naibu wake kutokuwa wabunge wala kutokana na vyama vya siasa, alisema linafaa maana litasaidia spika kuendesha bunge kwa mujibu wa sheria na taratibu zake bila upendeleo.

Aidha ,alipongeza kuwekwa kwa kipengele cha rais anayechaguliwa kupata kura zaidi ya kura asilimia 50 na kuwa hatua hiyo itawezesha kupatikana kwa kiongozi aliyechaguliwa na watu wengi.

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Mch.  David Mwasota, alisema rasimu ni nzuri na imezingatia matatizo na kero za wananchi na kwamba rasimu imeonyesha  kuondoa  mianya ya kuwagawa Watanzania.

“Matatizo yote yaliyokuwa yanawasumbua wananchi kwa muda mrefu  tangu Nyerere aondoke yamekuja vizuri ikiwa ni pamoja na masuala ya muungano, kwani kama kila nchi ina bendera na wimbo wake,” alisema na kuongeza:

“Sio kwamba mambo yote yamekamilika, hiyo ni generally tu (kwa mtazamo wa jumla). Na mambo mengine yaliyo ndani yake tunaona yamekaa vizuri. Mbali na kwamba ni jumla, lakini tunaiona nuru kwa mbali inaanza kutokea nchini.”

Hata hivyo, msemaji wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mch. John Kamoyo, alisema kuwa ni mapema mno kutoa maoni kuhusu rasimu hiyo kwani ni siku moja tu imepita tangu kutangazwa kwa umma wa Watanzania.

Kamoyo alisema kuwa unahitajika muda maalum kwa viongozi kukaa na kupitia na kwa pamoja watatoa maoni kuhusu rasimu hiyo.

No comments:

Post a Comment