Vyuo vya KKKT vyataka maslahi ya madaktari yaboreshwe

Kiongozi wa  KKKT , Askofu Dk Alex Malasusa
Baraza la uongozi wa vyuo vikuu vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) chini ya mwavuli wa Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira  (Tuma),limeitaka serikali kupitia 
Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), kuboresha maslahi ya madaktari na watumishi wa sekta ya afya nchini badala ya kuacha wanataaluma hao wakafikiria kutimkia nchi za Kusini mwa Afrika kusaka maslahi. 
Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof. Esther Mwaikambo akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Tiba cha KCMC kwa niaba ya Mkuu wa Kanisa hilo nchini.
Askofu Dk. Alex Malasusa, alisemawanataaluma hao licha ya kutakiwa kuwa wazalendo kwa taifa lakini pia Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, inapaswa kuwekeza kwa kulinda wataalamu hao wasijiingize katika vitendo vya rushwa na kukimbilia nje ya nchi kutafuta maslahi yaliyoboreshwa.

Awali,Mkuu wa chuo hicho, Prof.Egbert Kessy, alisema kuwa Tanzania imeendelea kukumbwa na upungufu wa madaktari licha ya kuwepo ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kujiunga na fani hiyo kila mwaka na kwamba kwa takwimu za sasa, daktari mmoja anahudumia wagonjwa kati ya 26,000 hadi 30,000.

Kessy alisema kiwango hicho ni kikubwa mara tano zaidi ya kile kinachotakiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na kusema ipo haja ya wahitimu kuwa wazalendo, na kupenda kufanya kazi nyumbani badala ya kukimbilia nje ya nchi kutafuta kazi zenye mishahara mikubwa.

Kwa mujibu wa Prof.Kessy, karibu asilimi 60 ya madaktari wanaohitimu mafunzo nchini hukimbilia kutafuta ajira nchi nyingine Kusini mwa jangwa la Sahara.

Source Nipashe

Happy Birthday Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa


Makamu wa Rais Dkt.Bilal azindua Benki ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania;Maendeleo Benki.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa benki hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo, Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
 Utepe ukikatwa kuashiria kufungua Benki ya Maendeleo, wakati wa hafla ya uzinduzi

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo watumishi wa Mungu,Viongozi wa Serikali na kutoka katika mashirika mbalimbali walipohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo watumishi wa Mungu,Viongozi wa Serikali na kutoka katika mashirika mbalimbali walipohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
Makamu wa Rais  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Rose Mushi, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu na kuwa manager mradi wa Benki na kuwa katika kamati ya watu kumi waliokua wanaisimamia hiyo project. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.

Makamu wa Rais  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.

Waziri Mkuu mstaafu Lowassa aendelea kulia na kiwango duni cha elimu

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ameelezea kusikitishwa kwake na kiwango duni cha elimu katika shule za sekondari za kata na katika baadhi ya vyuo vya elimu ya juu.

Akizungumza katika harambee ya kuchangia mfuko wa elimu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa kijitonyama jijini Dar es Salaam jana, Lowassa alisema, kiwango cha elimu katika shule hizo kinamsikitisha kwani ni cha chini.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM) allisema: ”Napenda niseme wazi kuwa kiwango cha elimu katika shule zile za kata na baadhi ya vyuo vikuu kwa kweli ni vya chini, hili mimi linanisikitisha sana kwa sababu elimu bora ni mkombozi kwa mtoto wa Kitanzania.

” Hata hivyo alipongeza kanisa kwa kusaidia juhudi za Serikali katika kuimarisha na kuboresha elimu na kusababisha shule nyingi za kanisa kuwa na kiwango bora cha elimu.

Lowassa alisema baadhi ya watu wamekuwa wakisema mambo mbalimbali kutokana na kusindikizwa na marafiki zake katika harambee kadhaa na kumuunga mkono kwa kuchangia. Alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa marafiki zake ambaye ni wakili maarufu, Sadock Magai, kuwasilisha michango ya marafiki wa Lowassa katika harambee hiyo ambao walichangia Sh. milioni 50.

Miongoni mwa marafiki zake waliomchangia ni Lawrance Masha, Innocent Macha, Bashir Awale, Hamis Kindoroko na  Lemmy Bathelemew.

Aidha, walikuwapo Mbunge wa Segerea ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga aliyechangia Sh. millioni tatu na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, aliyechangia Sh. millioni mbili.

Lowassa alimpongeza Azan kwa kuchangia bila kujali Imani yake ya kidini. ”Nampongeza na kumshukuru sana Mheshimiwa Idd Azan kwa kuja kwake kunisindikiza na kuchangia, hii ndiyo Tanzania ninayoijua, isiyo na dini, watu wa dini zote mnashirikiana,” alisema Lowassa.

Katika Harambee hiyo, jumla ya Sh. millioni 615 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa Sh. milioni 250.

Source: NIPASHE

Mama Regina Lowassa azindua rasmi DVD ya Glorious Worship Team.

Mama Regina Lowassa mke wa aliyekua Waziri Mkuu mstahafu akijibu maombi ya Lisala iliyosomwa na Glorious Worship Team.

Paul Clement
Angel Bernad na Emmanuel Mabisa 
Angel Bernad na Emmanuel Mabisa wakisoma Risala kwa Mgeni Rasmi
The Voice ndani ya Nyumba

Mc Chavala akiwa namgeni rasmi Mama Regina Lowassa



Mbunge wa CCM Asunta Mshana wa kwanza na Mgeni rasmi Mama Regina Lowassa katikani akiwa na wageni wengine aliombatana nao
Picha kwa hisani ya Jimmy Temu Blog

 Ruge Mutahaba  Clouds Media Group