Ikiwa imesalia siku 1 uchaguzi wa Marekani ....Israeli, mhubiri Bill Graham wajaribu kumbeba Romney.

Barack Obama
Ikiwa imesalia siku moja Wamarekani wapige kura kumchagua rais atakayeongoza nchi hiyo kwa miaka minne, Wayahudi wanaoshi marekani ambao wengi ni wafanyabishara wakubwa wameweka wazi msimamo wao kuwa  wanamuunga mkono mgombea wa chama cha Republican, Mitt Romney, huku Mwinjilisti wa kimataifa Bill Graham, akishutumiwa kwa kujiingiza katika siasa na kumpigia debe mgombe huyo.

Kwa upande wa Wayahudi imeelezwa kuwa wanaomuunga mkono Mitt Romney, wakiongozwa na kampeni za siri siri zinazoanza kwenye Chuo Kikuu cha Tel Aviv, huku wakikaririwa wiki chache zilizopita kuwa Barack Obama hana chaguo zaidi ya kuwapa mkono wa heri katika vita yake na Iran itakayoanza mapema mara baada ya uchaguzi wa Marekani.

Hata hivyo shirika la utangazaji la BBC lilibainisha kwamba miongoni mwa mataifa 21 waliotoa maoni yao juu ya uchaguzi wa Marekani wiki iliyopita, asilimia 55 wanamuunga mkono Obama na Romney akijitwalia asilimia tisa za maoni hayo.

Wakiulizwa wanaona nani atashinda katika kinyang’anyiro kikali kwenye uchaguzii nchini Marekani, asilimia 57. 2 za Wayahudi wa Israel wasema Romney na Obama alijipatia asilimia 21.5.

Waarabu wa Israeli ambao idadi yao inakaribia asilimia 45 wanamuunga mkono Obama na Romne wanampa 1, tu.
Mitt Romney
Hata hivyo,  mtazamo wa Waisraeli wanaona kwamba ikiwa Romney atashinda katika sakata hilo ni wazi kuwa watakuwa na maslahi naye kwani wanaona ni msaada mkubwa kuhusiana na vita yake na Iran, kuliko akishinda Obama, ambapo kwenye eneo hilo maoni yanaonyesha Romney asilimia 40 na Obama 19 ingawa si wote wanaoamini hilo.

Sambamba na hilo tetesi zinaeleza kwamba ushindi wa Obama utakuwa mbaya kwa Waziri Binyamin Netanyahu, kwa kuwa maoni ya watu wake wanataka Romney ashinde ambaye wanaamini anaweza kuwa mtu mzuri wa Netanyahu.

BILLY GRAHAM ALAUMIWA
Mwinjilisti wa kimataifa wa Marekani, Billy Graham, ameshutumiwa vikali na wananchi nchini humo kwa kumkingia kifua Mitt Romney katika kinyanyiro cha urais, huku wakimuelezea kwamba amekuwa akijiingiza katika masuala ya siasa sana wakati yeye ni mtumishi wa Mungu kwa kukipendelea chama cha Republican.

Mwinjilisti wa kimataifa wa Marekani, Billy Graham
Utetezi wake kwa chama cha Republican umepelekea viongozi wengi wa kisiasa kuacha kwenda kusaka ushauri kwa kiongozi huyo wa masuala ya kiroho kwani awali walikuwa wakifanya hivyo na hata mwaka 2008 wakati wa uchaguzi viongozi wengi walikwenda kumtembelea na 2010 Rais Obama na Senator John McCain waliwahi kumtembelea nyumbani kwake.

Hata hivyo, Romney mwezi uliopita aliwatembelea Bill Graham na mwanae Franklin Graham, katika mji wao uliopo Kaskazini mwa Carolina.  Na hapo alimsifu kiongozi huyo ambaye ni muumini mzuri wa dini ya Mormon kwa mtazamo wake alisema siasa zake ni safi.

No comments:

Post a Comment