Vyuo vya KKKT vyataka maslahi ya madaktari yaboreshwe

Kiongozi wa  KKKT , Askofu Dk Alex Malasusa
Baraza la uongozi wa vyuo vikuu vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) chini ya mwavuli wa Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira  (Tuma),limeitaka serikali kupitia 
Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), kuboresha maslahi ya madaktari na watumishi wa sekta ya afya nchini badala ya kuacha wanataaluma hao wakafikiria kutimkia nchi za Kusini mwa Afrika kusaka maslahi. 
Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof. Esther Mwaikambo akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Tiba cha KCMC kwa niaba ya Mkuu wa Kanisa hilo nchini.
Askofu Dk. Alex Malasusa, alisemawanataaluma hao licha ya kutakiwa kuwa wazalendo kwa taifa lakini pia Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, inapaswa kuwekeza kwa kulinda wataalamu hao wasijiingize katika vitendo vya rushwa na kukimbilia nje ya nchi kutafuta maslahi yaliyoboreshwa.

Awali,Mkuu wa chuo hicho, Prof.Egbert Kessy, alisema kuwa Tanzania imeendelea kukumbwa na upungufu wa madaktari licha ya kuwepo ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kujiunga na fani hiyo kila mwaka na kwamba kwa takwimu za sasa, daktari mmoja anahudumia wagonjwa kati ya 26,000 hadi 30,000.

Kessy alisema kiwango hicho ni kikubwa mara tano zaidi ya kile kinachotakiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na kusema ipo haja ya wahitimu kuwa wazalendo, na kupenda kufanya kazi nyumbani badala ya kukimbilia nje ya nchi kutafuta kazi zenye mishahara mikubwa.

Kwa mujibu wa Prof.Kessy, karibu asilimi 60 ya madaktari wanaohitimu mafunzo nchini hukimbilia kutafuta ajira nchi nyingine Kusini mwa jangwa la Sahara.

Source Nipashe

No comments:

Post a Comment