AFLEWO Tanzania yakutanisha wachungaji katika kuelekea AFLEWO 2014

Kukutana huko kumetokea siku ya jana kata Hoteli ya Peacock Dar es salaam, kukutana huko kumeambatana na chai ya asubuhi (Pastor’s Breakfast) kwa lengo la kuwashilikisha wachungaji hao maono na mipango ya huduma ya AFLEWO 2014 na kuomba ushiriki wa wao na washira wao katika maadalizi kwa ajili ya Mkesha huo unaotegemea kufayika mwakani mwezi wa sita.

Kusanyiko limetokea siku chache kabla ya uzinduzi wa usajili na Mass Kwaya ambapo unaanza Jumapili hii saa 9:00 mchana Katika kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga jirani na Chuo cha mzumbe, usahili huo utaendelea mpaka Januari na kufunga usajili wa kujiunga na Mass Kwaya hiyo,

Siku ya jana kusanyiko hilo lilikuwa likiongozwa na Walezi wa huduma ya AFLEWO Tanzania  ambao ni Pastor Paul Safari (DPC), Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), Mwenyekiti Geoffrey Obielo na Administrator wa AFLEWO Tanzania Anna Abella Munyagi.

Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa ni pamoja wao na kuwa walezi wa AFLEWO wa sehemu kidogo katika kutoa ushirikiano pale itakapotakiwa,huduma zao kusaidia kuwa ruhusu waumini wenyewe uwezo wa kuimba kuja siku ya Jumapili ujiunga na AFLEWO Mass Kwaya,tutakapo karibia siku ya tukio mwakani kutoa nafasi yaAFLEWO kwaya kuhudumu Makanisani kwao ikiwa ni sehemu kuitangaza na taharifa kuwafikiwa watu katika makanisa mbalimbali ili uja kuhudhulia Mkesha huo.

Kwa mara ya kwanza Tanzania AFLEWO ilinza kwa kufanyika mwaka 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, 2012 ilifanyika katika kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga, AFLEWO 2013 ilifanyika katika Kanisa BCIC Mbezi Beach,Mwaka 2014 inategemewa kufayika mwezi wa sita tutakufahamisha mahala takapo fanyika siku zinavyozidi kwenda.

NB:Katika usajili wa Kwaya ya waimbaji vigezo wa waimbaj  na wapigaji wa vyobo ni waliokoka na Yesu Bwana na Mwokozi kwao pia uwe ueujua kuimba.Karibuni sana bila kukosa!

Mlezi wa AFLEWO Tanzania Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus),
Mlezi wa AFLEWO Tanzania Pastor Paul Safari (DPC)
Watumishi wa Mungu mbalimbali wakiwa makini kumsikiliza mzungumzaji katika kusanyiko hilo
Wachungaji kutoka huduma mbalimbali wakiwa makini kumsikiliza mzungumzaji katika kusanyiko hilo



Pastor Fred Okello kutoka Upper Roo Ministry,Pembeni ni ni mchungaji mwakilishi kutoka Mlima wa Moto kwa Mama Rwakatare Mikocheni B.

Mama Shegga

Bishop Mwende toka DPC








Kwa mawasiliano zaidi

+255 712 586 643
+255 757 332 062
aflewodar@gmail.com 

No comments:

Post a Comment