Maaskofu wakuu nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja.
Pia walisema kwamba hawatakubali kuona viongozi wa dini kwenda kinyume na maagizo hayo nchini humo.
Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana
wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini
kwa maelewano kwamba hawatashiriki ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia walipiga
marufuku maombi yoyote maalumu kwa wanandoa wa jinsia moja licha ya
ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza
kufanya hivyo iwapo wanajihisi.
Hata hivyo walidai viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasiyo rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
Uganda
Kwa upande wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na
mswada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa
ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa
mwaka 2009.Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema
Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa,
kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment