Aprili 25, mwaka huu dunia ilipiga hatua kubwa katika safari ya kuelekea kwenye serikali moja, dini moja na sarafu moja, wakati viongozi zaidi ya 300 walipofanya maamuzi magumu na kutoa kile kinachoelezwa kuwa ni tangazo la hatari.
Kwa kauli moja, baada ya kujadili kwa kina, wakala pamoja na kunywa pamoja, viongozi hao walitoa azimio linalosomeka:“Sisi, washiriki 300 kutoka zaidi ya nchi 70 za mabara sita, tukijumuisha Wayahudi, Wakristo, Waislamu ni miongoni mwa dini zilizokutana Doha Ritz Carlton kwa ajili ya kongamano kubwa linaloandaa maisha bora zaidi ya mwanadamu kuishi. Tunaiandaa dunia kuwa kisiwa kimoja chenye muelekeo mmoja tukiabudu pamoja ......”
Pamoja na mambo mengine zingatia maazimio ya kuwa wamoja kuishi pamoja na kuabudu pamoja.
Hebu jiulize ni vipi Waliookoka (Pentekoste) Waislamu, wabudha, wapagani na waabudu shetani wataabudu pamoja kwa umoja?
Ni Mungu yupi anayekubaliana na dini zote hizo zenye mielekeo na misingi tofauti? Usistaajabu kwa kuwa wakati umefika na viongozi hao isipokuwa Wapentekoste, aliendelea kutamka hivi:
“ Katika Kongamano letu lililodumu tangu Aprili 23 hadi 25, 2013 tunasema kuwa, tunatambua ukarimu wa Sheikh Hamad Bin KhalifaAl-Than, na watu wa Qatar walioshirikiana na waandaaji wa kongamano hili, Wizara ya mambo ya kigeni na Chuo kikuu cha Qatar.”
Kabla ya kufikia maazimio, uongozi wa kongamano chini ya uenyekiti wa Dk. Aisha al-Mannai, Dk. Ibrahim al-Naimi na Waziri wa Sheria, Mheshimiwa Hassan Bin Abdulla Al-Ghanim, waliwakaribisha washiriki na kuwataka kuzingatia mapendekezo yaliyomo kwenye dhima ya kongamano isemayo `Mwenendo bora katika mjadala wa mambo ya imani.
Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika kongamano hilo ni pamoja na kuhakikisha kuwa somo la ushikiano wa upendo, ukilenga katika dini moja na kumuabudu Mungu mmoja na fundisho moja la dini linafundishwa kwa kila taifa kabila na lugha.
Njia za siri zilizokubaliwa kutumika katika promosheni ya hiyari ni pamoja na misaada zaidi kwa mataifa yatakayoitikia na kuanza kufundisha somo la dini moja ukiwa ni mtaala rasmi utakaotumika kwenye mashule yote duniani.
Kuondoa tembo zenye kuleta ubaguzi wa miungu, kama vile mavazi ya dini, kama misalaba, hijab na mengineyo na kufuata vibao vya amri kumi za Mungu au mikutano ya maombi yenye kubagua wengine.\
Pamoja na maamuzi ya siri, maamuzi ya wazi ni pamoja na kuimarisha taasisi ya Interfaith kila nchi na kusimamia mpango wa ibada za pamoja ili kuwazoezesha watoto wa kizazi kipya kushirikiana katika ibada.
Wachunguzi wa mambo ya imani wanaeleza kuwa maamuzi ya mkutano wa Doha ambao ni wa 10, tangu taasisi hiyo ianze kukutana katika taifa hilo la kiislamu kama kituo chake rasmi ni hatari kuliko mengine yote yaliyowahi kufikiwa.
Baadhi ya viongozi wenye kuhemika sana katika ulimwengu wa dini walihudhuria mkutano huo, isipokuwa Wapentekoset ambao wanaamini kuwa ushirika huo ni wa kuandaa kiti cha Mpinga Kristo anayetajwa katika Bibilia kwenye kitabu cha Ufunuo 13.
Katika maadhimisho ya kumi ya Kongamano hilo la imani zilitolewa tuzo maalumu kwa wale waliostahili kutunzwa , tuzo hiyo inaitwa “Doha International Award for Interfaith Dialogue 2013”. Kati ya waombaji 150 kutoka kwa watu binafsi na mashirika kutoka kila kona ya Ulimwengu, tuzo ilimwendea Dk. Muhammad al-Sammak ambapo watu watatu binafsi na mashirika matatu nao pia walitajwa kipekee kama waliostahili shukrani kwa mchango wao kuhusiana na kongamano hilo na kufikia mafanikio hayo.
Katika kipindi maalum baada ya uzinduzi, washindi wote wa tuzo kutoka Lebanon, Bosnia, Marekani, Morocco na Kanada walibadilishana uzoefu wao na washiriki wa kongamano hilo.
Kongamano lilikuwa na vipengele vikubwa vinne:
Katika kipindi cha Taaluma, ilijadiliwa kuwa wanafamilia wana wajibu mkubwa katika kuwakuza vijana katika misingi ya roho hiyo ya Interfaith. Vyuo vikuu na Mamlaka za Elimu kwa ujumla wanahimizwa kuingiza mtaala wa imani moja katika mfumo wao na inapaswa kufundishwa kuanzia ngazi ya familia. Ilihimizwa kuwa watafiti kutoka taasisi za elimuya juu watanufaika wakifanya kazi zao kwa ukaribu na mashirika ya Interfaith, lengo likiwa kuendeleza mihadhara ya Interfaith duniani kote na kila mtu lazima ielimishwe kwanza kabla ya kushurutishwa ikibidi.
Sheria
Wazungumzaji katika kipengele cha sheria walizungumzia mambo muhimu ya kuanzisha sheria za kijamii, ,kiuchumi na kitabibu katika ngazi mbalimbali za miji kwa mtazamo wa ushirikiano kidunia na Umoja wa Mataifa kwa dhana ya kinga- miongoni mwa haki nyingine mbalimbali.
Walisisitiza kuwa na chombo cha umoja wa taasisi wa kisheria kama chombo chenye kushirikisha dhana na kuhudumia watu wa imani zote. Waislamu, wakristo na wayahudi watashikamana pamoja katika kutafuta njia bora za kupiga vita umaskini, ambapo watu wengi hawaelewi chochote juu ya hili.
Umoja kama huu unapaswa kushereheshwa, ili kwamba umma uelewe umuhimu wao katika mambo yenye kujenga. Kongamano la Doha linaweza kuifanya kazi ya kukuza ushauri wa kisheria wa pamoja kwa ajili ya masualaya kisheria ya siku za usoni.
Utatuzi wa migogoro na Amani
Taarifa zote zilizitaka jumuiya zote za Interfaith kuendelea kushirikiana kwa dhati ili kupata uwanja wa pamoja katika kufanikisha kuunda jumuiya za kisheria kwakuwajengea uwezo viongozi wa kidini na kijamii ili kuushinda mgawanyiko uliopo sasa.
Wale wanaoshjindania mambo ya kijinga watakandamizwa kwa hoja ili kukubali kukaa pamoja na kujenga dunia moja yenye ladha moja na yenye kuheshimu utu wa mtu.
Tamaduni za vyombo vya habari
Kongamano limeona kuwa mwingiliano wa vyombo vya habari katika maisha ya kila siku, hasa katika karne moja iliyopita ni dhahiri kwamba vimekuwa msaada mkubwa katika jamii inayotuzunguka, kutokana na nguvu iliyopo katika vyombo hivyo, lakini pia vimekuwa mchango mkubwa katika kuinua mambo mbalimbali.
Hivyo kuna haja ya kuwa na utamaduni moja wa kuchambua mwenendo wa vyombo hivyo na promosheni maalumu kwa wale watakaitazama ineterfaith kwa jicho chanya.Inaamini kuwa hizo ni harakati za mwisho kabisa katika kuelekea kumpata mpinga Kristo atakaye usuka suka ulimwengu akiulazimisha kumuabudu. Tayari idadi kubwa ya makanisa yametia sahihi mkataba wa kuundwa kwa umoja wa kidini.