Mchungaji Gwajima;Ndoto yangu lazima itimie.

Siku cha baada ya mchungaji Mchungaji Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kueleza tukio la kunyweshwa sumu kwa nia ya kufanya aharibike akili,ameibuka na kusema hawezi kufa hadi ndoto aliyo nayo juu ya Tanzania itimie,ikiwa ni pamoja  na mikikiti kugeuka kuwa madarasa ya Sunday Schools za watoto na Masheikh na Maimamu wakikimbia mbele ya msalaba wa Yesu Kristo.

Mchungaji Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima

“Wewe leta sumu kama unavyoweza ,wewe leta majambazi,wewe leta wezi siwezi kufa mpaka ndoto yangu itimie ” alisema mchungaji Gwajima alipokuwa kanisani kwake Jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Katika mahubiri hayo pia sehemu yake imewekwa katika tovuti ya Kanisa lake,Mchungaji Gwajima alisema katika ndoto yake haina budi kutimia kabla hajaondoka duniani aliona majeneza yakiletwa Nchini kwa ndege kwa ajili ya kufufuliwa.

Huku kila mara akilejea kibwagizo cha “Ninayo ndoto haijatimia bado ,” Mchungaji Gwajima alisema kuwa ameoneshwa kuwa Tanzania ikigeuka na kuwa Ufalme wa Mwanakondoo,huku ikiwa imefunikwa na utukufu wa Mungu huku ikiwa isivyo kawaida jambo litakalotimia kabla ya kifo chake.

“Muota ndoto hafi kabla ndoto yake haiatimia,Yusufu hakufa hadi ndoto yake ilipo timia,Farao hakufa hadi ndoto yake ilipotimia,ninayo ndoto haijatimia” alizidi kusema kwa ujasiri mkubwa na kuongeza:
Chombo cha Mungu hakiwezi kurudi mbinguni kabla hakija maliza kazi”

Mambo mengine mchungaji Gwajima aliyataja kuwa ni sehemu ya ndoto yake kuwa lazima yatimie kabla ya kufa kwake ni pamoja na ndoto aliyoota ikionesha kwahubiri kutoka Tanzania wakiichoma Tanzania kwa moto wa Mungu.

“Niliona wahubiri kutoka Tanzania wanainuka na kuichoma Dunia,niliona makaburi yanafunguka kwa jina la Bwana,” alisema.

Awali mchungaji Gwajima alisisitiza kwamba muda wake wa kufa bado kabisa haujafika kwasababu ya ndoto aliyo nayo juu ya taifa la Tanzania na kazi ya Mungu anayohitajika kuifanikisha.
“Lazima nitimize ,nimepewa uwezo wa kuanza na uwezo wa kumaliza”,Alimalizia kwa kusema I have a dream

Chanzo:Nyakati

1 comment: