Yaliyojili katika Tamasha Kubwa Kwa ajili Ya Maandalizi Ya Mkutano Wa Bonke


Dr. Huruma Nkone wa Kanisa la VCC


Kushoto ni Mchungaji mwenyeji wa kanisa la TAG magomeni mikumi akiwa na Dr Huruma Nkone.

Rivers of Joy kutoka  Kanisa la VCC kwa Dr. Huruma Nkone


Sasali Mc wa Event



Bomby Johnson akiwa RiverS of Joy kutoka VCCT
Vuvuzela pia zilikuwepo
 Nextlevel toka CCC Upanga
Music Director Samuel akiwaongoza Nextlevel toka CCC Upanga
 Miriam Mauki


Upendo Nkone akienda sawa na mashabiki
source:jimmytemu.blogspot.com

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal: Udini usitugawe


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewataka Watanzania kukataa kugawanywa kwa misingi ya udini.Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitr mjini Tabora jana, Dk. Bilal, alisema ni busara waumini wa dini na madhehebu kujenga utamaduni wa kuvumiliana hasa  zinapotokea hitilafu miongoni na kati yao.Pia, Dk. Bilal alikemea ubaguzi unaotokana na kabila, rangi, jinsia au mahala mtu alipo au anapotoka.

“Kaeni pamoja na kutafuta muafaka kwa njia ya majadiliano ya amani na upendo, pasipo kutawaliwa na jazba wala chuki. Tukumbuke kauli na angalizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba vita ya dini haina mshindi,” alisema.Dk. Bilal, alisema Tanzania imekuwa kisiwa cha amani na utulivu, jambo lisilompendeza kila mtu kutokana na kuwapo wanaotutazama (nchi) kwa jicho la husda na kuiombea mabaya.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal



“Wanatuombea tufike mahali tuharibikiwe ili wao wafurahi. Lakini wakumbuke kuwa dua la kuku halimpati mwewe," alisema. Alisisitiza kuwa amani katika taifa au jamii yoyote ni sharti la kwanza katika mchakato wa kuleta maendeleo.

Alisema anaamini viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusaidia kujenga maadili mema katika taifa hili na kwamba watu wakishiba imani ndani ya nafsi zao, wakaelewa na kuzingatia mafundisho ya dini zao, maovu yataondoka kati yao.

Alisema, uwapo wa amani na utulivu unaifanya serikali kupata ahueni, kwamba badala ya kutenga bajeti   kubwa kupanua magereza, kugharamia wafungwa na mahabusu na uendeshaji wa mahakama, rasilimali hizo zitaelekezwa katika mipango mingine ya maendeleo.

Dk. Bilal alisema katika siku za hivi karibuni, yameibuka matukio kadhaa yanaoashiria kutaka kuvuruga amani na utulivu wa taifa na kwamba hujuma hizo zinafanywa na watu wachache wasiolitakia mema taifa kwa maslahi yao binafsi.

Aliwahakikishia wananchi kuwa serikali ipo madhubuti na itahakikisha inapambana kwa nguvu zote kudhibiti hujuma zote zenye nia mbaya ya kuchafua sifa njema ya amani na utulivu wa Tanzania.
“Watanzania tumeishi kama ndugu na taifa moja kwa muda mrefu na kamwe hatutakubali tunu hii njema ivurugwe kwa kisingizio chochote kile,” alisema.

Aliongeza kuwa kamwe serikali haitakuwa tayari kuona Mtanzania anaishi kwa hofu na mashaka ndani ya nchi yake kutokana na vitendo vya wahuni wachache.

“Kila itakapobidi, tutawasaka, tutawakamata na kuwakomesha kwa rungu la mkono wa sheria. Nawahakikishieni kwamba Tanzania yetu itabaki nchi salama ya amani na utulivu na ya kupigiwa mfano daima.“

Alisema uhuru wa kuabudu katika taifa hili umejengewa misingi ndani ya katiba na kutokana na ukweli huo, kila mmoja anapaswa kuheshimu imani au dini ya mwenzake pasi kujiona kwamba imani au dini yake ni bora zaidi.

“Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia mwamko mkubwa kwa taasisi hizi kuanzisha shule za msingi, vyuo hadi vyuo vikuu jambo ambalo sisi katika serikali tunaridhishwa nalo na kuhamasisha kasi zaidi ya kuimarisha sekta ya elimu," alisema.

Alihimiza kuongeza kasi zaidi katika kuboresha sekta ya elimu na kuongeza kuwa uhai wa taifa hili na lolote lile duniani utategemea ubora wa elimu inayotolewa leo

Source: NIPASHE 

Padre aparamia paa la kanisa kujiokoa Baada ya kuona majambia yakimeremeta.

Makanisa manne makubwa ya Coptic nchini Misri, yamechomwa moto jijini Cairo kutokana na mvutano wa kisiasa unaondelea nchini humo, tangu baada ya jeshi kupindua serikali iliyokuwa inaongozwa na Rais Mohamed Morsi na kumweka wa muda, ni katika ghasia hizo, Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki alilazimika kuparamia paa la kanisa ili kujiokoa baada ya kuona waasi wakimjia mbio na majambia mikononi.

Habari zinaeleza kuwa wafuasi wa chama ya Muslim Brotherhood, waliandamana mpaka karibu na makanisa hayo, yaliopo nje kidogo ya viunga vya Jiji la Cairo, na kuanza kuwashambulia wakristo na kuchoma moto makanisa, na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za thamani katika makanisa hayo.

Akizungumzia mkasa huo, Padre Kassim Yusuph (kasisi), ambaye ni mmoja wa waathirika na kanisa lake kuchomwa moto jijini humo, alisema, aliona kundi kubwa la waandamanaji wa chama cha Brotherhood, wakiwa wameshika majambia  makali wakivamia eneo hilo na kuanza kufanya fujo wakipiga Wakristo na kuchoma huku wakiimba nyimbo za kejeli 


Padre huyo alisema kundi hilo liliwaona kama wao (yaani Wakristo) kuwa ni miongoni mwa waliokuwa wakishinikiza Morsi kuondolewa madarakani. Yatuatayo ni baadhi ya maneno ya waandamanaji wa chama hicho cha kiislamu: “Nyinyi wasaliti wakubwa, mmeunga mkono Rais Morsi kutolewa madarakani, sasa mtaipata.”

Hata hivyo, Padre Yusuph, alisema alijiokoa kwa kupanda kwenye paa, na kurukia nyumba nyingine, ambapo aliweza kuwatoroka wafuasi hao wenye hasira kali, na hivyo kunusuru maisha yake.
“Ilinibidi nipande juu ya paa ili kuweza kunusuru maisha yangu, kwa kuwa walikuwa na silaha kali za kudhuru watu wetu, japo kwa sasa hali ni shwari kidogo,” alisema Padre Yusuph.

Mvutano huo umesababisha machafuko na mauaji ya watu zaidi ya 100, tangu maandamano ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohamed Mursi ambaye kwa sasa amewekwa kizuizini kusikojulikana na jeshi la nchi hiyo.
Maandamano rasmi ya kumng’oa rais yalianza mwaka jana kutokana na kupitisha sheria ya kujilinda iliyotaka awe juu ya mamlaka zote, kutoka kwenye mahakama za nchi hiyo, hivyo kuchochea hasira kwa wananchi pamoja na wanaharakati wanchi hiyo.

Waziri Nchimbi aliangukia Kanisa

Majanga yanayoonekana kuchipuka kila iitwapo leo, katika taifa la Tanzania na inayosababisha vifo kwa raia wasio na hatia, imeelezwa kuwa, suluhisho lake kubwa ni Kanisa kwani linamamlaka ya kimungu ya kutokomeza.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alitoa rai hiyo, hivi karibuni jijini Dar es Salaam, na kukazia kuwa endapo kila mkristo atasimama  katika nafasi yake kumtafuta Mungu ataliponya taifa linaloandamwa na vurugu za hapa na pale.  

Alisema, kwa sasa taifa limeanza kulegalega kimachafuko na kulifanya kuwa na sifa mbaya kitu ambacho ni tofauti na awali lilipokuwa likijulikana kama kisima cha amani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi

 “Kanisa ni kitu cha muhimu sana katika nchi yoyote duniani, maana lina nguvu ya kimungu na uwezo wa kukomesha mambo yanayolikabili taifa ikiwa watakatifu watamuomba Mungu kwa kumaanisha,” alisema Dk. Nchimbi.

Mbali na hilo, alisema lazima kanisa kwa kushirikiana na Serikali, wakemee wale wote wanaotaka kuharibu amani ya nchi ya Tanzania, ambayo ilikuwa mfano wa kuigwa katika mataifa mengine duniani, hivyo kufanya nchi kuwa na watalii wa kutosha.

“Kuna watu wanania mbaya ya kutaka kuharibu amani ya nchi yetu, hao lazima tuwawajibishe ili tuzidi kudumu katika amani, tuwakatae kwa njia yoyote, hao ndio maadui wa taifa letu, sisi wenyewe serikali hatutaweza bila kanisa kuingilia kati,” alisema Waziri nchimbi.

Waziri Nchimbi huku akionekana kuvaa sura ya huzuni ghafla alisema kuwa, amani iliyokuwepo awali sasa inavuja damu, na kuweka wazi kuwa ili kuindoa hali hiyo wakristo wakae vizuri kwa Mungu na kumsihi ainusuru Tanzania.

Hakusita kukemea wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu kwa lengo la kuleta mtafaruku nchini, kuacha mara moja, huku akiahidi kushughulikiwa ikiwa hawataacha nia mbaya waliyonayo kwa taifa.

Akizungumzia suala la maadili, alisema hivi sasa maadili kwa vijana yameshuka hali inayopelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa, hivyo akawasihi wazazi kuwafundisha watoto wao maadili mema.

“Hivi sasa taifa linapoteza nguvu kazi kutokana na kushuka kwa maadili, kitu pekee ni wazazi kujikita kuwafundisha watoto wao kumpenda Mungu ili kukomesha hali hii ya watoto wetu kupotelea duniani,” alisema Waziri Nchimbi.

Sambamba na hilo, aliwataka watumishi wa Mungu kujikita kuwafundisha waumini wao kudumisha amani, na kukemea migogoro isiyo na tija kwa taifa.

“Nawaomba watumishi wa Mungu na viongozi mliopo hapa mjikite kuwafundisha waumini wenu kudumisha amani, na kukemea migogoro ya hapa na pale isiyo na tija kwa taifa,” alimalizia Waziri Nchimbi.

Kanisa la TAG lazidi Kupaa...!

Takwimu zilizotolewa katika kikao cha Baraza la Waangalizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), kilichofanyika mjini  Dodoma siku kadhaaa zimepita, zinaonesha kukua kusiko kwa kawaida katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kuwashangaza hata watu kutoka mataifa yaliyotangulia kupata muamko wa Injili kama vile Marekani. 


Takwimu hizo zinaonesha ongezeko la kila eneo kwa zaidi ya asilimia 100, katika kipindi cha miaka mitano tu yaani kuanzia mwaka 2008-2013, mfano; mwaka 2008, kanisa lilikuwa na Sehemu (section) 75, na sasa lina Sehemu 226. Hadi kufika mwishoni mwa mwaka jana, kanisa hilo linaloongozwa na dira yake ya maendeleo ya ‘Miaka 10 ya Mavuno’ lilikuwa na watumishi wenye vyeti mbali mbali 5,026, na makanisa 5007, yaliyoenea nchi nzima na kulifanya kuwa kanisa kubwa na linalokua kwa kasi zaidi miongoni mwa yale ya Kipentekoste Tanzania. Jambo lililolipua shangwe za wajumbe wa baraza hilo kutoka kila kona ya Tanzania, ni ukweli kuwa ukuaji wa kanisa unakwenda sambamba na ukuaji wa elimu, ujenzi na upanuzi wa Vyuo vya Biblia, vya kupanda makanisa na msisitizo wa kimaadili. 
Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabs Mtokambali
Takwimu pia zinaonesha kuwa, kanisa hilo limekuwa kiidadi likiongezeka kwa zaidi ya asilimia 200, tangu lilipozindua dira yake ya maendeleo iliyoweka lengo la kufikia kila roho inayopotea dhambini Tanzania. Akisoma taarifa hiyo, mbele ya mamia ya wajumbe wa bbaraza hilo, Katibu Mkuu wa TAG, Rev. Ron Swai, alisema kuwa, hadi kufika Desemba mwaka jana, watenda kazi 2280, walikuwa tayari wamehitimu masomo katika vyuo vya kupanda makanisa na kuingia shambani kumtumikia Mungu. Katika kipindi hicho, kanisa limeweza kununua magari ya thamani kwa maaskofu wake nchi nzima, wakurugenzi wa Idara, na sasa mradi wa kugawa piki piki kwa waangalizi, tayari umeanza ambapo baadhi yao walitarajiwa kukabiziwa vyombo hivyo vya kurahisisha utumishi katika kazi ya Bwana Ijumaa iliyopita mjini Dodoma.

 Pamoja na vyombo vya usafiri, kanisa hilo limejikita katika Uinjilisti, likiwanunulia Wainjilisti wa kitaifa vyombo vya kisasa vya kuhubiria pamoja na vifaa maalumu vya uinjilisti kwa njia ya sinema ili kuwafikia watanzania wote. Mradi huo wa ununuzi wa piki piki za kisasa aina ya Yamaha, kutoka Japani utagharimu shilingi milioni 800,na tayari Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabs Mtokambali amepata mshirika katika kazi ya Mungu atakaye gharamia mradi huo. 

Ni kwa kuguswa na matokeo chanya ya dira ya maendeleo ya Kanisa la TAG, Mtumishi wa Mungu kutoka Marekani, Dk. David M. Oliver, ambaye pia ni rais wa huduma ya Living Water LLC, yenye makao yake North Canton Ohio Marekani, aliwaambia mamia ya waangalizi hao kuwa wanapaswa kumshukuru sana Mungu kwa kuwapa viongozi wa kanisa wenye wingi wa hekima na maono makubwa ya kulifikisha mbali kanisa. Dk. Oliver alikuwa akifundisha somo linalohusu Nguvu ya Uponyaji wa Baraka-Mwongozo wa kusikiliza, ambapo alianza kwa kufafanua maana ya Neno Baraka.

 “Neno Baraka linatokana na neno la kilatini ‘benedicere’ likiwa na maana ya kusema kitu vizuri, ‘kusifu’ ‘inua’ au kutakia mema,”alifafanua Dk. Olvier katika somo lake hilo. Huku akinukuu Maandiko Matakatifu kutoka vitabu vya Warumi 5:8 na Yohana 11:25-26, alisisitiza: “Lazima tujifunze kuishi kwa neema, rehema na Baraka za Mungu, bila kujaribu kupata utajiri kutokana na hivyo. Baraka msingi wake ni kweli na hubeba nguvu ya Mungu…..” Dk. Oliver alifundisha kwa kina misingi ya baraka za Mungu na jinsi ya kupokea na kubariki wengine, akitoa mifano kadhaa ya maisha na utumishi wake.

Glorious Worship Team-GWT- Living Water Centre Kawe

Billy Graham: America Needs Our Prayers More Than Ever


At my age, there are a lot of things that health and strength no longer permit me to do. Sometimes when Franklin is visiting, I jokingly offer him this advice: “Don’t get old!” But there are still many things I can do, and one of them is pray. I’ve been praying fervently that we might have a fresh spiritual awakening in America.

If ever there was a time this country needed the intervention of God, it is now. We can and should pray for America as a whole, but remember that when God sets out to change a nation, He begins by changing people. It starts with individuals. The more I pray, the more deeply I feel that My Hope America is the right outreach for this country today.

Evangelist Billy  Graham
I am already hearing reports about the people who have given their hearts to Christ this summer during the early phases of this outreach, and it thrills me.

In November, the month I turn 95, we will have a new My Hope America video/TV special available across the country—several wonderful, real-life stories of people whose lives were transformed by Jesus Christ interwoven with a message from my heart about the healing power of the gospel. I’m already at work on this.

Along with all the encouraging visits from grandchildren and great-grandchildren this summer, I’ve had a video camera crew helping me tape, from my home, the things I feel strongly that God is leading me to say to America. Please pray that God will work in the completion of this program and that He will use it in a mighty way.

You can invite people you know to watch the program with you in November. Ask God to touch their hearts as they watch. Thousands and thousands of believers in every part of the country are preparing to do that.

Evangelist Billy Graham and the 42nd President of the United States
President Bill Clinton


Who do you know—loved ones, friends, co-workers—who need to understand and experience the life-changing power of the gospel? Are you praying faithfully for them right now, specific people you long to see transformed now and for eternity?

God longs to see them transformed as well, and He invites you to partner with Him as He seeks to draw them to Himself. If you want to see someone’s heart healed and eternal future secured, you must be praying.

A Christian may feel unsure at times of how best to do that. God understands. The Bible says, “We do not know how to pray as we should, but the Spirit Himself intercedes for us” (Rom. 8:26, NASB). That means when we intentionally and faithfully lift the names of our lost friends and loved ones to the throne room of heaven, it is the Holy Spirit who is pleading, mourning and praying through us. In this way, we become actual partners with God—“workers together with Him” (2 Cor. 6:1, NKJV)—and our efforts are raised from the low plane of doubt and hesitancy to the high plane of creativity with God.

As a co-laborer with God, you need not be anxious about how to make it all work. You cannot draw anyone to Christ, but God can: “For thus says the Lord God: ‘Indeed I Myself will search for My sheep and seek them out’” (Ezek. 34:11). Ask Him to do that.

Make sure your pastor knows about My Hope America—already more than 16,000 churches in all 50 states have signed up to participate. Meanwhile, I encourage you to sign up right now as an individual. Plan to go through a My Hope America training session at a church in your area, or take the easy online training at home (you’ll need about three hours total, spread out at your own pace). There is no fee or cost.

This is a huge undertaking, but we strongly believe the outreach and all needed materials should remain free of charge to those who participate. We are trusting God for the financial resources, and we are asking Him to lay it on your heart to help with a generous and sacrificial gift for My Hope America.

Most of all, we ask for your prayers and participation so that the hope of the gospel can touch not only people across the nation, but people you personally know and care about. The Bible says, “Let him who thirsts come. Whoever desires, let him take the water of life freely” (Rev. 22:17). Join me in asking God to give people that thirst.