Padre aparamia paa la kanisa kujiokoa Baada ya kuona majambia yakimeremeta.

Makanisa manne makubwa ya Coptic nchini Misri, yamechomwa moto jijini Cairo kutokana na mvutano wa kisiasa unaondelea nchini humo, tangu baada ya jeshi kupindua serikali iliyokuwa inaongozwa na Rais Mohamed Morsi na kumweka wa muda, ni katika ghasia hizo, Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki alilazimika kuparamia paa la kanisa ili kujiokoa baada ya kuona waasi wakimjia mbio na majambia mikononi.

Habari zinaeleza kuwa wafuasi wa chama ya Muslim Brotherhood, waliandamana mpaka karibu na makanisa hayo, yaliopo nje kidogo ya viunga vya Jiji la Cairo, na kuanza kuwashambulia wakristo na kuchoma moto makanisa, na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za thamani katika makanisa hayo.

Akizungumzia mkasa huo, Padre Kassim Yusuph (kasisi), ambaye ni mmoja wa waathirika na kanisa lake kuchomwa moto jijini humo, alisema, aliona kundi kubwa la waandamanaji wa chama cha Brotherhood, wakiwa wameshika majambia  makali wakivamia eneo hilo na kuanza kufanya fujo wakipiga Wakristo na kuchoma huku wakiimba nyimbo za kejeli 


Padre huyo alisema kundi hilo liliwaona kama wao (yaani Wakristo) kuwa ni miongoni mwa waliokuwa wakishinikiza Morsi kuondolewa madarakani. Yatuatayo ni baadhi ya maneno ya waandamanaji wa chama hicho cha kiislamu: “Nyinyi wasaliti wakubwa, mmeunga mkono Rais Morsi kutolewa madarakani, sasa mtaipata.”

Hata hivyo, Padre Yusuph, alisema alijiokoa kwa kupanda kwenye paa, na kurukia nyumba nyingine, ambapo aliweza kuwatoroka wafuasi hao wenye hasira kali, na hivyo kunusuru maisha yake.
“Ilinibidi nipande juu ya paa ili kuweza kunusuru maisha yangu, kwa kuwa walikuwa na silaha kali za kudhuru watu wetu, japo kwa sasa hali ni shwari kidogo,” alisema Padre Yusuph.

Mvutano huo umesababisha machafuko na mauaji ya watu zaidi ya 100, tangu maandamano ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohamed Mursi ambaye kwa sasa amewekwa kizuizini kusikojulikana na jeshi la nchi hiyo.
Maandamano rasmi ya kumng’oa rais yalianza mwaka jana kutokana na kupitisha sheria ya kujilinda iliyotaka awe juu ya mamlaka zote, kutoka kwenye mahakama za nchi hiyo, hivyo kuchochea hasira kwa wananchi pamoja na wanaharakati wanchi hiyo.

No comments:

Post a Comment