Mara kadhaa siku zimepita wanatheolojia wabobevu walinukuliwawakionya kuhusu hatari kubwa inayolikabili kanisa la Bwana wakati zoezi la uasi mkuu wa kimaandili, utu na hata kanuni za Muumba lilipokuwa likiendelea katika wigo wa siasa na harakati. Kisha Julai 17, mwaka huu hatua nyingine kubwa sana ikafikiwa wakati Waziri Mkuu wa Uingereza David Comeron aliposaini hati ya kuruhusu mashoga, kufunga ndoa kisheria.
Wiki zimepita nilipost ripoti hatua hiyo kwa undani zaidi na kiapo cha Waziri huyo mkuu wa taifa lenye nguvu na hila nyingi. Siku chache baada ya tukio hilo hatua mbaya zaidi ya kuelekea kwenye uharibifu imewadia ambapo mahakama kuu imeombwa kuliamuru kanisa limuasi Mungu.
Kwa mujibu wa Shirika laUtangazaji la Uingereza (BBC) ingawa mbele ya mahakama ni wanaume wawili waliofungua mashtaka mahakamani wakiiomba mahakama kulilazimisha kanisa kuwapa haki ya kufunga ndoa rasmi mbele ya madhabahu, mpango huo ni mpana zaidi na umebeba watu wasioonekana.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Comeron |
Hatua hiyo inaelezwa na mabingwa wa sheria wa London kuwa ni hatua ya juu sana katika kuelekea kwenye mateso ya kanisa kwani amri ikishatolewa na mahakama, mchungaji atakayegomea ndoa hizo anaweza kufungwa gerezani.
“Profesa John Wycliffe, Mhadhiri mbobevu wa sheria za dini katika vyuo vikuu vya Uingereza na hata mataifa mengine ya Ulaya akiandika katika Twiter alisema: “Hili ndilo nililotegemea, yale yote ya Cameron yalikuwa yakiandaa hili na wakati umefika wa kanisa kuingia katika mateso. Asomaye na afahamu kuwa chukizo la uharibifu linaingia patakatifu.”
Hawa wanaume wawili wasingekuwa na kiburi cha kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza hatua kubwa kiasi hiki, kulishitaki kanisa na taasisi zote za kidini zinazoshikilia msimamo wa kimaadili.
“Hawa jamaa wanatimiza kile bosi wao alichoahidi kuwa atahakikisha kila taifa linaisujudia sheria yake ya uasi wa kimaadili, huu ndio ujanja wa kiingereza,”alisema.
Walalamikaji wanajigamba kuwa waliotiliana mkataba wa mahusiano ya wao kwa wao mwaka 2006, baada ya serikali kuidhinisha mambo hayo, wanataka wakabariki ndoa yao kanisani.Serikali ya Uingereza katika mahojiano kwenye sherehe za kile ilichokiita ushindi dhidi ya wahafidhina,ilidai kuwa makanisa hayalazimishwi kufunga ndoa madhabahuni, lakini kanisa la Anglikana haliruhusiwi kabisa kufungisha ndoa hizo.Anglikana ndiyo dini rasmi ya taifa la Uingereza na Mkuu wake akishachaguliwa huidhinishwa familia ya kifalme ndipo ashike madaraka ya kuliongoza kanisa.
Ndoa ya jinsia moja |
“Ni kitu cha aibu inapofikia mahali tunalazimishwa kuwapeleka Wakristo Mahakamani ili tu eti watutambue rasmi, inanivunja moyo kwa sababu mimi binafsi napenda kuwa na `BONGE` la sherehe kuanzia kanisani, na hii sidhani kama inaweza kuja yenyewe bila sisi wenyewe kuhimiza kwa nguvu za amri ya Jaji.”
Ilibainishwa kuwa, tofauti na ilivyo Marekani, nchini Uingereza kanisa la England limeshikamanishwa sana na Serikali. Lakini pamoja na harakati za usimamiaji wa haki za binadamu, chini ya uongozi wa Rais Obama, makanisa ya Marekani tayari yameanza kushauriwa kujiandaa kuwa na mtikisiko kama huo na hata kuburuzwa mahakamani na makasisi kufungwa jela watakapokataa kutii amri halali ya mahakama.
Taasisi na mashirika makubwa kadhaa duniani yanashauri makanisa kuanza kujijengea wigo wa kisheria wa kujihami dhidi ya yeyote atakayeonekana kuunga mkono kufungisha ndoa za jinsia moja makanisani mwao.
Ushauri mmojawapo kutoka taasisi moja ya kibabtisti, Kusini mwa Califonia, unaonya kuwa ni muhimu kwa wachungaji kuchukuwa hatua madhubuti za kulinda maadili ya kitheolojia ikiwa ni pamoja na namna ya uendeshaji wa sherehe za ndoa, ushauri na shughuli nyinginezo zinazowiana kama vile; matumizi ya mali za kanisa, ajira na uanachama.
Mwanasheria Kelvin Snider, wa taasisi ya masuala ya kisheria ya Pacific, ananukuliwa akiyahimiza makanisa kupembua upya na kuifanyia kazi haraka sera ya ndoa itakayokuwa kielelezo kizuri.Alisisitiza kuwa, sera hiyo haipaswi kuhusishwa na kanuni za kikanisa ila akapendekeza lazima sera hiyo iangazie mambo muhimu kama vile; muundo wa kanisa, Bodi ya Kanisa, Baraza la kanisa au hata uanachama na ikibidi katiba zibadilishwe na kuingiza kipengele cha utii wa kanuni na sheria ya Biblia kama sifa muhimu kwa mwanachama wa kanisa.
Aidha, alibainisha kuwa, sera iliyopendekezwa na PJI inasema ndoa ni ushirika ulioasisiwa na Mungu.”
“Ilikuwa taasisi ya awali kabisa iliyoasisiwa na Mungu kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu kitabu cha Mwanzo, ambako agano la kale manabii waliifananisha taasisi hii na mahusiano yaliyopo baina ya Mungu na watu wake.
“Yesu katika Agano Jipya alielezea kusudi halisi na vigezo vya ndoa, ambapo ndoa inafananishwa na uhusiano uliopo kati ya Kristo na Kanisa, hivyo kanisa linapaswa kuitazama ndoa kama Taasisi ya Kiroho iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe,” alisisitiza na kuongeza:
“Sera itamtaka kila mtu anayetaka kufanya sherehe itakayomshirikisha mwajiriwa yeyote wa kanisa, au hata mtu akitaka kutumia vyombo vya kanisa, lazima mambo hayo yatazamwe kikatiba kwa kuzingatia vipengele husika vya imani.”
Chini ya sera hii, kanisa linaweza kujiwekea masharti kuwa, wafanyakazi wake kamwe hawapaswi kushiriki kwa namna yoyote kwenye vyama vya watu wa ndoa za jinsia moja na kwamba, mali ya kanisa kamwe haitatumika kwa namna yoyote katika kufanikisha shughuli yoyote ya kishoga.
Kwa upande wa Uingereza, jambo hili ni tofauti kwa sababu ya mahusiano makubwa yaliyojengwa kati ya kanisa na Serikali. Hii ndiyo kusema baadhi ya sheria za kikanisa zimemegwa moja kwa moja kutoka sheria mama za Serikali.
Wiki jana Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, mbele ya waandishi wa habari, na timu yake inayoshughulikia hati inayotambua haki za mashoga, akiishukuru kwa ushirikiano na kazi kubwa iliyofanyika hadi muswada kuwa sheria. Hapo alipata wasaa wa kueleza nia yake ya kuusambaza duniani kuokoa mahusiano ya jinsia moja ambapo alidai kuwa wanyanyasika na kunyimwa uhuru wao na kuahidi kusimamia mpango huo kwa gharama ya kifo.
Wataalamu wengine wanaonya kuwa harakati hizo za Uingereza zikishapitishwa na Mahakama itakuwa rahisi kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola kama Tanzania kushurutishwa na wakubwa kuitii amri hiyo.
No comments:
Post a Comment