Mchungaji wa Kanisa afumaniwa na mke wa mtu

TOFAUTI na inavyoaminika na wengi kuwa watumishi wa Mungu ni watu safi, safari hii Mchungaji Obed Ntimba wa Kanisa la Anglikana Gongo la Mboto, Dar es Salaam amejikuta akivunja agano la Muumba baada ya kunaswa gesti akiwa na mke wa mtu.
 
 Tukio hilo la aibu lilimkuta mchungaji huyo Ijumaa iliyopita saa saba na nusu za mchana katika gesti moja (jina lipo) iliyopo nyuma ya Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar.
 
Siku moja kabla ya tukio, makachero wetu walitonywa kuhusu dhambi hiyo na mtu wa karibu na watu hao akisema kuwa anaumia kwa sababu mchungaji huyo ana mke na watoto na mwanamke huyo, Rose ni mke wa mwanajeshi kwa hiyo aliamini tendo wanalotaka kulifanya ni uovu katika jamii.
 
 Mtoa habari wetu huyo alisema tukio hilo lilipangwa kukamilika kesho yake Ijumaa katika gesti hiyo ndipo kazi ya kuwafuatilia hatua moja baada ya nyingine ilianza.
 
Ijumaa saa sita mchana, mtonyaji wetu alipiga simu  na kuweka wazi kwamba wawili hao wapo njiani kuelekea gesti, kila mmoja kwa usafiri wake.
 
 Ndipo makachero wetu  walipowatonya polisi na kuambatana nao mpaka kwenye gesti hiyo na kujipanga kwa mbinu za kisasa za kutoonwa na ‘adui’.

 Makachero hao  walifanikiwa kupata ramani ya chumba walichoingia wawili hao ambapo ‘rumu’ namba 1B ndiyo iliwasilishwa kwamba Rose na mchungaji wake wamo humo.

Saa saba na nusu mchana, Makachero wetu na polisi waliingia hadi mapokezi ya gesti hiyo kwa kificho na kutoa maelekezo kwa mhudumu. Mhudumu aliongozana nao hadi mlangoni na kugonga lakini haukufunguliwa.
 
 BAADA YA DAKIKA TANO
Wakati mlango huo ukigongwa na mhudumu bila kufunguliwa, mchungaji huyo alisikika akisema na kuuliza:
“Subirini kwanza.”
“Lakini ninyi ni akina nani?”
 
 Baada ya dakika tano kupita, mlango ulifunguliwa, mchungaji akakutana na macho ya timu nzima. Alipigwa butwaa asijue la kufanya huku akitetemeka, Rose alikuwa ndani ya khanga moja!
 
 MCHUNGAJI MSOBEMSOBE HADI POLISI
Polisi waliwabeba msobemsobe wote hadi Kituo cha Polisi cha Urafiki-Ubungo, Dar ambapo kila mmoja alianza kujieleza.
 
 MCHUNGAJI APANGULIA HUDUMA YA KIROHO
Kituoni hapo, Mchungaji Ntimba alipobanwa kuhusu sababu za kuingia gesti na mke wa mtu, alisema waliingia kwa ajili ya huduma ya kiroho kwani mwanamke huyo alikuwa anataka kufungua kanisa ndipo alipomuomba yeye amsaidie.
 
 “Mimi sikuwa na lengo baya jamani. Huyu dada alihitaji kufungua kanisa, akaniambia ili nimshauri hawezi kukaa  sehemu ya wazi kwa kuwa mume wake ni mwanajeshi anaweza kuonekana na watu wakampa taarifa.
 
 “Ndipo nikaamua kwenda naye katika nyumba ile ya kulala wageni kwani wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya huduma, wakitokea nchi mbalimbali huwa wanalala pale na wahusika wa pale wananifahamu sana.
 
 “Baada ya kuingia gesti nilibanwa na haja ndogo, nikaenda kujisaidia. Cha kushangaza niliporudi nilimkuta huyu dada amevua nguo zote na kuanza kunishawishi lakini sikuwa na lengo hilo jamani,” alijitetea mchungaji huyo.

 Baadhi ya picha zilizopo  zinamuonesha mchungaji huyo akiwa amevaa suruali lakini amesahau kufunga zipu huku kondom zikiwa pembeni kitandani!
 
 MSIKIE MKE WA MTU SASA
Baada ya mchungaji kutoa maelezo yake, mke wa mtu naye alianza kutiririka ya kwake huku akionesha ushahidi wa meseji za simu ambazo mchungaji huyo alikuwa akimtumia akimshawishi kumpa penzi.
 
 “Huyu mchungaji nilikwenda kwake kwa lengo la kufanya kazi kanisani lakini kuanzia hapo amekuwa akinishawishi kuwa anataka nimpe penzi ili aweze kuniweka katika sehemu nzuri kanisani.
 
 “Nilikuwa nakataa, lakini akasema tukutane pale gesti tuongee zaidi. Nilikataa kukutana gesti, akaniambia pale ni ofisini, mara nyingi akiwa anaongea na waumini mambo muhimu ya huduma ya kiroho huwa anakutana nao pale.

 “Nikakubali lakini kabla hata hatujaongea chochote alianza kuvua nguo zake na kuanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiwa na ‘kinga’ kabisa na mimi nikavua nguo lakini kabla hajatimiza lengo lake ndipo wakaingia watu wakiwa na askari.
 
 “Mimi nashukuru sana kwa sababu hawa ndiyo wameniokoa. Nilikuwa nikisikia habari za huyu mchungaji kuwa ana tabia ya kuwafanyia wasichana wengi vitendo hivyo na kweli leo ndiyo nimeamini,” alieleza mwanamke huyo.
 
 Katibu wa kanisa hilo (jina halikupatikana mara moja) alimuombea msamaha mchungaji kwa waandishi huku akionesha kuumizwa na kitendo hicho baada ya kuoneshwa ushahidi na kukiri kwamba una ukweli tofauti na alivyokuwa akifikiria awali kabla ya kuachiwa kwa dhamana

Mdau wa Blog lutenant Albert Monyo apata jiko









Kanisa lavamiwa Jijini Dar

Vitendo vya kuvamiwa kwa makanisa nchini, vimekosa mwarobaini hivyo kuvutia maadui wa ukristo kuendelea kuharibu nyumba za ibada bila hofu. Tukio la hivi karibuni, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mbezi Kati, kuvamiwa usiku tena wakati ambao vijana walikuwa wakiendela na mkesha ni ushahidi kuwa hali inazidi kuwa mbaya badala ya suluhisho kupatikana.
   
 Mchungaji Samson Swai wa kanisa hilo, akizungumza na chazo cha habari alisema kuwa, Ijumaa flani majira ya saa saba usiku, alipigiwa simu na vijana waliokuwa katika mkesha kanisani hapo na kumjulisha kuwa palikuwa na mtu aliyefahamika (jina tunalihifadhi kwa sasa) ameliharibu kanisa kwa kubomoa milango yote.
  
Aliongeza kuwa mara baada ya taarifa hiyo alipiga simu kituo cha Polisi Kawe, na kuwajulisha kuhusu tukio na walipofika eneo la tukio,mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa maeneo hayo alikwisha kimbilia nyumbani kwake.

  Alisema, uharibifu uliofanywa na mtu huyo majira hayo ya usiku mnene bila sababu ya msingi ni kuing'oa milango vibaya.Kwa mujibu wa Mchungaji Swai, Polisi walionyeshwa nyumba anamoishi mtuhumiwa huyo na walipofika nyumbani kwake kwa lengo la kujua sababu ya kufanya uharifu huo, hakuwafungulia mlango licha ya kumgongea  kwa muda mrefu lakini  jitihada hizo ziligonga mwamba, hivyo Polisi kuahidi kumfuatilia.
 Mchungaji Swai aliweka wazi kuwa, ikiwa Serikali haitaiangalia kati suala la uvamizi wa makanisa na kulishughulikia kwa jicho pevu; huenda vikatokea vita vya kidini, wakristo watakapochoka na matukio hayo kila kona.

 Mtumishi huyo alisema baada ya kushindwa kumpata mtu huyo, Polisi waliondoka eneo hilo, na kesho yake mtu huyo aliendelea kujigamba kuwa, Jeshi la Polisi limeshindwa kumtia hatiani ili aeleze nani anamtuma kufanya uhalifu katika nyumba ya Bwana.

Mtu huyo anayehisiwa kuwa, pengine alikuwa na silaha ya moto, anadaiwa kuendelea kutamba mitaani kuwa hakuna wa kumfanyajambo lolote na ataendelea na mashambulizi yake.

Pengine Serikali isipokuwa makini na kung'oa mizizi hii, hali ya vurugu inaweza kuchukua nafasi mpya na kusababisha kutoweka kwa amani na kuifanya Tanzania yenye sifa ya kuwa 'kisiwa cha amani' kupoteza sifa hiyo ya kipekee na kuingia kwenye sintofahamu.

Chanzo chetu kilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, ambaye alisema kuwa, taarifa ya kuvamiwa kwa kanisa haijafika mezani kwake na kuahidi kulifuatilia, na kubainisha kibarua hicho amemwachia OCD kulifuatilia kwa karibu ili apate taarifa.

Semina ya Neno la Mungu na Mwl Christopher Mwakasege Dar es salaam.


Ikulu yawajibu Maaskofu wa Kipentekoste

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni, amepinga vikali madai yaliyotolewa na maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste nchini, kuwa Serikali imepuuza majina yaliyopendekezwa na makanisa hayo kwa ajili ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Balozi Ombeni, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka, alisema Serikali haikupuuzia kundi lolote lililoainishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko, kuwakilisha mapendekezo ya Bunge Maalum la Katiba.

Alisema walijaribu kutafuta mapendekezo ya makanisa hayo kwenye Kanzi Data ya Msingi (Primary Data Base), lakini hawakuona chochote.

"Uchambuzi ulifanywa ili kubaini kama kulikuwa na mapendekezo kutoka Baraza kati ya mapendekezo 850 yaliyowakilishwa, lakini hakukuwa na taarifa za majina ya waliopendekezwa,"alisema Dkt. Turuka na kuongeza kuwa;

"Majina ya maaskofu watano walioshiriki katika utoaji taarifa kwa vyombo vya habari yalitumika ili kubaini kama wao pia walikuwa miongoni mwa waliopendekezwa."

Alisema utafutaji huu haukubaini kuwa Baraza lilikuwa moja ya taasisi zilizowasilisha maombi. Alisisitiza kuwa hakukuwa na jina hata moja la viongozi wa Bara walioitisha mkutano na vyombo vya habari kutoa taarifa za kulalamikia uteuzi wa wajumbe kutoka Baraza hilo kwa madai kuwa wametengwa.

Mbali na hilo, alisema kuwa juhudi za Serikali zilijielekeza kutafuta endapo kulikuwa na mapendekezo ya kundi hilo. "Hata hivyo utafutaji haukubaini majina ya viongozi hao kuwepo katika orodha hiyo,"alisisitiza Dkt. Turuka.

Kwa mujibu wa Dkt. Turuka, kulikuwa na uwezekano pia Baraza liliwasilisha mapendekezo ambayo yalifika kwa Katibu Mkuu Kiongozi nje ya muda uliopangwa kisheria wa Januari 2, mwaka huu.
Alisema uchambuzi wa mapendekezo 52 ambayo yaliwasilishwa nje ya muda haukubaini kuwepo kwa mapendekezo kutoka kwa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania. Alisema juhudi za Serikali katika kufuatilia uwepo wa mapendekezo kutoka Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania hazikuweza kuthibitisha kuwa Baraza lilituma mapendekezo yake kama ilivyokuwa imeagizwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Kwa msingi huo, alisema tamko la Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste kudai kuwa wamebaguliwa halina ukweli, kwani uchunguzi waliofanya haujathibitisha kuwa Baraza lilipeleka mapendekezo.
"Ni vyema Baraza likafanyia kazi kwa nini kama kulikuwa na mapendekezo hayakufikishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Dar es Salaam) au Katibu Mkuu Kiongozi (Zanzibar)...tunaamini kabisa kama mapendekezo hayo yangekuwa yamewasilishwa, Rais angechagua mwakilishi kutokana na mapendekezo hayo," alisema.

Alisema Baraza hilo kutokuwa na wawakilishi, lakini litawakilishwa vyema na wajumbe walioteuliwa. Hivi karibuni maaskofu watano wa Makanisa ya Kipentekoste waliitisha mkutano wa waandishi wa habari wakilalamikia mjumbe wao kutopata uwakilishi katika Bunge hilo la Katiba ambalo limeanza juzi.

source Majira

Mapadre wa Tanzania matatani

Wakati Umoja wa Mataifa (UN), ukilikalia kooni Kanisa Katoliki kwa kile ulichodai kuwa halijafanya bidii kuwashughulikia makasisi wake wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kudhulumu watoto kingono, imebainika kuwa makasisi wawili wa Tanzania waliotuhumiwa kupokea misaada kutoka kundi la kishetani la Freemasons wametimuliwa bila huruma.

Wiki iliyopita, ripoti ya Umoja wa mataifa ilitolewa hadharani ikiyalaumu makao makuu ya Kanisa Katoliki Vatican, kwa kupuuzia au kuwalinda makasisi wake wenye kashfa ya kudhulumu watoto kingono, likataka hatua za haraka kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufichuliwa kwa mafaili yenye kashfa hiyo.

Wakati hali ikiwa hivyo, chanzo cha habari hii kililifanya mahojiano na mmoja wa wataalamu wa Kanisa hilo (Kasisi mashuhuri) ambaye alinza kwa kusema:
“Umoja wa mataifa hauwezi kulazimisha mabadiliko yoyote ndani ya Kanisa Katoliki, ni kweli kuwa kashfa hizi zipo, lakini haziwezi kulifanya kanisa libadili kanuni zake, likifanya hivyo litakuwa sio kanisa tena.”

Kisha aliongeza: “Kanisa Katoliki haliwezi kuongozwa na UN, linasheria zake kali, ni kwa sababu tu watu hawajui, mfumo wake wa ndani ni mkali na hauchukuliani na uovu, kuna makasisi wawili wametimuliwa nchini kwa kutuhumiwa kupokea pesa na misaada kutoka kundi la Freemasons.”

Akiongea kwa kujiamini  Kasisi huyo, alisema makasisi waliotimuliwa ni kutoka Wilaya ya Same na Arusha  na mwingine  wa Mwanza alienda baa na baada ya kulewa alizua tafrani na kupigana, na kutokana na hali hiyo kanisa limeshamfukuza mara moja.

“Nakuambia Askofu wa Jimbo la Mwanza alipopata habari hizo alitoka na barua mkononi na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake na kumsimamisha kazi. Huu ni ushahidi kuwa kanisa letu lipo makini, ingawa wengi wenu hamjui,” alisema mtoa habari wetu.

Akifafanua kuhusu tukio la kutimuliwa kwa makasisi waliopokea misaada ya kundi la Freemasons, alisema kuwa,  zamani makanisa  ya Katoliki yalikuwa yakipokea msaada kutoka Vatican, lakini utaratibu huo haupo kwa wakati huu na makanisa yanajitegemea kwa kuanzisha miradi yao, na hapo ndipo wengine walipopokea fedha  kutoka kwenye makundi  kama Freemasons.

Alisema kuwa baada ya kanisa kubaini taarifa hizo lilichunguza na kuwabaini mapadre kutoka Arusha na Same, kisha kuwasimamisha kazi wakisubiri uamuzi mgumu kutoka kwa Papa huko vatikani.
Kulingana na Taratibu za Kanisa Katoliki Padre anaweza kusimamishwa kazi na Askofu wake kwa mujibu wa taratibu na sheria za ndani ya kanisa (Canon Law) lakini hawezi kuvuliwa upadri kwani mwenye mamlaka hayo ni Baba Mtakatifu yaani Papa aliyeko madarakani.
Kisha chanzo cha habari yetu kiliendelea:

“Mfano miongoni mwa hoja nne za Umoja wa mataifa ni ukali wa wasimamizi wa shule za Katoliki, na ni kweli shule zina misimamo mikali sana. Kanisa limekataa kukubali kusikia kutoka nje kwa kuwa litapoteza ubora wa mafundisho yake, alisema na kuongeza:

“Unajua hapa kuna shinikizo la kuwataka mapadre waoe, lakini, si rahisi kukubalika. Misimamo ya mapadre imegawanyika kati ya Mashariki na Magharibi, mapadre wa Mashariki katika mataifa kama ya Urusi na Ukraine kabla ya kusimikwa wanaulizwa iwapo wanataka kuoa au laa, lakini wa Magharibi wanashikilia msimamo wa kutooa na hao ndio ninaowaunga mkono.”

“Ukiwa Padre ni lazima ujikane na ujitoe sadaka; sasa ukiwa na mke na familia si lazima utaipendelea kuliko wito wa kazi ya Mungu? Mimi kama kanisa litapitisha sheria ya kuoa nitaachana na ukasisi kwa kuwa sitaweza kutimiza wito wangu.”

Hata hivyo akaonya kuwa wale wote waliowahi kula kiapo cha ukasisi, hata wakiacha kamwe hawawezi kuishi vyema na wanawake wala kupata Baraka za Mungu.

“Angalia hata huyu Dk….(jina tunalihifadhi) aliacha upadre na kuamua kuoa lakini amekaa  na mke wa pili sasa na bado  hajafanikiwa  hata cheo anachotaka hawezi kukipata kwa kuwa aliacha kiapo chake, na  kuingia kwenye siasa,” alisema.

Alisema kuwa hata yeye amekuwa akitegwa na akina dada, lakini ameshinda majaribu kwa kuwa muwazi kutangaza hadharani wale wanaomjaribu ikiwa ni pamoja na kuwataja mimbarani.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bi. Kirsten Sandberg, kiongozi wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za watoto (CRC) alionya kuwa ukimya  wa Vatican kuhusu matukio ya kunyanyaswa  watoto kingono ni hatari  na lazima uvunjwe mara moja, wahusika watolewe ndani ya wigo mzito wa Roma na kuachiwa vyombo vya sheria.

Kisha aliongeza: “UN inaitaka Vatican kuwaondoa kwa haraka makasisi wote waliowahi kupata kashfa ya ngono na kashfa zote zinazojulikana lazima zichukuliwe hatua haraka.”

 Taasisi hiyo inayochunguza haki za watoto iliitaka mamlaka ya kiti kitakatifu cha Roma “Holy See” kubadili sera zake ambazo zinaonekana kuwa kichocheo cha makasisi wake kumalizia haja zao za kingono kwa watoto.

 “UN inaitaka Vatican kubadili msimamo wake mkali kuhusu utoaji wa mimba, matumizi ya vidonge au mbinu za kuzuia mimba ambayo imepitwa na wakati na haiwezi kutekelezeka katika nyakati hizi.
 Vaticani katika majibu yake ilisema kuwa itaichunguza ripoti yenyewe pamoja na waandaaji wake kabla ya kutoa msimamo wake. Hata hivyo kundi la makasisi waliosaidia kufichua vitendo hivyo Marekani limeikaribisha ripoti hiyo kwa mikono miwili. Wakati Vaticani ikidai kuchunguza riporti hiyo tayari baadhi ya yale yaliyotajwa na Umoja wa mataifa imeshayatupilia mbali ikisema ni  maovu na yasiyopaswa kujadiliwa na kanisa hilo kulingana na utamaduni wake.

Wachambuzi wanasema kuwa kwa kawaida kanisa hushikilia sheria zake zijulikanazo kama Canon Law, kuwa zinapaswa kutangulizwa mbele kabla ya sheria za kawaida za kijamii “criminal law” katika kushughulikia masuala yanayojitokeza ndani na ya kanisa

Kutoka Kwa Pastor Carlos Kirimbai

Sio kawaida yangu kuanza somo na ushuhuda ila hili nimeamua kulianza na ushuhuda kutokana na unyeti wa somo lenyewe.
Pastor Carlos Kirimbai Manna Tabernacle Bible Church

Miaka kadhaa iliyopita kuna dada mmoja ambaye nilikuwa namfahamu, alikuwa akiteswa sana na hali ya kutopata watoto. Ni jambo lilikuwa linamsumubua sana kwenye ndoa yake na alikuwa amenishirikisha na nikamwandalia kitini chenye ahadi... za Mungu juu ya kupata watoto na nikamhakikishia kuwa ahadi za Mungu zote katika Kristo Yesu ni ndiyo na amina.

Lakini pamoja na hayo bado huyu dada akaendelea kuteswa na hiyo hali ya kutopata watoto. Ikitokea anapata uja uzito ule uja uzito unatoka ukiwa na miezi michache sana. Hii ilinisumbua sana kama Mchungaji wake maana neno la Mungu lipo wazi kuwa hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba wala aliye tasa miongoni mwa watu wa Mungu. Neno la Mungu lipo wazi kabisa kuwa watoto ni Baraka itokayo kwa Mungu na uzao wa tumbo ni thawabu Yake. Hii ilinisumbua sana maana huyu dada alikuwa ameokoka na hapakuwa na sababu yoyote ya msingi kwanini awe anateswa kwa namna hii.

Siku moja nikiwa naliwaza hili ili nipate solution ya Kimungu juu ya tatizo la huyu dada nikasikia moyoni maneno yanayopatikana kwenye moja ya maandiko nitakayotumia katika fundisho hili: “Agano na mauti, mapatano na kuzimu.” Nilishtuka sana maana niliisikia as clear as wewe unavyoweza kusikia mimi nikisema na wewe. Nikauliza huko huko moyoni, Lakini Mungu huyu ni mtoto wako ana agano na wewe na mapatano na wewe kupitia damu ya Yesu, iweje tena awe na agano na mauti na mapatano na kuzimu? Nikasikia tena maneno hayo hayo yakijirudia. Nikajua this is serious. Nikauliza tena huko moyoni How? Nikasikia wazi wazi “BLOOD GUILTINESS.” Nikashtuka maana nilielewa sasa Mungu anasema nini. Nikauliza Mungu huyu binti kaua mtu? Jibu lilinishtusha sana. Aliniambia ameua watu sio mtu. Nikasema kwa sauti nikiwa peke yangu, “My God! Whaaaaaaaat?!!!!!!” akarudia tena, ameua watu sio mtu. Sasa hapo naongea kwa sauti ya wazi wakati Yeye Mungu ananisemesha moyoni.

Nilikaa sakafuni chumbani kwangu nikasema, Mungu hapa sikuelewiiiii! Kaua watu gani! Akaniuliza hivi wewe hujui watu wanavyo ua na hawajioni kuwa ni shida? Nikamdaka hapo hapo. Nikaambiwa mwite muulize. Nilimtafuta huyu binti nikamwambia nahitaji kuonana na wewe. Tukapanga siku atakayokuja kuniona alipokuja sikumzunguka nikamwuliza binti embu niambie umemwua nani na umewaua wangapi maana Mungu ananiambia hupati watoto kwa kuwa wewe ni mwuaji. Alishika kichwa akasema “My God!!!” akainama huku machozi yanamtoka. Nikamwuliza binti umeshawahi kutoa mimba? Akaniambia ndiyo mchungaji. Sikutaka kumpotezea wakati maana alihitaji suluhisho la haraka kwa ajili ya uteka wake. Nikamwambia sasa mwanangu kutoa kwako mimba kumegeuza tumbo lako la uzazi badala ya kuwa chanzo cha uhai na mahali pa salama pa kumkuza mtoto, pamekuwa kiwanda cha kuulia watoto wanaoingia hapo. Tumbo lako lina agano na mauti na mapatano na kuzimu kwa sababu umekuwa ukiua watoto ambao wamekuwa wakiingia humo ndani. Akaniambia ni kweli Pastor. Nikamwambia unateswa na hatia ya damu na hilo litabidi tu livunjwe. Neno linasema tuungamiane dhambi zetu sisi kwa sisi na kuombeana tupate kupona. Hapo akawa kaungama dhambi yake. Nikamwongoza sala ya kuvunja hilo agano na mauti na mapatano na kuzimu sawasawa na ilivyofunuliwa kwenye neno. Nikaomba naye akalia sana. Akasema sasa Pastor nina amani. Nikamwambia nenda sasa kazae. Namshukuru Mungu ule uteka wa miaka ulivunjwa na sasa huyu dada na mumewe wana watoto.

Kama umeua kwa kukusudia au kutokukusudia inawezekana unateswa na shida hii ya hatia ya damu. Inawezekana kabisa umeingia katika agano na mauti na mapatano na kuzimu ambayo yanakutesa na kuzuia au kuua vitu vyako vingi.Tutalifuatilia hili jambo kimaandiko na kuleta suluhisho la msalaba kwa tatizo hili gumu ambalo linatesa maisha ya wengi.

Daudi alifanya kosa la kuzini na mke wa mtu akampa huyo mke wa mtu mimba alafu akafunika hilo kosa kwa kuua mumewe. Kama ambavyo sisi tunafanya uasherati au uzinzi tunampa mtu au kupewa mimba na katika jitihada za kufunika hiyo aibu tunaamua kuitoa hiyo mimba ambayo kimsingi ni kuua.

Yai la mwanamke likishakutana na mbegu ya kiume na mimba ikatungwa Yule ni mtu katika hatua zake za awali. Hutoi bonge la damu au bonge la nyama unaua mtu na unamwaga damu usiyo na hatia.

Daudi alipogundulika alilikwenda mbele za Mungu kwa toba lakini pamoja na toba akaomba aponywe na damu za watu.

Zaburi 51: 14.

14Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,Uniponye na damu za watu,Na ulimi wangu utaiimba haki yako.

Damu za watu zilileta shida katika maisha ya Daudi.

Naipenda inavyosema kwenye bibilia ya kiingereza:

“Deliver me from the guilt of bloodshed,……”

Kimsingi anaomba akombolewe na hatia ya damu aliyoimwaga.

Utashangaa pale awali Daudi alipotubu baada ya nabii Nathan kuja na kuiweka wazi dhambi yake, aliambiwa amesamehewa ila athari za dhambi yake hii ziliachiliwa juu yake na ndicho Daudi alichokuwa anashughulikia hapa kwenye haya maombi ya Zaburi 51.

I Samweli 12: 10 – 14.

10Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. 11BWANA asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. 12Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. 13Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. 14Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.

Pamoja na kwamba alisamehewa dhambi yake lakini kuna mauti ilifunguliwa kuingia kweye nyumba ya Daudi kupitia kitendo chake cha kuua mtu. Unapotoa mimba unaifungulia mauti kuingia katika maisha yako hususa kwenye uzazi wako. Haijalishi ni mwanaume au ni mwanamke. Ukitoa mimba au kusaidia kutoa mimba umeua au umesaidia kuua.Daudi alitamani kumjengea Mungu nyumba lakini akaambiwa hataweza kujenga kwa sababu mikono yake ilikuwa na damu. Hii roho ya mauti na kuzimu unayoifungulia maishani mwako kwa njia ya kuua itakugharimu sana. Itakunyanganya mpaka uwezo wa kujenga.

Bahati mbaya sana sio wasioamini tu wanatoa mimba siku hizi mpaka waaminio na mbaya zaidi waliyo ndani ya ndoa. Aibu ya mama kushika mimba mapema mno baada ya mtoto kuzaliwa labda miezi michache inawafanya waitoe. Ni kuua huko. Ni kuuondoa uhai wa mtu asiye na hatia. Umemnyima mtu asiuone mwanga wa jua, yote kwa sababu ya kuficha kitu.

Mungu anachukia mikono iliyo myepesi kumwaga damu.

Mithali 6: 16, 17.

16Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA;Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo,Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

Kama Mungu anaichukia mikono imwagayo damu niambie ni kwa namna gani mikono hiyo hiyo kazi zake zinabarikiwa? Unakwama kimaisha, kitaaluma, kibiashara, kikazi, kimasomo, yote kwa dhambi ya kumwaga damu isiyo na hatia. Mbaya zaidi kuna kuwa na mauti imeachiliwa inayoharibu hata kilichopo.

Kaini aliimwaga damu ya nduguye Habili ikamletea madhara makubwa sana.

Mwanzo 4: 8 – 12.

8Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua. 9BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

Kaini alikuwa ni mkulima na aliitegemea ardhi na bado hakuzingatia hilo, akaimwaga damu ya nduguye kwenye uwanda ule ule ambao alikuwa anautegemea umpe mazao. Ile damu ikamlilia Mungu. Alinyamazisha sauti ya Habili lakini hakunyamazisha sauti ya damu ya Habili. Mungu akamwambia Kaini kuwa amelaaniwa katika ardhi iliyopokea damu ya ndugu yake, atakapoilima haitampa mazao na sio hivyo tu atakuwa mtoro au mzururaji na mtu asiye na makao. Ninaamini huu uzururaji wa Kaini na kutanga tanga kwa Kaini kulisababishwa na yeye kudhani ni hapo alipo ndo pana shida so anajaribu na kwingine na kwingine na kwingine asijue uhusiano wake na ardhi ambao ndo chanzo cha mapato yake umeharibiwa kupitia tendo lake hilo la kumwaga damu. Kaua ili yeye hakuuawa bali shughuli zake ndo zikauawa.

Unatumia kipato chako kuua alafu bado unategemea utaendelea tu kubarikiwa kupitia chanzo hicho. Ndo ushaachilia mauti kwenye shughuli zako. Umefanikiwa kuficha aibu ila hujafaikiwa kuzuia athari za uuaji wako.

Musa aliua mtu akamzika akijua hakuna aliyemgundua, kumbe kuna aliyemwona. Sawa umewaficha watu, je shetani umemficha, Mungu naye umemficha? Itakuja kutakwa tu mikononi mwako. Umeinyamazisha sauti ya kimwili ila ya kiroho umeshindwa kuinyamazisha na ndo inayolia kisasi kisasi kisasi. Hakuwa na hatia na ukamwua. Huwezi kuepuka athari za mauti na kuzimu.Musa akaja kujua watu wamejua na hiyo ikaifungulia hatia ya damu maishani mwake akakimbia na kutokomea jangwani kwa miaka 40 na kuchelewesha ukombozi wa wana wa Israeli kwa miaka 30.

Maana Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa wana wa Israeli watakaa utumwani miaka 400 lakini wakaishia kukaa utumwani miaka 430 kwa sababu ya hatia ya damu iliyomkamata Musa. Alijaribu kufanya miaka kumi kabla ya wakati akaachilia hatia ya damu ambayo ilimkimbiza kwa miaka 40. Usiendelee kuiacha hatia ya damu ikutese. Inakucheleweshea mambo yako bila sababu. Yesu ameshakufa msalabani amechukua dhambi zako mpaka hatia yako ya damu. Damu Yake iliyomwagika kwa ajili yako inakunenea mema kuliko damu ya kina Habili au hao ambao umemwaga damu zao pasipo hatia yoyote.

Nilishangaa sana nilipokuwa nafuatilia kazi za damu ya Yesu.

Ina samehe na kukomboa.

Efeso 1: 7.

7Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.

Utasamehewa na kukombolewa na athari mbaya za hatia ya damu kama ukitubia makosa yako ya kuua na kumwaga damu isiyo na hatia.

Kuna wakati Daudi alipokuwa mfalme kulikuwa na ukame katika ufalme wake miaka mitatu mfululizo. Alipomwuliza Bwana akakuta ni hatia ya damu ndo sababu ya hayo majanga.

II Samwli 21: 1.

1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.

Ukame ule ulisababishwa na kiti cha Ufalme na ikafungulia shida kwenye himaya nzima iliyo chini ya kiti hicho Ukame. Wewe nawe ni mfalme wa Kahimaya kako. Damu isiyo na hatia uliyo mwaga au kwa kutoa mimba au vinginevyo imesababisha huo ukame unaopitia katika maeneo mbali mbali ya maisha yako. Daudi akataka kujua nini kifanyike na jawabu likawa watu wa nyumba ya mhusika wa kuua wauawe ili kuridhisha kisasi cha damu iliyomwagika na ilipofanyika hivyo, mvua ikanyesha. Sisemi lazima mtu afe. Kuna aliyekufa ili kuvunja hatia ya damu inayokutesa na Jina Lake ni Yesu maana imeadikwa adhabu ya amani yetu iliwekwa juu Yake. Unapokuja kwa Yesu na kuikiri dhambi yako ya kuua utapokea msamaha na athari za hiyo dhambi na hatia ya umwagaji damu itavunjwa maishani mwako kwa Jina la Yesu na mvua itaanza kunyesha tena. Ukame utavunjwa na utaanza kuexperience uhuru kamili katika uchumi wako. Fikiria taifa zima liliingia kwenye maafa ya kiuchumi kwa sabau ya hatia ya damu.

Je kuna uwezekano kuna maafa ya kifedha maishani mwako kwa sababu ya hati ya damu? Je kuna vurugu za kifamilia kwako kwa sababu ya hatia ya damu? Je inawezekana mambo yako hayaendi kwa sababu ya hati ya damu?

Ndugu tengeneza ukitumia mwanga unaopata kwenye hili somo ufunguliwe utembee katika uhuru ambao Kristo amekununulia kwa uhai na damu Yake.

Wakati wa Agano la Kale kulikuwa na kitu kinaitwa miji ya makimbilio.

Kumbukumbu 19: 1 – 6.

1 BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa yenye nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nawe ukawafuata, na kukaa katika miji yao, na katika nyumba zao; 2itenge miji mitatu iwe kwako katikati ya nchi yako, akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki. 3Itengeze njia, igawanye na mipaka ya nchi yako, akurithishayo BWANA, Mungu wako, iwe mafungu matatu, ili kwamba kila mwenye kuua mtu apate kukimbilia huko. 4Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kuua mtu, atakayekimbilia huko awe hai; atakayemwua mwenziwe pasipo kukusudia, wala hakumchukia tangu hapo; 5kama aingiapo mtu na mwenziwe mwituni kwenda kukata kuni, akapeleka mkono wake na shoka ili kukata mti, likatoka shoka katika mpini, likampiga yule mwenziwe hata akafa; basi na akimbilie katika miji hii mmojawapo awe hai; 6asije akaandamiwa mwuaji na mwenye kulipiza kisasi cha damu, moyo wake ukali na hasira, akampata kwa njia kuwa ndefu, akamwua; wala hana haki ya kuuawa, kwa kuwa hakumchukia tangu hapo.

Hii miji ya makimbilio ilikuwa kwasababu ya wale ambao wameua bila ya kukusudia ili wakimbilie huko ili mlipiza kisasi cha damu asije akawaua wakati ni jambo wamelifanya kwa kutokukusudia. Hii ina maana kuwa kama mtu alifanya kwa kukusudia asingeweza kukimbilia kwenye hii miji. Hata angekimbilia mlipiza kisasi cha damu angekuja tu kudai atolewe. Sasa wewe umeua kabisa kwa kukusudia alafu unajifanya unakimbilia kwa Yesu kujificha. Hutaepuka kisasi cha mlipiza kisasi cha damu isipokuwa Yesu kaingilia kati na kwa njia ya wewe kuitubu hiyo dhambi maususi, ili sadaka ya Yesu ya Uhai na Damu Yake vichukue nafasi yako wewe ili kukuepusha na athari za mlipa kisasi cha damu.Usifanye shingo yako ngumu. Usipotezee maana haipotezeki. Mruhusu Yesu akuweke huru na athari za mlipa kisasi cha damu uliyomwaga ili wewe uwe huru.

Unapomwaga damu ili kuficha majanga yako, umekimbilia chini ya maneno yasiyo ya kweli na kwa njia hiyo umeachilia agano la mauti na mapatano ya kuzimu. Ni hilo agano na mauti na hayo mapatano na kuzimu ndo yanaua kazi zako, furaha yako, amani yako, na vitu vingine vilivyokuuzunguka.

Isaya 28: 15.

15Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;

Ukifanya tu maneno ya uwongo kuwa kimbilio na kujificha chini ya maneno yasiyo kweli unajiingiza kwenye agano na mauti na mapatano na kuzimu.

Umeificha hiyo mimba kwa kuua, umeunyamazisha huo ukweli kwa kuua, haya sasa mauti ina wewe, kuzimu haikuachi.

Ila kuna habari njema hapa:

Isaya 28: 16.

16kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

Jiwe hili lililowekwa Sayuni ni Yesu Kristo na amewekwa mahususi kushughulika na hili agano na mauti, na haya mapatano na kuzimu.

Isaya 28: 18.

18Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.

Njoo kwa Yesu ubatilishiwe hilo agano na mauti na kuangushiwa chini hayo mapatano na kuzimu.

Mwendee Yesu na mwanga huu uliyoupata na ufunguliwe kabisa na athari mbaya za Hatia ya damu kwa Jina la Yesu. Usisahau kuvunja hilo agano na mauti na mapatano na kuzimu kwa Jina la Yesu ili uwe huru.

UMEBARIKIWA NA UMEREHEMIWA

Soul Music Gosple Concert


The Kingdom expands when Christians take risks for the Gospel

Steve Stewart is the founder of Impact Nations, an international ministry passionate about sharing the Gospel and healing power of Jesus among the poorest communities around the world.

His heart is to see the Kingdom of God advance, both through supernatural intervention and the practical support of Christians. He believes that we are all called to be active in God's plan for redemption, and that the western Church must learn from the faith movement gaining momentum in countries such as India, where house churches are growing in spite of intense persecution in some areas.
Steve and his wife Christina
"There is a certain irony that although we in the West pursue vicarious adventure through entertainment, we are reluctant to speak in large terms. Although we in the church should be the most vocal in calling people up to a great purpose, the great adventure of living in the Kingdom of God, we settle for small things in this present age," Steve writes in his book, 'When everything changes'.

"We put our desires and hopes off into the Age to Come. With over half the world suffering in extreme poverty, with more slaves living now than at any time in history, there has never been a greater need for men and women to rise up and activate their faith.

"This is a joyful, exuberant call to action," he says.

Christian Today got the opportunity to catch up with Steve, and learn more of his desire to see people capture God's vision to see people lifted out of hopelessness and desperation across the globe.

CT: One of your passions is to see people become active in God's redemptive plan. Why is it so important?

SS: Romans 8:19-22 tells us that all of creation is groaning, waiting for the sons - and daughters - of God to be revealed. We are called to participate in the rescue, reconciliation and restoration activity of God's Kingdom. This is what we were made for.  The Kingdom is in our DNA and when we start to move in its rhythm, we come alive. It amazes me that the Creator of everything invites us to partner with Him in His great purpose.

CT: How can the Church be released to become less passive?

SS: Jesus has always invited and challenged men and women to a lifestyle of active faith. To follow Him (Matthew 4:19-20) means movement from something to something. Discipleship is never static. As Jesus said in John 12:26: if we want to be His disciples, then we must follow Him, and if we are going to follow Him, then we must be where He is. One of the key ways that Jesus forms us is through the movement of following Him into new situations. At the end of the Sermon on the Mount, Jesus says that the only difference between the one who builds his life on the rock and the one who builds on the sand is putting Jesus' words into practice. Moving from theoretical belief to active participation is one of the greatest dividing lines in the 21st century church.

Maaskofu wakataa ushoga Uingereza

Maaskofu wakuu nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja.

Pia walisema kwamba hawatakubali kuona viongozi wa dini kwenda kinyume na maagizo hayo nchini humo.
Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa maelewano kwamba hawatashiriki ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia walipiga marufuku maombi yoyote maalumu kwa wanandoa wa jinsia moja licha ya ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza kufanya hivyo iwapo wanajihisi.
Hata hivyo walidai viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasiyo rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
Uganda
Kwa upande wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na mswada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009.Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.

Source:Mwananchi