Maaskofu waomba serikali kuingilia kati


VIONGOZI wa makanisa wa Zanzibar wametoa malalamiko yao ya vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa kisiwani humo na kutaja vitendo 23 huku wakiitaka Serikali kuingilia kati
Katibu wa umoja wa Wachungaji wa Zanzibar Jeremiah Kobero alisema kuwa licha ya makanisa matatu yaliyochomwa na kubomolewa katika vurugu za sasa, kuna matukio 23 ya uchomaji moto makanisa yametokea tangu mwaka 2001.
Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na uchomwaji moto wa makanisa ya The Church of God na Sloam yaliyofanyika mwaka 2011, makanisa mawili yaliyoko Masunguni yote mwaka huo huo, Kanisa la EAGT la Fuoni mwaka huo, kanisa la Pefa mwaka 2009, kanisa la Mwera mwaka 2012, kanisa la Redeemed lililiopo Dilikane mwaka 2001 yote ya mkoa wa Mjini Magharibi.
Alitaja pia makanisa yaliyochomwa katika mkoa wa Kaskazini kuwa kanisa la Tunguu, Unguja Ukuu, kanisa la CMF, Chukwani na Manyanya.
Alitaja pia kuwepo kwa tabia hiyo kisiwani Pemba akisema kuwa imekuwa ni tabia kwa wakristo kusumbuliwa.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la TAG Kariakoo Zanzibar Dickson Kaganga aliwataka Viongozi wa serikali kuchukua tahadhari mapema kabla vurugu hazijatokea.
“Wakristo tumewafundisha kuvumilia…juzi walipovamia hapa walichoma moto biblia 50, ingekuwaje sisi tungechoma japo kitabu kimoja cha Kurani? Hayo makanisa yote yaliyochomwa, taarifa ziko polisi, lakini ukienda kutoa taarifa unaulizwa, una kibali? Yaani wanakutafutia tena kosa” alisema Askofu Kaganga.
Kaganga ambaye wakati wote alikuwa akibubujikwa na machozi aliwataka Wazanzibar kutambua umuhimu wa muungano kuwa ni pamoja na kuenezwa kwa dini.
“Unapoona makanisa yanaenea hapa, ujue na kule bara misikiti inaenezwa na Wapemba ambao ni wajasiri wa biashara. Hiyo ndiyo faida ya muungano ndiyo faida ya kuoleana” alisema.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa askofu wa TAG kitaifa Askofu Magnus Mhiche alihoji kitendo cha wahuni kuvamia makanisa ilihali Serikali ikiwepo madarakani,
“Mimi siamini kama ni Waislamu wamefanya haya, ila najiuliza, kama siyo wao basi ni wahuni. Hivi kweli wahuni wanatawala Zanzibar?” alihoji.
Naye Askofu wa kanisa kuu la Anglican Michael Hafidhi aliiomba Serikali kudhibiti mahubiri yanayotukana dini ya kikristo kwa njia ya kaseti akidai kuwa yanachochea vurugu.
“Zipo Kaseti zinazotukana ukristo, zinachochea vurugu, tunaomba serikali idhibiti. Hata ile kamati yetu ya ushirikiano wa dinio nayo imekufa inabidi ifufuliwe.
Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Jongo aliwataka Waislamu kuchukuliwana na Wakristo akisema kuwa hata Mtume (SAW) alifanya hivyo wakati akiitetea dini yake.
“Hata Mtume wetu alipopata taabu alipokuwa Madina alikimbilia kwa Wakristo. Mpaka uislamu ulipoenea Makka yote. Hata alipotoka Medina na kwenda Mecca aliyempeleka hakuwa muislamu. Nashangaa leo ninaposikia eti Waislam wanachoma makanisa” alisema Jongo na kuongeza,
“Hawa ni waislamu gani, mbona wamechoma hata bendera ya CCM, wamechoma bar na kunywa bia. Nini hasa malengo yao?
WAZIRI wa nchi katika Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Aboud amepiga marufuku mihadhara na maandamano yanayofanywa na vikundi vinavyopinga muungano akisema kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria.
Waziri Aboud aliyasema jana hayo baada ya kutembelea kanisa la Assemblies Of God lililopo eneo la Karikoo mjini Zanzibar lililochomwa moto na kubomolewa kutokana na vurugu zilizozuka kufuatia kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa kundi la Jumuiya za mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho).
Katika ziara hiyo ambayo aliongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, Waziri Aboud alisema baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi yanayosabaisha vurugu.
“Baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi, yanachochea vurugu zote hizi…. Maneno ni sumu, ndiyo tumeiingiza nchi katika machafuko yote haya” alisema Waziri Aboud na kuongeza,
“Sisi kama Serikali tumewaita wenye makundi hayo na kuzungumza. Tumewaambia, kama mtu hataki dini aje kwenye majukwaa ya siasa. Tumekosea kuwaachia watu waanzishe vyama na vimesajiliwa kisheria kwa lengo la kueneza dini, lakini sasa wanaleta uchochezi.
“Kuanzia sasa ni marufuku kufanya maandamano na mikusanyiko yoyote ya aina hiyo” alisisitiza Waziri Aboud.
Naye IGP Said Mwema alisema kuwa jeshi hilo limeongeza ulizni katika maeneo maalum yenye usalama mdogo hasa makanisa.
“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tunadhibiti maeneo maalum ili yasiendelee kuvamiwa. Tunafanya uchunguzi, ili kuhakikisha nani, kwa nini na wako wapi” alisema IGP Mwema.
Alisema jeshi hilo kwa sasa lina kikosi maalum kwaajili ya kuongeza nguvu ya kudhibiti machafuko kisiwani humo na kwamba hadi jana jeshi hilo lilikuwa limekamata watu 46 na kati yao 43 wamefikishwa mahakamani huku wengine watattu wakifanyiwa uchuguzi.
Aidha IGP Mwema alikiri kwamba jeshi hilo limecghelewa kuzuia uhalifu huo na kwamba hatua iliyopo sasa ni kudhibiti usiendelee.
“Kuna mifumo mitatu ya ulinzi, kwanza ni kuzuia kabla mambo hayajatokea, kwa hapo sisi tumeshachelewa. Tuko hatua ya kudhibiti yasiendelee na baada ya hapo tutajenga amani iwe endelevu” alisema.
Wakati huo huo Chama Cha Mapinduzi CCM kimesikitishwa na vurugu zilizotokea ambazo wanaamini kuwa zimeandaliwa na Jumuiya za Uamsho na kuitaka serikali kuchukua tahadhari kubwa katika suala hilo kwani kama hatua hizio hazijachukuliwa huenda likaleta maafa makubwa.
“Cham cha Mapinduzi kinaalani vitendo hivyo na kuzitaka serikali zote kudhibiti hali ya amani na utulivu tulioizowea na kuwachukulia hatua kali wote waliosababisha vurugu hizi” alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kwa upande wake chama cha Chadema kimelaani vurugu hizo zilizofanywa kwa makusudi na vijana ambao wanaonekana wameshapata mafunzo maalumu kwa kusaidiwa na chama kimoja cha kisiasa kinachounda serikali ya umoja wa kitaifa.
“Chadema tunavitaka vyama vya siasa kuandaa makundi ya vijana ambayo mwisho wake wanakosa kuwapatia kazi na hatima yake kuwa vikundi vya kihalifu nchini” ilisema taaifa hiyo iliyotiwa saini na Hamad Yussuf Naibu Katibu Mkuu.
Chama Cha Wananchi CUF kimelaani vurugu hizo na kusema zimesababishwa na chuki binfasi, ukosefu wa hekima, matumizi ya nguvu za dola na uchochezi wa makusudi kwa wale wasiopendeleaq maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar.
“Vitendo vya watu wachache na kuharibu mali za watu ni uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa kizanzibari, uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua bila ya uonevu wala upendele” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Salim Bimani.

A One Night Seminar-Dar-es-Salaam Workers Christian Fellowship


Vurugu zasababisha Kanisa kuchomwa Moto Zanzibar


Kwa kile kilichoonekana kuwa ni uvunjikaji wa Amani katika Visiwa Vya Zanzibar hasa kwa Jamii ya Wakristo inazidi kuwa tete baada ya Kanisa la TAG eneo la Kariakoo Visiwani Zanzibar linaloongozwa na Bishop Dickson Kaganga Visiwani humo kulipuliwa kwa kitu kinachosadikika kuwa ni bomu na kuteketeza sehemu kubwa ya madhabahuni mwa kanisa hilo na sehemu za Milango ya Kanisa hilo.

Kanisa hilo lililokuwa na uwezo wa kuchukua Waumini zaidi ya 1000 limechomwa moto ikiwa ni mara ya pili baada ya mara ya kwanza kitu kinachosadikika kuwa ni bomu kutupwa ndani ya kanisa hilo mwanzoni mwa mwaka huu na bomu hilo kushindwa kulipuka wakati wa Ibada.
 

                                                Gari iliyokuwa ikitumiwa na Pastor Dick

Baada ya Uchunguzi wa Polisi katika tukio la kwanza Polisi walisema bomu hilo lilokuwa na uwezo wa kuteketeza kila kitu kilichomo ndani ya Kanisa hilo lakini ajabu halikuweza kulipuka wakati lilikuwa tayari kwa kulipuka.

Kumekuwa na hali ya Sinto fahamu kwa Wakristo wengi wanaoabudu katika Makanisa Visiwani Zanzibar na kasi ya Serikali katika Kushughulikia masuala haya imekuwa si ya kuridhisha.

                                                      Pastor Dick alipokuwa akihojiwa leo na

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWALIMU MWAKASEGE

Semina ya Neno la Mungu na Mtumishi wa Mungu Christopher Mwakasege ikitarajiwa kuanza majira ya saa 12 jioni na kuendelea,waimbaji kadhaa watanzania wa injili nchini humo watakuwepo kuhudumukatika semeina hiyo,ni pamoja na J'sisters  Flora Mbasha na mumewe wako nchini Marekani i,Watanzania na wakazi wa mji wa Maryland na maeneo mengine watakwepo kuhudhulia katika semina hiyo ili kusikia kutoka kwa Mungu,Kama una ndugu yako huko pia unaweza kumkaribish katika semina hiyo.

Malawi kuharalisha sheria ya mapenzi ya jinsia moja



Rais wa Malawi,Joyce Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994.
Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.


Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada kwa nchi za kiafrika ambazo hazitatambua haki za mashoga.
Rais Banda alichukua hatamu za uongozi mwezi jana kutoka kwa mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliyeaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.
Hadi sasa rais huyo amegeuza baadhi ya sera zake ikiwemo kushusha thamani ya sarafau ya nchi kwa lengo la kuanza kupata msaada .

Wafadhili wengi walisitisha msaada chini ya utawala wa Mutharika, wakimtuhumu kwa uongozi duni pamoja na ukandamizaji.Katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la anchi Banda alisema kuwa baadhi ya sheria zilizopitishwa na bunge, zitafutiliwa mbali kama hatua ya dharura ikiwemo sheria zinazopinga vitendo visivyo vya kawaida.


Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani mjini Blantyre, anasema kuwa rais anaungwa mkono na wabunge wengi, na kwa hivyo ataweza kuwashawishi wabunge kubatilisha sheria hiyo.

source :.bbc.swahili








WAKATI UMEFIKA SASA KUPENDEKEZA WASHIRIKI WA AFRICA GOSPEL MUSIC AWARDS.

 


Kwa muda sasa watanzania wamekuwa hawajui lolote kuhusu namna ya kushiriki katika TUZO ZA MUZIKI WA INJILI BARANI AFRIKA(Africa Gospel Music Awards) ingawa wanapenda. Toka tuzo za Muziki wa injili Barani Afrika zilipoanza, mwamko kwa watanzania kushiriki umekuwa mdogo, na hii ni kutokana na sintofahamu kwa wadau wa muziki huo kuanzia kwa

1.Wanamuziki wenyewe
2.Mameneja wa wanamuziki hao
3.Waandishi wa habari na Kanisa kwa ujumla.
Hivyo basi Kuanzia tarehe 21st April 2012 mpaka 21May 201 ni muda wa kupendekeza washiriki na tumebakiwa na takribani wiki moja tu ya kupendekeza. Ili kupendekeza unatakiwa;

a)Uandike kategori ambayo unataka mwanamuziki wa injili kutoka Tanzania aingie
b)Jina la mwanamuziki mwenyewe kisha utume jina hilo na
c)kazi yake aliyofanya kwa mwaka 2011 April – 2012April na
d)sababu ya kumchagua kwenda kwenye email;
nominations@africagospelawards.com
Mfano

Category: BEST ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
I do nominate : Christina shusho from Tanzania
Song:Thamani ya wokovu wangu
Reason:Her songs has restores many souls to the Kingdom of GOD
Kisha unatuma kupitia email tajwa hapo juu
Vipengele(categories) ambavyo unatakiwa kuchagua mtanzania wa kutuwakilisha ni pamoja na;

1. GROUP/CHOIR OF THE YEAR
2. MALE ARTISTE OF THE YEAR
3. FEMALE ARTISTE OF THE YEAR
4. BEST ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
5. EVENT OF THE YEAR

Kwa kufanya hivyo utakuwa umemuwezesha mwanamuziki wa injili kutoka nchini kuingia kwenye Nomination pull ya Tuzo hizo. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 7th July 2012 jijini London nchini Uingereza, wakati zoezi la kupiga kura baada ya nomination list kutoka, litaanza tarehe 1May-30june 2012.

Watanzania, tuamke na Kuwapendekeza washiriki wa Tuzo hizi toka Nchini Tanzania ili tuweze kuinua Muziki wetu wa Injili. Kwa Pamoja tutafanikisha hili. Kwa kupata undani wa tuzo hizo unaweza Tembelea: http://africagospelawards.com/

Kanisa La FGBF Lamfanyia Maombi Mbunge Deo Filikunjombe

SIKU moja baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kupokelewa jimboni na wapiga kura wake kama mfalme Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(F.G.B.F) linaloongoza na askofu Zacharia Kakobe wilayani Ludewa lamfanyia maombi maalum .

Huku mwenyewe akiahidi kuendelea kupambana na Vitendo vya ufisadi kwa Taifa bila kuogopa na kuwaomba Waumini wa Kanisa hilo na madhehebu mengine pamoja na wapiga kura wake wote kuzidi kumwombea zaidi Kwani kazi iliyopo mbele yake ya kupambana na ufisadi ni nzito yahitaji maombi.Kanisa hilo limfanyia mbunge Filikunjombe maombi hayo jana katika ibada maalum ambayo iliandaliwa na uongozi wa Kanisa hilo kama njia ya kuungana na vyama vya siasa na wananchi wa jimbo hilo kuutambua mchango na kazi nzito ya mbunge huyo katika kupambana na vitendo vya ufisadi nchini.

Katika maombi idaba hiyo Mchungaji wa Kanisa hilo Faustin Sambilanda.alisema kuwa kazi ilinayofanywa na Filikunjombe katika kulipigania Taifa ni kubwa na hivyo kila mtanzania na kila kiongozi wa dini wanaowajibu wa kuendelea kumwombea mbunge huyo na wengine ambao wapo kwa maslahi ya watanzania .


Alisema kuwa uamuzi wa mbunge Filikunjombe kuwemo katika orodha ya wabunge wasio na imani na waziri mkuu Mizengo Pinda na kupelekea Rais Jakaya Kikwete kubadili baraza baraza lake na mawaziri na kuwaondoa wale waliotuhumiwa kwa ufisadi si jambo dongo na kuwa wananchi wa Ludewa wanaungana na watanzania katika kuunga mkono uamuzi wa wabunge wapambanaji wa ufisadi akiwemo Filikunjombe.Hata hivyo alisema wanaweka utaratibu wa kuendelea kumfanyia maombi maalum kwa ajili ya kazi nzito anayoifanya ambayo silaha pekee ni maombi na si vinginevyo .
                                               Filikunjombe akiombewa Siku Ya Leo.

Kwa upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kuupongeza uongozi wa kanisa hilo la )F.G.B.F) kwa kuutambua mchango wake katika Taifa bado alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa dini katika jimbo hilo na kuwa yeye ni kiongozi wa makanisa na misikiti yote katika jimbo hilo.Alisema yeye ni mbunge wa wote na wakati wote atawatumikia bila kuwabagua hivyo wakati wote ataendelea kuwakutanisha Waumini na wananchi wote bila kuwabagua .


Mbunge Filikunjombe alisema kuwa matumaini yake ni kuona yeye na wananchi wake wataendelea kushirikiana na kuwa yeye alitakiwa kuwa Paroko kutokana na awali kujikita zaidi kusomea uparoko ila sasa amekuwa mwanasiasa.Japo alisema kuwa kazi zote ni za kijamii na kuwa siku zote amekuwa akiwaombea wanananchi wake wa Ludewa na kuwa lazima na wao wazidi kumwombea ili kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuongozwa na Mungu.

Nabii Malisa Aliyekataliwa Coverage Kwenye Media Za Kikristo Atikisa Jiji La Dar-es-Salaam

Baada ya media za Kikristo katika Jiji la Dar-es-Salaam Kukataa kumpa Coverage ya Matangazo Nabii Malisa Kutoka Katika Jiji la Mwanza ametikisa Jiji la Dar-es-Salaam kwa Kuweza Kujaza Ukumbi wa PTA ali maarufu Karume Hall.
Nabii Malisa akimuhoji Mwanamama aliyekuwa amekuja na Mgongo Ya Kutembelea katika Semina Hiyo.

Gazeti la Nyakati pekee ndilo lililokuwa limetoa tangazo kwa ajili ya kuwaalika Watu katika Mkutano Huo Mkubwa iliofanyika katika Ukumbi wa PTA.

Nabii Malisa ambaye hana tawi lolote katika Jiji la Dar-es-Salaam lakini aliweza wakusanya Watu kuhudhuria katika Mkutano huo.
Kati ya Mambo yaliyoleta Utata katika Mkutano wa Nabii Malisa ni kitendo cha kualika watu ambao kwenda Kusafisha nyota zao zilizofifia. Blog ilimuuliza Mmoja wa viongozi wa kanisa moja kwanini hawakumpa ushirikiano Nabii Malisa alisema "Kwa watumishi wa Dar-es-Salaam tunafahamiana, huyu kijana Mwanza kwenyewe bado kuna utata wa huduma yake, kuingia kichwa kichwa kushirikiana nae pasipo kujua foundation teachings zake unaweza kuta unapoteza watu bure"
Umati Wa Watu Waliohudhuria Semina Ya Nabii Malisa Katika Ukumbi wa PTA 
Katika Siku 3 hizo wagonjwa kutoka hospitali mbalimbali katika Jiji la Dar-es-Salaama walipelekwa katika Ukumbi huo na kufunguliwa kwa uweza wa Nguvu za Mungu.
Akifundisha kuhusu nidhamu ya Pesa, Nabii Malisa alisema Watu wengi wamekuwa na nidhamu ya Pesa wakiwa hawana Pesa ama Zinapokuwa zimepungua, aliuliza watu waliohudhuria ni nani aliyewahi kuwa na nidhamu ya Pesa alipokuwa kwenye Neema, na watu walishindwa kutoa majibu. Nabii Malisa amemaliza Siku 3 za Kinabii siku ya tarehe 6 May, 2012 Katika Jiji la Dar-es-Salaam.

AFRICA LETS WORSHIP 2012 (AFLEWO)

  Aflewo 2012,at Ccc Upanga















Sehemu ilipofanyika Aflewo 2012 kwa ndani
Aflewo 2012 Mass Choir ikifanya maandalizi ya mwaishi mwisho siku chache kabla ya Event hiyo kuanza @ Ucc Upanga

Wakiingia kwa stage


Aflewo 2012 Mass Choir kama wanavyonekana katika madhabahu wakiongoza sifa
Baadi ya Viongozi wa Aflewo Event Pastor Safari na Kagaruki kutoka kanisa la Dar es salaam Pentecostal Church (DPC)

Pastor Safari akitoa Neno kwa Ufupi


Mmoja wa wabeba maono ya Aflewo kutoka Kenya alikuwepo kuwakilisha Aflewo ya Group ya Kenya ambayo hawakuweza kufika.


The Voice walikuwepo kuhudumu pia

Hapa  ilikuwa full shangwe before the Lord
Maombi na Toba kwa ajili ya Tanzania, East Afrika na Africa kwa ujumla yalifanyika

MKUTANO WA CHRISTIAN BLOGGERS

Jumamosi tarehe 21 April, 2012 tumeona tukutane uso kwa uso pale karibu na Mlimani City Survey kuanzia saa 3 mpaka saa 5 asubuhi.

Madhumuni ya Kukutana ni kwanza kufahamiana sisi kwa sisi, lakini pia kujifunza kwa pamoja namna ya kuanzisha (kwa wale wanaoanza), Kuboresha muonekano wa blog zetu "Technical Part" Steve Jobs aliwahi sema "designing is not just what it looks like but how it works " .

Ninafahamu tunao Bloggers walio ughaibuni kwa sasa,kuna wengine wako nje ya Dar.. lakini ninaamini kuanzia hapa tutapiga hatua ya kupashana habari.

Ninatamani Jumamosi wale wenye nafasi tujitokeze, na kama kuna watu wa magazeti haya ya Kikristo una connection tafadhari tuwasiane kwa ajili ya kazi tunayotaka kufanya nao.

Pamoja na hayo kwa wadau wote wanaotembelea blogs za Gospel nchini wanaalikwa kwa ajili ya kutoa mchango wao ili kuboresha blogs za Injili nchini.Kumbuka, Blog Kama MADHABAHU inaweza KUUJENGA ufalme wa Mungu na pia inaweza kuuharibu.

Usikose mtumishi. 


TAMASHA LA PASAKA 2012 UWANJA TAIFA

Rebecca Malope Mwimbaji wa Injili kutoka South Africa, akihudumu katika Tamasha la Pasaka Uwanja wa Taifa,

Waimbaji waliohudumu katika Tamasha hilo Upendo Nkone,Upendo Karahilo na Christina Shusho wakiwa wanaingia Uwanjani.

Rose Mhando akiwa na Rebecca wakiwa wanaaga mara baada ya kuhudumu.


Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya nje Mheshimiwa Bernald Membe (White) akifatilia na kupata upako kupitia Nyimbo toa kwa wanamuziki tofauti waliokuwa wakitumbuza kwenye Tamasha la Pasaka ambalo kwa kiasi kikubwa limekusanya mamia ya wanachi. 







 

Baadhi ya atu waliojitokeza uwanjani hapo.


Sehemu ya Hightable kama wanavyoonekana Mh Nape,Dr Fernandes,Askofu Gamnywa na Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya nje Mheshimiwa Bernald Membe

"THE NEW COVENANT" MBEYA CONFERENCE










THE VOICE WAREKODI LIVE DvD ALBUM

The Voice wakifanya vitu vyao ukumbini hapo

The Voice hapa vocal ilikuwea Babu kubwa wakiimba pamoja na mmpiga-solo mahiri  Bro Sam Yona nyuma mwenye Gitaa

The Voice wakiwasalimia mamia ya watu waliojitokeza ukumbini hapo

Hapa ni kiasi tu cha wadau waliojitokeza kutazama Event hiyo katika ukumbi wa Jumba la Makumbusho unaotazamana na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es salaam
 Mama na Mwana

Bloggers nao hawakupitwa na Event Hiyo

Rebecca Malope ndani ya Uwanja wa taifa Tamasha la Pasaka!


RebeccaMalope akijulikana kama Malkia wa muziki wa injili Africa amezaliwa 1968 katika kijiji cha Lekazi karibu na mji wa Nelsprut, Mpumalanga. Malope hakuendelea sana katika elimu na ni mambo machache sana yanafahamika kuhusiana na enzi za utoto wako. Akiwa katika umri mdogo Malope alipata ugonjwa uliopelekea kutoweza kutembea na madaktari walidhani asingeweza kutembea tena katika maisha yake.
Familia yake ilikuwa masikini sana na ndipo yeye na dada yake(Cynthia) waliamua kumbilia katika jiji la Johannesburg kitongoji cha Evaton kwa ajili ya kutafuta kazi kujikimu na maisha.
Mwaka 1986,Malope alishirika kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uimbaji “Shell Road to Fame,(Music talent search) lakini hakufanikiwa kufika mbali. Malope hakukata tamaa ndipo mwaka uliofuata alishiriki tena na kuibuka mshindi(Best Vocalist) na wimbo Shine on. Ushindi huu ulimsogeza mbali sana kimuziki na ndipo alipokutanishwa na muandaaji(producer) mashuhuri Sizwe Zako na akapata meneja wake wa kwanza akijulikana kwa jina la Peter Tladi.
Dr. Rebecca Malope
Album yake ya kwanza  ilikuwa na nyimbo za kawaida za kijamii,album haikufanya vizuri sokoni na ndipo alipoamua kujiingiza moja kwa moja kwenye muziki wa injili. Alipata sapoti kubwa sana kutoka katika radio mbalimbali kwa nyimbo zake za gospel kitu ambacho hakikuwa kawaida sana Africa Kusini.
Mwaka 1990 Rebecca alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Kusini,na mwaka 1993 ilikadiriwa watu zaidi ya milioni moja walimpigia kura kama mwanamuziki bora wa kike kwenye Coca Cola Full Blast Music Award Music Show, na alishinda kwa mwaka huo na 1994 pia. Kwenye mauzo, Album zake zote kumi za kwanza ziliingia kwenye hadhi ya dhahabu(gold). Katika kipindi hiki kopi zaidi ya milioni 2 zilikuwa zimeshauzwa sokoni. Mwaka 1995 kwenye CD yake ya Shwele Baba, kopi zadi ya milioni moja zilikuwa zimeshauzwa ndani ya wiki tatu toka uzinduzi wake,na hii iliweka rekodi ya aina yake katika historia ya soko la muziki Africa kusini.
Dr. Rebecca Malope
Mwaka 1996 haukuwa mwaka mzuri sana kwa Rebecca,alipoteza baba yake mzazi, kaka yake na dada yake. Wote walifariki katika mazingira ya kutatanisha wakifuatana. Lakini hili halikumfanya Rebecca kukata tamaa na kuacha huduma bali alisonga mbele na kazi hii ambayo yeye anaamini ni kutoka kwa Mungu mwenyewe na hataacha kumtumikia. Kati ya mwaka 1995 na 2004 Rebecca amezunguka ulimwenguni akiwa na band ya Pure Magic akimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.
Mwaka 2003 Malope alitunukiwa udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Natal kwa mchango wake mkubwa kwa jamii na muziki nchini Africa kusini. Na Desemba mwaka huo huo alishinda tuzo ya Kora(Kora music award) mwanamuziki bora wa Injili.
Katika wanamuziki ambao alishirikiana nao kwa karibu sana na wamekuwa na mchango mkubwa kwake ni pamoja na marehemu Vuyo Mokoena.

Mwaka 2004 Malope alianza TV show yake “Gospel time” ambayo inafanya vizuri sana. 
Mwaka huu wa 2012 tarehe 25,February ,Malope  amefanya Live recording katika jiji la Pretoria, na hii ni album ya 31. 

Msama Promotions waandaaji wa matamasha ya makubwa ya injili Tanzania,Katika Tamasha la Pasaka la mwaka huu wanamleta Malkia wa muziki wa injili Africa, Dr.Rebecca Malope katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 08/04/2012.siku ya pasaka.
Rebecca Malope ataongozana na band yake ya wanamuziki 13. Ameahidi kufanya makubwa siku hiyo katika uwanja wa Taifa.

Baadhi ya Tuzo ambazo Dr. Rebecca Malope amewahi kutunikiwa.

Music awards
1994 – Best Gospel Singer

1997 – Best Selling Album for Uzube Nam’

1998 - Best African Gospel Artist & Best Selling Album for Angingedwa

1999 – Best Female Artist and Best African Gospel for Somlandela

2002 – Best Gospel Artist for Sabel Uyabizwa

2003 – Best African Gospel Artist for Iyahamba Lenqola

2004 – Best African Gospel Artist for Hlala Nami