Kibarua chaota nyasi kwa kuombea mteja

Mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Bi. Anhue Doan (59) amejifukuzisha kazi baada ya kumuonea huruma mteja kisha akamuombea kabla ya kumhudumia.

Mkasa huo wa aina yake ulitokea katika duka moja la dawa la Walmart, huko Calfonia  nchini Marekani,  na tukio hilo likanaswa na kamera za usalama.


Viongozi wa duka hilo kubwa la dawa walibaini tukio hilo baada ya kuangalia  picha zilizopigwa za kamera ya CCTV  zilizofungwa ndani ya duka hilo, ambazo zilimuonesha  mhusika  akimshika shika mkono mteja aliyefika kununua dawa kwenye duka hilo, huku akilia.

Tukio hilo lilitafsiriwa kuwa alikuwa akimwombea, jambo ambalo ni marufuku kufanyika katika mazingira ya kazi, japo yeye kama mkristo ilikuwa wajibu na wito wake.
Hata hivyo mwanamama huyo ameamua kulipeleka shauri hilo katika Mahakama ya shirikisho iliyopo California kwa kubaguliwa na kutengwa katika misingi ya dini.

Wakili wa mama huyo, Bi. Darren Harris, kutoka Gould & Bowers LLP, akiongea na ABC News alisema, mteja wake hakuwa akimuombea mteja aliyekuja kuhitaji huduma kama ilivyoelezwa, badala yake alikuwa akiongea naye akiwa amemshika mkono.

Alisema kabla ya kufukuzwa kazi alipewa barua ya onyo ambayo hata hivyo haikuonyesha madai ya kuombea mtu, isipokuwa kwa fikra potofu mtu anaweza kuonekana kama yuko kwenye maombi na kwamba si ruhusa kwa mtu kama yeye ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya kuchanganya mambo ya imani yake na taaluma.

Hata hivyo msemaji wa Walmart, alisema kampuni yao ina sera  zinazoheshimu uhuru wa kuabudu  na kwamba haiwanyanyasi  wala kuwatenga watu kwa misingi  ya dini.

"Tunatoa uhuru wa kuabudu wa kutosha, hata hivyo tutaendelea na uchunguzi,"

Walmart, ina maduka  makubwa ya madawa na imeajiri zaidi ya  watu 1.4 million nchini Marekani pekee.

Inaeleza kwamba June 2011, Bi. Doan, aliandika barua kwa mwajiri wake ili awe na kibali cha kuwaombea wateja na ili waweze kupokea uponyaji kwa nguvu za Mungu, lakini hakukubaliwa,  huku akipewa onyo kwamba ikiwa atabainika amefanya tendo hilo atafukuzwa kazi.

Wakili wa Bi. Doan anaamini anabainisha kuwa, anachojua mteja wake ni msumbufu hasa pale alipomtumia ujumbe wa barua pepe meneja wake dhidi ya wenzake ambao walikuwa wakija na vinywaji kwenye pharmacy, kupiga na kupigiwa simu na wengi hawafuati maadili ya eneo la kazi.

Doan alisema majukumu yake amepewa mtu mwingine ambaye si muumini wa dini ya kikristo, kitu ambacho alisema ni unyanyasaji wa  kiimani.

Alieleza kuwa meneja wake alikwenda ofisini kwake na kumuonyesha tape ikionyesha tendo alilokuwa akilifanya la kumshika mkono mteja lakini haikuwa na sauti.

Hata hivyo wakili wa mwanamama huyo alisema kuwa, mteja wake anatakiwa afanye kazi kwenye nafasi aliyonayo hadi hapo atakapostaafu.

No comments:

Post a Comment