Mauaji ya raia wasio na hatia ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana wadogo wa kimarekani kwa kutumia silaha za moto, yanaakisi ukengeufu wa kimaadili na si dhana ya mapenzi yao juu ya silaha wanazomiliki kama wengi wanavyodhani.
Mchungaji Will Marotti, wa Kanisa la New Life lililopo maeneo ya Connecticut, akiongea na OneNews kuhusiana na sakata la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa wanafunzi na mkuu wao na kijana mmoja kabla naye kutimiza azma yake ya kujiua alisema ni ukengeufu wa maadili.
Alisema katika jamii inayothamini maisha ya binadamu, umiliki wa bunduki si tatizo kubwa. Watu huishi maisha bora yenye kuthamini na kuamini juu ya uadilifu; hawahitaji kuchunga maisha yao kwa bunduki, au njia yoyote isipokuwa inapolazimu kujihami.
“Hivyo sivyo katika muonekano halisi wa maisha yalivyo leo katika hali hii ya mabadiliko makubwa duniani. Katika jamii hiyo ambayo imeruhusu utoaji wa mimba, na kunyonga bila maumivu, maisha kwao imekuwa kitu rahisi,” alisema na kuongeza:
“Mwanamke anaporuhusiwa kuua mtoto asiyemtaka akiwa tumboni mwake, hiyo ni kuhujumu maisha kwa kutoyathamini. Kama hilo halitoshi anaporuhusiwa kubadili mtoto anayekua tumboni mwake, kutoka kitu kisichohalisi hali hufanya maisha yaonekane kuwa kitu kinachoweza kuchezewa.”
Mbali na hilo alibainisha kwamba haya ni maisha wanayoyataka ya kudhani kuwa mwanadamu anaweza kucheza na nguvu za Mungu kwa kucheza na maisha.
Kadhalika aliweka wazi kuwa, kama mwanamume anahaki ya kumhudumia mkewe anapokuwa akisota katika matibabu na wakati akiwa mahututi katika hospitali ya Terry Schiavo, ujumbe huo uko wazi na unaeleweka; kwa maana huwezi kutenganisha utashi na ukiri kwa jumla.
Kwa namna nyingine alieleza kuwa, siku hizi utakuta watoto wakifurahia kuangalia picha za mapigano na michezo yenye kuburudisha katika luninga, vitu vinavyohamasisha machafuko. Watoto wa kimarekani na wazazi wao wamejifunza michezo inayoondoa maisha.
“Watu wasioamini kuwa maisha ni sadaka inayoweza kuondolewa kwa mihemuko kwa kusababisha kifo, hata pale ambapo kifo kingeepukika. Hivyo, hutokea ulinzi wa kuepusha machafuko ya halaiki, jibu ni kwamba kuheshimu maisha na kujilinda binafsi siyo kumiliki bunduki,” alisema na kuongeza:
"lazima tufahamu kuwa tuko kwenye mapambano si suala la kuamini kuwa Mungu yupo shetani kadhalika, si wakati wa kusema Mbingu ipo na jehenamu, nchi yetu iko kwenye mapigano sasa, najua wakristo mnajua kuwa wajibu wenu ni nini.”
Watumishi wengi kipindi hiki alieleza kuwa, wanakuwa na safari nyingi kutoka sehemu moja hadi nyingine, mimi nawatia moyo kwamba wanatakiwa kutulia makanisani na kuzidi kumtafuta Bwana hata katika kipindi cha Krismas.”
Aliendelea kueleza kwamba ulinzi uko kwa Bwana na kwenye silaha ambazo watu wamekuwa wakiona kama ni mungu wao na hilo ndio maana limekuwa likileta maafa makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia.
“Kwa namna moja ama nyingine ninaweza kusema kwamba watu wamemsahau Mungu wa Kweli, tumesahau kukaa mikononi mwake; kingine ni kutubu kabisa kwa uovu mwingi ambao tumekuwa tukiufanya, tumwombe Mungu alinde shule zetu na watoto, kinyume kabisa dhidi ya shetani,” alisema.
No comments:
Post a Comment