Maandalizi ya Mpinga Kristo........., Umoja wa Dini 5O wazua Balaa!

Papa Benedict, Lutheran wahusika,Makanisa Mengine yajiweka kando pia Quran na Biblia zasomwa kwa pamoja

Wakati wengine wakiendelea kubishania uhalali wa ibada za mafuta na vitambaa, hatua kubwa ya kufikia umoja wa kidini yaani United Religious, utakaokuwa na nguvu kuzidi Umoja wa Mataifa (UN) imefikiwa hivi karibu, baada ya dini zaidi 50 kuandaa ibada siku ya Jumapili na kutumia Bibilia na Qura’n.

Taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la New York Times, ilisema: “Mihimili mikuu mitatu kuelekea mfumo mpya wa dunia ambayo ni Umoja wa kiuchumi duniani, Serikali moja na Dini moja. Masikio ya wengi yameelemea kwenye mihimili miwili zaidi kuliko ule wa tatu ambao wameupuuzia. Lakini huu wa tatu ambao ni dini ya pamoja (kwa maana ya imani moja) ndio usukani na sasa unakaribia kufikiwa. Huu ndio unaojulikana kama ‘Interfaith.’ 
Papa Benedict XVI
 Makongamano na mikutano inaendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku duniani, huku viongozi wakuu akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja. Imani ya kuwa na dini moja "Interfaith" imekuwa ikisisitizwa kote duniani na viongozi wa dini mbalimbali wakitumia mashirika (NGOs), mashirika ya misaada, na taasisi mbalimbali, wanasisasa wakubwa wametumiwa kuipa msukumo kwa fedha nyingi katika sayari hii.”
Kisha taarifa hiyo iliongeza: “Hivi karibuni baadhi ya makanisa katika Amerika yamekwenda mbali zaidi katika suala hilo. Juni 26, mwaka huu, Kathedral ya Kitaifa (National Cathedral) katika Jiji la Washington D.C. iliandaa ibada ya pamoja  na zaidi ya makanisa 50 yalishiriki kusoma Quran wakati wa Ibada ya Jumapili.”
Wachambuzi wa siasa dini wanaeleza kuwa hiyo ni hatua katika mkakati mkubwa wa kuundwa kwa shirikisho kubwa la kidini katika kipindi cha mpito kuelekea kuzaliwa rasmi kwa umoja wa kidini  ulimwenguni, ukishinikizwa kwa kipengele cha haki za Binadamu.
Somo kuu katika Jumapili hiyo lilikuwa “Kushirikishana imani, Kushirikiana maombi na kuelewana.” Lengo likielezwa kuwa ni kuonesha upendo wa Wakristo kwa Waislamu waishio Amerika.
Miongoni mwa makanisa yaliyoshiriki ni: Christ Church lililopo jijini New York City,
All Saints Church lililopo Pasadena California, Park Hill Congregational huko Denver,
Hillview United Methodist lililopo Boise, Idaho First United Lutheran, katika mji wa San Francisco, St. Elizabeth's Episcopal Church, huko Honolulu, Makanisa makubwa (dini mbalimbali) yapatayo 26 katika Amerika yamehusika na mpango huo.
Interfaith logo
Imeelezwa kuwa usomaji huo wa Quran ni mpango maalumu wa kulainisha dini zenye misimamo mikali ili kuonesha kuwa upo uwezekano wa kufanya ibada pamoja na kumaliza tofauti zilizowatenga zamani.
Mpango huo mkubwa unatarajiwa kua endelevu ukijumuisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu kwa njia ya kusikia na kusoma aya kadhaa, za Qur'an mara kwa mara ili watu wazoee kuwa pamoja na mwisho waunganishe mioyo yao pamoja na kuabbudu pamoja.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, Interfaith, Waamerika wana uhuru wa kusoma Quran popote wanapotaka. Lakini kwa Wakristo hawana nafasi ya kusoma na kujifunza kitabu hicho, hivyo kuwepo kwa utaratibu wa kuisoma kila Jumapili wanapokutana kanisani kwenye Ibada na kutawafanya waielewe na kuwa na ‘umoja’ na Waislamu na kuonyesha kutowabagua; jambo ambalo linaonesha dalili ya kuzaliwa kwa kitu kipya duniani.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Kikristo duniani hawako radhi na muendelezo huo. Brannon Howse, mmoja wa viongozi mashuhuri alisema: “Watu hao wamekana uungu wa Yesu Kristo; wamekana ukweli wa maandiko matakatifu; wamekana uvuvio wa Biblia, ni vipi tushirikiane nao na kusoma kitabu chao kwenye ibada zetu?”

Qur'an

Kisha aliendelea: “Inasikitisha, hii siyo mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba umoja huo umepata nguvu miongo kadhaa na baadhi ya wakuu wa dini ulimwenguni wamehusika.
Kwa mfano; habari zilizopatikana kupitia CNS zinaeleza kuhusu muungano mkubwa ‘interfaith’ wakati Papa alipotembelea jiji la Washington 2008.”
Alisema kuwa wakati Papa Benedict XVI alipofika kituo cha, Pope John Paul II Cultural Center kilichopo Washington kwa mkutano wa jioni wa dini zote ‘interfaith’ zilikuwepo dini mbalimbali ambazo hapo awali isingekuwa rahisi kukutana na kuabudu pamoja. Waislamu, Wahindu, Wayahudi na dini nyingine zilipata nafasi zilishiriki; isipokuwa Assemblies of God,hii haikuthubutu hata kusogelea.
Viongozi wa Dini kubwa katika Amerika wanahusika sana na umoja huo "Interfaith movement," kwa mfano; Brian McLaren, mmoja wa viongozi wa juu wanaoendesha umoja huo, inasemekana kuwa mwaka 2009 alisherehekea Ramadhan na hata kuvaa mavazi yanayovaliwa na wahusika.
Katika sherehe hiyo; Rick Warren, mshirika wa Baraza la Uhusiano wa Nje, alikuwa Mgeni rasmi na mnenaji kwenye Kongamano la kitaifa la Waislamu huko Amerika ya Kaskazini, (Islamic Society of North America).
Baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo Rick Warren, Robert Schuller, Brian McLaren, Richard Cizik na Bill Hybels walitia sahihi barua kwa Jumuiya ya Kiislamu iliyokuwa na kichwa kisemacho;  ‘Kumpenda Mungu na jirani yako’
Barua hiyo iliweka bayana kuwa viongozi wa Kikristo wanamtambua Allah kuwa sawa na Mungu wa Wakristo.
Barua hiyo ilisema:“Kabla hatujashikana mikono; katika kukubaliana na barua yetu, tuwatake radhi kwa kuomba msamaha kwa Muumba wa wote. Kwa Waislamu muumbaji ni Allah.
Kwa barua hii, baadhi ya viongozi wa Kikristo wanamuomba na wanatubu kwa jina la Allah, na wanamtambua kuwa ndiye Mungu.”
Kama tulishindwa kurejesha amani na kuwa pamoja, sasa tumesahihisha mawazo yetu na kwamba tunaweza sasa kutakasa nafsi zetu.”
Barua hiyo ndiyo iliyozua hofu duniani kuwa  huenda wakati sasa umewadia wa baadhi ya viongozi kudhihirisha hali ya vuguvugu  na kukosa msimamo wa kiimani.
“Kwa kweli  huu ni usaliti wa hali ya juu, kuandika barua na kueleza kuwa Allah ndiyo Mungu anayeabudiwa na Wakristo  ni mwanzo wa kuelekea katika  dini moja na utawala wa Mpinga Kristo,” alisema Mchungaji Jonathan Emmanuel, wa Nigeria.
Alisema kuwa anautazama mwelekeo huo kama jambo la hatari kwa kuwa Biblia katika  kitabu cha
Yohana 14:6 , Yesu anasema: “...Mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.”
Kiongozi huyo alisema kuwa ukweli wa ki-Biblia uko wazi na wala hauna kificho kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kufika mbinguni. Ikiwa unaamini hivyo  ni vipi uandike tena barua ya hatari kama hii ya  kumhusisha Allah na ufalme wa Mungu?
Kisha aliongeza: “Katika amri kumi; awali kabisa tunakutana na maandiko yasemayo; “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usifanya sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni , wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao, nami nawarehemu maelfu  wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
 (Kutoka 20:3-6) 

Source Jibu La Maisha

Kanisa lagomea mashoga kununua nyumba wengine wapigwa mawe hadi kufa.

WATU wawili wa jinsia moja (mashoga), walioonyesha azma yao ya kutaka kuishi pamoja kama mume na mke, wiki iliyopita walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa kununua nyumba huku mmiliki wa Bakery akigoma kuwauzia keki ya harusi yao na wengine kupigwa mawe hadi kufa nchini Kenya.

Hayo yalitokea wiki iliyopita nchini Marekani, baada ya watu hao, waliokuwa kwenye uhusiano wa siri kwa miaka miwili kuamua kuudhihirishia ulimwengu kwamba wao ni mume na mke, kinyume na mpango halisi wa Mungu ambao ni ndoa ya muke na mume.




Sakata lenyewe lilikuwa hivi; Kanisa moja lilikuwa likiuza nyumba yake (mansion), tangazo likachapishwa kwenye mitandao na watu wakajitokeza kutoa ofa, lakini miongoni mwao walikuwemo mashoga wawili.

Katika kuchekecha nani wa kununua nyumba hiyo, kanisa likafikia muafaka kwa mashoga hao ambapo awali hawakuwatambua kama ni mume na mke, wenye mahusiano haramu.

Baada ya kubaini uchafu huo, huku watu hao wakiwa na pesa kamili, ghafla waliambiwa na wauzaji ambao ni kanisa kwamba, wanasikitika hawatoweza kuuza jumba hilo kwa watu ambao ni mashoga, kwa kuwa matumizi yake yataendana na wahusika.

Mashoga hao ambao ni; Bw. Alain Beret na mkewe Bw. Jim Fairbanks, baada ya kuambiwa habari hizo, huku wakijiandaa kufanya sherehe ya kukata na shoka, mara waingiapo ndani ya Mansion hilo, walinga’aka.

“Huku ni kunyanyapaliana, jambo kama hili kufanyika katika uso wa dunia mapema kiasi hiki ni mbaya, ni lazima likomeshwe,” alisema huyo anayeitwa mume (Beret) na kuongeza:

“Kwa kweli siamini hiki ninachokiona, tuko katika karne hii ya 21, lakini bado tuna kitu cha ubaguzi.”

Hata hivyo msemaji mmoja wa kanisa hilo akiongea na mashoga hao aliwaambia: “Nimeongea na Askofu juu ya nia yenu ya kununua jumba hili, nilimueleza nyie ni watu wa namna gani, kwa msingi huo tunasikitika kutoendelea mbele kuhusiana na jambo hili, hofu yetu ni kuhusiana na matumizi yake.”

Jumba hilo la kifahari lilijengwa mwaka 1890 ambalo pia ni la kihistoria.

Sambamba na hilo, mmiliki wa duka moja maarufu kwa kuandaa keki za sherehe nchini humo mjini Colorado, Bw. Jack Phillips amekataa kuwauzia keki mashoga wawili waliotaka kufunga ndoa wiki iliyopita.

Duka hilo lilijulikana kwa jina la Masterpiece Cake Shop, imeelezwa kwamba lilipokea oda ya kutengeneza keki, lakini lilipobaini kuwa mashoga ndio walikuwa katika shamra shamra za kufunga ndoa wakagoma kuikamilisha.

Katika mkasa huo, Bw. Dave Mullin na Bw. Charlie Craig,waliambiwa na mmiliki  wa duka hilo kuwa  asingeweza kuuza bidhaa zake kwa watu wanaotaka kufanya mambo kinyume na mpango wa Mungu, lakini watu hao walidhani alikuwa akiwatania, ndipo siku ya harusi ilipowadia na kwenda kuchukua keki wakakutana na ujumbe ule ule.

Baada ya jambo hilo, ambalo waliliona ni udhalilishaji; waliingia kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yao yaliyosomeka namna hii: “Tumekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, tukaamua sasa kuwa kitu kimoja kwa kufunga ndoa, lakini cha ajabu tulipoenda kwa muuzaji maarufu wa keki mambo yakawa mamabaya.” 

Kisha aliendelea: “Tulitarajia kuchukua muda mwingi kuelezea namna tunavyotaka keki yetu iwe, lakini haikuwa hivyo, neno langu la kwanza lilikuwa, tunataka kuoana na akatukatiza hapo hapo, tulishangaa.”

Hata hivyo baada ya maoni ya Dave Mullin na Charlie Craig kutundikwa katika mitandao hiyo ya kijamii, (Facebook) watu zaidi ya 1000 walikasirishwa na kitendo hicho, huku wengine  wakiamua kwenda moja kwa moja hadi kwa mmiliki kupinga alichokifanya muuza keki huyo.

Miongoni mwa waandamanaji waliokwenda moja kwa moja hadi Masterpiece Cake Shop,  ni Bw. Cate Owen aliyeeleza kwa uchungu kuwa, wamekuwa wakisapoti biashara za wazawa, lakini ikiwa naye anatoa huduma kwa ubaguzi basi na wao hawatakuwa radhi kumuunga mkono.

Wakati hilo likifanyika huko Marekani, nchini Kenya nako mashoga wawili walijikuta mikononi mwa kundi kubwa la watu wenye hasira kali baada ya kubambwa kona wakivunja amri za Mungu katika maeneo ya Kayole, ambapo walipigwa mawe na mmoja kufa papo hapo, mwingine akifanikiwa kukimbia, lakini mwisho wa siku mwili uliacha roho kama mwenzake.

Mashoga hao ambao walikuwa ni baba lishe (food venders), inadaiwa kwamba walikuwa wakifanya mchezo huo mchafu kwa miezi kadhaa.

Inaeleza kuwa siku ya tukio walikubaliana kukutana karibu na majengo ya Kanisa Katoliki, eneo linalobainishwa kwamba lina msitu kiasi fulani, wakiwa hapo huku giza likinyemelea walianza kazi iliyowapeleka na ndipo mtu mmoja alipowaona na kuita watu na zoezi zima likachukua nafasi yake.


Wakati zoezi hilo likiendelea mmoja aliweza kukimbia, huku akimuacha mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Kamau akishambuliwa vikali.

Baada ya mauaji ya Kamau, kundi hilo lilimtupa kwenye dampo ambalo lilikuwa karibu na walipokuwa wakifanya ushenzi huo.

Hivi karibuni Rais wa Marekani, Barrack Obama alitamka hadharani kutambua ndoa za jinsia moja, jambo lilipokelewa kwa vifijo na wachache na wengi hasa watumishi wa Mungu kupinga vikali, huku wachambuzi wa masuala ya siasa wakichanganua kuwa hilo limekuja ili kumng’arisha katika medali za siasa, hasa ikizingatiwa wanatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu wa urais mwezi Novemba 2012.

Love Tanzania Festival yazidi kukamilika baada ya Mwinjilisti Andrew Palau Kuwasili Nchini

Mwinjilisti na Mwandaaji wa Love Tanzania Festival Andrew Palau  amewasili nchini tayari kwa ajili ya tamasha linalotegemewa kuwa kubwa ambalo halijawahi kutokea Nchini Tanzania hapo mwanzo.

Jana siku ya Jumapili Andrew Palau alihubiri  katika kanisa la City Christian Center (CCC) Upanga pia ibada hiyo ilirushwa live kupitia kituo cha Radio cha Clouds FM ambayo ilikuwa inasikika Duniani Kote.

Mwinjilisti Andrew Palau amewasili na timu yake kwa ajili ya Tamasha hilo kubwa la Love Tanzania Festival litakalofanyika katika Viwanja vya Jangwani siku ya tarehe 11/12 August, 2012.

Pia kuanzia tarehe 11hadi12 Andrew Palau na waimbaji wengine wa Kimataifa kama Lubben, Don Moen and Nicolle watakuwa wakihudumu pamoja,Waimbaji wa Tanzania watakao hudumu ni Christina shusho, Masanja, The Voice na Upendo Kilahiro.atakuwa katika viwanja vya Jangwani akihudumu.

Mwainjilisti Andrew Palau akihubiri katika Ibada ya Jana siku ya Jumapili  CCC Upanga

Bishop Mwenisongole wa Kanisa la CCC  akiongoza maombi na Mwainjilisti Andrew Palau katika Ibada siku ya jana.
Lubben akihudumu  katika kanisa la CCC Upanga akishirikiana na Praise Team

Kanisa la TAG kufanya Uchaguzi wa Askofu Mkuu Dodoma

Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali

MKUTANO Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), ambao unafanyika kila baada ya miaka minne unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali, unaanza  Jumatano tarehe 8, Agosti mjini Dodoma na kuendelea kwa karibu wiki nzima.

Kwa mujibu wa takwimu za makao makuu, zaidi ya watumishi wa Mungu 3000 wanatarajia kukutana Dodoma  na Mkutano Mkuu utafanyika katika Chuo Kikuu cha  Dodoma, ukitanguliwa na  vikao vya Halmashauri kuu  na Baraza la Waangalizi.

Akiongea na waandishi wa habari, katika mahojiano maaalumu wiki iliyopita,  Naibu Katibu Mkuu (Shughuli) wa kanisa hilo, Mchungaji Uswege Mwakisyala, alisema kuwa, mkutano huo mkuu utafanyika Chimwaga mjini Dodoma, na watu watakaohudhuria wanakadiriwa kufikia  3000,  ingawa sio wote watakao piga kura.

Mchungaji Mwakisyala alieleza kuwa, siku ya Jumatatu (Agosti 6, 2012) kutakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu, huku kikifuatiwa na kikao cha Baraza la Waangalizi kitakachofanyika siku ya Jumanne.

Alibainisha kwamba siku ya Jumatano ndio mkutano mkuu utaanza kufanyika ambao utahitimishwa Ijumaa.

Hata hivyo Mchunagji Mwakisyala akitolea ufafanuzi juu ya utaratibu wa kuwasili mkoani humo alitanabaisha kwamba, Halmashauri Kuu watawasili siku ya Jumapili, tayari kwa kuanza kikao Jumatatu na waangalizi watawasili Jumatatu.

Mbali na hilo aliongeza kwamba, Wachungaji wote watakaowasili siku ya Jumanne, Agosti 7, 2012 watatakiwa kwenda moja kwa moja katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

“Jumapili watawasili Halmashauri Kuu, Jumatatu Baraza la Waangalizi na Jumanne wachungaji wote, na itakuwa ni vizuri ikiwa wataingia kwa makundi makundi, kwa kufanya hivyo magari yatawaingiza moja kwa moja hadi  chuoni,” alisema.

Katika mkutano huo mkuu, Kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi watasindikiza uchaguzi huo.

Uchaguzi uliopita ulifanyika Oktoba 2008, ambapo Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali, alichaguliwa kuliongoza kanisa hilo, huku Makamu wake akiwa Dk. Magnus Muhiche, na nafasi ya Katibu Mkuu ikichukuliwa na Mchungaji Ron Swai.

Katika muhula wao wa uongozi, Askofu Mkuu, Dk. Mtokambali, na timu yake walikuja na Kauli mbiu ya Miaka Kumi ya Mavuno iliyokuwa na lengo la kuleta watu milioni mbili kwa Yesu.

Wakati wanaingia madarakani, kanisa hilo lililokuwa na waumini 200,000 mwaka 2008, lakini hadi sasa (Mwaka 2012) lina waumini 433,546. Wachungaji walikuwa 2600 sasa wako 4527, makanisa yalikuwa 2134 sasa yako 4492.

Pia Seksheni zilikuwa 75, lakini sasa ni 204 huku majimbo nayo yakibadilika kutoka 10 hadi 25.

Kimsingi uchaguzi wa TAG, huongozwa na Roho Mtakatifu mwenye na hakuna wagombea wala kampeni, bali Bwana mwenyewe hujitwalia viongozi.
Wasimamizi wa uchaguzi wanatarajiwa kuwa wamisheni kutoka Marekani.

Love Tanzania Festival kufanya maajabu Viwanja vya Jangwani.

Kipeperushi cha mkutano cha Andrew Palau ambavyo vimezagaa Tanzania kila kona
Love Tanzania Festival ikiongozwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Andrew Palau wameandaa tamasha kubwa la injili lenye lengo la kukutanisha zaidi ya makanisa 800 kwa ajili ya kumsifu na kumwabudu Mungu katika Jiji la Dar es Salaam kwenye viwanja vya jangwani.

Tamasha hilo ambalo litafanyika Jumapili ijao litasindindikizwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho, The Voice na Massanja Mkandamizaji ambaye atakuwa akitoa ushuhuda wa maisha yake na jinsi alivyompekea Bwana Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake pamoja na waimbaji wa nje ya nchi akiwemo Don Moen, Dave Lubben na Nicole Mollen.

Akiongea na Blogs, Prosper Mwakitalima ambaye ni miongoni mwa wafanikishaji wa tamasha hilo alisema kuwa tarehe 11-12/08/2012 Jangwani patakuwa hapatoshi kutokana na tamasha hilo la Love Tanzania Festival ilivyojipanga katika kuhakikisha kila mtu atakayehudhulia mahali hapo anakutana na Bwana Yesu kwa njia tofauti tofauti bila ya kuwasahau watoto.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila, rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu litakuwa .ni kusanyiko kubwa la kihistoria ambalo inaweza ikawa haijawahi kutokea katika nchi ya Tanzania kutokana na kwamba watu wamejiandaa kwa maombi na kumtumikia Bwana kwa muda huo wa siku mbili.
Kwa mujibu wa Prosper Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.
Mmoja wa waimbaji kutoka USA, Nicole Molen ambaye naye atashiriki kwenye tamasha hilo la Jangwani

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August  7:00Asbh – 10.00 Asbh Mbeba maono wa Love Tanzania Festival  Mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika Kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) Tarehe 7 August 10Asbh katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE  kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.
Muimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Don Moen ambaye naye atashiriki katika Viwanja vya Jangwani

Love Tanzania Festival Katika Ukumbi wa Karimjee Hall Tarehe 8 August  12:00 jioni kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na Injili ya Yesu Kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni Kutafanyika maozoezi (Rehearsal) ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX  kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.

Baadhi ya Michezo itakayoambatana na Mkutano mkubwa wa Injili

Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia Neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.               
                 
Pia Huduma ya upimaji Macho na kutoa Miwani itafanyika kwenye vituo vilivyotajwa hapo chini
                                     
Kituo cha 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni




Kutafuta Mikataba na Kusimamisha Kuuza Muziki

 Kwa mwimbaji yeyote wa nyimbo za Injili anayehusika...

PRESS RELEASE:
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.


Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.

Pastor Benjamin Dube Kuhudumu ndani ya Uganda wiki hii.

Mchungaji na mwimbaji mkongwe wa Nyimbo za Injili nchini Afrika ya kusini Pastor Benjamin Dube ambaye Pastor Benjamin Dube is a music ministerial visionary, anointed songwriter and singer, music producer, mentor / father and pastor to many musicians and an inspiration to secular artists in South Africa katika medani ya muziki wa injili, siku ya Ijumaa anatarajia kufanya onyesho katika hoteli ya Serena jijini Kampala nchini Uganda ambako amepata mwaliko maalumu wa kihuduma kupitia huduma ya Gospel Healing Center International (GHCI) ambao wameandaa usiku wa kusifu.
                             
Pastor Dube ambaye tayari amewasili nchini Uganda kwasasa baada ya kusafiri pamoja na timu yake asubuhi ya leo, anasubiriwa kwa hamu nchini humo na mashabiki wake pamoja na wapenzi wa muziki wa injili kutokana na kazi yake njema anayoifanya katika ulimwengu wa muziki wa gospel ambapo katika onyesho hilo atashirikiana na waimbaji wenyeji wa nchini humo ambao nao wamealikwa katika onyesho hilo.

Mwimbaji wa Kundi la The Voice Jijini Dar es salaam apata Ajali

Obedi John Mark Mwimbaji wa kundi la The Voice linaloundwa na vijana watano amepata ajali jana usiku majira ya saa tatu maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa anatumia usafiri wa bajaji. kupitia ukurasa wao wa Facebook kundi hilo limetujulisha hivi;-''Mwimbaji mwenzetu Obedi John Mark amepata ajali maeneo ya Sinza Kamanyola, akiwa na usafiri wa bajaji akiwa anaelekea Magomeni...Kwa sasa hali yake si nzuri yuko chini ya uangalizi wa Daktari Mvungi ndani ya Hopitali ya Kinondoni na ameumia sehemu za Kichwa, wapendwa tuzidi kumuombea apone haraka''.


Obedi Mark katika pozi.
Aidha mwana blogger mwingine unlce jimmytemu kupitia blog yake amefanya mazungumzo na mdogo wake Obedi nakueleza kuwa hali yake sio nzuri amepata michubuko kwenye Mikono Miguu na sehemu za uti wa mgongo.Kwa sasa yupo hospital Muhimbili.
Gospel Vision inamtakia afya njema Obedi Mungu ahusike katika matibabu yake, tungependa kumuona akijumuika na wenzake katika huduma ya kumwinua Kristo.AMEN

The Voice

Mbunge aitaka serikari ya Tanzania kujenga ubalozi Israel nchini.

Bi Asumpta Mshama Mbunge wa Nkenge Kwa tiketi ya CCM

Hoja hiyo imeibuliwa bungeni hivi karibuni na Mbunge wa Nkenge Kwa tiketi ya CCM, Bi Asumpta Mshama, ametumia andiko hili kujenga hoja ya Tanzania kufungua ubalozi kamili huko Israeli. “And it shall be, that whoso will not come up of all the families of the earth unto Jerusalem to worship the King, the LORD of hosts, even upon them shall be no rain” (Zechariah 14:17). Kwa wale wasiomfahamu, ni mama yao wale akina “J sisters”, mabinti wanaoimba nyimbo za injili.

Nakumbuka alijibiwa na naibu Wa Wizara Ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim alieleza kuwa Tanzania haendeshi mambo yake Kiroho sababu kama Taifa halina dini ispokuwa Waumini wake, vile vile alieleza kwa sasa Tanzania haijatenga fedha za ajili ya Uanzishwaji huo wa Ofisi ya kibalozi, aliendelea kueleza kuwa Tanzania ina Mwakilishi wa Heshima huko Tel Aviv.

Thanks Giving Ya Uncle Jimmy Temu



Mwahabari wa Kikristo na Blogger anayefanya vizuri katika Tasnia ya Habari , Uncle James Temu ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi Cha Rise and Shine na Sunday Special Kutoka Praise Power FM na Mmiliki na mwendeshaji wa Blog ya www.unclejimmytemu.blogspot.com ameandaa siku maalum ya Kumshukuru Mungu kwa Blog yake Kutimiza Mwaka mmoja Mpaka Sasa.

Uncle Jimmy ameeleza kuwa blog hiyo ambayo mwezi huu wa July imetimiza Mwaka imepiga hatua kubwa sana mpaka sasa katika upashaji wa habari ndani na nje ya Tanzania.
Blog hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya kupasha habari za Kikristo na injili imekuwa ikisomwa na watu mbali mbali walio ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha Mwaka mzima sasa na kutoa michango yao ya mawazo kwa maendeleo ya Blog hiyo.


Blogger huyo James Temu au Uncle Jimmy amesema siku ya tarehe 20 July, 2012 kuanzia saa 1 usiku mpaka saa 3 usiku ameandaa Event Ya Kumshukuru Mungu itakayofanyika katika hotel ya Tamal maeneo ya Mwenge. Katika event hiyo Kutakuwa na Wanamuziki Wa Injili wanaovuma hapa nchini wakiongozwa na Dar-es-Salaam Band, Kutakuwa na Vinywaji pamoja na Chakula kitakachopatikana katika event.
Uncle Jimmy amesema Event hiyo haitakuwa na Kiingilio sababu ni siku maalum ya Kumshukuru Mungu. Pia alitoa mwito wa Kuwakaribisha Watu wote Bureeeeeeeeeeeee kabisa Bureeeeeeeeee kuweza Kuhudhuria Cocktail  Thanks Giving Ya Blog hiyo inayotimiza Mwaka.
Kumbuka ni tarehe 20 July, 2012, Saa 1-3 Usiku, Kiingilio ni Bure, Kutakuwa na Live Bands, Wanamuziki wa Injili, Wacheza Filamu Mbalimbali, Watangazaji wa Radio, Wasikilizaji wa Radio na Wewe Msomaji pia Unakaribishwa kwa ajili ya Siku ya tarehe 20 July, 2012.



Kwa Hisani Kubwa ya www.unclejimmytemu.blogspot.com