Askofu Paschal Kikoti afariki dunia
Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, limepata pigo la kumpoteza askofu wake wa kwanza, Paschal William Kikoti (55), aliyefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Taarifa za kifo kicho zilitolewa kwa waumini juzi usiku katika Kanisa Kuu la kiaskofu na Makamu Askofu wa jimbo hilo, Padre Patrick Kasomo.
Alisema kuwa Askofu Kikoti alipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu Jumapili iliyopita, majira ya saa moja asubuhi wakati akioga bafuni, na ndipo alipoanguka ghafla kisha kupoteza fahamu.
Padre Kasomo alifafanua kuwa, Askofu Kikoti aligunguliwa baadaye na mapadri na masista walipokuwa wametoka kwenye ibada ya misa ya kwanza saa 2:30 asubuhi huku akiwa ajitambui.
“Baraza la Maaskofu lilitafuta usafiri wa ndege siku hiyo, ambayo ilimsafirisha hadi mkoani Mwanza na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu hadi hapo juzi saa 2:30 jioni alipofariki dunia,” alisema.
Taarifa hiyo ya Padre Kasomo, iliwashtua waumini wengi ambapo baadhi yao walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio na wengine kuzirai.
Askofu Kikoti alizaliwa mkoani Iringa katika Parokia ya Nyabula mwaka 1957 na kupewa daraja la upadre Juni 29, 1988 humo humo mkoani Iringa.
Mnamo Januari 14, 2001 Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, aliliunda jimbo jipya la Mpanda na kumteua Kikoti kuwa askofu wa kwanza kuliongoza.
Kuhusu mazishi, Padre Kasomo alisema kuwa mwili wa marehemu Askofu Kikoti utawasili jimboni humo kwa ndege leo ukitokea Mwanza na unatarajiwa kuzikwa rasmi Jumamosi katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Mpanda.
Mauaji ya Mhubiri wa kiisilamu nchini Kenya yasababisha ghasia na uvunjifu wa Amani.
Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa
kiisilamu ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo
la Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa risasi
mjini Mombasa pwani mwa Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine
kujeruhiwa katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na
mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo
ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa.
Hali
ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu
kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya
mjini Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya
leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika
mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia
maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali
kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na
polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.
Aboud Rogo
Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari
lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa
za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya
umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya
kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya
Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati
za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo
alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa
anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini
Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa
risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya
Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa kujihihusisha
vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.
Wapiganaji wa al
Shabaab
Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea
vikwazo vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema
kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa
vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu
la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth
Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu
na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo
alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali
hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya
kigaidi.
bbcswahili
Kasoro zashamiri Sensa ya Watu na Makazi
Sensa ya Watu na Makazi jana iliingia siku yake ya tatu, huku kasoro kadhaa ikiwamo ukosefu wa vifaa, upungufu wa makarani
na watu kugoma kuhesabiwa vikiripotiwa.Katika baadhi ya maeneo hadi
jana, wananchi walikuwa hawajaanza kuhesabiwa kwa kile kilichoelezwa
kuwa ni kutokana na ukosefu wa vifaa na makarani.
Ofisa Uhamasishaji wa Sensa Taifa, Said Ameir alikiri kupata taarifa za kasoro hizo lakini akaeleza kushangazwa na chanzo chake, akisema: “Vifaa tulivigawa maeneo mbalimbali nchini kulingana na mahitaji. Tunashangazwa na taarifa hizo kwamba hata wengine wamekosa reflector (makoti ya kuakisi mwanga) na vitambulisho.”
“Tunachofanya sasa ni kuchunguza tatizo hilo limeanzia wapi na limesababishwa na nini. Vilevile tunajitahidi kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapelekwa sehemu hizo ili kazi hiyo iendelee kama kawaida.”
Alisema pamoja na kasoro hizo, kazi hiyo inaendelea vizuri na itakamilika ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.
Kasoro
Baadhi ya makarani wa Kata ya Ubungo wamesema baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi wamekataa kushirikiana nao.
Mratibu Msaidizi wa Sensa kata hiyo, Pertronia Lyamuya alisema tatizo jingine ni baadhi ya waumini wa Kiislamu kugoma kuhesabiwa kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wakazi wa Kinondoni Shamba, Dar es Salaam.
Katika baadhi ya maeneo, makarani, walilazimika kutumia polisi kutekeleza majukumu yao. Baadhi ya mitaa ambayo polisi walitumika ni Juhudi, Kingugi na Kiburugwa iliyoko Temeke. Mitaa hiyo ilikuwa imebandikwa matangazo ya kuwahamasisha watu wasishiriki Sensa.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Engerasia Lyimo alisema kazi ya kuhesabu watu ilisimama kwa muda kusubiri polisi wa kuwasindikiza makarani hao kwenye nyumba hizo ili kulinda usalama wao.
Lyimo alisema katika Mtaa wa Kingugi, alijitokeza mjumbe wa shina wa CCM (jina tunalo),ambaye aliwahamasisha wakazi wa eneo lake wasijitokeze kuhesabiwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Basihaya, Kinondoni, Daniel Aron alisema kaya nane zilikataa kuhesabiwa kwa maelezo kwamba hazioni umuhimu wake. Alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa Ofisi ya Kata ya Boko.
Alisema kimsingi, changamoto kubwa katika eneo lake ni uchache wa vifaa kiasi cha makarani kushindwa kuanza kazi hiyo.
Msimamizi wa Kata ya Buguruni, Wilaya ya Ilala, Stella Mshana amesema kuwa baadhi ya watu wamekataa kuhesabiwa, wengine kutokana na imani za kidini na wengine kwa kutoelewa umuhimu wake.
“Maeneo ya Mnyamani tumekutana na vikwazo lakini kusema ukweli idadi yao ni ndogo kuliko wanaotupa ushirikiano. Unaweza ukakuta labda katika watu sabini, mmoja ndiye anakataa,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amesema Serikali itaendelea kupambana na kundi la watu wanaojihusisha na kusambaza ujumbe wa kupinga kushiriki Sensa.
Alisema jana kwamba hadi sasa Polisi inawashikilia watu wanne kutoka Wilaya za Temeke na Kinondoni.... “Kijana mmoja alijulikana kwa jina la Yusuph Ernest alikamatwa akisambaza ujumbe huo maeneo ya Magomeni Kagera.”
Arusha, Watu wasiojulikana, juzi walibandika mabango yanayowazuia makarani wa Sensa kutekeleza wajibu wao katika Kata za Ngarenaro na Unga Ltd. Mabango hayo yalibandikwa katika eneo la Daraja la Ngarenaro.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo pamoja na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Arusha, Magreth Martin walisema hadi jana hakukuwa na tukio la kukwamisha Sensa licha ya kuwapo kwa tukio hilo.
“Nawashukuru sana wananchi wa Arusha kwa kushiriki vyema Sensa katika siku hizi mbili za mwanzo baada ya kuelimishwa na kuelezwa umuhimu wake kwa mipango ya Serikali na maendeleo ya taifa licha kuwapo baadhi ya watu waliojaribu kuwashawishi kususia.”
Tanga,Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ibrahim Matovu wamewaagiza makarani wa Sensa kwenda kuwahesabu wanawake ambao waume zao wanadaiwa kukimbilia kusikojulikana kukwepa kuhesabiwa.Walitoa amri hiyo baada ya kuripotiwa kuwa baadhi ya Waislamu wa Kijiji cha Kigombe, Muheza, wamekimbilia porini kukwepa kuhesabiwa.
Inadaiwa kuwa baadhi ya wanaume waliondoka na kutoa amri kwa wake zao kutohesabiwa vinginevyo wangepewa talaka.
Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Kigombe, Mashauri Kanyama alisema tatizo hilo limesababisha baadhi ya makarani kushindwa kutekeleza kazi zao kikamilifu.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kigombe, Mohamedi Hatibu alisema baadhi ya wakuu wa kaya wametishia pia kuwapa talaka wake zao iwapo watahesabiwa.
Kilimanjaro
Baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro wamesema Sensa ya Watu na Makazi imekwenda vizuri.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walilalamika kwamba makarani walikuwa wakisuasua kufanya kazi hiyo.
Walisema makarani wamekuwa wakitumia muda mwingi na kwamba waliotegemea kuhesabiwa Jumapili, hawakuwaona makarani.
“Tulitegemea tutahesabiwa Jumapili na wengi hatukutoka nyumbani tukiwasubiri hasa ikizingatiwa ilikuwa siku ya mapumziko,” alisema Eben Ndosi, Mkazi wa Njiapanda Himo, Wilaya ya Moshi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mto Mabungo, Wilaya ya Moshi, Estarick Mbuya alisema kazi hiyo ni ngumu lakini itafanikiwa.
Wananchi wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro wamehimizwa kujitokeza kuhesabiwa katika Sensa bila kujali wito wa kutojiandikisha.Msimamizi wa Kata ya Masama Mashariki, katika Kitongoji cha Modio, Mwalimu Bernedicta Kilasara alisema katika taarifa yake kuwa mpaka kufika jana jioni, kaya 320 zilikuwa zimeshahesabiwa nyingi zikiwa za waumini wa Kiislamu.Kilasara alisema Waislamu wa Kitongoji cha Modio walikuwa wakihimizana kujiandikisha.
Igunga walipwa
Wenyeviti wa vitongoji wilayani Igunga, Tabora wameanza kulipwa posho zao za Sensa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga, Protace Mgayane alisema wenyeviti hao kutolipwa fedha hizo ilikuwa ni moja ya sababu za kutofanikisha kwa kiasi kikubwa kazi hiyo kwani viongozi hao ndiyo wanaofahamu maeneo yao pamoja na jamii ya eneo husika.
Wilaya ya Igunga ina wenyeviti wa vitongoji 632 na kila mmoja atalipwa Sh10,000.
Alisema fedha hizo ni kutoka katika bajeti ya Sensa ambayo imetokana na marekebisho yaliyofanywa katika baadhi ya matumizi ili kuwalipa viongozi hao muhimu wa vitongoji.
Ngorongoro,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutowaficha na kuwaandikisha watu kutoka Kenya, katika Sensa ya Watu na Makazi inayoendelea nchi nzima.
Lali alisema wananchi kutoka nchi hiyo jirani wamekuwa na uhusiano na mwingiliano wa kikoo na wakazi wa Ngorongoro hasa wa jamii ya Kimasai na kwamba hawatakiwi kuandikishwa kama Watanzania.
“Naomba kutoa wito kuwa wanaopaswa kuandikishwa ni Watanzania na kama kuna hao wageni kuna taratibu zake na wasiandikishwe kama ni Watanzania,” alisema Lali.
Ngorongoro ni moja ya wilaya za mpakani ambazo watu wake wana uhusiano mkubwa ukiwamo wa kikoo na moja ya koo hizo ni ya Loita ambayo ni ya Wamasai waliopo Kenya na Tanzania.
Watimuliwa Morogoro
Baadhi ya makarani wa Sensa katika Tarafa ya Turiani, Morogoro wamedai kufukuzwa kwenye baadhi ya kaya kwa kutuhumiwa kuwa matapeli kutokana na kukosa fulana na kofia kama Serikali ilivyotangaza kwenye vyombo vya habari.
Tukio hilo lilitokea juzi ambako karibu makarani wote wa Sensa kwenye tarafa hiyo hawakupata sare licha ya kuwa na vitambulisho jambo ambalo baadhi ya wenye kaya walikataa kuwakubali.
Serikali kupitia vyombo vya habari, ilishatangaza kwamba makarani wa Sensa watafika kwenye nyumba wakiwa wamevalia fulana na kofia zilizoandikwa Sensa, mifuko myeusi, lakini makarani wa Turiani hawakutekelezewa hayo.
“Nilifanya kazi ya ziada kumwomba mwenyekiti wa kitongoji ili anisaidie kuwaelimisha kwani walikuwa wanakataa,” alisema karani mmoja wa Kitongoji cha Kigugu.
Alisema changamoto nyingine ni kuchelewa kwa baadhi ya vifaa vya Sensa pamoja na kutumia ramani ya mwaka 2004 ambayo imepitwa na wakati kwani baadhi ya watu waliotajwa kuwamo walishafariki au walishahama.
Habari hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Pamela Chilongola, Aisha Ngoma, Kelvin Matandiko, Zaina Malongo, Zacharia Osanga, Aziza Masoud, Geofrey Nyang’oro, Dar; Josephine Sanga - Moshi, Mustapha Kapalata - Igunga, Hussein Nyari - Hai, Mussa Juma - Arusha, Mustapha Kapalata - Igunga, Peter Saramba, Arusha, Lauden Mwambona, Turiani.

source: mwananchi
Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani,"Viongozi wa Dini chanzo cha migogoro"
| Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani |
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Augustino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuacha kuwa chanzo cha migogoro
makanisani na badala yake kurudi zaidi kwa Bwana Yesu ili kuweza kutimiliza
kusudi walilopewa katika utumishi wao.
Rai hiyo aliitoa juzi siku ya Jumapili katika sherehe za uzinduzi wa miaka
hamsini ya Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) zilizofanyika katika
ofisi za makao makuu ya shirika hilo maeneo ya Muhimbili wakati alipohudhulia kama
mgeni rasmi wa tukio hilo.
Alisema tatizo kubwa lilipo makanisani kwa hivi sasa
linasababishwa na viongozi wenyewe ambao badala ya kumtumikia Mungu wamegeuka
na kuangalia vyeo hivyo basi ni vyema kurudi kwa Bwana ili waweze kumtumikia.
“Migogoro mingi iliyopo makanisani hivi sasa matatizo
makubwa yako kwenye uongozi wala sio wanaoongozwa cha muhimu tu ni kwamba
viongozi warudi zaidi kwa Bwana wanayemtumikia” alisema Jaji Augustino
Ramadhani.
Sherehe hizo
zilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo Jaji Angera Kileo, Askofu Philemon Tibanenason,
Mweka Hazina wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Donata Mugassa pamoja na viongozi wa
shirika hilo, Mwenyekiti Dk. Edda Mwandi aliyekuwa mwenyeji wa sherehe hizo
pamoja na Katibu Rev. Emaus Bandikile.
Scripture union kuzindua Jubilee ya miaka 50 kwa kishindo
| Aliyekuwa Mwenyekiti wa Scripture Union Tanzania, Bw.Chuwa (Katikati) akiwa pamoja na baadhi ya watendakazi wa wakati huo |
| Jaji wa Mahakama ya Rufaa Engera Kileo akiongoza maombi ya shukurani kwa ajili ya uzinduzi wa kutimiza miaka 50 ya Scripture Union Tanzania |
Studio ya Kisasa ya NIKO AMBAYE NIKO yazinduliwa Dar.
Studio ya Kisasa ya NIKO AMBAYE NIKO yazinduliwa Dar,tukio hilo ni la Kihostoria maana halijawahi kutokea kuwepo na studio
kubwa kiasi hicho katika kuzalisha mziki wa Injili kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki pia kazi za hapo ni
nzuri zenye uwezo na viwango vya juu zaidi,shughuli hiyo aliudhuliwa na Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini Dk. Lawrance
Kametta akiwa pamoja na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake,Rogathe
Swai pia walipata mda kujaribu vifaa vya Studio Niko Ambaye Niko,ambapo Mkurugenzi ni Steve Wambura.Ambapo waliiweka wakfu studio huyo tayari kwa kazi,pia kumwombea Steve Wambura kwa kumbandika Mikono kwa kazi hiyo.
|
| Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini Dk. Lawrance Kametta akiwa pamoja na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake, Rogathe Swai wakijaribu vifaa vya Studio Niko Ambaye Niko jana |
| Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiwa pamoja na Mgeni rasmi Dk. Lawrance Kameta na Makamu Askofu aliyemaliza muda wake, Rogathe Swai wakati wa uzinduzi wa studio hiyo. |
| t | |
| Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiweka wakfu studio hiyo |
| Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akiombewa na Watumishi wa Mungu, (kushoto), Mchungaji Timbothy Wambura |
| Mkurugenzi Steve Wambura wa Studio ya Niko Ambaye Niko akitoa maelekezo kwa watumishi wa Mungu. |
Pallangyo Brothers wampa shetani kipigo Uyole Kati
Waimbaji watatu kutoka
Arusha, wanaounda kundi la Pallangyo Brothers, wenye kimo kifupi (Kibirikizi)
kwa kushirikiana na Kanisa la flani Uyole Kati
mjini Mbeya, wameleta mamia msalabani katika mkutano mkubwa wa Injili wa siku
sita.
Mkutano
huo uliokuwa ukiendeshwa katika viwanja vya Kanisa hilo, huku Mhubiri akiwa
Askofu Steven Mulenga toka Mombo mkoani Tanga, uliokusanya mamia ya wakazi wa
mji huo, waliokuwa wakisumbuliwa na mapepo, huku wengine wakibubujikwa na
machozi baada ya kutua mizigo yao msalabani.
Akihubiri
katika mkutano huo, Askofu Mulenga, huku akisindikizwa na ujumbe uliokuwa na
kichwa kisemacho; FILIPO
ALIVYOMDHIBITI SIMONI MCHAWI KWA JINA LA
YESU, alisema,
Yesu alidhihirishwa ili kuzivunja kazi zote za shetani.
Alibainisha
kwamba, mwanadamu yoyote akimwamini Mungu ni wazi kuwa hakuna jambo lolote
linaloweza kushindikana, huku akielezea kwamba, dhambi ndiyo inayomtenganisha
mwanadamu na Muumba wake.
Mtumishi
huyo aliweka wazi juu ya hilo alisema: “Hata leo Yesu yu hai na anaweza kumpa
mtu mahitaji yake wakati wowote anapoitwa.”
Askofu
Malenga, huku akiwa sambamba na Mchungaji mwenyeji wa Uyole Kati, Immanuel
Mwalyenga alitanabaisha kwamba, hata yale ambayo watu wameyakatia tamaa, Bwana
anaweza kuleta ukombozi na kumuaibisha shetani.
Katika mkutano huo, Pallangyo
Brothers walikuwa na mguso wa pekee kwa jamii, huku watu wakijiuliza namna
maumbo yao yalivyo, lakini wanaweza kumnyang’anya shetani mateka.
Huduma ya uimbaji katika mkutano
huo, mbali na kuwepo kwa Pallangyo Brothers pia walikuwepo wengine kama akina Amani
Mwasote, Kwaya kutoka makanisa mbalimbali na kwaya wenyeji Usiogope na Kedroni.
Ingawa mkutano huo ulifanyika
wakati wa kipindi cha maonesho ya Kikanda ya Nanenane ambayo pia huvuta watu
wengi, lakini Mungu hakuweza kuruhusu shetani afanye uharibifu kwa kuwakalia
watu wa Mungu na hivyo kwa uwingi wao walikusanyika kwenye mkutano huo mkubwa.
Katika mkutano huo watu zaidi ya 60
waliokolewa, wengine walifunguliwa katika vifungo vya magonjwa na maonezi ya
pepo wabaya, huku wengine wakileta vitu vyao ambavyo walitumia kwa uganga vichomwe
moto.
Moja ya vitu vilivyomuacha shetani
taabani ni la mama mmoja kutoka kijiji cha Isyonje wilayani Rungwe ambaye baada
ya kusikia tangazo la mkutano kupitia Redio Ushindi, alisafiri hadi Uyole kusikia
Bwana anasema nini juu ya maisha yake na katika siku ya pili ya mkutano
alifunguliwa kutokana na mapepo ambayo yalikuwa yamemtesa kwa muda mrefu.
Kama hilo halitoshi, mwisho wa
mkutano Askofu Mulenga wakishirikiana na Mchungaji Kiongozi wa Uyole Kati
Immanuel Lyego Mwalyenga, pamoja na jopo la wachungaji waliohudhuria mkutano
huo, walifanya maombi ya kuliombea Taifa kwa kushika bendera ya Tanzania.
Waamini
hao wapya, waliompokea Bwana Yesu katika mkutano huo; wanaendelea na mafundisho
ya msingi yanayoongozwa na Mchungaji Bahati Mwandemba katika kuhakikisha
wanaendelea katika imani na kufanyika baraka kwa Kanisa, Taifa na jamii kwa
ujumla
RC, Paroko kutokomeza mauaji kanda ya ziwa
| Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo. |
Rai hiyo ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuelezwa kwa nyakati tofauti na wakazi, wilayani humo kuwa kundi hilo linajihusisha na mauaji ya watu na kisha kunyofoa viungo vya mwili hasa sehemu za siri.
Akiwa katika kijiji cha Bugorola Ndikilo alielezwa kuwa, hivi sasa wakazi wa Wilaya hiyo wanashindwa kutimiza majukumu yao vyema wakihofia kuuawa na kundi ambalo hata hivyo wahusika wake hawajulikani.
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili wilayani Ukerewe kuhamasisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agositi 26, 2012 aliahidi kuwa serikali ikitumia vyombo vyake vya dola itafanya kila linalowezekana kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.
Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikilalamikiwa na watu wengi na kwamba wanajipanga kuhakikisha wanalimaliza kabisa kwa sababu liko chini ya uwezo wao.
Naye Paroko wa Parokia ya Nansio, Padri Masaga akiongelea jambo hilo, huku akiahidi kuwa bega kwa bega na kamanda huyo; aliitaka serikali kutokaa kimya badala yake ikemee maovu hayo, ikiwa ni pamoja na vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini.
Mtumishi huyo wa Kanisa Katoliki ambaye aliendelea kubainisha kwamba anasikitishwa na tabia ya serikali kubaki kimya bila kutoa tamko na hata kukemea mambo kama haya ya mauaji ya watu na kisha kunyofolewa viungo sehemu za siri na kikundi cha Makilikili.
Hata hivyo uchunguzi wa Polisi unaonyesha kuwa hofu hiyo imesababishwa na uvumi ulioenea takribani miezi miwili iliyopita, baada ya kuwepo vifo vya watu watatu ambao kati yao wanaume wawili wamepigwa hadi kufa kwa tuhuma za wizi; huku mwanamke mmoja akipoteza maisha katika harakati za kutoa mimba.
Wakati huo huo; watu watatu wamekufa maji wilayani Ukerewe, Mwanza baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba na kuzama katika ziwa Victoria.
Habari zilizopatikana toka kisiwa kidogo cha Kweru na kuthibitishwa na Polisi zinasema kuwa katika mtumbwi huo wa kasia walikuwemo watu 15 na kati yao watatu walikufa maji huku wengine 12 wakiokolewa na wavuvi waliokuwa karibu na eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mery Tesha alisema watu hao walikumbwa na mkasa huo wiki iliyopita majira ya saa 10.00 jioni, wakati wakitokea kijijini kwao Buzegwe kwenda kisiwani Kweru kuhani msiba wa ndugu yao.
Habari zaidi zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Leberatus Barlow zimewataja waliokufa kuwa ni Mgalla Yustinian (55), Pascazia Lyaganga (55) wakazi wa kijiji cha Buzegwe na Nyanjala Dotha (45) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Bukongo.
Diwani wa kata ya Kagunguri, Misana Ghatawa, akiongelea tukio hilo, alisema watu hao walipata mkasa huo muda mfupi baada ya kuondoka katika mwaloni wa Ilondo, miili yao tayari imepatikana na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya wavuvi walioshuhudia tukio hilo walisema, mtumbwi huo ambao ulionekana kulemewa na mzigo, ulizama baada ya kupigwa na mawimbi makubwa ya ziwa Victoria na kuongeza kuwa, kama wangekuwa na vifaa vya uokozi pengine wote wasingepoteza maisha.
Jaji atoa hukumu mtoto abatizwe.
Jaji wa nchini Uingereza, John Platt ametoa hukumu ya mtoto wa miaka 10 abaki kuwa mkristo
na ikiwezekana abatizwe kabisa, baada ya kuwepo kwa msuguano baina ya wazazi wake
ambao mmoja alitaka awe mkristo.
Hukumu
hiyo ilitolewa wiki iliyopita katika Mahakama ya Romford, baada ya wazazi wa
mtoto huyo kusuguana tangu Novemba 2011 huku mama akipinga mtoto wake wa miaka
10 kubatizwa kwa maelezo ya kigezo cha umri huku akitaka tendo hilo lifanyike
akiwa na umri wa mika 16.
Baada
ya kutoelewana, mama ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara
moja alifungua kesi mahakamani ili iweze kuruhusu mwanaye kutobatizwa kwa
kigezo cha kutojua baya na zuri, huku baba naye akidai ni muda muafaka na
hakuna ulazima wowote wa kusubiri miaka 16.
Malalamiko
mengine aliyokuwa akidai mama huyo ni umri wa mwanaye huyo kuwa ni mdogo kiasi
cha kubadilisha imani. Jambo lililopokelewa na baba kwamba anaweza kueleza
kulingana na sheria za Mungu na kwamba hata nyakati za Biblia Mungu aliweza
kumtumia Daudi aliyekuwa mdogo.
Hata
hivyo mwisho wa siku mahakama hiyo haikukubaliana na mama huyo na kumuamuru
kuwaachia watoto wawe wakristo na wabatizwe na kwa sasa wanapewa mafundisho
yanayoelezea nini maana ya kubatizwa na watakapomaliza watakuwa huru kubatizwa.
Wazazi
hao walifikia mafarakano hayo baada ya kugombana na hivyo kuamua kutengana na
hapo baba aliamua kubadili dini na kuwa mkristo.
Happybirthday Joyce Chalse,Mtangazaji wa Praise Power Radio asherekea siku ya kuzaliwa.
Mtangazaji wa Praise Power Radio afanya sherehe ya kumbukumbu ya
siku yake ya kuzaliwa kwa namna ya pekee,sherehe hiyo ilikuwa na kusifu na
kuabudu tofauti na nyingine zinavyokuwa.
Mtangazaji huyo ambaye ni Joyce Chalse aliyejumuika na ndugu wa karibu,marafiki na wazazi katika kufanikisha siku hiyo,watangazaji mbalimbali wa Redio na Bloggers mbalimbali walikuwepo kumpa kampani Mtangazaji huyo na kufanikisha shughuli nzima!

| Joyce Chalse akitoa Neno la Shukrani kwa wegeni waliofika. |
| Joyce Chalse akiwa na mumewe |
| Joyce Chalse akiwa na mume wake na mtoto wake wa kwanza kati ya wawili |
| President Chavalla katikati Mc Pilipili kwa pembeni mtangazaji wa Praise Power wakifungua
Shampaign
|
| Vijana wa Apostle Ndegi baada ya kupiga kazi Living Waters ndio waliongoza sifa siku hiyo. |
| Mc Pilipili akiwa kazini kama kawaida yake |
| The Blogger Uncle Jimmy-unclejimmytemu.blogspot.com |
| The Blogger Papa Sam Sasali bila kukosa -samsasali.blogspot.com |
| Living Waters wakiwa kwa stage wakifanya mambo yao. |
| Lisa na mwenzie wakiwakilisha Praise Power Radio |
| Living Waters kutoka Makuti Kawe wakihudumu siku hiyo. |
Subscribe to:
Posts (Atom)