Askofu Hotay wa Kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro akabidhiwa rasmi kiti chake cha Uaskofu.

Wakati zikiwa zimepita siku chache mara baada ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali pingamizi la waumini wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro juu ya Uaskofu wa Askofu wa kanisa hilo Stanley Hotay (Leo)kanisa hilo limemuweka rasmi kazini askofu huyo sanjari na kutangaza msamahaa kwa waumini hao watatu kwani wamechangia sana kanisa hilo kupoteza muda kwenye kesi hiyo pamoja na aibu kubwa kwenye masikio ya watu wengi

 Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka

Askofu Stanley Hotay
Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka sasa wameshatangaza Msamaha  kwa watu hao ambao walitia aibu kanisa hilo hivi karibuni

 Askofu huyo alisema kuwa hapo awali baadhi ya waumini akiwemo yeye mwenyewe walikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na  kesi hiyo lakini kutokana na ukweli na haki  ya Askofu Hotay aliweza kupata haki yake kupitia mahakama  Septembe  tano mwaka huu huku waliofungua kesi hiyo wakishinndwa kusonga mbele

 Mbali na hayo alisema kuwa kuna masaa mengi sana ambayo yamepotea katika Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na waumini watatu lakini kanisa kama kanisa linapswa kuhakikisha kuwa linatoa msamaha wa kweli ambao unatoka ndani ya Mioyo yao kwani watu hao walidanganywa na hata kufikia hatua ya kutoka nje ya Kundi bila kujua kuwa hali hiyo inachangia sana hata mmonyoko wa Kanisa na aibu sana

 Katika hatua nyingine alisema kuwa kanisa hilo limempa Nafasi ya kuongoza jimbo hilo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo na kutokana na hali hiyo kiti hicho ambacho alikuwa hakitumii kutokana na kesi ambayo ipo mahakamani sasa anaanza kazi rasmi kwa kuwa sheria inamruhusu huku waumini wa  kanisa hilo nao wanatakiwa kumpa ushirikiano na kukumbuka Viapo mbalimbali ambavyo vinatumika na kanisa hilo

 Naye Askofu Stanley Hotay aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa ili ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe kuwa unatoa msamaha hata  kwa wale ambao wamekuwa ni vikwazo vya kushindwa kufikia katika malengo mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa ingawaje vikwazo ni vingi sana katika safari ya Ushindi

 Askofu huyo alifafanua kuwa pamoja na kuwa amepita katika wakati mgumu sana hasa wa kuwa na kesi ya kutotambulika na waumini wake lakini bado ana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwatumikia hao hao na kuwafanya wabadilishe fikra kwani hapo awali hawakujua wanachokifanya hali ambayo ilizaa aibu kubwa sana mbele ya kanisa la Angilikana dayosisi ya Mout Kilimanjaro.

 Aliwataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanasahau hilo na kuanza kufikiria upaya kwani bado kanisa hilo lina muitikio mkubwa sana wa kuweza kuwasaidia waumini pamoja na jamii kwa kuweza kuhamasisha maendeleo ambayo ndiyo yana amani kwa maslahi ya Taifa la Tanzania

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ukabidhiwaji wa kiti hicho kwa askofu huyo ambaye hapo awali alikuwa ameshasimikwa kama askofu wa kanisa hilo alisema kuwa wakristo wanatakiwa kujua hakuna dhambi mbaya sana kama dhambi ya kutamani madaraka kwani dhambi hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa migogoro sana

 Bw Mulongo aliongeza kuwa ni vema kama mtu anayetamani Madaraka hata kama ni ya Uaskofu basi kuomba Mungu kna wala sio kuwa chanzo cha kuanzisha Kesi ambazo hazina Tija na ambazo zinapotosha hata maana halisi ya Wokovu huku tamaa kama hizo zikiwa ni chanzo pekee cha kuweza kusababisha amani kutoweka



Source:fullshangweblog.com

Waandishi wa habari kuandamana kimyakimya nchi nzima kesho asubuhi.

LENGO NI KULAANI MAUAJI YA DAUD MWANGOSI, KUTOA MATAMKO.
Waandishi wa habari nchini kesho wataandamana nchi nzima kwa amani kulaani kuuawa kwa mwandishi mwenzao, Daud Mwangosi aliyeuawa Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, Iringa.

Maandamano hayo ambayo yatakuwa ya kimyakimya yatafanyika katika mikoa yote nchini kuanzia saa 2:00 asubuhi na waandishi watakaoshiriki katika maandamano hayo watavaa ama nguo nyeusi au watafunga vitambaa vyeusi mkononi ikiwa ni ishara ya kuomboleza na kulaani kuuawa kwa mwenzao.



Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), Theophil Makunga alisema kuwa uamuzi wa kufanyika kwa maandamano hayo ulifikiwa katika kikao cha jukwaa hilo kilichofanyika Dar es Salaam juzi.

Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam, maandamano hayo yamepangwa kuanzia katika Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Mtaa wa Jamhuri ambacho Mwangosi alikuwa akikitumikia na kupita katika Mtaa wa Azikiwe, Barabara ya Bibi Titi hadi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambako maandamano hayo yatahitimishwa.

Alisema baada ya kufika katika viwanja hivyo, yatapokewa na viongozi wa TEF na kisha baadhi ya waandishi waliokuwapo katika eneo la tukio watatoa ushuhuda wa kilichotokea na kufuatiwa na mjadala kuhusiana na mauaji hayo na kutoa tamko la pamoja.

Marehemu Daud Mwangosi akiwa kazini wakwanza kushoto.
“Kutatolewa ushuhuda kutoka kwa waandishi wa habari ambao walishuhudia tukio la kuuawa kwa mwandishi mwenzao, wataeleza kwa kina hali halisi na ukweli waliouona siku ya tukio,” alisema Makunga.

Alisema tayari wamekwishawasiliana na Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ambako wamepeleka barua ya kuomba ulinzi kesho wakieleza njia watakazopitia siku hiyo.

“Tunafanya matembezi ya amani, kimyakimya kwa lengo la kulaani tukio la kusikitisha la kuuawa kwa Mwangosi. Ni mwandishi wa kwanza hapa nchini kuuawa akiwa kazini na doa kubwa kwa nchi yetu na vyombo vya dola, hivyo lazima tulilaani tukio hilo.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema, hajapokea barua hiyo na kusema kwamba inawezekana ipo kwa wasaidizi wake na hivyo kuahidi kuifanyia kazi.

“Sijaiona barua yao, inawezekana ipo kwa maofisa wangu au wameipeleka kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, nitafuatilia kujua ili kuona jeshi langu litafanya nini,” alisema.

Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jane Mihanji alisema kwamba lengo la maandamano hayo ni kulaani mauaji ya Mwangosi na zaidi ni kufikisha ujumbe kwa Serikali.

“Hatukupendezwa na mauaji hayo, yametuumiza na hatutopenda yatokee tena, tunayalaani na kuomba hatua kali zichukuliwe,” alisema Mihanji.

Maandamano mikoani
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan alisema, sambamba na maandamano hayo Dar es Salaam, pia waandishi wengine mikoani nao wataandamana kuungana na wenzao kulaani mauaji hayo ya mwenzao.

Maandamano ya mikoa yote nchini yatasimamiwa na klabu zote za waandishi wa mikoa husika na kwamba maandalizi yake ni pamoja na kubainisha njia watakazopitia kwa upande wa mikoani, yamekwisha kamilishwa. Alisema maandamano hayo yatapokewa na wenyeviti wa klabu ambao watatoa matamko mbalimbali kuhusiana na kifo cha Mwangosi.

“Kila mkoa hapa nchini utashiriki maandamano, wataandamana kwa amani kuungana na wenzao kulaani kifo cha mwandishi mwenzao, nao kama ilivyo kwa Dar es Salaam watavaa nguo nyeusi au vitambaa vyeusi mkononi,” alisema.

Alisisitiza kwamba kama itakavyokuwa kwa yale ya Dar es Salaam, maandamano hayo hayatahusisha kiongozi yeyote wa Serikali, chama cha siasa au wanaharakati, bali waandishi wa habari wenyewe viongozi wao.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya maandamano hayo yamekamilika. Alisema yataanzia katika Viwanja vya Ghand Hall, kupitia Barabara za Uhuru, Mlango Mmoja, Nyerere na kuingia katika Barabara ya Miti Mirefu, Pamba, Barabara ya Kenyatta hadi Uwanja wa Nyamagana.

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali alisema, ofisi yake ilikuwa katika maandalizi ya kufanikisha maandamano hayo akisema kwamba hadi leo jioni watakuwa katika nafasi nzuri ya kutangaza njia watakazopitia na mahali yatakapoishia.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya, Christopher Nyenyembe alisema kwamba pia wako katika maandalizi ya kukamilisha maandamano hayo.

“Tunazo sababu za kuandamana kuungana na wenzetu nchi nzima, tulikwisha toa tamko letu kulaani mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kususia kuandika habari za polisi, lakini katika maandamano hayo tutatoa tena tamko,” alisema.

Askofu TAG aonya kukithiri vurugu na mauaji ya raia Nchini.

Askofu Mkuu wa jimbo la Mashariki la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk Lawrence Kameta ametahadharisha kuhusu mauaji na ghasia zinazotokea nchini kwamba siyo dalili nzuri ya amani.

Askofu Kameta ametoa kauli hiyo baada ya kutokea mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi hivi karibuni ambaye anadaiwa kuuawa na polisi katika mkutano wa Chadema.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa Ibada ya kuwasimika viongozi wapya wa jimbo hilo, Dk Kameta alisema kama mambo hayo yataachwa yaendelee kuna hatari ya nchi kuingia kwenye machafuko.

Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa na kwamba viongozi wa dini wanapaswa kuiombea nchi kwani Serikali peke yake haiwezi kuleta amani.

“Vifo, ghasia na maandamano siyo dalili nzuri ya amani. Sisi kama viongozi wa dini  tuna sehemu yetu katika kuleta amani hivyo tuchukue jukumu hilo,” alisema Dk Kameta.

Alisema pia kuna haja ya kuviombea vyama vyote vya siasa ili viwe na sera nzuri zitakazoepusha machafuko.
“Si kwamba tukifanya hivi tutakuwa tunaleta siasa makanisani kwa sababu kama vurugu zikitokea hata kanisa linaweza kuwa kuathirika,” alisema.

Pia aliwaasa viongozi wapya waliosimikwa katika jimbo hilo kuwa na hofu ya Mungu na kuwa waaminifu katika utumishi wao.

Alisema kama viongozi wakikosa uaminifu madhara yake ni makubwa kwani kanisa linaweza kuporomoka kimaadili na kukosa nguvu ya kuliwakilisha taifa.

Mch. Dar kukabiliana na mafundisho potofu.

Akemea wanaotukuza kundi la Freeemasons, aelezea fursa sahihi za kubarikiwa na kufanikiwa.

Kutokana na kuibuka kwa wimbi kubwa la mafundisho yenye kupotoa imani, kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo kadhaa vya habari, Mchungaji Ron Swai wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dar es Salaam Calvary Temple (DCT), amejitolea kukabiliana na mfumuko huo.

Mchungaji Swai, alibainisha hayo siku chache zilizopita kanisani kwake, wakati wa ibada maalum ambapo alibainisha kuwa, katika nyakati hizi za mwisho, kuna kundi la watu ambao aidha kwa kutokujua Neno la Mungu kwa usahihi, ama kwa makusudi, wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotoa maandiko na kuwahadaa watu kwa matangazo yao ya baraka.

Mchungaji Ron Swai wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dar es Salaam Calvary Temple (DCT)

“Niko radhi kupambana na mafundisho potofu yanayotolewa na baadhi ya watu kupitia vyombo mbalimbali vya habari, nitatoa mafundisho yatakayowatoa watu kwenye mtazamo hasi na kuwarejesha katika msingi imara wa kufahamu Neno la Mungu na kuliishia,” alisema Mchungaji huyo na kuongeza:

“Yameibuka mafundisho mengi yenye falsafa potofu ambayo mtu akibarikiwa kwa wakati huu anasemwa kuwa amejiunga na Freemason, akikosa wanamwita akaombewe, ili abarikiwe, lengo ni kuwachanganya watu ili wasielewe Neno sahihi la Mungu.”

Aidha Mchungaji Swai, aliwataka watu kuondokana na dhana hiyo potofu, badala yake walisome Neno la Mungu, kwa usahihi, waliishi na kutekeleza yote yaliyoelekezwa humo ili wapate Baraka ambazo ziliahidiwa na ziko tayari kwa yule anayeamini.

Mtumishi huyo wa Mungu alisema atahakikisha anatumia vyema madhabahu takatifu ya Mungu kuhubiri, kufundisha kwa usahihi Neno, bila kupindisha ili kubadilisha mwelekeo wa falsafa potofu iliyogandamana ndani ya mioyo ya watu wengi walioumizwa.

Mbali na hilo Mchungaji huyo alisema, ameamua kufundisha somo hilo linalohusu kanuni sahihi ya kubarikiwa kwa mtu wa Mungu, baada ya kukutana na watu wengi walioumizwa na mafundisho potofu waliofika katika Kanisa la DCT kuomba msaada.

Aidha Mchungaji Ron, aliwataka watu kuelewe kwamba, kabla ya vitu vyote, Freemasons na mambo mengine Mungu alikuwepo na aliishatoa ahadi kwa wamchao, na kuwa jambo kubwa kwa sasa ni kuingia kwenye utekelezaji wa kumdai Mungu na sio kukimbilia ibada za maombezi ambazo mifumo yake inafanana sana na uganga wa kienyeji.

“Nasema Freemasons sio kila kitu, Mungu ni zaidi ya Free masons, watu wamefikia mahali hawamchi Mungu wa kweli, badala yake wanatoa heshima na utukufu kwa vitu vusivyofaa kabisa,” alisisitiza Mchungaji Swai

Mchungaji Ron, alikemea vikali tabia ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu na kutumia vibaya mimbari kuwahadaa watu kwa utabiri wao kwa lengo la kujipatia pesa.

“Nasema achana kabisa na mambo hayo, umtukuze Mungu wa kweli ili upate Baraka zake zisizokuwa na majuto,” alisisitiza Mchungaji Ron.

Kilichoojili katika Uzinduzi wa Album ya Mwanamzimki wa Injili Paschal Kasian katika viwanja vya sifa.

Mwanamzimki wa Injili Paschal Kasian kutokea Bongo Star Search mpaka kuwa mwanamziki mkubwa wa Injili Nchini akitokea katika mashindano ya Bongo Star Search chini ya udhamini wa kampuni ya Bechmack Production.
Wiki hii iliyopita alifanya uzinduzi wa album yake ya nyimbo za Injili katika viwanja vya sifa viliyokuwa vikijulikana kama viwanja vya fisi hapa zamani na kuudhuliwa na wadau mbalimbali.

Katika Uzinduzi huo Mkurugenzi wa Bechmack Production na Mwanzilishi wa Bongo Star Search Madam Ritha  ndiye aliye kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo wa Kijana wake aliye fanikiwa kimziki kutoka katika Bongo Star Search miaka aliyopita .


Paschal Kasian na Madam Ritha wakidancde kuelekea kwa stage



Paschal Kasian akifanya vitu vyake kwa stage na wenzake
Madam Ritha akiinadi album ya Pascha Kasian

Madam Ritha akikata utepe kwa Kuzindua Album ya Paschal Kasian

Idadi ya Mashabiki wa Paschal Kasian walijitokeza kuangalia uzinduzi huo katika viwanja vya sifa


Debora Ntepa, Tunu Pinda kuteta na wanawake, Mabinti Diamond Jubilee


Mchungaji Deborah Ntepa wa Huduma ya The Palm of Deborah kwa kushirikiana na huduma ya Oasis of Healing Ministry, ya Ubungo jijini Dar es Salaam, anatarajia kuwa na kongamano la aina yake la wanawake na mabinti katika ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee kwa siku mbili.

Kongamano hilo ambalo mgeni ramsi atakuwa ni mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Tunu Pinda na Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba; litakuwa ni la kinabii juu ya maendeleo ya wanawake na mabinti wa kitanzania.

Wanenaji watakaokuwa katika kongamano hilo kubwa ni kutoka nchi mbalimbali wakishirikiana na Mchungaji Deborah Ntepa.

Vitabu mbalimbali vya Mchungaji Deborah Ntepa, vilivyoandikwa kwa umahili mkubwa kupitia uvuvio wa Roho Mtakatifu vitauzwa katika kongamano hilo.

Chakula cha mchana kitatolewa siku ya Jumamosi bure

Kongamano hilo la siku mbili litafanyika  Septemba 8-9, 2012.

Mchungaji Deborah Ntepa
Bi. Tunu Pinda

Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba
KWA MAWASILIANO ZAIDI:

Email:
ancientntepa@hotmail.com
deborahpros@hotmail.com

                   SIMU:  
0713 - 212 440; 0715 - 029 602
0755 - 029 602.

Waumini wapiga kura kuingia na bunduki kanisani.


 Kukithiri kwa mashambulizi katika makusanyiko ya watu wengi nchini Marekani kumepelekea  baadhi ya wamarekani kupiga kura na kuamua kubeba silaha za moto kama bunduki wakati wa Ibada ili kujilinda.

Kwa mujibu wa utafiti uliosimamiwa na taasisi iitwayo, “Public Religion Research Institute (PRRI), ya Marekani kura hiyo ilihusisha watu 1006 waliochaguliwa kwa kuzingatia makundi yote na asilimia 55 walieleza kufurahishwa na utaratibu wa kubeba bunduki na bastola zenye risasi za moto makanisani, wakati wa ibada.

Miongoni mwa asilimia  55 waliopendekeza ubebaji silaha wakati wa kumuabudu Mungu, asilimia 38 wanatoka katika chama cha Republican kinachowakilishwa na Mitt Romney, anayechuana vikali na Rais Barrack Obama wa Democratic katika kinyanganyiro cha urais, kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

“Unajua tumeamua kufanya utafiti huu, ili kupata maoni tofauti baada ya mahakama katika Jimbo la Georgia kuruhusu watu kuingia na bunduki katika nyumba za ibada, kutokana na kuwepo kanuni kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo mtu hapaswi kuingia na silaha kama bunduki,” alisema Mkurugenzi wa PRRI Bw. Daniel Cox.

Alisema kuwa utafiti huo uliofanyika kati ya Agosti 8 na 12, uliainisha maeneo mbalimbali ambayo watu wanaweza kuwa huru kwenda na bunduki na yapi yasiyofaa; na hayo ni pamoja na kutokuwa na silaha kwenye vyuo vikuu na maeneo ya huduma za serikali.

Sambamba na hilo, utafiti pia ulichanganua kuwa, asilimia 68 ya wamarekani walifurahishwa na sheria ya uhuru wa kuwa na silaha. 


“Licha ya utafiti huu juu ya udhibiti wa silaha, watu wengi nchini Marekani wanasema kwamba kama ulivyo uhuru wa kikatiba wa kutumia silaha , basi hilo nalo ni jambo la muhimu kama ulivyo uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria,” alisema Mkurugenzi mtendaji wa PRRI, Dk. Robert  Jones, na kuongeza:

“Lakini hakuna cha ajabu kwa kuwa wanaounga mkono suala zima la kuwa na uhuru wa bunduki ni wamiliki wa bunduki

Julai 20, 2012 kijana mmoja alivamia ukumbi wa sinema na kukuta watu wakiendelea kuangalia sinema ya The Dark Knight Rises, akawafyatulia risasi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, jambo lililosababisha watu 12 kupoteza maisha na wengine 58 kujeruhiwa.

Kama hilo halitoshi Agosti 5, 2012 kanisa moja Sikh Temple la Oak Creek, lilimiminiwa risasi za moto na watu sita waliuawa huku wengine wanne wakijeruhiwa.

  

Ibada ya Shukrani Life Changers Temple-Kibaha


Tamasha Kusifu na Kuabudu siku ya Jana CCC chini ya CASFETA

Siku ya Jana Katika Kanisa la City Christian Centre  Upanga (CCC) kulikuwa na Tamasha la Kusifu na Kuabudu lililokuwa limeandaliwa na uongozi wa Casfeta-TAG Mkoani Dar es salaam,Katika Tamasha hilo walipata kushiliki Neno lililoongozwa Mchungaji Deo Lubala kutoka Word Alive Ministry.

Wanafunzi,wanavyuo vya elimu ya juu na wadau mbalimabali katika kila kona ya Jiji la Dar es salaam walionekana kuhudhulia kwa wingi kwa kile kilichoonekana kuwa ni Kumsifu na Kumtukuza Mungu.

Ibada hiyo ilipambwa na Nextlevel Team,John Lisu,Rivers of Life chini ya Pastor Paul Safari,Word Alive Praise and Worship Team na Casfeta Mass Choir.
Mchungaji Deo Lubala- Word Alive Ministry 

Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika Tamasha hilo siku ya Jana kama wanavyoonekana.
Pastor Paul Safari
John Lisu

Backup team ya John Lisu
fullshangwe


Baadhi ya Viongozi wa Dini na Casfeta-TAG wakifuatilia Tamasha hilo
Casfeta Mass Choir




John Kagaruki akifanya 
vitu vyake akiwa na Lawrence

 akipuliza pembe kuashilia mambo moto 

Kanisa lafunzwa juu ya katiba

Kanisa la Tanzania kwa mara nyingine limetakiwa limetakiwa kutumia fursa mbalimbli zinazopatikana kwa kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike kwa lengo la kuleta ukombozi na kulinusuru taifa na changamoto ambazo kwa upande mwingine zimekuwa zikihatarisha amani iliyopo, huku likitambua kuwa ndilo mhimili wa nchi,Elimu hiyo ya katiba inazidi kutolewa makanisani kuhakikisha waksristo wanaelewa elimu hiyo.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Wakili Magdalena Rwebangira wakati akitoa semina juu ya kanisa na Katiba, iliyofanyika katika kanisa la City Harvesty lililopo Garage, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumuwezesha mkristo kutambua umuhimu wa katiba na jinsi ya kusimama kudai haki yake.
Wakiri huyo alisema kuwa kanisa lazima liitumie katiba katika kudai haki na sii kukaa kimya huku wakristo wakibaki kulalamika pindi linapotokea tatizo lolote, linalohusu masuala ya kanisa na kusema kuwa huko ni kushindwa kutafuta haki yao ya msingi kwa masilahi ya kanisa na taifa kwa ujumla.


Wakili Magdalena Rwebangira
Kadhalika Bi.Rwebangira alilikumbusha kanisa kutambua kuwa nchi hivi sasa iko katika mchakato wa kuandaa katiba mpya, hivyo kuwataka kutumia nafasi hiyo katika kutoa maoni yao juu ya kile wanachokihitaji huku akiongeza kuwa ni sehemu ya pekee ya kanisa kuhusika zaidi na si kurudi nyuma katika mambo ya kiserikali kama hayo.
Aliongeza kuwa lazima maoni ya uhuru wa kuabudu katika katiba ijayo uzingatiwe, kutoingiliwa kwa namna yoyote katika ibada zinazo fanyika, kutoangalia masuala ya kidini ikiwa ni pamoja na kanisa kupewa nafasi ya kutosha katika kumhubiri Kristo wa kweli, huku akisema kuwa nchi iko mikononi mwa kanisa.


Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kutoa elimu juu ya mambo ya Katiba Dk.Paul Shemsanga, ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Victory Gospel Assembly Tanzania aliyepata nafasi ya kutoa elimu siku hiyo alisema kuwa ni wakati wa kanisa kutambua nafasi yake na kuitumia ipasavyo na wala si kubaki likilalamika.


 Mchungaji Kiongozi wa kanisa la City HarvestYared Dondo
Aliongeza kuwa mambo magumu ambayo kwa namna moja ama nyingine kanisa limesahau wajibu wake, hivyo nchi kuzidi kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoleta mfarakano na amani tuliyojaliwa na Mungu kuzidi kutoweka siku hadi siku.
Askofu huyo alisema kuwa umefika wakati kanisa kutokaa kimya, na badala yake kusimama kidete katika maeneo yote, kwa lengo la kuleta ukombozi ndani ya taifa la Tanzania na kukomesha migogoro inayojitokeza. 
“Lazima katika Katiba, kanisa lishiriki sana, lazima tuzungumzie uchumi, umiliki wa ardhi, kutokubali ushawishi kutoka nchi za nje ikiwa ni pamoja na masuala ya kuabudu kutoingiliwa” alisema Askofu huyo. 


Aidha akikazia zaidi Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo la City Harvest, Architecture Yared Dondo, ambao kuanzia siku chache zilizopita wameanza kufanya ibada zao katika kanisa lao jipya lililopo Garage jijini hapa, alisema kuwa ni lazima kanisa kuwa makini na suala la Katiba ili mambo yanapoharibika badaye kanisa lisiweze kulalamika.


“Lazima Kanisa kuwa makini na kutopuuza suala hili la Katiba ni muhimu sana, ili badaye tusije tukawa watu wa kulaumu, kama hatutasimama kama wakristo, ambao tuna dhamana kubwa juu ya nchi hii,” alisema Mchungaji huyo.