Kukithiri
kwa mashambulizi katika makusanyiko ya watu wengi nchini Marekani
kumepelekea baadhi ya wamarekani kupiga
kura na kuamua kubeba silaha za moto kama bunduki wakati wa Ibada ili
kujilinda.
Kwa
mujibu wa utafiti uliosimamiwa na taasisi iitwayo, “Public
Religion Research Institute (PRRI), ya Marekani kura hiyo ilihusisha watu 1006 waliochaguliwa kwa kuzingatia makundi yote
na asilimia 55 walieleza kufurahishwa na utaratibu wa kubeba bunduki na
bastola zenye risasi za moto makanisani, wakati wa ibada.
Miongoni mwa asilimia 55 waliopendekeza ubebaji silaha wakati wa
kumuabudu Mungu, asilimia 38 wanatoka katika chama cha Republican
kinachowakilishwa na Mitt Romney, anayechuana vikali na Rais Barrack Obama wa
Democratic katika kinyanganyiro cha urais, kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo
unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu.
“Unajua tumeamua kufanya utafiti huu,
ili kupata maoni tofauti baada ya mahakama katika Jimbo la Georgia kuruhusu
watu kuingia na bunduki katika nyumba za ibada, kutokana na kuwepo kanuni kuwa
kuna baadhi ya maeneo ambayo mtu hapaswi kuingia na silaha kama bunduki,”
alisema Mkurugenzi wa PRRI Bw. Daniel Cox.
Alisema kuwa utafiti huo uliofanyika
kati ya Agosti 8 na 12, uliainisha maeneo mbalimbali ambayo watu wanaweza kuwa
huru kwenda na bunduki na yapi yasiyofaa; na hayo ni pamoja na kutokuwa na
silaha kwenye vyuo vikuu na maeneo ya huduma za serikali.
Sambamba na hilo, utafiti pia
ulichanganua kuwa, asilimia 68 ya wamarekani walifurahishwa na sheria ya uhuru
wa kuwa na silaha.
“Licha ya utafiti huu juu ya udhibiti wa
silaha, watu wengi nchini Marekani wanasema kwamba kama ulivyo uhuru wa
kikatiba wa kutumia silaha , basi hilo nalo ni jambo la muhimu kama ulivyo
uhuru wa kuongea bila kuvunja sheria,” alisema Mkurugenzi mtendaji wa PRRI, Dk.
Robert Jones, na kuongeza:
“Lakini hakuna cha ajabu kwa kuwa
wanaounga mkono suala zima la kuwa na uhuru wa bunduki ni wamiliki wa bunduki
Julai 20, 2012 kijana mmoja alivamia
ukumbi wa sinema na kukuta watu wakiendelea kuangalia sinema ya The Dark Knight
Rises, akawafyatulia risasi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, jambo
lililosababisha watu 12 kupoteza maisha na wengine 58 kujeruhiwa.
Kama hilo halitoshi Agosti 5, 2012
kanisa moja Sikh Temple la Oak Creek, lilimiminiwa risasi za moto na watu sita
waliuawa huku wengine wanne wakijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment