Maelfu ya watu walijipanga
foleni siku ya Jumamosi kando kando mwa barabara za mji mkuu wa Lebanon,
Beirut katika siku ya pili ya ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki
duniani Papa Benedict wa kumi na sita
Umati huo ulipeperusha bendera za lebanon na vatican huku msafara wa magari ya Papa ukielekea katika ikulu ya rais wa nchi hiyo.Papa alifanya mazungumzo na Michel Suleiman wa lebanon ambaye ndiye rais pekee mkristo katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Wakati wa ziara hiyo papa alipongeza ushirikiano na utangamano miongoni mwa wakristo na waislamu nchini lebanon huku akishutumu watu walio na misimamo mikali ya kidini.
No comments:
Post a Comment