Kauli hiyo aliitoa siku chache zilizopita wakati wa sherehe za shirika linaloshughulikia watoto waishio katika mazingira magumu na wanawake wanaojifunza ujasiriamali la DMI, mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Joseph Mkirikiti.
Askofu Mkuu wa Kanisa katoliki Jimbo Kuu la Songea, Nobert Mtega |
"Watoto hawana walinzi zaidi ya sisi wenyewe,na inatakiwa kutambua kuwa taifa bila watoto bado halijakamilika. Wao ni sehemu ya msingi katika jamii yoyote ile," alisema Askofu Mtega na kuongeza:
"Nawaambieni kama tutaachilia mambo haya ya kutumia silaha ovyo, yakaendelea kwa kweli tutakuwa tunatafuta machafuko ambayo yatahatarisha maisha ya watu wasio na hatia kabisa.”
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Joseph Mkirikiti. |
Mtumishi huyo wa kanisa Katoliki alisema kuwa kutumia silaha ovyo dhidi ya binadamu tena kwa yule asiyekuwa na hatia ni jambo la kishetani ambalo halistahili hata kidogo kwa kuwa linaweza kumkaribisha shetani katika jamii husika.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Songea, Bw. Joseph Mkirikiti aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa shughuli hiyo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ya kuwahudumia watoto waishio katika mazingira magumu, huku akiyaomba mashirika mengine kuiga mfano huo.
Mbali na hilo, alichanganua kwamba jambo la msingi la kuangalia kwa makini ni eneo lililokosewa katika kumlea mtoto ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ya kudumisha amani iliyopo ili vizazi viendelee kuwa na neema ya mafanikio.
No comments:
Post a Comment