Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka
Askofu Stanley Hotay |
Askofu huyo alisema kuwa hapo awali baadhi ya waumini akiwemo yeye mwenyewe walikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na kesi hiyo lakini kutokana na ukweli na haki ya Askofu Hotay aliweza kupata haki yake kupitia mahakama Septembe tano mwaka huu huku waliofungua kesi hiyo wakishinndwa kusonga mbele
Mbali na hayo alisema kuwa kuna masaa mengi sana ambayo yamepotea katika Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na waumini watatu lakini kanisa kama kanisa linapswa kuhakikisha kuwa linatoa msamaha wa kweli ambao unatoka ndani ya Mioyo yao kwani watu hao walidanganywa na hata kufikia hatua ya kutoka nje ya Kundi bila kujua kuwa hali hiyo inachangia sana hata mmonyoko wa Kanisa na aibu sana
Katika hatua nyingine alisema kuwa kanisa hilo limempa Nafasi ya kuongoza jimbo hilo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo na kutokana na hali hiyo kiti hicho ambacho alikuwa hakitumii kutokana na kesi ambayo ipo mahakamani sasa anaanza kazi rasmi kwa kuwa sheria inamruhusu huku waumini wa kanisa hilo nao wanatakiwa kumpa ushirikiano na kukumbuka Viapo mbalimbali ambavyo vinatumika na kanisa hilo
Naye Askofu Stanley Hotay aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa ili ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe kuwa unatoa msamaha hata kwa wale ambao wamekuwa ni vikwazo vya kushindwa kufikia katika malengo mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa ingawaje vikwazo ni vingi sana katika safari ya Ushindi
Askofu huyo alifafanua kuwa pamoja na kuwa amepita katika wakati mgumu sana hasa wa kuwa na kesi ya kutotambulika na waumini wake lakini bado ana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwatumikia hao hao na kuwafanya wabadilishe fikra kwani hapo awali hawakujua wanachokifanya hali ambayo ilizaa aibu kubwa sana mbele ya kanisa la Angilikana dayosisi ya Mout Kilimanjaro.
Aliwataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanasahau hilo na kuanza kufikiria upaya kwani bado kanisa hilo lina muitikio mkubwa sana wa kuweza kuwasaidia waumini pamoja na jamii kwa kuweza kuhamasisha maendeleo ambayo ndiyo yana amani kwa maslahi ya Taifa la Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ukabidhiwaji wa kiti hicho kwa askofu huyo ambaye hapo awali alikuwa ameshasimikwa kama askofu wa kanisa hilo alisema kuwa wakristo wanatakiwa kujua hakuna dhambi mbaya sana kama dhambi ya kutamani madaraka kwani dhambi hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa migogoro sana
Bw Mulongo aliongeza kuwa ni vema kama mtu anayetamani Madaraka hata kama ni ya Uaskofu basi kuomba Mungu kna wala sio kuwa chanzo cha kuanzisha Kesi ambazo hazina Tija na ambazo zinapotosha hata maana halisi ya Wokovu huku tamaa kama hizo zikiwa ni chanzo pekee cha kuweza kusababisha amani kutoweka
Source:fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment