Hatima ya Kansia la Evangelistic Assemblies of God (EAGT), baada ya aliyekuwa mwasisi wake, Askofu Mkuu, Dk. Moses Kulola, kumaliza kazi yake duniani, inasugua vichwa, huku Makamu wake akiwa na kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa kabla ya mrithi halali jina lake. Aliacha ukuu na mamlaka mbinguni, alipoteza vyote, hata mwili na heshima yake, akatufia msalabani, alipomaliza kazi akatuachia wosia wa kuenenda ulimwenguni kote kuihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Huo ndio wa maana kuliko vyote. Inatupasa sasa kukubali kuacha vyote ili tunapoihubiri injili iwe halisi kwetu na tusiwe kwazo kwa watu wasiookoka. Watu wanatusoma kama barua wanategemea maisha yetu yatoe taswira nzuri kwa watu wengine, ili wamwamini Bwana Wetu Yesu Kristo.”
Tena akaongeza: “Nilifurahishwa na jambo moja kuu katika maelezo ya Askofu Dk. Mtokambali, kwenye taarifa yake kwa waandishi wa habari, aliposema kuwa, milango iko wazi kwa majadiliano ya upendo ili kumaliza mgogoro wa mali, nadhani huo ni ufunguo wa kufikia maridhiano, tukumbatiane tuonesha upendo wa kweli wa Kristo.”
Marehemu Askofu Mkuu, Dk. Moses Kulola |
Akifafanua zaidi alisema: “Sisi ni mwili mmoja katika Kristo Yesu, tunalima katika shamba moja na tunavuna katika shamba hilo hilo, mambo ya mgawanyiko kama wa kanisa la Korintho, ambapo watu walijiita wa Paul, wa kefa na wa Apolo, hayawezi kuushinda upendo wa Kristo. Ukristo halisi ni kupoteza vyote na kupata mbingu.”
“Jamani mbona tunakuwa kama kaka wa mwana mpotevu? aliyelalamika wakati ndugu yake (mwana mpotevu), anapochinjiwa ng’ombe. Lakini tukumbuke moyo wa babaye ambaye hakujali mali za dunia hii, bali alifurahi kuungana tena na kuwa familia moja. Natamani siku moja EAGT na TAG, wakawa tena familia moja wakiaminiana wakipendana na kula pamoja. Namlilia Mungu aivunje vunje miyo ya watu waukumbuke upendo wa Kristo.”
Kisha anaendelea: “Kwa kuwa TAG, wamefungua milango ya kumaliza haya mambo kwa upendo, ni wakati wa EAGT, kuchukua nafasi ya mwana mpotevu na kurejea nyumbani, kukaa chini kuzungumza haya mambo kwa upendo wa Kristo, kuwa tayari kwa yote kwa kuwa mahakama kamwe haiwezi kuleta upendo kwa wanandugu wa kiroho waliotofautiana. Nina hakika mwamuzi wetu ni Bibilia na kamwe hukumu za mahakimu na majaji haziwezi kuturejeshea upendo, najua baba zangu watasoma maoni yangu haya, nawasihi wayachukulie umakini kwani jamii inashindwa kuyaona yale tunayohubiri katika matendo.”
“Hapa simaanishi EAGT, ife na kurudi kuwa kanisa moja la TAG, laahasha! Namaanisha kuwa ndugu wa kiroho, wanaoaminiana na kutenda kazi ya Mungu kwa umoja,upendo na mshikamano, ambao Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Mtokambali ameurejea sana katika hotuba yake mbele ya wanahabari.”
Kanisa la EAGT, ambalo kwa sasa linaongozwa na Kaimu Askofu Mkuu, linatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu mwaka 2015, ili kumpata mrithi halisi wa Askofu Kulola, aliyetwaliwa hivi karibuni.Miongoni mwa mambo yenye mijadala mikuu ndani na hata nje ya kanisa hilo, ni swali la nani wa kuvaa viatu vya Askofu Kulola, na nani hasa aliyeandaliwa kuwa mrithi wa kiti hicho.
Lakini kutokana na uchunguzi wa chanzo cha habari hii, inasemekana kuwa, miongonmi mwa wale wanaotupiwa jicho ni Leonard Mwenzarubi, wa Kanda ya Kaskazini, kwa kile kinachoonekana kuwa ni mtu asiye katika makundi makubwa, kama vile kanda ya Ziwa na Mbeya.
Hata hivyo bado kauli ya mwisho aliyoisema kiongozi huyo akiwa hospitalini imehifadhiwa kama silaha ya kuamua nani atakayeliongoza kanisa na kuimarisha mfumo wake wa kiuongozi.
Uchunguzi uliofanywa na chanzo cha habari hii umebaini kuwa baadhi waumini wa EAGT, bado wanatafakari kauli za mwisho za kiongozi wao ambazo zinatarajiwa kuamua nani akalie kiti chake.
Wapo wanaopendelea nafasi ya Askofu Mkuu kushikwa na mchungaji kijana atakayeweza kuzunguka nchi nzima kuliunganisha kanisa na kuondoa migawanyiko ya kikanda ambayo inadaiwa kuwepo hata wakati Dk. Kulola akiwa hai.
No comments:
Post a Comment