Papa Francis ataka Kanisa Katoliki kuwaelewa watu wote.
Kiongozi wa Kanisa la Roman Duniani Papa Francis anasemani lazima kwa kanisa Katoliki kuacha kuangalia masuala kama ndoa za jinsia moja, utoaji mimba na matumizi ya madawa ya kuzuia mimba na badala yake liwe kanisa la kuwapokea na kuwaelewa watu wote.
Katika mahojiano yaliochapishwa siku chache zilizopita na jarida la Civilta Cattolica Papa alionya kwamba mpaka Kanisa lipate uwiano mpya katika desturi zake za kuwatenganisha watu na kuonyesha huruma , muundo wake wa masuala ya kiutashi unaweza kuanguka kama fungu la karata.
Amesema kanisa katoliki lijione kama hospitali kwenye uwanja wa vita baada ya vita na kufanya kazi ya kuponyesha vidonda vikubwa vya kijamii badala ya kuhangaika na kanuni ndogo ndogo.
Source:voaswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment