Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Jimbo la Mashariki Kusini, Dk. Lawrence Kametta, amewakemea wanaonywesha watu mafuta, maji kutoka Israeli na kutumia vitambaa, wakati wa ibada zao kwa kile alichosema ni sawa na kuvaa hirizi.
DK. Kametta aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa Kongamano la Viongozi wa makanisa yaliyoko katika Jimbo hilo na wake zao, lililofanyika katika kanisa la TAG Buguruni jijini Dar es Salaam.Alisema kuwa, wakati huu wa mwisho wa dunia, wamezuka baadhi ya watu, wanaowahadaa watu wakiwauzia maji, mafuta, chumvi, sabuni na vitambaa, wakisema kuwa ni vitu vya baraka kutoka nchi takatifu ya Israeli, kile alichokifananisha na mtu anayetumia hirizi kuagua watu.
Askofu Kametta pia alikemea tabia hiyo, akisema kuwa kitendo cha kuwauzia watu chumvi, vitambaa, mafuta, maji na vitu vinavyofanana na hivyo ni biashara ambayo lengo lake siyo kumtumikia Mungu bali ni kwa minajili ya kujinufaisha tu.
Askofu Kametta |
“Nashangazwa sana na tabia iliyozuka nyakati hizi kwa baadhi ya watu wanaojiita kuwa ni watumishi wa Mungu, ambao wanawauzia watu maji, wakidai kwamba ndiyo yaliyobatiziwa Yesu kutoka mto Yordani, jambo ambalo halina ukweli wowote, kwani maji aliyobatiziwa Yesu yaliondoka siku ileile,” alisema Askofu na kuongeza:“Msikubali kudanganywa na watu ambao wanatafuta mbinu tu ya kujinufaisha wakipotosha maandiko, mjihadhari nao na wala msiwaunge mkono.”
Aliwataka wakristo, hasa viongozi kutojihusisha kabisa kwenye vitendo kama hivyo, badala yake wajihadhari wawe mfano wakitumia nafasi zao kukemea maovu, na mafundisho yasiyofaa huku wakisimamia neno lililo hai na kufundisha kweli ya Mungu na kushika haki yote.
Akifundisha somo la Kiongozi na Matoleo, Dk. Kametta alisema, kiongozi yeyote wa kiroho anatakiwa kumtumikia Mungu pamoja na mali zake, akitambua kuwa, mali alizonazo vyanzo vyake ni Mungu mwenyewe.
Aidha, pamoja na masomo mengine aliyofundisha, Askofu Kametta, aliwataka Viongozi hao kuwa waadilifu katika utumishi wao, wakitumika kwa ushirikiano pamoja na baba zao wa kiroho na kuepuka migogoro ndani ya makanisa, ili kuleta ufanisi katika kazi ya Mungu.
Naye mama Askofu kametta alitoa wito kwa wazee wa makanisa kuangalia jinsi watakavyo wawezesha wake za wachungaji, kwa kile alichodai kuwa, wamekuwa wakiwategemeza Wachungaji na kuwasahau wake zao.
Mtambue kuwa huduma ya mchungaji inategemea sana maombi ya mama, hivyo tunawaomba wazee wa kanisa kuwajali na hata ikibidi kuwaendeleza kimasomo, kwani mmekuwa mkiwaendeleza tu wachungaji na kusahau wake zao jambo ambalo limesababisha tofauti kubwa katika maendeleo ya Kanisa.
Wakati huohuo, Askofu Kametta akimkaribisha mmishonari wa Tanzania nchini Madagasca, Poul Balela, hukubiri katika kanisa la Amani Christian Centre, alihimiza wale walioitwa na Bwana Yesu kujitoa kwa hali na mali kuwafikia wasiofikiwa ndani na nje ya Tanzania.
Akitoa mfano Askofu Kametta alisema wakati fulani akiwa katika kuhubiri huko kwa wasonjo, alilazimika kuwa katika wakati mgumu, akanywa supu yenye inzi wengi, lakini hakutetereka kwa kuwa alijua anayemtumikia ni nani.
“Umisheni ni kujitoa maisha yako kwa Bwana Yesu moja kwa moja, huyu mmishonari ni mtume wa Mungu aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya wengine, nilifika kwa Wasonjo mahali ambapo alikuwa akifanya umisheni na nilikunywa supu yenye inzi wengi nakumbuka nilikuwa na mmarekani mmoja akaniangalia akaniambia kunywa kama ilivyo, usiteme, ukitema mate tumeharibu kila kitu,”alisema na kuongeza:
No comments:
Post a Comment