Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, amezitaka mamlaka zinazohusika kuvifuta vyama vyote vya siasa vinavyoendeshwa kwa misingi ya ukabila havivurugi nchi.
Askofu Kakobe, amezungumza Kanisa kwake hivi karibuni kwenye ibada ya sikukuu ya Krismas
alisema miaka kadhaa iliyopita nchi haikuwa akiandamwa na vitendo vya ukabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.
Alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu kimejulikana kuwa vinendeshwa kikabila tofauti na sasa ambapo hali imekuwa mbaya.
Alisema kuna baadhi ya vyama nya siasa nchini ambavyo kwa kipindi kirefu vimeendeshwa kikabila, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.
Askofu Kakobe, alizishauri mamlaka zinazohusika kuvifuatilia vyama hivyo kuvifuta katika orodha ya vyama vya siasa kwani ni hatari katika mustakabadhi wan chi na wananchi wake.
Akizungumza suala zima la uongozi wanachi, hususani kitendo cha mawaziri kadhaa kuondolewa katika nyadhifa zao, alisema ubovu wa viongozi unachangia na mfumo wa kuteua viongozi.
Askofu Kakobe alisema kwa kawaida uongozi ni kipaji, hivyo watu wanapoona kunakuwa na viongozi wasiowajibika kikamilifu, wajue kuwa kuna tatizo katika uteuzi wao. Moja ya tatizo kubwa linaloathiri nchi kwa sasa alisema ni kuchagua watu kwa kuangalia maenao wanayotoka.
No comments:
Post a Comment